“Uislamu uliziteka nchi zilizoishinda katika vita vya msalaba na hivyo kuingiza fani mbali mbali na ustaarabu katika maisha ya ulimwengu wa Wakristo.
Maisha ya walatini yalikuwa na kutu katika baadhi ya makonde ya harakati ya mwanadamu, kwa mfano kama vile uhandisi wa ujenzi. Athari za Uislamu ziliingia katika ulimwengu wa Kikristo muda wote wa karne ya kati. Ama Sicily na Andalusia (Hispania) athari ya ufalme mpya wa Waarabu ulidhihirika zaidi na kupanuka.”