Arnold J. Toynbee

quotes:
  • Dini ni Maisha
  • “Dini ni katika vipaji muhimu vya mwanadamu. Tunatosheka kusema kuwa mtu kukosa dini humsukuma kwenye hali ya kukata tamaa kiroho, inamlazimisha kutafuta nguvu ya kidini kwenye sahani zisizomiliki chochote ndani yake.”


  • Mwalimu wa Wanadamu
  • “Mwenendo wa Mtume wa Waarabu umechukua (umeshuka) akili za wafuasi wake; na haiba yake ikapanda kwao juu zaidi. Waliamini ujumbe wake kwa imani ambayo imewafanya wakubali Wahyi ulivyokuwa ukiteremka kwake. Kama ambavyo matendo yake (kama yalivyorekodiwa na Sunnah) ilikuwa ni chanzo cha kanuni. Kanuni ambazo haziishi katika kupanga maisha ya Kiislamu peke yake, bali yaliambatana vile vile na mahusiano ya Waislamu Wafunguzi (kwa nchi nyingi) na raia zao na wasio Waislamu.”


  • Ujumbe wa Utume wa Muhammad.
  • “Muhammad alitumia muda wake wote kufanikisha ujumbe wake katika kudhamini hizi mandhari mbili katika mazingira ya jamii yake ya kiarabu, hayo mawili ni Umoja katika Fikra ya dini, kanuni na nidhamu ya utawala na hukumu. Yote yalitimia kwa fadhila za nidhamu ya Uislamu ambayo ulibeba mgongoni mwake umoja na utawala wenye mamlaka kwa pamoja. Uislamu ukawa na nguvu kwa fadhila hiyo, nguvu yenye msukumo na utisho imewahamisha waarabu kutoka kwenye umma wa kijahili na kuwa ulioendelea.”


  • Ushindi wa Mateka.
  • “Uislamu uliziteka nchi zilizoishinda katika vita vya msalaba na hivyo kuingiza fani mbali mbali na ustaarabu katika maisha ya ulimwengu wa Wakristo. Maisha ya walatini yalikuwa na kutu katika baadhi ya makonde ya harakati ya mwanadamu, kwa mfano kama vile uhandisi wa ujenzi. Athari za Uislamu ziliingia katika ulimwengu wa Kikristo muda wote wa karne ya kati. Ama Sicily na Andalusia (Hispania) athari ya ufalme mpya wa Waarabu ulidhihirika zaidi na kupanuka.”