Tarekh ya mitume:Mohammad

Tarekh ya mitume:Mohammad

Tarekh ya mitume:Mohammad

Bishara ya Mtume wa mwisho

Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ni mwisho wa mitume na manabii, Issa – (‘Alayhi salaam) amewabashiria Bani Israil kuja mtume wa mwisho, Allah amesema: “Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!” (61:6),

Hivyo basi bishara ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) ipo katika Taurati na Injili. Allah amesema: “Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.” (7:157),

Bali Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) amechukua ahadi na mkataba kwa manabii wamuamini Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) na wamnusuru yeye kama atatumwa kwao wakiwa hai, na wawaambie kaumu zao hilo ili habari yenyewe ienee baina ya Ummah zote, Allah amesema: “Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia.” (3:81)

Qur-aan imeashiria bishara hizo, na kuthibitisha ukweli wa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam), Allah amesema: “Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya Kitabu” (13:43),

Na katika aya nyingine: “Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale. Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? ” (26:196-197)

Na akazungumzia kuhusu msimamo wa Ahlul kitab ambao ilipasa kuwa ndio wa mwanzo na waumini kwa kumjua kwao kama walivyokuwa wakiwajua watoto wao: “Wale tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao; na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua.” (2:146),

Allah Mtukuka amesema: “Na alipo wajia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kuthibitisha yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale walio pewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu hicho nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui.” (2:101),

Tabiri zile zikathibitika kwa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam), na kuwa yeye ndie Mtume ambae Allah amezungumzia kuja kwake, hata hivyo kundi moja miongoni mwao likaficha haki likiwa linajua, na wakiacha yaliyokuja kwenye vitabu vyao vitakatifu nyuma ya migongo yao kama kwamba hawafahamu.

Dawah ya Mtume (Swala Llahu 'alayhi wasallam) na miujiza yake mikubwa

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) alikuja na Tawhidi: Yaani kumpwekesha Allah peke yake bila kumshirikisha kama walivyo kuja Mitume na Manabii waliotangulia, Allah Mtukuka amesema: “Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.” (21:25),

Kama alivyotumwa kusadikisha Mitume na manabii waliotangulia, bila ya kutofautisha chochote katika kuwaamini wao: “…hatutafautishi baina ya yeyote katika hao…” (2:136),

Bali yule ambae atamsadiki na kumuamini Muhammad bila ya kuamini mtume yoyote au nabii aliokuja ndani ya Qur-aan-basi mtu hakumkubali wala kumuamini Muhammad: “Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo.” (42:13)

$The_Gospel_of_Matthew.jpg*

Injili ya Barnaba.

Muhammad …Mtume wa Mwisho.
“Kwa sababu Mungu atanipandisha kutoka ardhini na atabadilisha mandhari ya haini hadi kila mmoja wenu atadhania: pamoja na hayo pindi anapokufa mtu muovu mimi nitakuwa katika fedheha muda mrefu Ulimwenguni, lakini kutokana na mimi atakapokuja Muhammad Mtume Mtukufu doa hili litaniondoka.”

Na akatia mkazo kuwa yeye ni mja wa Allah: “Sema: Mimi ni mwanaadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.” (18:110),

Na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) alikuwa ni Umiyyi hasomi wala haandiki (yaliyoandikwa) kama ilivyokuja sifa yake katika vitabu vilivyotangulia ili Ahlul Kitab wamtambue ambao wanajua sifa zake zilizokuja ndani ya vitabu vyao; kama alivyosema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala): “Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.” (7:157).

Allah alipitisha miujiza ile kwenye mikono yake kama alivyopitisha katika mikono ya Mitume kabla yake – miujiza mingi ilikuwa ni ya kuonekana japokuwa muujiza mkubwa zaidi ulikuwa ni Qur-aan tukufu ambayo na ni yake kuna habari za wa mwanzo na za wa mwisho, ubainifu, uongofu, rehma na bishara: “…Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.” (16:89),

Na uoni kwa waumini: “Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu wanao yakinisha.” (45:20),

$The_Gospel_of_Matthew.jpg*

injili ya Barnaba

Injili inayotoa biashara ya Muhammad.
“Itabakia hivi hadi atakapokuja Muhammad Mtume wa Mungu ambaye muda atakapofika atauweka wazi uongo kwa walioamini sheria ya Mungu. Na imekuja katika Isaya: Mimi nimefanya jina lako Muhammad Ewe Muhammad Ewe uliye mtakatifu kutoka kwa Mungu Jina lako lipo milele. Na katika Habakkuki imekuja (3:3-6): “Mungu alikuja kutoka Temami, yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukaangaza mbingu kutokana na haiba ya Muhammad, nayo dunia ikajaa sifa yake. Au kama ilivyokuja katika Isaya: Nilichompa sitompa mwingine. Ahmad (jina lingine la Muhammad) anamhimidi Mungu mazungumzo yenye kuja kutoka kwa watu bora duniani: Viumbe watafurahi kwayo na kumtakasa kila kitukufu na kuadhimisha kila sehemu.”

Mtume Ummiy (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) akawabainishia watu walichotofautiana ndani ya Qur-aan: “Na hatukukuteremshia Kitabu isipo kuwa uwabainishie yale ambayo wanakhitalifiana, na kiwe Uwongofu na Rehema kwa watu wanao amini.” (16:64).

Msimamo wa watu wake kuhusu Dawah yake?

Pamoja na makafiri wa kikureishi kujua ukweli wake na amana yake na kwa sababu tokea mwanzo walimuita ‘Mkweli mwaminifu’ lakini pamoja na hayo walimkadhibisha, Allah akawapa changamoto wakusanyike wote, watu kwa majini na walete mfano wa Qur-aan hii: “Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.” (17:88),

Wakashindwa pamoja na uwezo wao wa lugha na akawapa changamoto nyingine baada ya kukusanyika walete aya kumi tu mfano wake: “Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.” (11:13),

Wakashindwa na akawapa changamoto nyingine ya kuleta sura moja inayokaribiana nayo. “Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake…” (2:23);

Walishindwa pamoja na uwezo wao wa lugha.

Ukamilifu wa neema na nusura ya Allah na kuunga mkono

Makafiri wa Kikureishi wakaendelea kumkadhibisha; Allah akamuamrisha kusubiri kama walivyosubiri Ulul ‘Azm katika mitume na manabii kabla yake: Ibrahim, Nuuh, Musa na Issa (‘Alayhi salaam) wote: “Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa…” (46:35)

$Goethe.jpg*

Goethe

Mwandishi na mshairi wa Ujerumani.
Kiigizo Chema na mfano wa juu.
“Nimetafuta katika historia mfano wa juu wa mtu huyu. Nikaupata kwa Nabii Muarabu Muhammad.”

Akasubiri na akaendelea na da’wah yake akiwalingania na kuwafundisha maneno yake na maneno ya Muumba wake, Allah akamtosheleza na kumlinda: “Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na Waumini walio kufuata.” (8:64), “Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake?...” (39:36)

Allah akamnusuru kama alivyowanusuru Mitume wengine: “Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.” (58:21),

$Michael_Hart.jpg*

Michael Hart.

Mwandishi wa Kimarekani.
Uliza na Qur-aan itakujibu.
“Nimesoma Qur-aan nikapata majibu kwa kila swali linalohusu maisha.”

Akasema Mtukuka: “Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda. ” (37:171-173), “Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” (40:51).

Makafiri wakataka kuzuia ujumbe wake na kuzima nuru yake, lakini Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) akatimiza neema yake: “Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia. ” (61:8-9).

$Abdul_AhadDawud.jpg*

David Benjamin Kelden

Kiongozi Mkuu wa Wakristo Mosol-Iraq
Na kwa watu ni Ahmad.
“Hakika ule msemo maarufu wa Kikristo: Utukufu ni kwa Mungu aliye juu. Katika ardhi ni amani, na kwa watu ni furaha. Haikuwa hivi, bali ilikuwa: Utukufu ni kwa Mungu aliye juu na katika ardhi ni amani na kwa watu ni Ahmad.”

Akakamilisha neema yake na kuudhihirisha Uislamu, akatilia mkazo juu ya Tawhidi ya Allah katika dini zote, akakamilisha neema yake kwa wanadamu kwa ujumbe huu na dini hii: “…Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini…” (5:3),

Bali aliihifadhi dini hii, na akaufanya ujumbe huu kubakia hadi Siku ya Kiama: “Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” (15:9);

$Henri_de_Castries.jpg*

Henri de Castriesry.

Luteni wa zamani wa jeshi la Kifaransa.
Qur-aan ni muujiza.
“Qur-aan inaongoza fikra na kukamata nyoyo, imeshuka kwa Muhammad dalili ya ukweli wake.”

Kwa hiyo huu ni ujumbe hitimisho wa ujumbe wote: “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu” (33:40),

Nao ni ujumbe wenye kubakia hadi pale ambapo Allah atairithi ardhi hii na waliomo.

Basi ni ujumbe gani huu wenye kubakia kwa hifadhi ya Allah hadi Siku ya Malipo…..?!