Tarekh ya mitume:Issaa

Tarekh ya mitume:Issaa

Tarekh ya mitume:Issaa

Maryam ('Alayha salaam)

Baba yake Maryam (‘Alahyi Salaam) alikuwa ni ‘Imran, mja miongoni wa waja wa Bani Israil, alitokana na kizazi cha Dawud (‘Alahyi Salaam), katika nyumba ya wacha-Mungu, mama yake Maryam alikuwa hashiki mimba, akatamani kupata mtoto; akaweka nadhiri kwa Allah kuwa akipata mimba atamtoa mwanae wakfu kuitumikia dini na msikiti mtukufu (yaani mpenzi katika nyumba tukufu): “Alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet’ani aliye laaniwa.” (3:35-36);

Allah akamkubalia mama yake Maryam nadhiri yake: “Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema…” (3:37)

Katika sura nzuri na mandhari ya furaha na njia ya waja wema wenye furaha; na hivyo basi Allah akasema: “…na akamfanya Zakariya awe mlezi wake…” (3:37)

Allah akamneemesha kwa mlezi wake ni nabii vile vile, inasemwa kuwa alikuwa ni mume wa mama yake mdogo au mume wa dada yake: “…Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” (3:37)

Ukarimu na utawala wa Allah kwake yeye, hivyo Mola wake akamkirimu, kumchagua, kumtoharisha, kumkamilisha na kumuamrisha kumuabudu: “Na angalia pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteuwa, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wote. Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao.” (3:42-43),

Maryam kumzaa Issa ('Alayhi salaam)

Kisha Allah alipotaka Maryam amzae Issa (‘Alahyi Salaam) alijitenga na watu wake: “Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki; Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.” (19:16-17)

Maryam akaogopa, akimdhania kuwa anataka kumfanyia uovu: “(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.” (19:18-19),

Maryam akashangaa: “Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?” (19:20).

Yule mjumbe akamwambia hii ni hukumu ya Allah, na Mwenyezi Mungu amekufanya kuwa aya (dalili) na jambo hilo ni jepesi kwake: “(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.” (19:21),

%%

Manabii ni watu bora zaidi.
“Baadhi ya yaliyopotoshwa juu ya Mitume ya Allah na manabii inataja kuwa walilewa, au kuangukia katika uzinifu, au kuamrisha kuwa watu ni yote hayo ni upotofu mbayo haifai na hailingani na watu wenye tabia za juu mbali ya kuwa wao ni watu waliokuwa bora zaidi…. Wao ni Manabii wa Allah, katika hayo ni yale yaliyokuja – katika Taurati kuhusu Dawudi (‘Alayhi Salaam) (Samweli (2) 11/2-26) na kutoka kwa Yoshua bin Nuun (mwana wa Nuni) (‘Alayhi Salaam) (Yoshua 6/24) na kutoka kwa Musa (‘Alayhi Salaam) (Hesabu:31/14-18) Musa (‘Alayhi Salaam), na mengine mengi yasiyokuwa hayo hayafai Mtume wa Allah.”

Kwa hiyo katika ambayo Mwenyezi Mungu ameyataka ni ishara ya kuzaliwa kwa Issa (‘Alahyi Salaam) kutoka kwa mama aliyetoharika ambae hakuzini au kufanya maovu na bila ya kuwa na baba (hii ni rehema kutoka kwa Allah na utekelezaji wa hukumu ya Allah Ta’ala. Hivyo kuzaliwa Issa (‘Alahyi Salaam) kukawa ni muujiza, miongoni mwa miujiza na aya miongoni mwa aya zake, mfano wake katika hilo ni mfano wa kuumbwa Adam bila baba: “Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka.” (3:59-60).

Aliposhika mimba alijiweka mbali na watu wake: “Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. ” (19:22)

Uzazi ukamjia: “Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!” (19:23),

Na hapa ndipo kulipotokea muujiza mwingine kwa Nabii wa Allah (Issa (‘Alahyi Salaam): “Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu.” (19:24-26),

Na aliporejea kwa watu wake, kukutana nao kulikuwa kubaya kwa Maryam mwenye kutoharika mwenye kujihifadhi: “Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. ” (19:27-28),

Nae hakuwajibu, bali: “Akawaashiria (mtoto)….” (19:29),

Wakachukizwa wakasema: “…Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi?” (19:29), “(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.” (19:30-33),

Lakini kundi moja la Mayahudi halikuamini, wakamtuhumu Al-Twahira kwa uzushi mkubwa: “Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa” (4:156),

Wakamtuhumu Al-Twahira kwa uzinifu, Allah akamkosha na tuhuma ile, na akamuelezea Maryam kuwa: “Na mama yake ni mwanamke mkweli.” (5:75);

Muumini wa Unabii na ujumbe wa Issa (‘Alahyi Salaam).

Meza ya chakula kutoka mbinguni

Allah akamneemesha Mtume wake na mja wake Issa (‘Alayhi salaam) na mama yake: “Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili…” (5:110),

Na akamtia nguvu kwa miujiza na alama: “…Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi mtupu! Na nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu.” (5:110-111),

Kisha ni kuwa Al-Hawariyyuun (wafuasi wake) walimtaka Issa (‘Alayhi salaam) amuombe Mola wake awateremshie chano cha kula kutoka mbinguni, Allah kasema: “Wanafunzi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni?...” (5:112),

Issa akawaogopea kutoshukuru kwao: “…Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. Wakasema: Tunataka kukila chakula hicho, na nyoyo zetu zitue, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe miongoni mwa wanao shuhudia.” (5:112-113),

%%

Issa anasisitiza katika Injili kuwa Mungu ni mmoja.
“Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndio hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.” (Marko Mtakatifu 12:28-35). Huu ni usia wa kwanza.

Kwa hiyo akamuomba Mola wake: “Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku. Mwenyezi Mungu akasema: Hakika Mimi nitakuteremshieni hicho. Lakini yeyote katika nyinyi atakaye kanya baadae, basi hakika Mimi nitampa adhabu nisiyopata kumpa yeyote katika walimwengu.” (5:114-115),

Hata hivyo baadhi ya walioteremshiwa walikufuru.

Vitimbi vya mayahudi na jaribio lao la kumsulubu Issa ('Alayhi salam)

Ama Mayahudi katika Bani Israil waliomkadhibisha Nabii wa Allah Issa (‘Alayhi salaam) kule kukufuru kwao na kukadhibisha kwao na vitimbi vyao viliendelea kwa Isa (‘Alahyi Salaam): “Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga.” (3:54),

Allah akamjulisha kuhusu vitimbi vyao, na jinsi ambavyo Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) atamuokoa kutokana nao: “Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.” (3:55),

Na walipoendelea kuvunja ahadi, vitimbi, ukafiri wao, na jaribio lao la kuuwa manabii wa Allah na kumtuhumu Al-Twahira Maryam (‘Alayha salaam) kwa uzushi Allah alisema: “Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi zao, na kuzikataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri kwa kufuru zao, basi hawaamini ila kidogo tu - Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa, Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu…” (4:155-157)

$Frederick Dolamark_Archbishop_of_Johannesburg.jpg*

Frederick Dolamark.

Mkuu wa Maaskofu Johannesburg.
Issa katika Uislamu
“Nilipousoma Uislamu nilipata sura nyingine tofauti za Masihi (‘Alayhi Salaam) ambazo ziliingiza katika nafsi yangu athari kubwa.”

Lakini Allah alimuokoa dhidi yao: “…nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu ….” (4:157)

Bali walimuua aliyefanana nae: “…bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (4:157-158),

Allah akamuokoa Mtume wake Issa (‘Alayhi salaam) na kumnyanyua kwake: “Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao.” (4:159).

%%

Injili inakanusha kusulubiwa na inathibitisha Kuinuliwa Mbinguni.
“Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.” (Yohana 8:59). “Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao.” (Yohana 10:39). “Hili limetokea ili yatimie yaliyokuja kwenye kitabu: Hakuvunja chochote katika mfupa.” (Yohana 36:19). “Huyu Yesu huyu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni.” (Matendo ya Mitume 1:11)

Huu ndio ukweli wa kisa cha Issa (‘Alayhi salaam): “Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. ”(19:34-35),

Kwa hiyo Allah kabainisha kuwa haifai Yeye kuwa na mtoto; kwa kuwa Yeye ni Muumba wa kila kitu na mmliki wake, na kila kitu kinahitaji na dhalili kwake, na wote mbinguni na ardhini ni waja wake, Yeye ndie Mola wao La ilaha illa Llah; ni Yeye na hakuna Mola mwingine asiyekuwa Yeye.