Dini hiyo ilingane na tabia nyema na matendo mema, Allah amesema: “Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka. Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” (6:151-153)
Na Allah akasema, “Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.” (16:90)
Haisihi dini ambayo italingania uongo au mauaji au dhulma au wizi au kuhaka na kupora na kufanya uasi au mfano wa hayo.
Itengeneze mahusiano kati ya Mwanadamu na Muumba wake, na mahusiano ya viumbe kwa viumbe, Allah amesema, “Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui. ” (12:40)
Hivyo basi inapasa dini hiyo kutengeneza majukumu ya mwanadamu kwa Mola wake, kadhalika itengeneze mahusiano ya viumbe na watu, Allah amesema: “Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia….” (4:36).
Dini hiyo imuheshimu mwanadamu na imkirimu wala isitofautishe baina ya wafuasi wake kwa tofauti zozote zile ziwe za kijinsia, rangi au kabila; kigezo cha kufadhilishwa na ubora ni kile anachokipata mwanadamu kutoka katika kazi yake, elimu na ucha-Mungu, Allah amesema: “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini…” (17:70)
Na akasema vile vile, “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” (49:13).
Nane: Dini hiyo imuelekeze mwanadamu katika njia sahihi isiyokuwa na kombo, na njia hiyo iwe ni tiba kwa mwanadamu na iwe nuru na muongozo wao, Allah amesema akielezea kuhusu majini baada ya kusikiliza kwao Qur-aan wakiambizana, “Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka.”(46: 30),
Na akasema Allah, “Na tunateremsha katika Qur’ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara. ” (17:82)
Nayo ni nuru na muongozo wa watu ambao unawaongoza watu kutoka kwenye dhuluma za ujinga (ujahili) na upotevu kwenda kwenye Nuru ya utiifu na furaha katika nyumba zote mbili, Allah amesema: “Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha.” (5:15)
Na Akasema Allah tena, “Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet’ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet’ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu. ” (2:256-257).