Ikiwa mtu binafsi hana budi awe na dini, basi haja ya jamii mbali mbali kwenye dini ni kubwa zaidi, Dini ni ngao yenye kuikinga jamii; na hiyo ni kwa sababu maisha ya mwanadamu hayasimami isipokuwa kwa kushirikiana na watu wake katika mambo ya kheri: “…Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui...” (5:2),
Na ushirikiano huu hautimii ila kwa mfumo unaopangilia mahusiano yake, na kuainisha majukumu yake na kudhamini haki zao, mfumo huu hauna budi kutoka kwa yule mpole mwenye ujuzi na elimu kwa anayohitajia mwanadamu, “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” (67:14)
Kila ambapo mwanadamu anapokwenda kinyume na dini, sheria yake na mfumo wake ndipo jinsi ambapo hupotea na kughibu na kudumbukia katika kiza cha shaka, upotevu, haya, taabu na mateso.
Hakuna katika ardhi yote hii nguvu ambayo ni sawa na nguvu ya dini au mtu kufuata dini katika kudhamini watu kuheshimu mfumo au utaratibu Fulani, na kadhalika kudhamini mshikamano wa jamii na utulivu kwa mfumo wake na sababu zote za usalama na siri katika hilo ni kuwa mwanadamu anatofautiana na viumbe vingine kwa kuwa harakati zake na matendo yake ya hiari yanayotawalia uongozi wake kitu ambacho hakitokei katika usikizi wake wala uoni wake, bali ni akida ya kiimani ambayo ina adabisha roho na kutakasa kiwili wili chake na kuifanya kuwa ni mwangalizi wa siri yake kama ambavyo inakuwa ni mwangalizi wa dhahiri yake, “Na ukinyanyua sauti kwa kusema...basi hakika Yeye anajua siri na duni kuliko siri.” (20:7).
Mwanadamu huongozwa na akida iwe ni sahihi au mbovu, akida yake ikitengemaa basi mambo yake yote yatatengemaa, na ikiharibika mambo yake yote yataharibika.
Kwa ajili hiyo dini ndio ikawa dhamana bora zaidi ya kusimamisha miamala baina ya watu katika misingi ya uadilifu na usawa, na hilo likawa ni jambo ambalo halina budi katika jamii, wala hatutokuwa tumekosea tukisema kuwa dini itachukua nafasi ya moyo katika kiwiliwili cha Umma mbali mbali.
Ikiwa dini kwa ujumla inachukua nafasi hii, na leo hii mtu akiangalia ataona dini nyingine na mila mbali mbali ulimwenguni, na kila jamii yenye dini fulani hufurahishwa nayo na hukamatana nayo. Kama hali ndivyo hivyo ilivyo ni dini gani basi ambayo ndio sahihi na ambayo itamthibitishia na kumkamilishia nafsi ya mwanadamu anachotaka kukifikia?! Na ni nini vidhibiti vya dini ya haki?!