Ni dini ipi ambao tunaweza kuipitishia vigezo vya dini ya haki?

Ni dini ipi ambao tunaweza kuipitishia vigezo vya dini ya haki iliyotangulia?

Ni dini ipi ambayo tunaweza kuipitishia vigezo vya dini ya haki iliyotangulia?

Vipengele vya dini mbali mbali

%%

Lakini Mwenyezi Mungu ni mmoja
“Watafiti wametaabika wakiwa wanahesabu idadi ya miungu ya dini za wanadamu: Idadi ya miungu ya Wamisri wa kale ni zaidi ya miungu mia nane, na idadi ya miungu ya Kihindu ni zaidi ya miungu elfu kumi, na mfano wa ushirikina huu kwa Wagiriki na Wabudha, na mengine miongoni mwa dini za watu za ardhini.”

Tunaweza kugawa dini mbali mbali kulingana na vyanzo vyake katika makundi mawili:

-Dini za Ardhi au za Wanadamu, sio za mbinguni wanadamu wanaziainisha na kuziendeleza wao wenyewe, sio zilizoshuka kutoka kwa Allah Ta’ala; dini hizi ni kama vile Ubudha, Uhindu, Umajusi na upagani, hizi ni dini ambao zipo mbali kabisa na dini ya kweli, dini hizi zinatokana na matamanio ya mwanadamu; “Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?” (45:23)

Sio dini kutoka kwa Mungu, bali dini za matamanio ya watu, hivyo basi utaona kuwa dini hizi zimejaa uzushi, udajali, matabaka na migongano, Allah Ta’ala amesema, “…Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi.” (4:82).

-Dini za Mbinguni kutoka kwa Allah, kama vile Uyahudi, Ukristo na Uislamu, na watu wenye dini hizi Muumba aliwaelekeza dini yao na kuridhia, Allah amesema, “Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.” (42:13)

Wasifu wa dini zilizotungwa na watu

$Tolstoy.jpg*

Tolstow

Mwanafasihi wa Kirusi
Sheria ya kweli
“Nimefahamu na kudiriki kuwa anachohitaji mwanadamu ni sheria ya mbinguni inayoweka haki na kuondosha batili.”

Bila shaka dini nyingi za ardhini ni kundi kubwa la fikra mbali mbali na mkusanyiko wa wanadamu waliochagua katika yanayonasibiana na matamanio yao, lakini baada ya muda mfupi mwanadamu akagundua kuwa haifai, kwa hivyo wao wakajaribu kuziendeleza, na wao hali kadhalika kuendelea katika kupotea, sifa za dini hizi za ardhini (watu) ni hizi zifuatazo:-

1-Ushirikina: Kila siku wanatengeneza Mungu mpya, Mungu wao anatengenezwa na mikono yao, wala hawafikiri kutokuwezekana kuwepo Mungu pamoja na Allah vinginevyo wangepigana au kugongana, Allah amesema: “Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo.” (23:91-92)

2-Utabaka: Dini za ardhi zimesimama katika matabaka na kuwafanya watu kuwa watumwa; kwani watu wameweka kwa ajili yao wenyewe na sio wengine; ili wafanikiwe katika lengo lao na wawafanye wengine kuwa watumwa, Allah amesema: “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” (49:13)

3-Na Mwenyezi Mungu akawakataza watu kuangaliana vibaya kwa kusema, “Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao” (49:11),

%%

Tabaka za Kijeuri
“Mgawanyiko wa kitabaka katika dini ya Kihindu uko kama ifuatavyo: Tabaka la weupe; Hili ni tabaka la watu wa dini na wanazuoni. Tabaka la Wekundu; linakusanya maamiri na wanajeshi. Tabaka la Manjano: linakusanya wakulima na wafanya biashara. Tabaka la Weusi linahusisha mafundi mikono na viwanda. Ama tabaka la tano ambalo linafahamika kuwa ni tabaka la watu duni (Untouchable-tabaka la chini kabisa) linahusisha wenye kazi duni. Na tabaka za juu linatumikisha matabaka ya chini na matabaka ya chini yanahudumia matabaka ya juu.”

Hivyo basi kwa Mwenyezi Mungu hakuna fadhila au hakuna ubora wa mweupe kwa mweusi, wala kwa ukoo fulani ukilinganisha na mwingine wala kaumu fulani dhidi ya kaumu nyingine. Ama dini za ardhi (zilizoundwa na watu) zinasimama kwa misingi ya tabaka.

4-Kwenda kinyume na maumbile (fitra): Dini za ardhi zinakwenda kinyume na maumbile sahihi ya mwanadamu, zinasimamia katika kumbebesha mwanadamu asiyoyaweza, zipo kinyume na mazingira, na tabia ya mwanadamu, akili sahihi, kwani wafuasi wake wamekuwa mbali na njia ilionyooka na wakabadilisha, Allah amesema: “Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.” (30:30)

5-Uzushi: Ni itikati au fikra iliyosimama juu ya mawazo matupu bila ya uwepo wa sababu za kiakili, au za kimantiki au za kielimu, na dini nyingi za ardhini zina uzushi usiokuwa na dalili yoyote au hoja, wala uzushi haujengwi ila kwa uzushi wenyewe, amesema kweli Allah: “…Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.” (27:64).

6-Migongano: Hizi ni dini ziliojaa migongano, kila kundi linasimama katika kupinga kundi jingine na huziendeleza fikra hizi pinzani, Allah amesema: “…Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi.” (4:82)

Lengo la dini za mbinguni

%%

Migongano ya Kibudha
“Mabudha wanakana Mungu na wanadai (au baadhi yao) kuwa Budha ni mtoto wa Mungu, na wanapinga roho na wanaamini kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa mtu mwingine.”

Ama dini za mbinguni ni neema kutoka kwa Allah ambazo Mwenyezi Mungu amewapa wanadamu ili awaongoze na kuwamulikia njia yake na kuwasimamishia hoja juu yake na kuwaepusha, upotofu, ushirikina, kwenda kinyume na maumbile (fitra) na akili kwa kuwatuma Mitume wafikishe ujumbe kutoka kwa Mola wao: “Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. ” (4:165).