“Hakuna Mungu isipokuwa Allah peke yake hana mshirika. Yeye haki na kila asiyekuwa yeye ni batili, ametuumba na ameturuzuku. Uislamu ni kujisalimisha kwa Mungu, kumnyenyekea yeye, kutulia kwake na kumtegemea yeye tu–na kuwa nguvu yote iko katika (istiqama) kunyooka katika hekima yake, na kuridhika kwa mgawo wake kadiri itakayokuwa katika dunia hii na katika akhera. Na kwa kadiri yoyote Allah atakavyotupa mtihani (na hata ikiwa ni mauti) basi inatakiwa kupokea hayo nyuso kunjufu na nafsi zenye ghera, zenye kuridhia vile vile na kujua kuwa hayo ni kheri na kuwa hakuna kheri zaidi ya hayo, kwani ni upumbavu mtu kuweka ndani ya akili yake dhaifu mizani ya Ulimwengu na hali zake, bali ni juu yake kuamini kuwa Ulimwengu una sheria adilifu, na hata kama itapotea katika ufahamu wake, na ya kuwa kheri ndio msingi wa ulimwengu, na kutengeneza (Islahi) ni roho ya ulimwengu…ni juu yake kufahamu hayo na kuamini na kufuata katika utulivu na Ucha-Mungu.”