- Tabia za Utume.
“Kwa hakika mimi nampenda Muhammad: Sababu ni ile tabia yake safi aliyonayo na mawazo na fikra zake. Kwa hakika mtoto huyu wa majangwani alikuwa ni mwanamme mwenye rai huru: Hujitegemea mwenyewe tu wala hajidai yasiyokuwepo, hakuwa mwenye kiburi!! Hata hivyo hakuwa dhalili, akisimama na nguo zake zenye viraka kama vile alivyompatia Mola wake na kama alivyotaka mwenyewe. Huzungumza na wafalme wa Kirumi na wa Kiajemi kwa maneno yake yenye kutetemesha anawaelekeza maisha haya na maisha ya akhera. Alikuwa anajua uwezo wa Nafsi yake, alikuwa ni mtu mwenye kupitisha azma yake, hacheleweshi kazi ya leo hadi kesho.”
- Mwenyezi Mungu hana Mshirika.
“Hakuna Mungu isipokuwa Allah peke yake hana mshirika. Yeye haki na kila asiyekuwa yeye ni batili, ametuumba na ameturuzuku. Uislamu ni kujisalimisha kwa Mungu, kumnyenyekea yeye, kutulia kwake na kumtegemea yeye tu–na kuwa nguvu yote iko katika (istiqama) kunyooka katika hekima yake, na kuridhika kwa mgawo wake kadiri itakayokuwa katika dunia hii na katika akhera. Na kwa kadiri yoyote Allah atakavyotupa mtihani (na hata ikiwa ni mauti) basi inatakiwa kupokea hayo nyuso kunjufu na nafsi zenye ghera, zenye kuridhia vile vile na kujua kuwa hayo ni kheri na kuwa hakuna kheri zaidi ya hayo, kwani ni upumbavu mtu kuweka ndani ya akili yake dhaifu mizani ya Ulimwengu na hali zake, bali ni juu yake kuamini kuwa Ulimwengu una sheria adilifu, na hata kama itapotea katika ufahamu wake, na ya kuwa kheri ndio msingi wa ulimwengu, na kutengeneza (Islahi) ni roho ya ulimwengu…ni juu yake kufahamu hayo na kuamini na kufuata katika utulivu na Ucha-Mungu.”
- Uzushi na Fedheha
“Wanadai wenye kasumba kuwa Muhammad hakutaka ila umaarufu wake binafsi na kujifakharisha na utawala.
Sivyo kabisa, naapa kwa Mungu ndani ya kifua cha bwana mkubwa yule mtoto wa jangwani, ni mwenye nafsi kubwa iliyojua huruma, kheri, wema, mapenzi na hekima, mwenye fikra zisizo kuwa na tamaa ya kidunia, na nia yake ilikuwa ni kinyume na kutafuta utawala na hadhi na kwa nini isiwe hivyo hali ya kuwa ile ni nafsi safi na mtu miongoni mwa watu ambao si zaidi ya kuwa na ikhlasi na makini.”