UKWELI WA UTUME NA UJUMBE WAKE

UKWELI WA UTUME NA UJUMBE WAKE

UKWELI WA UTUME NA UJUMBE WAKE

Kila Mtume ni katika ndimi ya watu aliotumiwa

Miongoni mwa hekima ya Allah Ta’ala ni kuwa kila Mtume ni miongoni mwa jinsi ya watu anaowatumia Mtume, Allah amesema: “Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo)….” (16:43)

Na azungumze kwa lugha ya watu wake ili wafahamu maneno yake, na maana yake, Allah amesema: “Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima. ” (14:4)

Kuhifadhiwa madhambi na ukamilifu wa mitume na manabii

Mitume wote husafika kwa utimilifu wa akili na usalama wa fikra zao, na ukweli na uaminifu wa kupokea amana za watu na kuhifadhi, na kuepushwa na dhambi ambayo huharibu mwenendo wa mwanadamu, na viwili wili vyao kuepushwa na vinavyochukiza na macho kutazama, Allah ametakasa nafsi zao na tabia zao, wao ni watu wakamilifu zaidi kwa tabia, na wenye nafsi zilizotakaswa zaidi na mikono yenye ukarimu. Allah Ta’ala amekusanya kwao tabia njema kama alivyokusanya kwao uvumilivu, elimu, usamehevu, ukarimu, ushujaa na uadilifu; kiasi cha kupambanuka katika tabia hizi baina ya watu wao, Mitume ni watu bora zaidi katika viumbe vyake, Mwenyezi Mungu amewachagua kubeba ujumbe na kufikisha amana, Allah amesema: “…Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake….” (6:124)

Na akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.” (3:33)

Na akasema kuhusu Issa (‘Alayhi salaam): “Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu). Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utuuzima wake, na atakuwa katika watu wema. ” (3:45-46),

Na Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alijulikana kwa watu wake kama “Mkweli mwaminifu.” Kabla ya kuteremshwa kwa utume, na Mola wake akamsifu kwa: “Na hakika wewe una tabia tukufu. ” (68:4).

Uanaadamu wa mitume na manabii

Hawa Mitume na Manabii pamoja na sifa alizowasifu nazo Allah Ta’ala miongoni mwa sifa tukufu, ila wao ni watu yanawafika yanayowafika watu wote, wao wanasikia njaa, wanaugua, wanalala, wanakula, wanaoana na wanakufa, Allah amesema: “Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya….” (13:38),

Na akasema Mtukuka: “Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa. ” (39:30)

Na akasema kuhusu Mtume wake Muhammad: “…Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua…” (33:37).

Na katika hali hiyo huenda wakateswa, au wakauwawa, au wakafukuzwa kwenye miji yao, Allah amesema: “Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.” (8:30)

Lakini mwisho wake wao kupata ushindi duniani na akhera.