“Nilipoamini tawhidi nikaanza kutafuta hoja na dalili mbali mbali ambazo zinathibitisha kuwa Qur-aan ni kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuwa Qur-aan ni kitabu cha Mwisho. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kutatua mas-ala haya: Qur-aan Tukufu ni kitabu pekee ambacho kinakubali na kutambua vitabu vyote kutoka mbinguni, wakati ambapo vitabu vyote inapinga vitabu vingine. Kwa hakika hii ndio moja ya sifa kubwa inayopambanuka Qur-aan Tukufu.”