“Hapo kabla Torati ndio iliokuwa muongozo kwa watu na msingi wa tabia zao. Hadi alipodhihiri masihi Wakristo walifuata mafundisho ya Injili. Kisha ikaja Qur-aan na kuchukua nafasi zao. Qur-aan ilikuwa ni pana zaidi na yenye maelezo zaidi kuliko vitabu viwili vilivyoitangulia kama Qur-aan ilivyoweza kusahihisha uzushi yaliyoingizwa kwenye vitabu vilivyotangulia. Qur-aan imekusanya kila kitu, imekusanya sheria na kanuni zote. Kwani hicho ndicho kitabu cha mwisho kutoka mbinguni.”