Dini ya furaha na Utulivu

Dini ya furaha na Utulivu

“Nilikuwa nikijiuliza: Kwa nini Waislamu wanahisi furaha imetawala katika maisha yao pamoja na ufukara wao na kukosa kwao maendeleo?! Na kwanini Wasweden wanahisi dhiki na huzuni pamoja na maisha mazuri, starehe na maendeleo makubwa wanayoishi nayo?! Hata nchini mwangu Uswisi nilikuwa nikipata hisia zile zile za Wasweden pamoja na kuwa ni nchi yenye maendeleo makubwa na kiwango cha juu cha maisha!! Mbele ya yote haya nimekuta kuwa nafsi yangu ina haja ya kusoma dini za Mashariki, na nikaanza kuusoma Uhindu, sikukinaishwa nayo sana, hadi nilipoanza kusoma Uislamu uliponivuta na kuona kuwa haugongani na dini zingine bali imebeba dini zote; nayo ni dini ya mwisho inayohitimisha, ukweli huu kwangu ukawa (umoja wa katiba ya wananchi) unapanuka kwa kupanuka kusoma kwangu hadi ikazama kwa ukamilifu akilini mwangu.”


Tags: