“Dini ya Manabii wote ilikuwa ni moja tu: Wao ni wamoja katika mwendo wao tokea Adam hadi Muhammad, vilishuka vitabu vitatu toka mbinguni navyo ni: Zaburi, Torati na Qur-aan. Mfano wa Qur-aan kwa torati ni mfano wa torati kwa Zaburi. Muhammad kwa mtazamo wa Issa ni kama vile Issa kwa mtazamo wa Mussa, lakini jambo la muhimu kulifahamu ni kuwa Qur-aan ni kitabu cha mwisho kutoka mbinguni imeteremka kwa watu na mwenyewe (Muhammad) ni Mtume wa mwisho. Hakuna tena kitabu baada ya Qur-aan wala Nabii baada ya Muhammad.”