“Kila tunapoangalia kwa kina ustaarabu wa Waarabu, vitabu vyao vya kielimu. Uvumbuzi wao, fani zao, inadhihiri kwetu ukweli mpya na upeo mpana. Na kwa haraka tumewaona Waarabu kuwa ndio watu bora katika karne za kati (Middle age) kuwa na maarifa kwa ajili ya elimu za waliotangulia.
Kwa muda wa karne tano vyuo vikuu vya Magharibi (Ulaya) vilitegemea vyanzo vya elimu na machapisho ya Waarabu. Nao ndio ambao waliiendeleza Ulaya kwa akili na tabia njema. Historia haijawahi kufahamu Ummah uliozalisha kama walivyozalisha Waarabu (Waislamu) kwa muda mfupi na hakuna watu wengine waliowafikia katika uvumbuzi na fani zingine.”