Dini ya Utukufu na Ukarimu


“Uislamu ni dini ya amani, usawa, uhuru, udugu, ukarimu na utukufu, yote hayo yanaonekana wazi kwenye hukumu zake, misingi yake na taratibu zake, kwa mfano Saumu katika Uislamu si kama saumu katika dini nyingine, kwa sababu matatizo ya mwanadamu si (mtu) kukandamiza mahitaji ya mwili wake kama vile wafanyavyo watawa kiasi kwamba kiwiliwili cha mmoja wao kinakuwa kama vile hekalu la mifupa inayotembea. Uislamu umenyoosha matamanio ya kiwiliwili na haujayakandamiza; Saumu katika Uislamu unazoesha nafsi ya mfungaji kusubiri na Jihadi dhidi ya matamanio maovu yaliyoharamishwa, na kumchunga Allah katika siri na dhahiri na kujitambuza ladha ya kukosa na njaa, ili mfungaji awaonee huruma waliokosa, kama ambavyo Saumu ni fursa ya kuupa mwili raha dhidi ya kuvimbiwa. Saumu humfaidisha mtu afya yake, roho yake na akili, na katika yote kuna kujiburudisha kwake, na umoja wake.”


Tags: