“Mgawanyiko wa kitabaka katika dini ya Kihindu uko kama ifuatavyo: Tabaka la weupe; Hili ni tabaka la watu wa dini na wanazuoni. Tabaka la Wekundu; linakusanya maamiri na wanajeshi. Tabaka la Manjano: linakusanya wakulima na wafanya biashara. Tabaka la Weusi linahusisha mafundi mikono na viwanda. Ama tabaka la tano ambalo linafahamika kuwa ni tabaka la watu duni (Untouchable-tabaka la chini kabisa) linahusisha wenye kazi duni. Na tabaka za juu linatumikisha matabaka ya chini na matabaka ya chini yanahudumia matabaka ya juu.”