General quotes

quotes:
  • Uko wapi ndani ya Ulimwengu huu.
  • “Picha hii ni ya mkusanyiko mkubwa wa sayari (galaxies) Sehemu yake ndogo huwakilisha sayari na njia zake ni zaidi ya 1,000,000,000,000 ya jua. Na jua ni kubwa kuliko ardhi kwa mara 1,300,000, na ardhi ni kubwa kuliko nyumba yako (kwa mfano mkuwa wa nyumba yako ni 500) kwa mara 1,020,144,000,000 na nyumba yako ni kubwa kuliko wewe mwenyewe kwa mara ngapi.”?!’


  • Jeuri na Dhuluma!!
  • Vikao vya Wanafalsafa huko Ulaya vilikuwa vikijadili: Je, mwanamke ana roho kama roho ya mwanamume? Je, ana roho ya mwanadamu au mnyama? Na wakahitimisha mjadala wao kuwa mwanamke ana roho. Lakini roho hiyo ni duni sana kuliko roho ya mwanamume.”


  • Issa anasisitiza katika Injili kuwa Mungu ni mmoja
  • “Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndio hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.” (Marko Mtakatifu 12:28-35). Huu ni usia wa kwanza.


  • Injili inakanusha kusulubiwa na inathibitisha Kuinuliwa Mbinguni
  • “Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.” (Yohana 8:59). “Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao.” (Yohana 10:39). “Hili limetokea ili yatimie yaliyokuja kwenye kitabu: Hakuvunja chochote katika mfupa.” (Yohana 36:19). “Huyu Yesu huyu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni.” (Matendo ya Mitume 1:11)


  • As-Samiry – Mtengeneza Ndama wa Sanamu
  • Haiwezekani Mtume wa Allah Harun kuwa ndie aliyetengeneza ndama na kulingania ushirikina: Mitume wote walikuwa ni walinganizi wa Tawhid. Atakayenukuu yasiyokuwa hayo amepotoka, mfano wa hayo yaliyokuja: “Harun akawaambia: Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; na wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyo kutoka katika nchi ya Misri.” (Kutoka: 32/2-4). Agano la kale.


  • Msikiti wa Ibrahim Al-Khalil katika msikiti wa Al-Ibrahimy katika mji wa Al-Khahil huko Palestina
  • Msikiti wa Ibrahim Al-Khalil katika msikiti wa Al-Ibrahimy katika mji wa Al-Khahil huko Palestina.


  • Kiburi na uharibifu wa Historia
  • “Katika karne ya kati Wakristo katika maandishi yao walianza kugawa watu kwa misingi ya kikabila na kitaifa kama ilivyotajwa katika agano la kale (Mwanzo) na kuongeza ugawaji wa tabaka jipya: Ikawa ni itikadi iliyoenea kuwa watu wa dini na makasisi wanatokana na kizazi cha Shemu. Wapiganaji wanatokana na kizazi cha Yafith. Mafukara wanatokana na kizazi cha Hamu watoto wa Nuhu (‘Alayhi Salaam). Ilifikia kuwa katika mwaka 1964 kumpeleka Senata wa Marekani Robert Byrd kutoka mji wa Virginia ya Magharibi kutumia kisa cha Nuhu kama sababu ya kubaki sera ya ubaguzi katika Marekani.


  • Mitume kudharauliwa
  • Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisakwa ndugu zake.” (Mwanzo: 9:20-25) na hivyo akawabariki Shemu na Yafethi.


  • Migongano ya Kibudha
  • “Mabudha wanakana Mungu na wanadai (au baadhi yao) kuwa Budha ni mtoto wa Mungu, na wanapinga roho na wanaamini kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa mtu mwingine.”



  • Tabaka za Kijeuri
  • “Mgawanyiko wa kitabaka katika dini ya Kihindu uko kama ifuatavyo: Tabaka la weupe; Hili ni tabaka la watu wa dini na wanazuoni. Tabaka la Wekundu; linakusanya maamiri na wanajeshi. Tabaka la Manjano: linakusanya wakulima na wafanya biashara. Tabaka la Weusi linahusisha mafundi mikono na viwanda. Ama tabaka la tano ambalo linafahamika kuwa ni tabaka la watu duni (Untouchable-tabaka la chini kabisa) linahusisha wenye kazi duni. Na tabaka za juu linatumikisha matabaka ya chini na matabaka ya chini yanahudumia matabaka ya juu.”


  • Lakini Mwenyezi Mungu ni mmoja
  • “Watafiti wametaabika wakiwa wanahesabu idadi ya miungu ya dini za wanadamu: Idadi ya miungu ya Wamisri wa kale ni zaidi ya miungu mia nane, na idadi ya miungu ya Kihindu ni zaidi ya miungu elfu kumi, na mfano wa ushirikina huu kwa Wagiriki na Wabudha, na mengine miongoni mwa dini za watu za ardhini.”


  • Mwanamke wa Kifaransa
  • “Huko Ufaransa moja katika majimbo yake kulifanyika mkutano mwaka 586 mazungumzo yalihusu mwanamke: Je, ni mwanadamu au sio mwanadamu? Hitimisho lilikuwa ni uamuzi wa waliohudhuria kuwa mwanamke ni binadamu, lakini ameumbwa kumuhudumia mwanamume, katika mwezi wa Februari mwaka 1938 ilitolewa kanuni ya kufuta kanuni zingine zilizokuwa zikimkataza mwanamke wa Kifaransa katika baadhi ya matumizi ya mali (baada ya hapo kuruhusu) na kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanamke wa Kifaransa aweze kufungua akaunti kwa jina lake katika mabenki.


  • Mwanamke mbele yao.
  • Katika sheria za kale za Kihindi tunasoma: Maradhi, mauti, moto, sumu, nyoka na moto yote vyote hivyo ni bora kuliko mwanamke. Haki ya mwanamke ya kuishi huisha kwa kuisha haki ya mumewe ambae ndie bwana na mmiliki wake. Akiona maiti yake inaungua nae hujitupa kwenye moto ule, vinginevyo ni haki yake kupata laana ya milele.


  • Mwanamke katika Sheria za mwanadamu.
  • Mwanamke katika Sheria za mwanadamu.


  • Sawa kwa Sawa
  • “Chuo kikuu cha Oxford hakijatoa haki sawa baina ya wanafunzi wa kike na wa kiume (katika Michezo na Umoja wa wanafunzi); isipokuwa kwa uamuzi uliotolewa tarehe 21 Julai mwaka 1964.”


  • Tone katika Bahari
  • “Hadi hivi sasa kubwa iliyoumbuliwa ni VY Canis Majoris iko mbali nasi kwa masafa ya miaka elfu tano ya mwanga na ni kubwa kuliko jua kwa 9,261, 000,000 yaani 9 Bilioni na mara 261 milioni!! Na jua ni kubwa kuliko ardhi yetu kwa mara 1,300,000.


  • Manabii ni watu bora zaidi
  • “Baadhi ya yaliyopotoshwa juu ya Mitume ya Allah na manabii inataja kuwa walilewa, au kuangukia katika uzinifu, au kuamrisha kuwa watu ni yote hayo ni upotofu mbayo haifai na hailingani na watu wenye tabia za juu mbali ya kuwa wao ni watu waliokuwa bora zaidi…. Wao ni Manabii wa Allah, katika hayo ni yale yaliyokuja – katika Taurati kuhusu Dawudi (‘Alayhi Salaam) (Samweli (2) 11/2-26) na kutoka kwa Yoshua bin Nuun (mwana wa Nuni) (‘Alayhi Salaam) (Yoshua 6/24) na kutoka kwa Musa (‘Alayhi Salaam) (Hesabu:31/14-18) Musa (‘Alayhi Salaam), na mengine mengi yasiyokuwa hayo hayafai Mtume wa Allah.”