Kila mwenye akili linganifu anaijua njia hii hata kama ataipinga hadharani, hujua kuwa njia hii ndio njia ya furaha ya milele, yeye ni kama waliosemwa na Allah baada ya kukana utume wa Musa (‘Alayhi Salaam) baada yakuwajia miujiza: “Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi!” (27:14).
Wengi wanaotumia akili zao vizuri (hata kama hawajasilimu) hujua kuwa njia hii ni njia pekee ya furaha ya wanadamu wote katika nyumba zote mbili (duniani na akhera).
Hii ndio njia…. huikiri njia hii kila aliyekuwa huru, shujaa katika kubainisha rai yake pamoja na dhiki aliyokuwa nayo na kificho, khofu haimzuii au kuwaogopea watu au kuogopea jambo jipya, au propaganda na sura ya siku nyingi iliyokwisha jijenga akilini mwake kuhusu kuipokea na kuikubali dini hii na kusilimu, wangapi katika watu waliojizuia kufuata njia hii kwa kuhofia udugu na maingiliano yao ya kijamii na hofu yao katika kushikamana na njia ya furaha, Allah Aliyetukuka amesema: “…basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” (3:175).
Hii ndio njia.. Naam ndio njia ya furaha, njia ya mambo matukufu, njia ya huruma na rehema, njia ya elimu, njia ya ustaarabu, njia ya tabia njema pamoja na mitihani ambayo ni sunnah ya maisha na kumjua mkweli miongoni mwa waongo. Allah Ta’ala amesema: “Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.” (67:2).
Hii ndio njia waliyopita manabii na waliotumwa kabla yetu, na njia waliopita masahaba watukufu na waliofuata baada yao kwa wema katika kila kaumu, kabila na lugha, na ndio ambao itaenea kwa wote na kuongoza katika mustakbali hivi karibuni.
Anasema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Jambo hili (Uislamu) litafika ilipofika usiku na mchana, wala Allah hatoacha nyumba yoyote ila Mwenyezi Mungu ataingiza dini hii kwa utukufu wa mtukufu, au kwa udhalili wa mnyonge, ni utukufu ambao Allah anaupa nao nguvu Uislamu, na udhalili ambao Allah anawadhalilisha nao ukafiri.” (Imepokewa na Ahmad).
Kuwa miongoni pamoja na msafara mtukufu katika njia hii ya furaha ya milele.
Hii ndio njia…huku ndiko kufaulu..na hii ndio furaha..ambayo inajaza moyo wa atakayepita ndani yake, usiinyime nafsi yako (fursa hii), Jihadhari, Ole wako na kudhulumu Nafsi yako, fuata njia ya furaha, Allah Aliyetukuka amesema: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (16:97).
Hii ndio njia…jilazimishe nayo, na uifurahie, na ishi maisha yako ya duniani kwa furaha iliojaa, utulivu, na raha, wala usisahau kuwa yaliyo kwa Allah ni bora na yenye kubakia, na raha ya akhera ni raha ya milele, Mola wetu ameifanya njia hiyo kuwa moja tu; furaha ya dunia na furaha ya akhera, na amekusanya katika njia (zingine) uovu wa dunia na adhabu ya akhera, Allah Aliyetukuka amesema: “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?” (20:124-125),
Na akasema vile vile: “(Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.” (20:126),
Jihadhari kusahau au kujisahaulisha njia hii..nayo ni njia ya furaha.
Hii ndio njia…ni njia nyepesi inaanza kwa tawhidi ya Allah katika moyo na kusadikisha katika kiwiliwili, na imani kwa manabii na walioteremshwa na kuishia katika furaha ya milele katika akhera, ambayo inaanza kwa kutamka shahada mbili; nazo ni: Ash-hadu an-Laailaha Illa llaah wa-anna Muhammadan Rasuulu llaah..na uishi maisha yake ukiwa na furaha, na ufe ukiwa na furaha, na uamke kutoka kaburini mwako ukiwa na furaha katika pepo ya milele yenye furaha…hii ndio njia…usipopita njia hii basi Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) hana wajibu juu yake isipokuwa kufikisha waziwazi, Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala): “Ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Hud na walio amini pamoja naye, kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa na adhabu ngumu.” (11:58).