Kabla ya kuja kwako katika Ulimwengu huu ulikuwa haupo kama Allah alivyosema: “Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?” (19:67),
Kisha Allah akakuumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha akakufanya msikivu na mwenye kuona, Allah Ta’ala amesema: “Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.” (76:1-2).
Kisha ukatoka kwenye udhaifu hadi kwenye nguvu na kurudi tena kwenye udhaifu, Allah Ta’ala amesema: “Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza.” (30:54),
Kisha mwisho ambao hauna shaka yoyote ndani yake ni mauti.
Na wewe katika hatua hizo unahama kutoka kwenye udhaifu mmoja kwenda kwenye udhaifu mwingine huwezi kuondosha dhara katika nafsi yako, wala huwezi kujiletea manufaa ila kwa kuomba msaada wa Allah kwako, nawe ukiwa ni fukara mwenye kuhitaji kulingana na maumbile uliyoumbwa nayo, ni vingapi unavyohitaji ili maisha yako yabakie, ambayo huna uwezo nayo, wakati mwingine ukapata na wakati mwingine ukakosa, na mangapi ambayo yanakufaa na unayatamani, unaweza kupata na wakati mwingine kukosa, na mangapi yenye kukudhuru na kuondosha matarajio yako na juhudi zako zikapotea na kukuletea mitihani na balaa na ukataka kuyaondoa katika nafsi yako hivyo ukayaondoa mara moja na kushindwa wakati mwingine. Je, hukuwahi kushitakia ufakiri na haja yako kwa Allah?, Na Allah anasema: “Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa.” (35:15).
Kirusi kidogo usichoweza kukiona kwa macho kinakusumbua na kukufanya mgonjwa usiyeweza kusimama, na huwezi kukizuia, na unakwenda kwa mtu dhaifu kama wewe ili akutibu, wakati mwingine hukupa dawa iliyokuwa sawa, na wakati mwingine hushindwa, na wote, mgonjwa na daktari msijue la kufanya…. Ni udhaifu ulioje kwako wewe Ewe mwanadamu!! Lau nzi akikunyang’anya kitu huwezi kukirudisha!! Amesema kweli Allah pole aliposema: “Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawatoumba hata nzi ijapo kuwa watajumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa.” (22:73).
Ikiwa huwezi kuokoa alichokunyang’anya nzi, Je, unamiliki nini katika jambo lako?! Utosi wako uko mkononi kwa Allah, nafsi yako ipo mkononi mwa Allah, moyo wako upo baina ya vidole vyake viwili katika vidole vya Rahman anavigeuza atakavyo, na maisha yako na mauti yako viko mikononi mwake, furaha yako na tabu yako vipo mkononi mwake. Harakati zako, utulivu wako, na kauli zako kwa idhini ya Allah, na matakwa yake, hivyo huwezi kutembea ila kwa idhini yake, wala hutofanya ila kwa matakwa yake, akikuwakilisha katika nafsi yako basi atakuwa amekuwakilisha katika unyonge, udhaifu, kupetuka mipaka, madhambi na hatia, na akikuwakilisha kwa mwingine, atakuwa amekuwakilisha kwa asiyemiliki kwako madhara wala manufaa wala mauti wala uhai wala kufufuliwa, hujitosha dhidi yake, japo kwa pepeso la jicho, bali wewe unalazimika kwake kwa pumzi yako yote ndani na nje, anakuenezea, neema na wewe unambughudhi kwa maasi na kufuru pamoja na dharura yako kubwa kwake kwa njia zote, umechukua kuwa ndio hisa na marejeo yako kwako na msimamo wako mbele yake.
Ewe mwanadamu kutokana na udhaifu na unyonge wako katika kuvumilia matatizo ya madhambi yako: “Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.” (4:28).
Allah alituma Mitume na kuteremsha vitabu, na kuweka sheria na kusimamisha mbele yako Njia ilionyooka na kusimamisha hoja, ubainifu na ushahidi na mpaka amekufanyia katika kila kitu alama yenye kuthibitisha upekee wake (kuwa Yeye Mungu ni mmoja), Uungu wake na Uola wake, pamoja na yote hayo bado utawaona baadhi ya watu wakitetea batili na kupinga haki na wakimchukua shetani kuwa ni walii kwao badala ya Allah na kujadili kuhusu batili: “Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika hii Qur’ani kila namna ya mfano. Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.” (18:54).
Je, neema za Allah ambazo zinageuka ndani yake zimekuliwaza mwanzo na mwisho wako?? Au hukumbuki kuwa umeumbwa kwa tone la manii? Na mwisho wako ni kwenye shimo, na utafufuliwa peponi au motoni! Allah Ta’ala amesema: “Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung’unyika? Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.” (36-77-79)
Na amesema vile vile: “Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha” (82:6-7)
Ewe mwanadamu kwa nini unajiharamishia Nafsi yako ladha ya Tawhidi na kumuadhimisha Allah Ta’ala, ladha ya kusimama mbele ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kutaka msaada wake akuepushe naufakiri na akuponyeshe maradhi na kuondosha matatizo yako na kusamehe madhambi yako na kuondosha madhara na kukunusuru unapodhulumiwa na kukuongoza unapobabaika na kupoteza, nakukufundisha usiyoyajua na kukupa amani utakapoingiwa na khofu na kukuhurumia wakati wa unyonge wako na kuwarudisha adui zako na kukupa riziki yako?!
Ewe mwanadamu kwa hakika neema kubwa ambayo Allah amemneemesha kwayo mwanadamu baada ya neema ya dini ni neema ya akili, ili mwanadamu aweze kupambanua baina ya yenye kumnufaisha na yenye kumdhuru na aweze kuifahamu maamrisho ya Allah na makatazo yake na aweze kujua lengo tukufu zaidi nalo ni uja wake kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) peke yake bila ya mshirika, Allah Ta’ala amesema: “Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni madhara mnamyayatikia Yeye. Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi” (16:53-54).
Ewe mwanadamu, kwa hakika mwanadamu mwenye akili hupenda mambo makubwa na kuchukia mambo ya hovyo, na kupenda kumwiga kila mwema na watukufu miongoni mwa manabii na waja wema, na kila mmoja hutamani awafikie pamoja na kuwa hawakuwadiriki, na njia ya kuelekea huko ni ile aliyoielekeza Subhaanahu kwa kauli yake: “Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.” (3:31)
Na akijifananisha nayo basi Allah humfikisha kwa manabii na waliotumwa, Allah Ta’ala amesema: “Na wenye kumt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!” (4:69).
Ewe mwanadamu na kuaidhi kujitenga kisha zingatia na uwe katika tafakuri kwa yaliyokujia katika haki, angalia dalili zake na zingatia hoja zake; ukiona kuwa ni haki basi jikusanye katika kufuata, wala usiwe mtumwa wa desturi na mazoea, najua kwamba kuwa Nafsi yako ni utukufu kwako kuliko rafiki zako, ndugu zako, mali zako na mirathi ya babu zako, na Allah Akawawaidhi Makafiri kwa hili na akawatamanisha nayo akasema Aliyetukuka: “Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali.” (36:46).
Ewe mwanadamu utakapojisalimisha hatopoteza chochote, Allah Ta’ala amesema: “Na ingeli wadhuru nini wao lau wangeli muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema.” (4:39),
Yaani, kitawadhuru nini lau wakimuamini Allah na yote aliyoteremsha? Kitawadhuru nini lau wakimuamini Allah na wakitaraji ahadi yake nyumba ya akhera kwa yule atakayefanya kazi yake vizuri?! Kitawadhuru nini lau wakitoa yale ambayo Allah amewaruzuku katika wajihi ambao Allah atapenda na kuridhia, nae akiwa anajua nia zao njema na zilizo chafu, na ni mwenye kujua kwa anayestahiki kuwafikishwa miongoni mwao. Hivyo kumuwafikisha na kumpa uongofu wake, na kumuelekeza matendo mema ambayo atamridhia kwayo, na mwenye kustahiki udhalili, kufukuzwa kutoka kwenye uwanja wake mtukufu wa kiungu ambae atakayefukuzwa mlangoni mwake amepata hasara na kukosa dunia na akhera?!
Uislamu wako haukuzuii baina yako na chochote kila unachotaka kufanya au kupata katika yale aliyokuhalalishia Allah, bali Allah atakulipa kwa kila amali mfanyayo ambayo unataka kwayo wajihi wa Allah, hata ikiwa ni katika yanayotengeneza dunia yako na kukuzidishia mali yako au cheo chako au utukufu wako, bali hata unachokitumia katika yaliyoruhusiwa ikiwa utatosheka na ya halali na kuacha ya haramu.
Ewe mwanadamu hakika Mitume wamekuja kwa haki, na wametimiza matakwa ya Allah, na mwanadamu ni mwenye kuhitajia maarifa ya sheria ya Allah, ili apite katika maisha haya kwa uoni na awe katika akhera miongoni mwa washindi, Allah Aliyetukuka amesema: “Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.” (4:170),
Na akasema tena Aliyetukuka: “Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu.”(10-:108).
Ewe mwanadamu hakika wewe ukisilimu hutonufaisha isipokuwa Nafsi yako tu, na ukikufuru hutoidhuru isipokuwa nafsi yako tu, hakika Allah ni mkwasi wa waja wake, hivyo basi haimdhuru yeye maasi ya wenye kuasi, hivyo Yeye haasiwi isipokuwa kwa elimu yake, na hatiiwi ila kwa idhini yake, Allah Aliyetukuka amesema: “Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu.” (6:104),
Na Allah alishaeleza kama ambavyo Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alivyojulisha:
“Enyi waja wangu hakika mimi nimejiharamishia dhuluma na nikajaalia baina yenu haramu, hivyo basi msidhulumiane. Enyi waja wangu nyote mmepotea ila yule niliyemuongoza ombeni uongofu wangu nitawaongoa.Enyi waja wangu nyote ni wenye njaa ila niliyemlisha, ombeni niwalishe nitawalisha. Enyi waja wangu nyote mko uchi ila niliyemvisha, ombeni kuvishwa nami nitawavisha.
Enyi waja wangu, nyote mnakosea usiku na mchana, nami ninasamehe dhambi zote, niombeni msamaha nitawasameheni.
Enyi waja wangu, nyie hamuwezi kunifikia mkanidhuru, wala hamuwezi kunifikia mkaninufaisha.
Enyi waja wangu lau wa kwanza wenu na wa mwisho wenu, na watu wenu na majini yenu walikuwa katika moyo wa mcha-Mungu mmoja miongoni mwenu, hilo halinipunguzii kitu katika ufalme wangu.
Enyi waja wangu lau wa kwanza wenu na wa mwisho wenu, na watu wenu na majini yenu walikuwa katika moyo wa mcha-Mungu mmoja miongoni mwenu, hilo halinipunguzii kitu katika ufalme wangu.
Enyi waja wangu lau wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu na watu wenu na majini yenu wamesimama katika wanga mmoja na wakaniomba na mimi nikampa kila mtu kwa mujibu alivyoomba, hilo halitonipunguzia chochote isipokuwa kama inavyopungua makamasi yanapoingia baharini.
Enyi waja wangu, kwa hakika hayo ni matendo yenu ninawahesabia, kisha ninawalipa kwayo, atakayepata kheri basi namshukuru Allah, na atakayepata yasiyokuwa hayo basi asilaumu isipokuwa Nafsi yake.” (Muslim).
Enyi wanadamu… Hii ndio njia, wala hakuna njia isiyokuwa hiyo kwa ajili ya furaha duniani na akhera.
Ama njia zingine ni njia za tabu, upotovu na mashaka, Allah Aliyetukuka amesema: “Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” (6:153)
Atakayefuata njia ya furaha ataifikia, na atakayefuata njia zingine atapotea na kuwa mbali na njia ya Allah, wala hatopita njia ya furaha.