Rashidi alipokaa tu kwenye meza alitoa ‘laptop’ yake na alipokuwa akishughulika kuiwasha Rashidi akamwambia
Maiko: Leo hii nitakuonesha kipande cha video nadra kuonekana, kipande cha nusu dakika tu, lakini si cha kawaida, kwani itatubeba na kutupeleka katika historia na zama zake, muda wa karne hivi.
Kwa kujali hayo kichwa cha Maiko na Rashidi vilikaribia ‘skrini’ ya laptop yake na macho yao yakalenga skrini.
Maiko: Oooh nzuri sana! Ni kiasi gani nilivyofurahi hali naangalia maisha yalivyo Uingereza, nchi yangu, maisha ya miaka mia moja iliyopita, angalia furaha katika nyuso za wapitao barabarani… mwangalie mtoto huyu na furaha aliyonayo! Yalikuwa ni maisha ya kawaida kabisa…ni maisha yaliyo karibu kabisa na nafsi ya mwanadamu.
Rashidi: Nitarejea kuonesha video hii ili uone jambo lingine muhimu.
Rashidi akiirejesha tena ‘klipu’ ile ya video huku akiendelea na mazungumzo yake na Maiko .
Angalia! Huyu mwanamke, na huyu wa pili, wanawake watano, angalia pamoja nami, wote hakionekani kwao isipokuwa kichwa kilichofunikwa kwa kofia na glovu, na mavazi yao ni mapana hayaonyeshi miili yao.
Maiko: Kweli kabisa.
Rashidi: Kama ni hivyo ni kitu gani kilichotokea?
Maiko: Kuhusu nini?
Rashidi: Katika jamii zenu.
Maiko: Unakusudia watu kwenda uchi na upungufu wa heshima?!
Rashidi: Haswa, lakini inaashiria vile vile kuwa hali hiyo inatokana na kuanguka kwa mfumo wa kimaadili kwa ujumla.
Maiko: Huu ni uhuru wa mtu binafsi, leo hii sisi ni jamii inayotukuza uhuru, na kila mmoja anayo haki katika kuchagua mfumo wa maisha autakao.
Rashidi: Bila ya shaka nafahamu hilo, jambo hili linahitaji mtu kufanya kikao au vikao vya mjadala kulizungumzia kwa umakini, hata hivyo kinachonivuta mimi ni kule kukubaliana kwenu kijamii kwa mabadiliko haya ya kimaadili na wote wakirejea katika rejea moja katika uchaguzi wenu.
Maiko-Haijifichi kwako kuwa kuna kinachoitwa ‘Utamaduni wa jamii’, na ndio ambayo watu hubadilika wakafanya matendo wanayofanya watu bila kurejea kwenye rejea, bila ya watu kushangazwa au kupingwa, na kupitia tamaduni hii huenda ikatokezea tofauti za aina kati ya chaguzi za mtu binafsi….
Rashidi: Ni nzuri sana, tukichukulia hali hii na tukitafiti kilicho cha sawa na makosa ndani yake, tutaona kuwa kitabu chenu kitakatifu kinalingania kwenye kujiheshimu na kutoonyesha mapambo; imekuja katika barua ya Paulo ya kwanza kwa Thimotheo (2:9-10)
“Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.”
Maiko: Ewe bwana haya yanawafaa wale wanawake wenye kujinasibisha na Kanisa tu, ama sisi katika maisha yetu nje ya Kanisa nilishawahi kukuambia hapo kabla kuwa, sisi tumekataza dini isituingilie katika maisha yetu tokea zama za mwanga na mwamko.
Rashidi: Lakini ewe rafiki yangu klipu hii tuliyoiona kuhusu wanawake wenye kujiheshimu barabarani na sio kanisani, na hilo ni baada ya hizo zama unazozitaja za mwamko, tena baada ya kupita karne nyingi….na hata kama nikikubaliana nawe kuwa dini haina nafasi katika maadili yenu bado ninajiuliza: Nini kilichotokea?! Nini kilichowabadilisha wanawake wenu kwenda kwenye hali hii ya kwenda uchi?!
Maiko: Wewe unaona jambo ambalo hukulizoea kwa mtazamo wako, lakini mimi naliona ni jambo la kawaida tu, hebu nikuzindue jambo katika klipu ile, nayo ni picha katika msimu wa baridi kali au kwa ujumla ni wakati wa baridi, na hili linaonekana katika mavazi ya wanaume na watoto katika msimu huu wa nguo zenye kiza….Huenda hali hiyo mnayodhania inatokana na sababu ya hali ya hewa ya baridi, hata hivyo haikatazi ukweli wa mambo kuwa; wanawake katika zama hizo walikuwa katika hali ya heshima zaidi na hata baada ya muda huo kwa wakati mrefu, ama ni nini sababu ya kilichotokea? Ni kwa sababu maadili na mitazamo ya watu imebadilika kutokana na maendeleo ya jamii.
Rashidi: Hii ni kadhia nyingine ambayo itabidi tuipangie muda wa kikao chake, nayo ni masuala yanayohusu maadili, mimi pamoja na ufahamu wangu kuhusu sayansi na njia zake, naona kuwa maadili yanatofautiana na kufuata kwake maendeleo haya unayoyasema.
Maiko: Hamna neno tulipangie hilo muda wake wakati mwingine, lakini hebu nikuulize bwana Rashidi, kwa nini nyie siku zote mnajali kumuangalia mwanamke kama kiwiliwili tu? Kwa nini jambo hili linawashughulisheni sana?!
Rashidi: Uislamu unamuangalia mwanamke na mwanamume kuwa wao ni wanadamu, na mwanadamu ameumbwa kutokana na kiwiliwili, roho na akili, hatuwezi hata mara moja kupuuzia chochote katika hayo, sio tu kiwiliwili chake, bali hata ile hisia ya uhayawani ndani ya mwanadamu, mwanadamu huyu hawezi kuwa juu na kupaa ili afikie kwenye kiwango cha juu ila kupitia mfumo kamili uliokamilika, ambapo ndani yake kuna maadili na masuala yake ya kiroho pamoja na taratibu za kijamii na kisheria, na nyie mlipodhani kuwa mmepata mwanga wa maendeleo na kutenganisha Kanisa, au kwa lugha nyingine dini na maisha, na kuridhia kwenu Kanisa kujitenga na mambo yake ya kiroho ili akili ijitupe nje ya mipaka ya dini na kiwiliwili, kuwa huru na kufanya mkitakacho, na kwa ajili hii shetani amepata uhuru mkubwa katika ustarabu huu wa kustarehe, kama anavyostarehe hayawani nje ya mipaka ya kimaadili na kidini, ili kushibisha matamanio yao ya kinyama na kuhamasisha mwanamke kuonesha maumbile yake kwa njia nyingi.
Maiko: Hata hivyo tunawaona wanawake wakiwa katika hali hii ya kwenda uchi asubuhi na jioni, wala matamanio haya unayoyaita ya kinyama hayatushughulishi.
Rashidi: Je, unadhani kuwa hiyo ni fadhila au maadili mazuri? Kwa hakika adhabu ya mtu aliyezoea kuangalia hali zenye kuhamasisha kama hizo ni mtu kupatwa na hali ya ubaridi wa jinsia, na linafuatiwa na dhara jingine kubwa kuliko hilo, nalo ni kuendelea kutafuta kitu kingine chenye kuhamasisha zaidi sio kile alichokizoea, kitu ambacho kinapelekea katika hali isiyokuwa ya kawaida ya kimapenzi.
Maiko: Hizo athari au madhara unayosema yapo ya namna mbali mbali; kuna ya karibu na ya mbali.
Rashidi: Ndio kuna madhara yanayofuatia hali hii hadi mtu kufanya uhalifu; na kama mtu hakupatwa na ubaridi huu wa jinsia kwa sababu ya mazingira ya kiwiliwili chake au kwa sababu za kijamii au za kimalezi, basi mtu huyu atapatwa na mfazaiko wa jinsia na matokeo yake yatakuwa ni kuongezeka kwa ubakaji, na hili ndilo haswa linalosajiliwa katika takwimu za matukio ya ubakaji, acha nikutajie kidogo:
Takwimu za Wizara ya Ndani ya Ufaransa imeashiria kutokea kwa matukio 4,412 ya ubakaji katika kipindi cha mwaka mmoja, yaani takriban wastani wa tukio moja kwa kila masaa mawili.
Huko Uingereza Polisi walifanya operesheni kubwa katika jiji la London kwa ajili ya kuwahamasisha wanawake kujifunza fani za kujilinda mtu binafsi, badala ya kusalimu amri pindi anapovamiwa na wanaume, na hiyo ni baada ya tangazo la kuzidi kwa uhalifu wa kutumia nguvu na ubakaji katika jiji la London kuwa asilimia 11% (kumi na moja) kwa muda wa mwaka mmoja.
Ama Amerika: Kituo cha wahanga cha taifa kimetangaza kunusuru haki za wahanga wa matumizi ya nguvu: Na wastani wa ubakaji uliopo Marekani imefikia 1.3% (asilimia moja nukta tatu) ya mwanamke aliyebaleghe kwa dakika moja, na kituo kiliongeza: Mwanamke mmoja kati ya wanane waliobaleghe huko Marekani walikumbwa na ubakaji, na hiyo ni mwaka 1991.
Ama katika mwaka wa 2009 takwimu zinaashiria kuwa mmoja katika kila wasichana watatu wa umri wa miaka 14 (kumi na nne) hubakwa, na ndani ya Marekani kuna nusu milioni ya ubakaji kila mwaka, na ya kuwa asilimia sitini na moja (61%) ya wasichana wa Kimarekani wamepoteza bikira zao kabla ya umri wa miaka kumi na mbili (12).
Kuna aina zingine za uhalifu, huitwa uhalifu wa kunyamaziwa, nayo ni kushambuliwa kazini kwa wanawake walio chini ya wakubwa wao kazini, kwa kawaida matukio haya hayaripotiwi; kwa sababu ya hofu ya mwanamke kuhusu kazi yake au tamaa ya kupata fidia au ugumu wa kuthibitisha.
Bila shaka namba hizi haziwakilishi ukweli wote; kwani kituo cha kuhamasisha wanawake wanaobakwa kinakadiria kuwa asilimia 35 (thelathini na tano) hunyamaziwa na kutoripotiwa ukilinganisha na asilimia moja tu inayotolewa taarifa yake.
Maiko: Hata hivyo tatizo kama la ubakaji ni tatizo gumu, lina mambo mengi ndani yake, kama vile kinafsi, kimalezi na kijamii, bali hata kiuchumi vile vile.
Rashidi: Hili ni kweli, hata hivyo hatuwezi kukana kuwa moja ya matatizo makubwa: Ni ile hali ya watu kushawishiwa kijinsia walau kwa kuangalia tu, kinachovutia kuangalia ni kuwa utafiti wa Marekani umefikia kuwa: uhalifu wa ubakaji hupungua wakati wa baridi, na huenda upungufu huu unatokana na kupungua kiwango cha wanawake kuvaa mavazi ya uchi, au ni kwa sababu watu hawatoki sana nje muda huu; kinachofanya kuwepo kwa nafasi ndogo ya kukutana, na hali zote mbili hizi zinathibitisha sababu yenyewe.
Maiko: Lakini mwisho wa siku ni kuwa wanawake wenyewe ndio wanaotaka hayo kwa matakwa yao, huo ni uhuru wa mtu binafsi kama nilivyokuambia, wala hatuwezi kuwazuia hilo.
Rashidi: Hili ndilo linaloonekana kwa nje, lakini ukweli ni kuwa viongozi wa jamii ya Magharibi wakiongozwa na wanaume, ndio ambao wamepelekea utamaduni huu wa kwenda uchi, na wakaupamba, na wakautayarishia mazingira saidizi, na wakavumbua njia rahisi za kuusambaza; ili wastarehe na mwanamke bila ya kuwepo kizuizi bali wao wameweka sheria zenye kudhulumu stara ya mwanamke, maisha yake na udhaifu wake; hivyo basi sheria iliyotungwa huko Magharibi huwa ni laini kwa hali ya mwanamume mbakaji zaidi kuliko inavyomuonea huruma mwanamke aliyebakwa; kitu ambacho kinasaidia kuhamasisha ubakaji, bali baadhi ya nchi za Magharibi zinahesabu ubakaji kuwa ni katika makosa ya maadili na sio miongoni mwa uhalifu wa kutumia nguvu.
Chukua mfano huu: Huko Finland, moja katika nchi inayohesabika kuwa iliyoendelea sana katika kumjali mwanamke, mtu mmoja alimlazimisha mwanamke kufanya nae mapenzi katika benchi la walemavu katika maegesho ya magari akimpigiza mwanamke yule kichwa chake ukutani na mikono yake nyuma ya mgongo wake, kulingana na mwendesha mashtaka jambo hili si ubakaji, kwani matumizi ya nguvu yaliyotumika yalikuwa madogo!!! Na yule mtu alilaumiwa kwa kumlazimisha muhanga wake kufanya tendo la ndoa na akahukumiwa jela kwa masharti (pamoja na kusimamisha utekelezaji wake) kwa muda wa miezi saba!!
Ewe rafiki yangu! Ni jamii ipi yenye amani kimaadili, ni jamii yetu ya leo hii, au ni ile jamii ya tokea karne iliyopita?! Je, ungependa kuangalia klipu mara nyingine?!
Maiko: Jambo lipo wazi bwana Rashidi, lakini kwa mtazamo wa Uislamu mnalionaje jambo hili?
Rashidi: Jambo hili linahitaji kikao, bali vikao vingine ili kulijadili.