- Miongoni mwa Alama za Kughurika.
“Hakika ni wakati muafaka kufanya utafiti kuhusu athari za Kiislamu juu ya Ulaya kwa wakati huu ambapo uhusiano kati ya Waislamu na Wakristo Waarabu pamoja na Wazungu wa Ulaya unaongezeka katika ulimwengu huu mmoja. Kwani imewahi kuonekana wakati fulani kabla katika karne za kati waandishi Wakristo wa Ulaya walitengeneza sura chafu kuhusu Uislamu katika maeneo mengi: Hata hivyo kwa fadhila za jaribio la watafiti katika karne iliyopita sura sahihi zaidi ya kuangalia mambo kwa mtazamo usio na upendeleo imeanza kutengenezwa katika akili za watu wa Magharibi: Na kwa sababu ya kuwepo mahusiano mazuri na Waarabu na Waislamu basi ni juu yetu kutambua fadhila zote tulizofanyiwa na Waislamu. Ama jaribio letu la kukana hayo ni alama miongoni mwa alama za uongo za kudanganyika.”
- Yuko wapi Kiongozi Afaae?
“Akipatikana kiongozi anayefaa ambaye atazungumza maneno yanayofaa kuhusu Uislamu. Basi kuna uwezekano wa dini hii kuibuka tena kama ni moja ya nguvu kubwa za msingi za kisiasa ulimwenguni kwa mara nyingine.”
- Suluhisho la Kiakili
“Qur-aan imeleta suluhisho la kiakili la matatizo ya zama hizi za Kiuchumi, kijamii na kimaadili: Kwa hili haiwezikani kutia shaka katika ile hekima ya Qur-aan kwa kuangalia mafanikio ya Muhammad katika kufikisha ujumbe ambao Mungu amemuarisha kuufikisha. Hivyo yapasa kwetu (kwa mtazamo wangu) kadiri ya misimamo yetu ya dini ilivyo kuzingatia ujumbe wa Qur-aan tangu kuchimbuka kwake huko Makkah.”
- Uadilifu na Usafi
“Maandalizi ya mtu huyu kwa kuvumilia mateso kwa ajili ya itikadi zake na tabia zake tukufu kwa wale waliomuamini wakamfuata na kumzingatia kuwa bwana na kiongozi wao, kwenye upande wa mafanikio makubwa aliyoyapata, yote hayo yanaonyesha usafi wa uadilifu wa usafi wa asili katika haiba yake. Hivyo yale madai kuwa Muhammad anajidai ni jambo lenye kuashiria matatizo zaidi wala halitatui. Bali hakuna mtu katika watu wakubwa katika historia ya watu wa Magharibi aliyepata heshima kubwa mfano wa Muhammad.”