Baada ya masaa mawili na robo ya safari, marafiki wawili walifika Paris, mji ambao Rashidi hajawahi kuutembelea hapo kabla. Marafiki hao wawili waliondoka kwenye kituo cha treni na ilielekea kuwa Maiko anaifahamu vizuri Paris na kuna uhusiano wa mapenzi kati ya Maiko na mji wa Paris.
Maiko: Rashidi! Hii ndio Paris mji mkuu wa Nuru…. hapo ndipo walimwengu walipojifunzia kauli mbiu ya (Uhuru, Udugu na Usawa), na misingi hii ya haki za mwanadamu zikaenea ulimwenguni kote.
Rashidi: Angalia Maiko…..mwanamke amekamatwa na polisi na sioni jambo lolote baya alilofanya!
Maiko: Ooh, amevaa nikabu, siku mbili zilizopita kanuni ya kukataza uvaaji nikabu imeanza kutekelezwa Ufaransa katika sehemu za umma, na huenda amekamatwa kwa ajili hiyo, huenda polisi huyu kamkamta ili amtoze faini kwa kwenda kinyume na sheria hii au anaweza kuwekwa hata ndani.
Rashidi: Katika sehemu za umma?! Yaani kanuni hii inamruhusu kuvaa nikabu nyumbani kwake….mashaAllah: ..uhuru wa hali ya juu kwa mwanamke kwa Kiislamu na kwa Waislamu! Nimekumbuka kanuni hii, na nimekumbuka kuwa kanuni hii haipo Ufaransa peke yake, ipo mfano wa kanuni hii huko Ubelgiji na pia kuna mji Kaskazini mwa Italia imepitisha kanuni hii vile vile, na kuna juhudi ya kupitisha mfano wa kanuni hii huko Holland na Uhispania, ama huko Australia serikali imewapa haki polisi ya kuangalia uso wa mvaaji nikabu ili kumfahamu.
Maiko: Ninaamini mwenyewe kuwa katazo hili linamkwaza mwanamke na uhuru wake binafsi kuvaa akipendacho, na kutolewa kwa kanuni hii huhesabiwa kuwa ni kurudi nyuma kwa uhuru wa Ufaransa, kwa hakika huku ni kugusa uhuru binafsi katika nchi ambayo kuna zaidi ya mada mia moja za kisheria zinazotaka kuheshimiwa kwa uhuru wa wengine.
Hata hivyo wao wanaona kuwa hilo linaendana na misingi ya dola yao ya kisekula ambayo inakataza matumizi ya nembo za kidini, kama ambavyo watawala wa Ufaransa wanaielezea nikabu kuwa ni aina mpya ya utumwa ambayo Jamhuri ya Ufaransa haikubali katika ardhi yake.
Rashidi: Misingi ya usekula inahadharisha matumizi ya nembo za dini katika dola yenyewe na taasisi zake za umma, lakini hazihadharishi kwa watu binafsi, kisha kwa nini basi tahadhari hii iwe ni kwa Waislamu peke yao tu? Je, hilo linafanyika kwa wenye kuvaa misalaba vifuani mwao au wenye kuvaa mavazi ya masista watawa?! Jambo la kushangaza kuhusu ufahamu wa utumwa kwa watu hawa katika mantiki yao, Je, kumsukuma mwanamke kuwa uchi na wanaume kustarehe nae kila pembe sio utumwa, na mwanamke kujisitiri kiwiliwili chake chote kwa uchaguzi wake na kwa matakwa yake ndio utumwa?! Naam ewe bwana wangu kwa hakika ni utumwa, lakini ni utumwa kwa Allah (Mungu), Mola wa walimwengu.
Sasa nimefahamu maana ya uhuru katika kauli mbiu ya mapinduzi ya Ufaransa, ni uhuru wa kutojihusisha na Mungu (Allah) na utumwa kwake, na sio uhuru wa viumbe, uhuru huu uliotolewa na utawala wa kisekula ambao umechukua nafasi ya Mwenyezi Mungu na kulimbikiza madaraka yake na kuyagawa na kuruhusu kwa wamtakaye na namna watakavyo. Walikuwa wakisema kuhusu uhuru, “uhuru wako utaishia pindi pale uhuru wa mwingine utakapoanza.” Je, wanahesabu watu kuangalia viwiliwili vya wanawake ni uhuru na haki na wakati huo huo wakaufunga na kuubana uhuru wa mwanamke wa Kiislamu?! Hili silo suala la hijabu, ni khofu waliyonayo Ulaya kuhusu Uislamu.
Maiko: Usikuze mambo bwana Rashidi, Waislamu wengi wanaishi Ulaya na wana haki zote kama walivyo watu wengine, na mbali na hiyo wanapata fursa za kielimu na kufanya kazi kuliko hata katika nchi zao.
Rashidi: Mimi sikuzi mambo, lakini nazungumza kwa sababu kuna ushahidi mwingi wa hilo, ni khofu tu ya Uislamu.
Maiko: Mfano nini?
Rashidi: Mfano: Kukataza minara kujengwa Uswisi, nchi ambayo ndio inayolinda haki za binadamu, nchi isiyofungamana na upande wowote, nchi yenye makubaliano na mapatano ya Geneva. Ni matatizo gani ambayo minara itasababisha au madhara gani katika jamii katika nchi ambayo Waislamu hawazidi asilimia nne tu ya wakazi wote, na kuna minara minne tu?!! Bila shaka ni jambo lililo wazi kuwa marufuku hii imebeba ndani yake khofu ya maradhi na msimamo wa uadui dhidi ya Uislamu.
Maiko: Pamoja na kuwa mimi binafsi sikubaliani na marufuku hii, isipokuwa ninafahamu kuwa minara hii ya adhana hupingana na maadili ya nchi zao, ndio maana wanapinga ili utambulisho wao usiguswe.
Rashidi: Ninapofikiria kuwa ni jinsi gani marufuku hii haigusi wala haienei na kusambaa katika alama na nembo zote za sehemu za ibada kama vile minara ya makanisa na mahekalu ya Mayahudi, basi wakati huo nafahamu mipaka ya usekula ambayo wanalingania katika nchi zao na kudai wamesimamisha misingi yake, na ninafahamu ukweli wa usawa wanaoulingania, na ya kuwa jambo hili haliishi hapo, bali linavuka mipaka kwenda kwenye kila nembo na alama ya Uislamu na hata ikiwa alama hii ni Mtume Muhammad mwenyewe, Mtume wa Uislamu, kama tulivyoona katika tatizo la kumchafua Mtume wetu kwa katuni kama ilivyotokea nchini Denmark na nchi zingine zilizoshabikia uadui huu.
Maiko: Bwana wangu, huu ni uhuru wa kujieleza, katika nchi zetu hakuna kitu kitakatifu au kinachokatazwa katika uhuru wa kujieleza, ni mara nyingi Yesu mwenyewe na nembo za dini nyinginezo zilikumbwa na zahama na dharau hizi.
Rashidi: Bali kuna matakatifu kwenu ambayo hayaguswi, hakuna uhuru wa kujieleza wala uhuru wa utafiti wa kielimu; baada ya jarida la Denmark lililochora katuni za Mtume Muhammad, kisha uadui ule kuenea katika baadhi za nchi za Ulaya, na nchi nyingi za Magharibi kutetea hali hiyo pamoja na kukosolewa kwa alama kubwa ya dini ya zaidi ya watu bilioni mbili ulimwenguni, na kukataa kwao kuomba radhi kwa hoja ya uhuru wa kujieleza…Mahakama moja huko Holland imewahukumu kundi la Waislamu huko Holland faini ya Euro elfu mbili mia tano kwa kueneza Katuni inayoonesha kuwa maangamizi makubwa waliyopata Mayahudi ni kitu kilichotengenezwa na Mayahudi au wameyakuza zaidi kuliko yalivyotokea, serikali ya Holland imetetea uamuzi huo kuwa Mahakama ya Ulaya ya haki za binaadamu ambayo inatawalia umuhimu mkubwa wa uhuru wa kujieleza inatetea kwa nguvu suala hilo.
Moja katika mahakama za huko Ufaransa katika mwaka 1998 ili muhukumu mwanafikra wa Kifaransa Bwana Roger Garoudy kwa tuhuma ya kutia shaka katika maangamizi ya Mayahudi, nae alitia shaka idadi iliyotajwa ya kuuwawa Mayahudi katika mikono ya wanazi huko Ulaya.
Katika mwaka 2006 mahakama ya Austria ilimhukumu mwanahistoria wa Uingereza David Irving jela miaka mitatu kwa sababu alipinga maelezo ya kuunguzwa kwa Mayahudi.
Katika mwaka 2009 mahakama nchini Ujerumani ilimpiga faini ya Euro elfu kumi Askofu wa Kikatoliki wa Uingereza Richard Williamson kwa sababu tu alisema kuwa wahanga wa Kiyahudi waliokufa katika kambi za maangamizi ya Nazi ni kati ya watu laki mbili hadi tatu tu.
Na wengineo wengi, wote hao hawakupata uhuru ule wa kutafiti au uhuru wa kuzungumza na kimbilio katika matukufu haya.
Maiko: Kinachothibitika ni kuwa kuna historia ya uadui baina ya Ukristo na Uislamu, ukiongezea hali ya sasa hivi inayoendelea ya matumizi ya nguvu ya Waislamu wenye kasumba, jambo lililowafanya watu wengi kuuogopa Uislamu kuliko mfano wanavyoogopa Uhindu na Ubudha. Je, utapinga kuwa baadhi ya matendo ya Waislamu huwa ni sababu kubwa ya kuwepo khofu dhidi ya Uislamu?
Rashidi: Ehe, hii sasa tunakaribia kwenye ukweli, sipingi kuwa baadhi ya matendo na makundi ya Waislamu ni sehemu ya makundi yenye uadui, na maadui hutumia hali hiyo katika kuchochea hali ya uadui na khofu dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hata hivyo wakati huo huo inatupasa tuweke mambo katika sehemu yake na katika uzito na ukubwa unaostahiki; sisi hatuwezi kupuuzia kuwa kuna mambo mengine ya operesheni na mikakati ya uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu, kwa kutumia matukio haya ambayo umeyataja ambayo lengo lake ni kufikia malengo ya makundi ya kibaguzi au ya kiadui dhidi ya Uislamu na Waislamu…. Vinginevyo kama sisi tutafuatilia matukio kwa uwazi bila upendeleo basi tutakuta kuwa hakuna kundi la kidini au la kikabila ambalo litakosa kufanya uadui hata kwa wale wenye kunasibiana nao, lakini kuyaonesha matukio haya au kuyasambaza kuwa ni Waislamu wote ndio wanayoyafanya au hata kuyapuuzia ndiyo ambayo yanayopaswa kuangaliwa kwa makini na hili linaingia katika ukurasa wa usahaulifu.
Maiko: Unakusudia nini kusema mambo mengine?
Rashidi: Nitakutajia baadhi ya hayo mambo, na sio yote:
Ulaya ilifungua milango yake kwa wahamiaji wa Kiarabu–na Waislamu kwa malengo maalumu, miongoni mwa malengo hayo ni: Kuongeza idadi ya watu huko Ulaya ili kuziba pengo la upungufu wa watu unaotokana na kuvunjika kwa familia huko Magharibi na hali ya kutotaka kuzaa kwa watu wake, na bila shaka ufunguzi huu wa kupokea wahamiaji wa Kiislamu haukuwa kwa kuwatumia watu wazima walioshiba adabu na desturi za Kiislamu, lakini ilikuwa ni tamaa ya kupata kizazi kipya kitakachozaliwa katika nchi za Magharibi ambacho inawezekana kukifinyanga katika ustaarabu mpya ambao utatengeneza jamii mpya na utamaduni mpya katika nchi za Magharibi baada ya miaka hamsini ya mwanzo…hivi ndivyo ulivyokuwa mpango wa ‘wanastratejia’ wa Magharibi.
Hata hivyo wana-stratejia hao wa Magharibi waliona ule mwamko wa kurejea katika Uislamu katika ulimwengu wa Kiislamu umehamia katika nchi za Magharbi, na ikawa ni kikuta cha njia katika njia ya kukamilisha kuwa changanya wahajiri wa Kiislamu na watoto wao katika ustaarabu mpya wa kimagharibi badala yake watoto na wasichana kuwa na hijabu au familia yenye kushikamana na Uislamu na misingi yao ya dini, hili sasa likawa ni kikwazo cha kufanikiwa kwa sera yao ya kuwachanganya kwa ukamilifu.
Kizazi hiki cha watoto wa kiislamu kikawa ni chanzo cha khofu katika kutekeleza ‘programu’ ile ya kuwaweka pamoja, na hivyo basi: Magharibi ilijikuta uso kwa uso na tatizo la kujitokeza kwa nguvu mpya ya watu inayobeba wasifu na utambulisho wa kiistaarabu tofauti na utambulisho wa watu wa Magharibi.
Hivyo basi, sababu kuu ya operesheni hii ya kibaguzi ni ile hisia chungu ya hatari ya kupoteza utambulisho wake, na hili ndilo lililopelekea katika kukerwa na kila alama ya nembo ya Uislamu; wao wanaogopa kuwa mandhari haya pamoja na kuwa ni madogo lau yakibakia yakiwa katika hali ya mpangilio wa Kiislamu bila shaka yataenea kwao… na hivyo kuamua kuyafuta yakiwa bado ni machanga; hivyo basi mgongano wa ustaarabu hivi sasa upo dhidi ya Uislamu baada ya kuondoka itikadi nyinginezo, na hili ndilo lililoelezwa na mwanafikra wa kimarekani bwana Samuel Hannington kuwa ni: “Migongano ya ustaraabu”, akionesha kuwa kuna harakati ya kifikra na ya kisiasa huku magharibi.
Maiko: Tumefika mgahawani, maudhui mpya uliyoanzisha yanahitaji mijadala mingi.