- Njia ya Ulimwengu
Nimesoma vizuri maisha ya Muhammad Mtume wa Uislamu mara nyingi, sikupata ndani yake ila matukufu ya tabia kama kinavyotakiwa kuwa.Ni mara ngapi nimetamani Uislamu kuwa ndio njia ya Ulimwengu.”
- Dini ya Dunia na Akhera
“Mwanadamu msomi anaelekea kwa tabia yake katika Uislamu. Kwa sababu ni dini pekee ambayo inaangalia mambo ya duniani na akhera kwa usawa.”
- Mwokozi wa Binadamu
Mwokozi wa Binadamu
“Kwa hakika ni katika Uadilifu Muhammad kuitwa, “Mwokozi wa Wanadamu”. Naamini kuwa mtu mfano wake lau angetawala ulimwengu huu leo hii angefanikiwa kutatua matatizo yake na hivyo furaha na amani ingechukua nafasi yake.”
- Misingi ya Amani na Furaha
“Ulaya hivi sasa imeanza kuhisi hekima ya Muhammad na imeanza kutamani dini yake, kama ambavyo itikadi ya Kiislamu itasafishika na tuhuma chafu za karne ya kati kutoka kwa watu wa Ulaya. Dini ya Muhammad itakuwa ndio mfumo ambao juu yake kuna misingi ya amani na furaha, na falsafa yake inategemea katika kutatua matatizo na vifungo.”