PAMOJA NA KASISI

PAMOJA NA KASISI

PAMOJA NA KASISI

(1)

Jioni familia ilirudi hotelini na Joji alipokea simu kutoka kwa John Luke ikimjulisha kuwa ahadi yake na Padri Luogi ni kesho saa nne asubuhi kanisani, na yeye atawasubiri…

Huyu John Luke ananijulisha ahadi yetu na Padri kesho lakini tutaacha wapi watoto?

Ima tuwachukue twende nao, au tuwaache katika bustani jirani na kanisa, kuna bustani nzuri sana.

Vizuri, nadhani itakuwa bora kufanya hivyo.

Ilipotimu saa mbili unusu asubuhi Joji na Katarina na watoto wao walikwenda kwenye bustani iliyo karibu na kanisa lile, ambapo kuna sehemu maalumu ya michezo ya watoto, hivyo wakawaacha Maiko na Sali hapo, na hiyo ni baada ya kuzungumza na muhusika wa sehemu hiyo na kumuomba awaangalie watoto..kisha hao wakaelekea kanisani; katika ahadi na Padri kulingana na ahadi waliyokubaliana. John Luke aliwapokea na kuwakaribisha, na wote wakaondoka kwenda kwa Padri Luogi ambaye aliwapokea kwa uchangamfu.

Karibuni sana Katarina, nimesikia juhudi zako kubwa ufanyazo Uingereza, Bwana akuhifadhi.

Hili nimejifunza kutoka kwenu, katika tuliyofaidi kutokana na elimu zenu.

Karibu Joji… John Luke amenijulisha kuhusu maswali yako, na yeye kafurahishwa sana na namna unavyofikiri, karibu, unataka nini?

Nina maswali manne, na sitopoteza wakati wako, la kwanza: Iweje kuna Mungu mmoja mwenye nafsi tatu kwa wakati mmoja? Nimesoma sana, na kusikia maelezo mengi, na bado sijafika popote bali (nisamehe) wakati mwingine nahisi kuwa Ukristo unafanana na Upagani.

Uso wa Padri ulibadilika, na akawaangalia John Luke pamoja na Katarina, kisha akaangalia chini ardhini na kusema:

Na la pili?

Je Yesu ni Mungu au ni katika wanadamu? Na je yeye ni Mungu muabudiwa au mtu tu aliyeuwawa? Je inahitajia Mungu afe ili awaokoe wanadamu?! Je isingekuwa bora kuwaokoa wanadamu akiwa ni hai bila ya kufa?

Na ya tatu:

Kitabu Kitakatifu kiwe ni Agano la Kale au Jipya ni katika vitabu vyake? Ni nani aliyefanya tarjama yake? Na ni nani aliyetufikishia? Na kwa nini kuna migongano katika toleo zake, ninaona haya kuwasomea wanangu, vipi hiyo itoke kwa Mungu?

Na ya nne?

Je historia ya dini na manabii ni historia tu ya mauaji na uchafu tu? Nachukizwa na matumizi ya nguvu na mauaji, na nachukizwa na kila anayelingania hayo, lakini vile vile nashangazwa na mtazamo wa kitabu kitakatifu kuhusu manabii na mitume, kama vile ambavyo ninashangazwa na maandiko kuhusu mauaji na uporaji!

Padri alinyanyua uso wake juu, akamwangalia Katarina na Joji machoni kabla ya kumgeukia John Luke.

John Luke kwa nini hukuniambia kuhusu maswali yake kabla?

Yeye mwenyewe hakuniambia kabla.

Padri alimuangalia Joji machoni kwa muda mrefu na kwa umakini mkubwa..kisha akaangalia juu kwa uso ulioonesha alama za machovu na msisitizo kwa wakati mmoja, kisha akapumua kwa nguvu.

Kijana wangu, wewe huwezi kufahamu majibu ya maswali haya kwa wepesi huu, kama ambavyo kuzielezea na kubainisha huchukua muda mrefu, kwa nini usiondoke kwenda kufanya ibada ya kumuabudu Mungu (Bwana) kuliko (maswali) haya?

Bwana wangu nimekuja kujifunza kwenu na kufaidika na elimu yenu, na yaliyokuwa ni marefu katika maelezo yake yanaweza kufupishwa na mwanazuoni.

Vizuri kijana wangu, katika dini yetu kuna siri mbali mbali ambazo hazipaswi kujadiliwa kama ambavyo kuna maandiko ambayo hapaswi kuyafahamu peke yako tu.

Bwana wangu kuhusu siri hizi, je itakuaje tunaamrishwa kufuata dini kutoka kwa Mungu halafu dini hiyo ikawa ni siri miongoni mwa siri? Je inawezekana vipi maandiko yakawa kutoka kwa Mungu kwa ajili ya watu wote lakini hayafahamiki ila kwa baadhi ya watu tu?!

Maneno yale yalianza kumchukiza Padri na uso wake kuonesha hayo, aliangalia chini kisha akasema:

Je mnaweza kutuacha peke yetu mimi na Joji?

Uso wa John Luke ulibadilika na akaonesha dhahiri kutofurahishwa na jambo hili, itawezekana vipi rafiki yake amwondoshe katika kikao alicho kitayarisha yeye…

Je unanitaka mimi nitoke pamoja na Katarina? Kwa nini je hii ni siri nyingine?!

Ninamuhitaji katika mazungumzo maalumu, mkitoka nitashukuru.

Katarina nenda kwa Maiko na Sali na unisubiri huko, na nitakuja baada ya muda si mwingi.

Katarina alimuaga Padri, na akamwombea baraka, na akamuhakikishia kuwa atahudhuria misa takatifu Jumamosi ambayo itaongozwa na Papa…alitoka pamoja na John Luke hadi bustanini….Pindi walipoondoka tu, Padri alimgeukia Joji.

Kijana wangu wewe ni mtu jasiri sana; sio ushujaa wa vita bali ni ushujaa uliomo ndani ya nafsi.

Asante sana Bwana wangu.

Kijana wangu, nami nitakuwa muwazi na jasiri kwako, huenda ukasikia usiyoyapenda.

Tafadhali, karibu kwani sio muhimu kusikia ninachopenda, bali cha msingi ni kusikia ninachohitaji.

Huenda ukashangazwa, kwa masikitiko hakuna jibu lililokata kuhusu kadhia hii.

Bwana wangu, je huoni kuwa imani haiwezi kuwa pamoja na shaka?

Unachosema ni sahihi, lakini siwezi kupata jibu linalokata, nimebaki na umri wangu huu wote nikitafuta jibu la maswali mengi miongoni mwayo ni haya uliyotaja, lau ukitaka nikujibu kwa jibu lolote ningefanya, lakini nimekuahidi kuwa jasiri na mkweli pamoja nawe, ukweli ni kuwa sijapata jibu sahihi.

Suluhisho ni lipi basi?

Mimi bado ni Padri, kwa sababu sijapata lililokuwa bora kuliko hili nililonalo sasa hivi, na kuwepo kwa maswali katika baadhi ya kadhia ni bora kuliko kuendelea kuwa na shaka katika kila kitu, au sivyo?

Swadakta, lakini kupata majibu ni bora kuliko hayo yote.

Ndio, na huenda ukapata majibu lakini ninakuhakikishia kuwa hutolipata ndani ya Kanisa, mimi nina muda wa miaka thelathini na ni kasisi wa kanisa hili, na sijapata jibu, hili ndilo ambalo ninalo.

Je ninaweza kukuuliza swali?

Karibu.

Kwa nini umewataka John Luke na Katarina watoke?

Huenda ukashangazwa na nitakachokisema! Hii ni kwa sababu ya upungufu wa ujasiri nilionao, hakuna anayependa kuwa dhaifu, anayeonekana hajui kitu mbele za watu wengine, haswa wanaoamini kuwa ana elimu, kisha wakiacha Ukatoliki au Ukristo–watakuwa nani? Wakanaji Mungu na dini kwa mfano, ninaamini kuwa kuwepo kwa shaka ni bora kuliko kuishi katika ulimwengu wa shaka.

Samahani, je hakuna Mapadri na watawa walio jasiri kuelezea hayo unayoyaeleza kwa sauti kubwa?

Wamepita idadi ya mfano wao katika historia ya Ukristo, ima waliuawa, au kupotezwa au kutoroka, kitabu kitakatifu pamoja na Upapa ni mgumu sana.

Kama ni hivyo basi wewe unaunga mkono uhusiano wa siri uliopo baina ya Vatican na vyombo vya usalama, kama alivyothibitisha hayo Eric Fratini katika kitabu chake “Karne kumi na tano za ujasusi Vatican” The Entity: Five Centuries of Secret Vatican Espionage

Kamwe....sio kweli, huko ni kuwabebesha (makosa) kutoka kwa Mprotestant Mmarekani kwa kanisa la Kikatoliki.

Vipi kuhusu mambo aliyoyataja?

Mengi katika hayo yana ukweli, lakini ameyaweka muweko wa kulibebesha lawama Kanisa la Kikatoliki na Upapa.

Lakini majasusi kuingia Vatican ni kweli, au kwa lugha nyingine kuwa Shirika la Kijasusi limejipenyeza ulimwenguni, au sivyo?

Kwa bahati mbaya ndio, lakini sio jambo la jumla, pamoja na kuwa kila mara linatokea.

Lakini kama ni hivyo mbona ukali wake hauonekani kwa watawa na Mapadri katika fedheha za Kijinsia?

Haiwezekani, kwani jambo hili hutokea sana, unadhani Kanisa litavunjika kwa sababu ya watoto?! Kama ambavyo sehemu ya kadhia hizi za kijinsia zipo katika Kitabu Kitakatifu, kisha akaendelea:

Bwana wangu, niwaambie nini akina Katarina na John Luke watakaponiuliza: Kwanini umewatoa?

Padri Luogi alinyamaza, kisha akaangalia chini na kusema:

Siku zote ukweli ni mzuri.

Asante sana bwana wangu nitafanya hivyo kwa ruhusa ya Bwana, kwa hakika nimefaidika nawe sana.

Asante sana, Mungu akubariki, nataraji kukuona katika misa ya Jumamosi takatifu, yakini ni bora kuliko shaka.

Joji alitoka na kwenda bustanini; alimkuta Katarina na John Luke wakimsubiri, alipofika tu John Luke alimuuliza:

Kwanini ametutoa? Kwa mara ya kwanza Luogi anafanya mambo bila ya kutumia diplomasia!

Joji hakutaka kuzungumza maudhui ya kutolewa, haswa zaidi baada ya kuona hasira za John Luke…

Muda wa chakula cha mchana umewadia, je tupo karibu na Grand Hotel ambayo ipo jirani na kwako ili tuweze kula na kuzungumza pamoja?

Ndio, ni muda wa dakika tano tu kwa kutembea.

Niruhusuni kwanza nataka kwenda kucheza na wanangu na baada ya nusu saa twendeni mgahawani….unasemaje Katarina?

Vizuri, hamna neno, pamoja na kuwa natamani sana kwa muda huo wa nusu saa utuambie kilichopita baina yenu na Padri, kwa ujumla baada ya nusu saa tutajua kila kitu.

Joji alielekea kwa watoto wake katika sehemu ya watoto akiwa anafikiri: Atawaambia nini John Luke na Katarina? Je awaambie kilichotokea kama ilivyo na iwe chochote kitakachokuwa? au afanye nini?
Baada ya nusu saa alirejea pamoja na wanawe….

Sisi tuna njaa sana, twendeni mgahawani.

Haya twendeni.

(2)

Walifika Grand Hotel baada ya kutembea kwa muda wa dakika tano hivi…Joji akainama karibu na Maiko na Sali:

Wepenzi wangu…mnaonaje mkale roshani?

Na wewe na mama mtakula wapi?

Tuna ahadi muhimu, ni bora mkae wenyewe roshani; ili mzungumze pamoja, na muangalie mandhari nzuri.

Vizuri, haya Sali twende.

Joji alikaa pamoja na Katarina na John Luke katika meza katikati….walipokuwa wakiangalia menyu. Joji alimgeukia John Luke……

Yuko wapi sahibu yako Muislamu?

Ninaogopea asije akataka kuzungumza nawe peke yako na ukatuacha sisi… hata hivyo atakuja muda sio mrefu ili achukue oda zetu.

Sio mimi niliyekutaka atuache pamoja na Padri, lakini ni sahibu yako Padri ndie aliyefanya hivi.

Lakini wewe ulimkubalia mara moja.

Ha Ha ha, je hataki kuwatii watu wa dini?! La msingi ni kuwa alitaka kuniambia mimi kuwa hakuna jibu la maswali yangu, na hakutaka muone udhaifu wake na maarifa yake machache.

Katarina alishikwa na hasira na kumwangalia Joji .

Haiwezekani kwa Padri Luogi kukosa majibu ya maswali yako mepesi!

Ninajua kuwa hana majibu, naye anajua kuwa mimi nafahamu hivyo, lakini kwa nini alitutaka tutoke? Nahisi katika maudhui hii kulikuwa kuna jambo jingine.

Mnaweza kumuuliza, nyie mnamjua zaidi kunishinda mimi, nadhani aliona vibaya Katarina kutoka peke yake.

Ulipita muda wakiwa kimya Joji aliona shaka kwa mara ya kwanza alipomuangalia Katarina, kama kwamba macho yake yalizungumzia wasiwasi uliokuwa ndani ya nafsi yake ambayo anajaribu kuishinda na kuificha. Huenda kimya chake kikafanana na Volkano wakati wa utulivu wake hauonekani isipokuwa wingu lake tu. Ama John Luke kimya chake kilikuwa ni kumshangaza rafiki yake alivyofanya kwa jambo linalofahamika wazi, kama ambavyo bado alikuwa na mashaka aliyoyasema Joji na kuna jambo lingine lililofichwa.
Mhudumu alikuja kuchukua oda, na akavunja ukimya uliokuwepo ….John Luke akamuuliza kuhusu Suleim mwenye hoteli, na akaomba waongee nae kama inawezekana …

Bwana Suleim yupo na marafiki zake wanaongea ofisini kwake, nitamjulisha maombi haya. Samahani mnahitaji nini kwa ajili ya chakula cha mchana?

Walimjulisha mhudumu wanachotaka, na Joji akamuelekeza mhudumu walipo Maiko na Sali ili wachukua oda yao… kisha akamuangalia John Luke kutaka kujua kitu!.....

Suleim ndie Muislamu uliyenijulisha?

Ndio, utakapomuona utadhania Mtaliano, kwa mnasaba anazungumza Kiingereza vizuri sana.

Vizuri, huenda akafika baada ya muda mfupi tumsikilize.

Katarina nae alianza kuzungumza

baada ya kupita ukimya sasa turudi kwa Padri… wewe unasema kuwa hakuweza kujibu maswali yako!

Ndio bali anasema kuwa maishani mwake anatafuta majibu ya maswali haya na mengineyo mengi, na hakuweza kufikia majibu yenye kukinaisha.

Haiwezekani!

Padri ambaye unamzungumzia ni rafiki yangu ewe Katarina na ninajua kuwa hajui majibu yake, kwani tumesha jadiliana katika hayo na mengine mara nyingi, lakini kinachonishangaza mimi ni kwa nini alitutaka tutoke?! Hili ndilo ambalo silifahamu!

Padri Luogi Stefano ni katika walionisaidia sana kuwa na yakini, itakuaje awe na shaka namna hii?!

John Luke alipumua kisha akaangalia juu na kusema:

Uzoefu wangu unaniambia: Kila elimu ya Padri ikizidi, hawi mkakamavu katika mazungumzo yake maalumu, na athari yake katika hotuba kwa watu inaongezeka kwa yanayonasibiana nao.

Unakusudia nini?

Unacho kisikia kutoka kwake ni mazungumzo ya jumla tu, anachokisema katika vikao vyake maalumu ni jambo lingine, kwa ujumlamimi nafahamu haya, unataka aseme nini katika mazungumzo yake na watu wote? Unataka aseme: Sisi hatumjui Mungu, au kitabu kitakatifu kimepotoshwa au kimetengenezwa?

Macho ya Katarina yalijaa machozi akiwa anasema:

Hapana, nataka aseme kuwa Bwana ni mkarimu, mwema, mmoja hata kama ana nafsi tatu, Yeye bwana ndiye aliyeteremsha Kitabu kitakatifu.

John Luke akimwangalia Katarina kwa huruma:

Tutafanya nini kama kitabu kitakatifu kinagongana chenyewe? Je unaweza kunibainishia kwa njia ya mantiki yenye kukinaisha –vipi tatu inaweza kuwa moja na moja kuwa tatu?!

Nataraji hutoniambia wanachosema makanisani, kwani nimesikia mara elfu na moja na bado sijakinaishwa nayo.

Bali nimekinai kuwa hayo ni kwa ajili ya mazungumzo tu kwa watu wa kawaida.

Joji alihisi wasiwasi na mgongano wa ndani alionao Katarina, kama vile Volkano inayopasuka ndani yake na kujisemesha mwenyewe:

Huenda mshtuko alioupata Padri ni mkubwa kuliko uwezo wake wa kuvumilia na hivyo alijaribu kubadilisha maudhui…

Mnaonaje tukaakhirisha mazungumzo yetu, kuna mtu anakuja.

Ooh huyo ni Suleim, karibu Suleim kuna mtu anataka kufahamiana nawe Karibu John Luke pamoja na wageni wako.

Wageni wangu hawajawahi kukaa na Muislamu, na wanataka wakae nawe…

Karibuni, mimi natoka Misri, na nyie kutoka wapi?

Kutoka Uingereza.

Waislamu Uingereza ni mara mbili ya Waislamu waliopo Italia.

Sawa sawa, lakini nimependa kujua Uislamu kutoka kwako, je kitabu chenu kitakatifu kina amini Agano la Kale na Agano Jipya?

Pamoja na elimu yangu ndogo ya itikadi ya Kiislamu lakini nitawajibu kadri nijuavyo….ndio, inaamini, lakini samahani, inaziona kuwa zimepotoshwa.

Je mnamuamini Musa na Yesu?

Tunaamini kuwa ni Mitume ya Mungu.

Je mnaamini Uungu wa Yesu?

Hapana, Waislamu wanaamini kuwa

ni Mtume aliyekirimiwa na sio Mungu.

Na kitabu chenu kitakatifu kinaitwaje? Na

kimewafikiaje?

Jina lake ni Qur’an, na kimetufikia kupitia Mtume Muhammad –mnataka kufikia nini?

Tunataka kuufahamu Uislamu na mafundisho yake?

Mimi sijui chochote kuhusu Uislamu, ninachojua ni utalii, biashara, lakini mnataka nini katika Uislamu.

Ni kwa sababu tunashangazwa sana na matumizi ya nguvu na ugaidi mlio nao?

Magaidi Waislamu tuliokuwa nao huharibu kila kitu kwa jina la dini.

Unasema kwa jina la dini, ni dini gani isiyokuwa na matumizi haya mabaya ya nguvu na ugaidi?

Ndio, Uislamu ni dini ya amani na sio ya ugaidi, lakini Waislamu wamepetuka mipaka ya dini na wako nyuma kimaendeleo na ni watu wenye kushadidia mambo.

Kwa mara nyingine je Uislamu upo nyuma au ni magaidi wapo nyuma?

Uislamu haupo nyuma lakini Waislamu ndio wapo nyuma? Lau mngekuwa ni Waislamu mke wako asingeweza kukaa hapa na sisi na kuzungumza nasi, je huku siko kuwa nyuma?

Kwa nini siwezi kukaa nanyi?

Kwa sababu unatakiwa uvae hijabu na kuwa mbali na wanaume, kwa kweli mimi nimeondoka Misri, ili niwe mbali na ujinga huu.

Je watu wako wa nchini mwako wanaona uonavyo?

Ha ha ha…Baba na mama yangu pamoja ni marafiki zangu mara nyingi huniambia; Fikra zako hazipo katika Uislamu.

Kwa nini?

Uislamu unatofautiana sana na Ukristo, nyie inatosheleza kusali Jumamosi au mara moja ili mbaki kuwa Wakristo, ama sisi yule ambaye haswali kila siku mara tano anazingatiwa kuwa katoka katika Uislamu, nyie mnaweza kuikosoa torati na injili, ama sisi ni kuwa atakayeongea dhidi ya

Qur’an basi atakuwa ametoka nje ya Uislamu.

Je una ndugu yako yoyote aliyepo hapo Italia?

Nipo Italia kwa muda wa miaka kumi na nimekataa kurejea kwetu, na kwa mara ya kwanza kabla ya wiki moja amekuja baba yangu, mama yangu na ndugu yangu na wataondoka baada ya siku tatu.

Je ninaweza kuwaona?

Ndio inawezekana, lakini samahani nyie kwa muono wao ni makafiri.

Kwa vipi?

Wewe unasema kuwa Mungu ni watatu, huku ni kumshirikisha Mungu, na hapo utakuwa umemkufuru Mungu.

Kwani kuna mpya gani? Na sisi tunasema wao ni Makafiri – kwani hawakuamini Uungu wa Yesu hamna madhara yoyote kwetu kama tutakutana nao.

Katarina alikuwa bado katika hali ya mshtuko kwa yaliyotokea kwa Padri, na hatoweza kuvumilia mshtuko mwingine.

Joji hatuna wakati usisahau kesho misa ya Jumamosi takatifu.

Tutapata muda wa kutosha ikiwa muda wao utaruhusu….ni muda gani tunaweza kukutana nao?

Muda wote wao wako nyumbani au hapa hotelini, nataraji watafika hapa baada ya dakika chache, na ukitaka muda mwingine nitawafanya wawasubiri…ninarudia tena: mimi sihusiki chochote kwa watakavyokuambieni.

Uso wa Katarina ulionesha haya kutokana na msisitizo wa Joji, na akamuambia kwa msisitizo:

Samahani… sijafahamu makusudio

yako Joji, lakini naona kama utashikilia hilo basi subiri dakika kadhaa, ili tusilazimike tena kurudi hapa hotelini.

Nitapanda kumuangalia Maiko na Sali na kisha kurudi.

Subiri, hao wanakuja, je niwaite wakae nasi?

Napendekeza bora uwaite, nawaangalia watoto mara moja kisha narudi upesi.

Nitawaita, mtabeba matokeo yake, haya ni maombi yenu…Mama, Baba, Khalid njooni…kuna wanaotaka kukaa nanyi.

Suleim unataka nini?

Khalid hawa ni marafiki zangu, wanataka kufahamiana nanyi, karibuni niwatambulishe:Huyu ndugu yangu Khalid, na huyu ni mama yangu, na huyu ni baba yangu…Khalid anazungumza Kiingereza, ama mama na baba wanajua kiasi tu, lakini hawawezi kuzungumza. Naomba mnipe ruhusa nitafuatilia mazungumzo yenu nikiwa kimya na sitoingilia kitu.

Hali zenu nyote, jina langu ni Khalid ni mhandisi majengo, nduguye Suleim, na huyu ni baba yangu Abdullah na huyu ni mama yangu Aisha.

Mimi ni John Luke, Mtaliano, ninafanya biashara.

Na mimi ni Katarina Mwingereza.

Karibuni nyote.

Joji alikuwa anarudi kutoka kwa watoto wake,
alitoa salamu na kumpa mkono Khalid na baba yake, alipotaka kumpa mkono mama yake alitabasamu na kurudisha salamu.

Samahani ….Lakini mama yangu hapeani mkono na wanaume, ila anakuambia karibu sana.

Naomba samahani, sikuwa najua hilo.

Tumeshafahamiana kabla hujafika, mimi ni Khalid ni mhandisi majengo nduguye Suleim, na huyu ni mama yangu na huyu ni baba yangu.

Mimi ni Joji mhandisi kompyuta kutoka Uingereza mnaionaje Roma nchi iliyojijenga yenye nguvu, dini na fani?

Kwa kuwa mimi ni mhandisi majengo; nianze maudhui kuhusu fani; Roma ni ya kipekee, ni nchi yenye ustaarabu, maendeleo makubwa ya kisasa, pamoja na kuwa kuna kitu ambacho sijafurahishwa nacho.

Ni kipi hicho?

Masanamu na watu kuyatukuza haikunifurahisha, haiwafikiani na malezi tuliyopata kwenye dini yetu, sisi tunazingatia kuwa jambo hilo ni la Kipagani na kuabudu asiyekuwa Mungu.

Joji alikumbuka kuwa nae alifanana na Waislamu kwa kutopenda kwake masanamu na Upagani, kadhalika alikumbuka masanamu miungu yaWahindu na Wabudha.
Khalid aliendelea….

Na hili linaniingiza katika maudhui ya dini katika Roma ambalo umeniulizia.

Samahani kukukatisha, unakusudia nini unaposema, ‘Katika malezi ya dini yenu!?’

Katika Uislamu hatumshirikishi Mungu na yoyote, na tunaamini kwamba inapasa aabudiwe peke yake wala asishirikishwe na chochote, wala haifai kuwanyanyua watu katika nafasi na cheo cha Mungu. Yoyote awaye katika watu hao, na ndio maana Mtume wetu Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Msichukulie kaburi langu kuabudiwa baada yangu, kwa hakika mimi ni mja wa Allah na Mtume wake.”

Ninafahamu kulingana na maneno yako kuwa sisi ni washirikina?

Anayeona Mungu kuwa ni watatu, kwetu huyo anamshirikisha Mungu.

Katarina aliingilia mjadala, kama kwamba kilichokuwa kifuani kwake kimemtoka….

Suleim, kaka yako haoni hivyo, anaona kauli hiyo ni ya kupindukia.

Ndugu yangu Suleim ni mkubwa wangu na ana heshima yake, na sipendi kutofautiana nae mbele za watu, lakini mimi binafsi ni mwenye kukinaishwa sana na mnachosema.

Joji akikatisha…

Kwa maana hiyo Musa na Yesu ni waongo?

Mungu anisamehe, sisi tunaamini ukweli wa Musa na Yesu, tunawaheshimu na tunawatukuza na tunaamini kuwa ni Mitume ya Mungu na ya kuwa amewateremshia kitabu…bali tunaamini kuwa itikadi zenu nyingi zinashusha hadhi zao.

Sisi tunashusha hadhi ya Bwana Yesu?

Nyie mnaamini kuwa ameuawa, ama sisi tunaamini kuwa hakuuwawa, bali miongoni mwenu wanamuona ni mtoto wa Zinaa? Je nyinyi hamuamini hivyo?

Na nyinyi….mnaamini nini kuhusu Yesu na Bikira Maria?

Tunaamini kuwa ni mja wa Allah na Mtume wake, na ya kuwa hakuuwawa wala hakusulubiwa bali walifananiziwa tu, na ya kuwa yeye alizaliwa na Maria bila ya baba kwa muujiza wa Mungu kama vile Adam alivyoumbwa bila ya baba wala mama. Yesu alizungumza utotoni na Mungu alimpa alama nyingi; alikuwa anaponya mbalanga na ukoma na kuhuisha kwa idhini ya Mungu na huwaambia watu watakacho kula na kuhifadhi majumbani mwao.

Hivyo basi mna mtazamo kamili kuhusu Yesu, na mnaamini Agano la Kale na Agano Jipya?

Ndio, tunaamini torati na injili kuwa vimeteremshwa na Mwenyezi Mungu.

Lakini katika kitabu kitakatifu Yesu ni Mtoto wa Mungu!

Tunaamini kuwa vimeteremshwa na Mungu lakini vimepotoshwa. Je katika baadhi ya Biblia mlizo nazo haikuandikwa kuwa Yesu ni mja wa Mungu na sio mwanae na wala sio Mungu?

Hapana, hatuna kitu kama hicho

John Luke alinyanyua nywele zake ndefu kwa upande wa mkono wake akasema:

Samahani kuwakatisha, lakini tunayo Biblia ya Barnaba, nayo ni Biblia iliyoandikwa karne ya kumi na tano na mtawa wa Kikatoliki alitoka katika Ukristo, makundi ya Kikristo hayajakubaliana nae wala kuikubali Biblia hiyo, kwa sababu alimzingatia Masiya ni mwanadamu na ni mtume wa Mungu.

Macho ya Joji yalikodoka akishangaa, na kusema:

Ni kweli! Kwa nini sasa makundi ya Kikatoliki hayajakubali?

Ndio, hayajatambua sio Ukatoliki wala

Uprotestant, ila makundi mengine ya Kikristo yaliyatambua, na mengi ya

makundi hayo yalisilimu baada ya hapo, na ndio maana inatuhumiwa kuwa ni miongoni mwa vitabu vya Waislamu.

Khalid alitabasamu na kusema:

Na kuna dalili kuwa (Barnaba) ni Biblia iliyokaribu na ukweli.

Unakusudia nini kusema karibu na ukweli? Je kuna nakala zingine zilizo za ukweli na zingine sizo?

Nakusudia iliyo karibu kutoka kwa Mola wa Ulimwengu na imeungwa mkono na moja katika muswada za kihistoria, au Biblia zilizopatikana katika moja ya pango la Bani Mizaar Misri, na historia yake inarejea hadi mwanzoni mwa karne ya tatu ya kalenda ya gregoria, na iliitwa Biblia ya Yahudha, ambayo ndani yake kuna maneno hayo hayo, na angalia kuwa ilikuwa kabla ya kutumilizwa kwa Mtume Muhammad.

John Luke kwa dharau.

Swadakta kwa yote usemayo, lakini Wakristo wengi hawaamini Biblia zote hizo.

Khalid akimuangalia nduguye Suleim:

Samahani kama nitakuwa nimewakera, yote ninayosema yanatokana na mapenzi yangu ya Yesu, na kitabu kilichoteremshwa kutoka kwa Mungu.

Hisia zilimchanganya Katarina, na akatokwa na machozi aliposikia neno “Mapenzi ya Yesu” kisha akasema:

Maisha yangu yote ni muhanga na mapenzi kwa Yesu, hivyo basi tunamuamini na yeye ndie mkombozi wetu na ndio maana tukaitwa Wakristo.

Mimi sio mtaalamu wa dini, bali ni mhandisi majengo, lakini inaelekea kuwa wewe ni mkweli kuhusu mapenzi yako kwa Yesu, je umesoma kitabu, My Great Love for Jesus Led Me to Islam “Mapenzi yangu makubwa kwa Yesu yamenipelekea katika Uislamu.” Mwandishi Mvenezuela Mkatoliki Simon Alfredo Caraballo.

Sijawahi kukisikia kitabu hicho, wala sidhani mapenzi yangu ya Yesu yataielekeza katika usiokuwa Ukatoliki!

Je itakudhuru kama utakisoma?! Kwani huna hakika na imani na Ukatoliki wako?!

Sijawahi kukisoma, vinginevyo ningekisoma.

Hii hapa nakala kutoka kwangu, chukuwa kama zawadi yako, sijui kwa nini nahisi kuwa wewe ni mkweli kuhusu mapenzi yako kwa Yesu, samahani si kama wengine yaani baadhi ya watawa na Maaskofu ambao wanaonekana kuwa wanakipa mgongo dunia, lakini wanavunja mapenzi hayo kwa Yesu.

Asante sana nitaisoma, na mimi nina hakika kuwa haitobadilisha chochote katika mapenzi yangu yaYesu au katika Ukatoliki wangu.

Unasema wewe sio mwanazuoni wa dini, kisha nakuona unazungumza lugha za watu wa dini, bali kwa lugha ya mtangazaji wa dini hii.

Uislamu unatutaka sote tuwe walinganizi wa dini hii, kisha akatabasamu na akamwangalia mama yake, na kusema: Mama yangu ndie aliyenilazimisha kuja na kuniambia hiyo ni fursa ya kuulingania Uislamu, na mimi sijui Kitaliano, na hii ndio fursa yangu ya kwanza.

Samahani, watu wote wanatamani kuja nchi za Kimagharibi, nchi zilizoendelea na utamaduni wa hali ya juu, na kuzikimbia nchi zilizo nyuma, na wewe unasema amekulazimisha?!

Ulaya imeendelea sana kuliko kwetu, na hili linawafanya wahajiri wafurahi kwa kufika huku, haswa kwa sababu ya dhulma za kisiasa, kidini na kiuchumi katika nchi zetu, lakini mimi nafanyakazi ya uhandisi katika shirika zuri, na nina mapato ya kunitosheleza, na baada ya kuanguka utawala wa kidikteta kwetu Misri hali yetu ni nzuri, na itakuwa nzuri zaidi siku za usoni Mungu akipenda.

Kwani haikuwa dhulma ya kidini na kisiasa huko kwenu sababu yake ni dini?

Haiwezekani Uislamu ukawa ni sababu ya dhulma hata siku moja.

Kwani hawakuwa ni Waislamu waliochoma kanisa la Watakatifu huko Alexandiria?

Hivi ndivyo ilivyosemwa hapo mwanzoni, na watu wote ulimwenguni waliamini nikiwemo mimi, pamoja na kushangazwa kwangu na jambo hilo.

Lakini baada ya dikteta Hosni Mubarak kuangushwa ambaye anapata msaada kutoka nchi za Magharibi ilithibitika kuwa ni vyombo vyake vya usalama ndivyo vilivyolipua. Nadhani wewe ni miongoni mwa mliosikia habari za mwanzo na hukupata taarifa ya habari ya pili kama ilivyo desturi za watu wa magharibi.

Lakini bado mpo nyuma (kimaendeleo) kwa sababu ya dini yenu!

Mama yake Khalid (Aisha) alimuashiria mwanae, na kusema:

Khalid mwambie kuwa sisi tupo

nyuma kwa sababu ya kuwa mbali na

dini yetu!

Khalid alihamisha aliyoambiwa na mama yake … chakula kilifika mezani Joji akajaribu kukamilisha mjadala uliopita…

Je mama yako na baba yako wanajua kinachoendelea katika mjadala huu baina yetu?

Ndio wanaufahamu vizuri, pamoja na kuwa hawawezi kuchangia kutokana na lugha, kwani Suleim hajawaambia tokea mwanzo, labda ilikuwa kabla hujafika.

Je ninaweza kumuuliza mama yako?

Mama unakaribishwa (kwenye mazungumzo) na mimi nitatafsiri atakachokuambia.

Je hutamani kuwa mkana dini, au Myahudi au Mnasara?

Mama (kwa tafsiri ya Khalid): Mungu anilinde, ewe mwanangu, hakuna anayependa kupotea kamwe.

Je sisi tumepotea?

Mama (kwa tafsri ya Khalid). Kama sio kupotea basi sijui maana ya kupotea, mimi ni mwenye furaha nimekirimiwa na mwenye utukufu katika Uislamu.

Je hii ni rai yako au rai ya Wamisri wote?

Mama (kwa tafsiri ya Khalid): Hii ni rai yangu kwa uchache, kwa bahati mbaya tuna watu, vile vile walioathirika ambao wanaona kufuata dini ni kuwa nyuma na kukosa maendeleo.

Kisha akamuangalia mwanae Suleim, akainamisha kichwa chake….

Lakini mwanamke amedharauliwa

katika Uislamu!

Mama (kwa tafsiri ya Khalid): Nani amekuambia hayo?! Umri wangu mimi ni miaka sitini na tano, pamoja na hayo naweza kumuamrisha mwanangu Khalid aje pamoja nami na kunitii kwa furaha kabisa, pamoja na kujua kuwa ni mwenye shughuli nyingi na hataki kuja. Na huwa ananitembelea na wanangu wa kike wanamtembelea mara tatu hadi nne na wakati mwingine mara tano kwa wiki na si hivyo tu bali wanamletea zawadi. Hawawezi kwenda kinyume katika ninayosema mimi au baba yao, je kunakukirimiwa kama huku? Sijui kama kuna ukarimu kama huu sio ukarimu.

Sijamuona baba yangu wala mama yangu zaidi ya miezi mitatu.

Khalid alianza kubabaika baada ya kusikia majibu ya mama yake, na akamuangalia Suleim ambae alianza kubabaika.

Unasema nini….?

Sitaki kukukera.

Kamwe tafadhali.

Anasema: Mfano wa Suleim ambae amejifunza kwenu, na kuchukua tabia zenu.

Mara ngapi tunawaona kwetu wakinywa pombe na bila kuwa na adabu!

Mama (tafsiri ya Khalid): sehemu nyingi watu wanapoteza dira na kupotea, lakini zama watakapojua muelekeo wao watatubia na kurejea kwa Mungu wao.

Maiko na Sali wakaja kutoka roshani baada ya kumaliza chakula chao…

Baba, ulituambia kuwa utarejea baada ya dakika ishirini, sasa imefika arobaini na tano, twende kama ulivyotuahidi?

Samahani, tumewashughulisha na watoto wenu.

Ooh, sikutanabahi na muda.

Asanteni sana Suleim, Khalid, Aisha na Abdullah …tumechukua wakati wenu mwingi, hii hapa kadi yangu, je mnaweza kunipa kadi zenu?

Hii hapa kadi yangu, kuna anuani ya barua pepe, nitafurahi ukinitumia rai yako kuhusu kitabu ewe Katarina.

Nitajaribu, asante sana.

Khalid alipoondoka pamoja na baba yake na mama yake, Suleim aliwaelekea wageni wake huku akiwataka radhi…..

Nimekuwa kimya kama nilivyowaambia, nawaombeni radhi kwa kila kosa lililotokea katika haki zenu hata hivyo niliwaambia tokea mwanzo na kukutahadharisheni lakini nyie ndio mliosisitiza.

Pamoja na kushtushwa walichokisoma, na pamoja na hoja zao nzito ila walikuwa watulivu na wanadiplomasia, kwa hivyo huna haja ya kuomba radhi…..Ha ha ha, bali nenda ukamuombe radhi mama yako kwa kuwa hukumtembelea kwa miaka mingi.

John Luke aliwaaga wote na kuondoka kwenda kazini, na Joji na Katarina walikwenda na watoto wao Trevi Fountain …Chemchem ilikuwa ni nzuri sana, walifurahi sana kuonana kumalizia siku yao nzima iliyobakia pembizoni mwake… kabla ya kuondoka kwao Katarina alitupa ndani yake sarafu ya fedha, Sali alimuangalia

mama yake kwa mshangao:

Katika ngano za Kitaliano kuwa atakayetupa kipande cha fedha hapa atarudi tena Roma.

Baba nipe sarafu ya fedha nitupe.

Usiamini binti yangu, huu ni ushirikina.

Najua kuwa ni ushirikina lakini nataka pesa ili niseme nami nimetupa katika Trevi Fountan.

Chukua hii yako na nyingine ya Maiko, na nataraji ewe Katarina usiwe mshirikina.

Katarina alijibu kwa umakini na

uwazi…

Nataraji nawe usifanye mambo kuwa magumu, yafanye mepesi, tupo matembezini.

(3)

Una nini Katarina?

Hamna kitu.

Je hupendezwi na chemchem na utalii pembezoni mwake…sijakuona ukicheka leo na kuzungumza kama kawaida yao?

Bali ilikuwa ni siku nzuri sana, huenda

akili yangu ikawa imechoshwa kidogo

Kwa kitu gani?

Kwanini ulikuwa unataka kukutana na Waislamu tuliokutana nao?

Ili kuwafahamu na kufahamu hadithi zao za kipuuzi na kuwa kwao nyuma, ili kumtayarishia Tom majibu atakaponiuliza kuhusu Waislamu.

Lakini ulikuwa ukihamasika na maneno yao.

Joji alitabasamu na kumuangalia Katarina machoni na kusema:

Mimi ndiye niliyekuwa nikihamasika?!

Katarina alifahamu makusudio yake…

Yeye anazidisha mapenzi yetu kwa Yesu.

Inaelekea kweli wanampenda Yesu na mama yake.

Unasema nini?!

Tofauti ipo katika Uungu wa Yesu, wao wanaona kuwa ni ushirikina, ukafiri na upagani.

Na sisi tunaona kuwa ni kumpwekesha Mungu na ibada.

Ha ha ha, je utakisoma hicho kitabu?

Sitaki kukisomaHa ha ha, lakini uliahidi utakisoma, je unahofia kukisoma kitabu kama alivyokuambia?!

Maneno gani haya Joji?! Kitabu hakina mbele wala nyuma!

Swadakta…Kwa nini hukisomi? Kuna kosa gani katika hilo?

Nani aliyekuambia kuwa nataka kukisoma.

Kwa mara ya kwanza nakuona dhaifu kwa hoja na kuutetea Ukatoliki, na kwa mara ya kwanza nahisi kuwa maneno madogo tu yanakutingisha.Sitosoma kitabu.

Ili uthibitishe kuwa unakiogopa kitabu chenyewe.

Kama ni hivyo nitakisoma basi.

Una nini Katarina?! Kwa nini huu udhaifu?!

Sijui, tokea kukutana na Padri nimepatwa na wasiwasi ndani mwangu, huenda ikawa kweli muoga wa kusoma kitabu.

Wewe sio muoga wewe ni jasiri, bali wewe ni mfano wa kuigwa kwa yakini, nakushauri ukisome kitabu hivi sasa; kinaonekana ni kidogo sana, na mimi ninafungua barua pepe, kwani jana nzima sijaangalia.

Pindi Katarina alipokaa kusoma kitabu, Joji alifungua barua pepe yake na macho yake yakimfuatilia Katarina juu ya hamasa yake wakati wa kusoma.. alipata majibu ya aliowatumia barua pepe na nukuu kutoka torati… kwani walimtumia maoni yao… aliyafupisha

na akawatumia tena wao.

Tom: Una maana hii ndio sababu ya unyama na Baraad? Inaelekea wasifu huo ni mzuri. Levi: Pamoja na kufahamu rai yangu katika unyama huu, lakini nyote mnaamini kuwa atakayeshambulia torati atakuwa ameshambulia dini zote za mbinguni. Habib: Nakubaliana nae kabisa, lakini waangalie Waislamu, pamoja na mimi kutowapenda imani yao inatofuatiana na torati. Adam: Maneno makubwa ya hatari, je inawezekana kuwa yanatoka kwa Mungu?

Kisha akawatumia barua hii:

Nasubiria leo mtazamo wenu kuhusu fikra na na sio kunukuu maandiko: “Hakika utatu uliopo katika ukristo ni ushirikina, ni maneno yasiyoeleweka na Mungu ni mmoja tu na Yesu ni mja wa Allah na Mtume wake.” Nasubiri majibu yenu kwa ufupi ni mimi.

Joji.

Joji alimaliza kazi yake katika kompyuta, na kumgeukia Katarina ambae alikuwa makini kusoma kitabu

kwa utulivu mkubwa…

Je umemaliza kusoma?

Hapana, subiri kidogo.

Akhirisha kusoma mpaka kesho, kuna jambo nataka kujadiliana nawe.

Subiri dakika chache tu namaliza.

Unaonekana kuhamasika sana na kitabu!

Dakika chache tu samahani.

Nitalala ikiwa ni hivyo.

Katarina alimaliza kusoma kitabu, halafu alimsogelea Joji ambaye

alikuwa amejilaza kitandani…

Samahani, nilikuwa mwishoni kumalizia kitabu na nilipenda kumalizia.

Inaonekana ni kitabu chenye kukinaisha!

Kwa kiasi fulani, hakina ubaya.

Nilitaka tupange mambo yetu ya kesho.

Kesho ni Jumamosi, je hatukualikwa na kasisi kuhudhuria misa?.

Ndio, ametualika, lakini je tutakwenda?

Ndio, tutakwenda, je tutaacha misa katika kanisa tukufu zaidi?

Haa – haa, kwa hivyo mapenzi yako juu ya Yesu yamekufanya uende kanisani na sio Uislamu?

Ijapokuwa kitabu ni kizuri kwa kiasi kikubwa ila mimi nitasali kanisani kesho.

Wapi tutawaacha watoto wetu?

Tutaenda nao kwenye misa.

Je huwaogopi makasisi?

Sijakufahamu?

Siwezi kuwachukua wanangu katika misa, mimi nawaogopea makasisi.

Unawaogopea nini?

Nawaogopea kutokana na tabia chafu ya makasisi kwa sababu ya kurudia rudia kusoma kwao Agano la Kale na Jipya Leo wewe unaongea kwa mafumbo, je unaweza kubainisha unakusudia nini?

Kwani hukusoma kuhusu habari za fedheha za kanisa kuhusu ngono? Je hukusoma kuhusu kesi zilizofunguliwa dhidi ya kanisa kuhusu watoto?

Sitosahau mahojiano yaliyofanyika na mmoja wa wale aliyebakwa kanisani.

Ama kwa hakika watawa na makasisi walikuwa ni wanyama na sio binadamu, na sipendi Maiko na Sali wakutane na mambo hayo huko.

Una nini “Joji? Mimi naenda kanisani kila wiki zaidi ya mara moja na halijatokea lolote mbele yangu, wasiwasi wa nini huu?

Je umewahi kupitia, kuona, au kukaa, au kujadiliana, au kusoma fedheha ya maadili katika kanisa?

Hapana.

Acha tukubaliane yafuatayo, ingia katika You tube na angalia vipande vya video vinavyozungumzia mambo hayo

humo, na ikiwa utaendelea kusisitiza kwenda nao, kesho tutawachukua

watoto wetu kwenye misa.Nitatumia muda huu kuangalia vipande hivyo kwa ajili yako, na kesho sote tutakwenda kanisani…umeanza kutumia lugha ile ile ya yule Muislamu tuliyekutana nae katika kuzungumza nami.

Haa –haa, inaelekea kama yalivyokuathiri mazungumzo nae yule bwana hali kadhalika vipande hivyo vitakuathiri. Lala salama ewe mpenzi wangu.Na wewe mpenzi wangu.

Walikumbatiana kwa muda mrefu, kisha Joji akalala na kumuacha Katarina akiangalia na kusoma habari za kufedhehesha za kijinsia juu ya kanisa, na kuhamia katika fedheha zingine ambazo sio za kijinsia, na hakuhisi muda ulivyokuwa ukipita…alirudia kukisoma kitabu “Mapenzi yangu makubwa juu ya Yesu ndio yaliyoniingiza katika Uislamu” na sijui kwa nini alichagua kusoma kipande hiki:
“Hakika imani ya kujitoa muhanga na kufa msalabani pamoja na kuwa inapingana na akili na fikra, kwa hakika imechangia kufungua mlango wa mapambano kwa kuacha matendo mazuri na kufanya matendo ya shari na madhambi, kama; kuua, kuiba, kupora, kuzini na mengineyo, kwa hakika Paulo alizembea umuhimu wa sharia, wasia, pamoja na matendo mema ambayo alikuja nayo Masiya ili kukamilisha na kuyalingania akasema katika risala yake kwenda kwa Rumia (3:28), “basi sisi tunaamini kwamba mwanadamu anakuwa mwema kwa imani na sio kwa mujibu wa hukumu za sheria”, na hata Adam haikumnufaisha amali yake (4:2) na akaja kuikomboa na kuokoka kwa kuwa tuna Imani kwa kusulubiwa Masihi juu yake amani, wala usiulize haki za wanadamu ikiwa ana imani hiyo, na katika kumjibu Paulo kwa riwaya iliyokuja katika ulimi wa Masiya katika Mathayo (19:5) mwenye kuvunja wasia huu mdogo na kuwafundisha watu haya hivi basi atahesabiwa ni katika ufalme mdogo wa mbinguni, ama mwenye kujua na akaenda, huyu atahesabiwa ni katika ufalme mkubwa wa mbinguni.”
Alirudia kusoma tena kipande….na kuzinduka kuwa muda ulikwenda sana, usiku ulikuwa mwingi, aliweka kitabu hicho pembeni mwake na kujitupa kitandani na kujisalimisha na mawazo yake hadi akalala.
Joji aliamka mapema asubuhi bila Katarina kuhisi kitu na kuoga na kuvaa nguo zingine….kisha alimsogelea Katarina ili amuamshe na kukuta kitabu kipo pembeni yake katika kurasa ya mwisho aliyofikia. Alichukua na kukisoma na kisha akakirudisha pale pale kilivyokuwa kimegeuzwa katika ukurasa ule ule.
Joji alikwenda chumbani kwa wanae na kumuamsha Maiko na Sali ili wajiandae, alirudi tena kumuamsha Katarina… na wakati wakitoka kwenda kupata staftahi katika Bafe hapo hotelini, Joji alimgeukia Katarina…

Leo tunatalii wapi?

Katika sehemu nzuri na bora zaidi.

Mama tunakwenda wapi leo?

Nimemuuliza baba akaniambia kuwa wewe utachagua wapi pa kwenda sisi leo?

Punde tu tutawaeleza mimi na baba yako.

Katarina aliwaomba watoto wake watangulie kidogo kwenda Buffet ya hapo hotelini, kwani alitaka

kuzungumza kidogo na Joji.

Tutakwenda wapi leo?

Je umeona na kusoma fedheha za kijinsia juu ya kanisa?

Ijapokuwa mara kwa mara nipo Kanisani, ila kwa yale niliyoshuhudia na kusoma ni mabaya zaidi kuliko uwezo wangu wa kuyasawiri mambo, na kama ni kweli, basi hawa ni wanyama na sio binadamu.

Hivi unaamini hayo ni kwa sababu ya mafundisho ya Paulo ambayo yanatenganisha kati ya imani na matendo mema? Na ndio maana ukatengeneza itikadi ya kujitoa muhanga na kukomboa.

Je umesoma kitabu?

Hapana, ila nimesoma sehemu ambayoilikuwa wazi kitabuni, kwani kuna tatizo gani nikikisoma?

Hakuna tatizo…nimeshangaa tu na ikiwa utakisoma ni vizuri, mimi sio muoga, na huenda sehemu hii uliyoisoma hasa ndio inaniletea tatizo kwangu, huenda tutapata fikra baadae, la muhimu, ni ipi rai yake juu ya pa kwenda

leo hii?

Hatuna budi kuhudhuria Misa kanisani.

Hapana shaka, ila ni baada ya kwenda kwanza katika bustani ya Villa Benbela, ni busani kubwa kabisa Roma na ndio nzuri zaidi.

Nahofia tutachelewa kwenye misa.

Haa haa, hatuchelewi ewe mtawa.

Sawa, tumekubaliana.

(4)

Eneo la bustani ya Benbela Round Villa linafikia kilometa tisa za mraba.. Sehemu pana ya kijani kibichi yenye kufurahisha kwa kupumzika. Pia imezungukwa na aina mbali mbali ya ndege hali iliyowafurahisha Maiko na Sali kuziangalia…

Chaguo zuri ewe mama yangu, siku ya leo hii ni katika masiku mazuri

kabisa kwangu.

Sehemu ni nzuri sana, je imekupendeza ewe Sali?

Ndio imenipendeza sana.

Tutakamilisha matembezi haya mazuri kwa kuhudhuria kwetu misa kanisani leo.

Maiko alilalamika kwa kusema:

Sitaki kwenda kanisani.

Joji alitikisa mabega yake na kumtazama Katarina….

Hayo ni matakwa ya mama yako muulize yeye.

Baada ya ziara za kutembelea vitu asilia, hapana budi tutembelee sehemu au maneno ya dini na kiroho.

Naomba udhuru mama, mimi sipendi kanisa!

Je hupendi kumuabudu na kumshukuru Mungu wako ambaye amekuumba, kukuruzuku na kukuhurumia?

Napenda kumuabudu Mola wangu, ila sio kwa kwenda kanisani.

Binadamu ambae hataki kumuelekea

Mola wake na kumuabudu na

kumshukuru, basi dunia itamsonga yeye..

Je wewe umedhamiria kwenda kanisani?

Joji alitaka kupunguza mjadala….

Ikiwa hutaki kumuabudu Mola wako na kumshukuru utapata hasara, ila

idhani kama ibada inafungamana na kwenda kanisani.

Tutaenda baada ya kukamilisha kustarehe katika bustani nzuri, lakini ole wako ukaacha ibada na shukrani kwa Mola wako ewe kipenzi changu.

Asante mama yangu, asante baba yangu, lakini kwa nini ibada imefungamana na kanisa tu?

Katarina alipenda kumaliza mjadala….

Sali njoo uangalie ndege yule kwa mbali…haya twende…

Maiko na Sali walienda haraka kunako ndege….

Maneno ya Maiko ni mazuri sana.

Ndio, lakini hayanifanyi ndio sababu katika mambo wasiyopenda watoto?

Je haikuwa kwenda kwenye misa ni mapenzi yako wewe?

Tutaendelea na mazungumzo yetu ewe mwanafalsafa usie na madhambi.

Familia ilimalizia muda wao wa asubuhi katika bustani baada ya hapo walipata chakula cha mchana… baada ya kumaliza kula Katarina aliwageukia watoto wake.

Sasa tunaelekea kwenye misa, na nakuombeni mswali kwa unyenyekevu na muwe makini kwa nafsi zenu.

Tujihadhari na nini?.

Kwa kitu chochote au mtu au tendo lolote la kuwaudhi au kuwakera.

Mfano wa nini?

Mfano wa kitu chochote kitakachowaudhi au kuwakera, je maneno yangu yako wazi ewe Sali na Maiko?!

Yameeleweka ila sijui kwa nini unatueleza hivyo? Je sisi tunakwenda kanisani au kwenye bustani yenye wanyama wakali?

Walipo karibia kanisani, Katarina alisogea karibu na Joji na kumnong’oneza….

Kwa hakika umenifanya niwe na wasiwasi, hivyo basi wewe kuwa makini na Maiko, na mimi niwe makini na Sali..

Sio kwa kiasi hiki, inaelekea wewe una wasiwasi sana, la muhimu kuwa makini tu.

Wote waliingia kanisani, na baba Mtakatifu alianza misa takatifu…ila Joji hakujali, wakati Katarina alikuwa ni mwenye kuvutwa sana na misa hiyo, lakini akiwa ni mwenye wasiwasi na asie na raha
Pindi walipotoka tu, Maiko alimparamia mama yake..

Asante mama, Misa takatifu ilikuwa nzuri, ni kiasi gani nampenda Yesu!

Alikuwa ni sababu ya kutukomboa sisi, na wanadamu wote na madhambi na makosa.

Sali aliuliza kitoto..

Mama.. hivi hakuna njia nyingine ya kututakasa na Bwana kupitia makosa yetu pasina Yesu kuuliwa, kwa hakika nimejisikia uchungu mwana Yesu kufa, na mimi nampenda na kwa ajili yake napata zawadi kila mwisho wa mwaka.

Maiko….

Mimi ni kama wewe Sali… huenda kwa sababu hii ndio maana sipendi kwenda kanisani, au ni kwa ajili hii siwapendi makasisi na watawa.

Mapenzi yako kwa Yesu ndio muokozi na mtetezi wako.

Maiko usisahau matendo mema, kwani imani peke yake haitoshi kama anavyotufundisha Yesu.

Familia ilirudi hotelini baada ya kutoka kwenye misa takatifu na watoto walienda chumbani kwao…na hapo Joji alimwambia Katarina kwa tabasamu la kijanja:

Ulikuwa na wasiwasi sana kanisani!

Wewe ulionekana hujali kabisa.

Ndio, vipi unataka nijali kitu ambacho sijakinaishwa nacho? La muhimu, safari yetu ni kesho kutwa, na tunataka kustarehe katika masiku yanayokuja kama tulivyostarehe katika masiku yaliyopita.

Mimi nimechoka sana, jana nimechelewa kulala, nalala sasa hivi.

Mimi nitafungua email yangu, halafu ndio nilale, je unaweza kunipa kitabu ulichopewa na Muislamu.

Je utakisoma?!

Huenda, kuna tatizo gani kama nitakisoma?

Hakuna tatizo, chukua…uamke salama.

Joji alichukua kompyuta yake na kufungua email, ili kupata majibu ya rafiki zake:

Habib: Nimechoka kuwafahamisha wanafunzi wangu wa Chuo Kikuu juu ya Mungu kuwa mmoja na hapo hapo kuwepo kwa utatu sikuweza kupata jibu, huenda mimi mwenyewe sijui, yapo uliyoyataja kwa ujumla kuhusu nakala za zamani kabisa za Injili. Tom: Hesabu inasema 3 ≠ 1, na watu wa mantiki wanasema: sehemu ya kitu kizima kinachukua hukumu ya kitu kizima kimoja, na baba yangu anasema: usizungumzie kitu usichokijua, na mimi nasema: niambie kile ninachoweza kuelewa ili nipate kukujibu, Haa haa. Adam: Ikiwa tutasema kwamba Yesu ni mja wa Mwenyezi Mungu na sio mshirika wake au mtoto wake, haimaanishi hivyo ni kumshushia hadhi yake. Levi: Huyu ni kama mfano wa tunavyosema sisi katika Uyahudi: “Hakika Uzayru ni mwana wa Mungu”. Nina hakika kuwa maneno hayo ni maneno yasiyofahamika.

Joji alirudia tena kuwatumia pasina kuwataja majina yao, kisha akaandika barua ifuatayo:

“Sehemu ya tatu: Je yawezekana kuwa Paulo ndio aliyeharibu Agano Jipya? Ni mimi Joji.”

Pindi akiwa anasoma barua zilizobakia, alikuta barua kutoka kwa Kakhi kama

ifuatavyo:

“Rafiki yangu Joji … nataraji upo mzima wa afya, wafanyakazi wote wanakusubiri, tunatamani kukuona hivi karibuni” Ni mimi Kakhi!! “Tanbihi, umekuwa nje ya kazi zaidi ya wiki moja mpaka sasa.”

Alihamanika na kutaka kufunga kompyuta yake ila alikumbuka ukurasa wa face book wa Adam na kuwa hajaufungua ukurasa wake kwa muda mrefu na kukuta makala mapya kutoka kwake ikisema: (Mafunzo kutoka kwa rafiki yangu anayetafuta furaha 3):

Rafiki yangu anayetafuta furaha amekumbana na matatizo ya kiafya katika kipindi hiki na kabla sijataja yale niliyojifunza kutoka kwake napenda niweke angalizo juu ya yale yaliyotokea kipindi cha kuugua kwake: Kawaida ya maradhi yanaambatana na udhaifu na hili limemtokea rafiki yangu huyu, na niliogopa pengine asikamilishe lengo lake, lakini ukweli na matarajio ndio yaliyomfanya kuvuka hilo, kwa hivyo kwa mwenye akili hatakiwi kuchukua maamuzi kipindi cha udhaifu na unyonge. Nilikaribia kuvuka mipaka katika muda fulani na kumwambia njia bora ya furaha ni hii nilipomuona amedhoofika, ila Mwenyezi Mungu amemponya. Nina hakika kuwa kipindi kijacho kitakuwa kigumu zaidi kwa rafiki yangu, na huenda nikawapa taarifa yake hatua kwa hatua. Turudi katika darsa zetu kwa mara nyingine, rafiki yangu bado ana hamu ya kujua njia ya furaha, na nimejifunza kutoka kwake yafuatayo: Hakika wale wanaokuzunguka ima wataathirika nawe, au wewe uwaathiri au upambane nao na kinachofanya kuwa hivyo ni yale yanayodhaniwa kuwa ni mapambano ya kifikra na kiimaani, na wengi wanaomzunguka wameanza kuathirika naye, na hii ni dalili tosha ya msisitizo wa jambo lake na ukweli wake, na kwa ujumla nadhani kumekuwa zaidi ya mtafiti mmoja katika hili, huenda nikawapeni habari nzuri hivi karibuni kuhusu njia ya furaha. Utulivu wa nafsi na kutoegemea upande mmoja katika kuamiliana na fikra ni muhimu zaidi katika kufikia njia ya furaha; na hivi ndio vitu anavyomiliki rafiki yangu huyu, ingawaje wakati mwingine anakosa kutokana na kubanwa. Umuhimu wa elimu, hata kama unadhani unajua ni lazima kujifunza, huenda unachokijua kisiwe kweli, kwa kweli rafiki yangu amenishangaza kwa kuwa na moyo wa kutaka kujifunza vitu tokea utoto wake na akili yake iliyofunguka vizuri. Kwa masikitiko –Rafiki yangu ana ufahamu mdogo wa kulinganisha au kufungamanisha kati ya matukio, kusoma na mijadala, ambayo ni muhimu sana katika kulinganisha kati ya fikra mbali mbali ili afikie katika njia ya furaha. Naamini kwamba rafiki yangu yupo katika hatua za mwisho katika kutafiti njia bora ya furaha, na katika kujibu maswali makuu ya maisha, nanitakufahamisheni katika darsa zijazo hivi karibuni.” Adam”

Joji alisoma majibu ya wasomaji na kuzingatia jibu la mmoja wa wasomaji aliyesema: “Inavyoelekea wewe unampenda sana rafiki yako, na unamuweka katika sura ya mfano bora wa kuigwa.” Na jibu la Adam lilikuwa kama hivi, “Ndio nampendelea kheri kama ninavyopenda kwa kila mtu; na Mungu anatuamrisha kuwapendelea watu kheri.”
Kisha akasoma makala nyingine ya Adam inayosema kuhusu mabadiliko ya kifikra,na akawa ameandika yafuatayo:

“Pamoja na ugumu wa kubadili fikra ila leo nimekumbana na uzoefu mpya, nilikuwa pamoja na tabibu wa Nafsi, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, na mwanafalsafa aliyepevuka, lakini bado anazunguka na kutanga tanga baina ya imani na fikra, alikuwa ni Mkristo halafu akawa kafiri, halafu akawa ni mtu aliyezama katika mambo machafu, amesoma Ubudha, Uhindu, Uyahudi na Ukristo, na anataka kuusoma Uislamu, anayo matatizo mawili. Tatizo la kwanza: Anafanya falsafa ndio hakimu wa kila kitu. Nilimjibu kwamba, “elimu ndio hakimu, na sio misingi yako ya kifalsafa, hakuridhika, ijapokuwa ameniahidi atayafikiria maneno yangu kwa mara nyingine.Tatizo lake la pili ni: Anafikiri kwamba kila dini ni janga na kuchukia kila dini, anazikosoa dini zote alizozisoma, je ni kitu gani mnachoninasihi kwake? Ni mimi Adam.

Joji alijua makusudio ya Tom, alifungua ukurasa wake na hajakuta kipya, na cha ajabu ni kuwa Tom hajafungua ukurasa wake kwa muda wa siku tano hivi, na sio tabia yake. Joji alifunga kompyuta yake, na kuchukua kitabu na kufungua haraka, kwani alijihisi kutaka kulala, lakini sehemu aliyokuwa ameanza kusoma ilimrusha usingizi na hivyo kuanza kusoma kwa mazingatio makubwa, na bila kujua kwa nini alipatwa na mshtuko ijapokuwa yalionekana ni maneno ya kawaida? Je, ni kwa sababu maneno hayo hayapo katika Ukristo?
Kiasi kwamba kuna ombwe kubwa kati ya ibada na kutaka kujitakasa na maisha au ni kwa sababu msemaji wa maneno yale alikuwa ni Mkristo?
“Mwandishi wa Kimarekani Michael H. Hart baada ya kuorodhesha na kuweka misingi muhimu katika kitabu chake, anasema: Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ni mtu pekee aliyefaulu kwa kiasi kikubwa katika Historia na ameonekana katika kila nyanja ya kidini na kidunia.. na kwa muunganiko huu wa kipekee ndio uliomfanya Muhammad awe ni mtu aliyeathiri katika historia ya kibinaadamu.” (The 100: A Ranking of the Most Influential Persons in History By Michael H. Hart) Joji alijilaza huku akituliza mawazo yake, na hakujitambua ila baada ya kufika asubuhi na Katarina kumwambia:

Haa amka, amka yote haya ni kwa ajili ya kitabu.

Oh… inaonekana unaniogopea, kuwa na amani, wala sijasoma kitabu.

Haa –haa –hali ni hii nawe unasema hukusoma kitabu, ingekuwaje kama ungesoma!

(5)

Haya fanyeni haraka… leo ndio siku ya mwisho kuwepo hapa Roma na tunataka kutembelea sehemu nyingi.

Mchana ulikuwa umesheheni mambo mengi… Familia ilitembelea bustani na sehemu za matembezi, na walipanda boti karibu na ziwa lililotengenezwa…. Na kuhitimisha matembezi yao kwa kutembelea soko….na wakati wa kutoka Joji alimfinya Katarina kidogo….na kutabasamu:

Mbona hujanunua msalaba, umekuwa humpendi Masiya?

Sijaacha kumpenda ila mapenzi yameongezeka kwa kumtii na kutenda aliyofanya na sio kwa misalaba tu.

Haya ndio nilikuwa nakueleza tangu kipindi, mapenzi sio misalaba, masanamu, utawa na ukasisi.

Achana na haya kwa sasa ewe Mprotestanti mbaguzi.

Au huenda mapenzi yangu kwa Yesu yatanifanya niwe Muislamu wa siasa kali, japo sijakisoma kitabu chenyewe.

Nadhani unafaa kuwa gaidi kama ambavyo inafaa kuwa Mhindu muabudu ng’ombe.

Haa haa.

Ilipofika jioni.. Familia ilielekea katika mgahawa wa kifahari pembeni ya mto Tiber, na kupata chakula cha usiku huku wakiwa katika furaha na hewa nzuri iliyokuwa inavuma pale walipo….

Nimekusikieni sana mnazungumzia dini, je dini ni muhimu sana kwa watu?

Bila shaka ni muhimu ewe Maiko.

Rafiki yangu shuleni anasema:Ukafiri ndio asili, na asili ndio ambayo tumeumbiwa, na mawazo ya dini na kufikiri juu ya dini ni katika maneno ya kizamani yaliyopitwa na wakati.

Na wewe ni ipi rai yako?

Naamini kuna baadhi ya mambo katika dini ni ushirikina na upotofu.

Pambanua kati ya kuwa na dini potofu au kuwa baadhi ya dini potofu.

Ila upotofu ni mwingi sana katika dini kama anavyosema rafiki yangu.

Kama nini ewe mwanangu mdogo?

Japo mwalimu shuleni amebainisha sana ila mimi bado sijaelewa itikadi ya utatu wala kujitoa mhanga na….

Labda ni vile umri wako ungali mdogo mwanangu, na pale utakapo kuwa mkubwa utaelewa.

Ananiambia rafiki yangu ambaye nimekuelezea: “Kila mtu utakae muuliza atakuambia wewe ni mdogo, lakini naamini wote hao hawajui hilo.” Je wewe unajua mambo haya?

Ndio, ndio kiasi fulani.

Na wewe baba yangu?

Ha ha ha, hapana, hapana kiasi fulani tu.

Nahisi maudhui haya ni magumu, je Mungu anatuchosha ili tufahamu?

Katarina alichoshwa na maneno hayo..

Ooof, na wewe mambo yako magumu kama baba yako, sivyo hivyo mwanangu bali ni mepesi zaidi.

Joji akiwa imara alisema..

Vizuri haiwezekani Mungu akaleta kitu ambacho akili haiwezi kukidiriki, ukiona hivyo ujue kuwa inakupasa usome sana ili ufahamu, ama mambo yawe kwa njia ya siri siri tu usikubali hilo.

Kama ni hivyo baba wewe unakubaliana na yule rafiki yangu?

Hapana, ukafiri ni ngano ambazo zinakwenda kinyume kabisa na akili.

Sijafahamu baba.

Je inawezekana kuwa dunia hii imejitokeza ghafla tu?! Na watu hali kadhalika wamejitokeza ghafla tu.?!

Wanaokana Mungu hawasemi hivyo baba, bali baadhi yao wanazungumza kulingana na nadharia ya Darwin ambayo tumejifunza katika elimu ya baolojia.

Ndio, nadharia ya Darwin ni nadharia za siku nyingi sana na sasa hivi imethibitisha makosa yake kielimu na kiakili.

Unaweza kumuuliza mwalimu wako wa sayansi, yeye anajua kuliko mimi, na nitakununulia kitabu kinachoelezea hilo, inapasa utegemee elimu na sio ngano za watu, hata kama wakati mwingine zikionekena ni za kielimu.

Lakini tatizo ni kuwa dini inakwenda kinyume na akili.

Haiwezekani, hakiwezi kimoja kikawa bila za kingine

Kwa vipi?

Ninaweza kukufupishia haya kwa maneno ya Einstein: “Elimu bila ya dini ni kilema, na dini bila ya elimu ni upofu”.

Unakusudia elimu ya makafiri ni kilema?

Bali ujinga wao ni zaidi ya elimu yao, na kile wanachofundisha ni kilema, kama ambavyo dini bila elimu inageuka kuwa ni maneno ya kipuuzi na siri mbali mbali; na kwa hiyo ni upofu…

Maiko alinyamaza kimya, Joji akawa anatafakari maswali haya ni mazito kutokana na umri wake au ni dalili ya uerevu na utambuzi, au ni ugonjwa wa shaka katika hali ndogo.
Familia iliporudi hotelini… John Luke alikuwa akiwasubiri katika ukumbi wa mapokezi, mara tu alipowaona alisimama na kuwatolea salamu.

Ni ziara ya ghafla, karibu sana.

Rafiki wa kasisi karibu sana, hatujakuona kwenye misa!

Sijahudhuria kwenye misa kiasi cha mwaka hivi.

Kama ni hivyo basi unawezaji kusuhubiana na kasisi?

Yaelekea kasisi ni mtukufu sana kwako, ijapokuwa ameshindwa kujibu maswali ya Joji na kutukimbia, nimethibitisha kwake yaliyojiri.

Joji kwa mshangao:

Je ulikuwa huniamini mimi?

Hapana, ila ni kwa kujiridhisha tu, kwani nilishangazwa na matendo yake, inaelekea kama ulivyosema, hakutaka kasisi Katarina kutoka peke yake.

Katarina alifungua macho yake kwa mshangao…

Kwa nini iwe mimi tu? Nimekuambia wewe kwamba yeye- anatenganisha maneno ya jamii kwa ujumla ambayo wewe ni mmoja wa wanaofaidika nayo, na kati ya maneno maalumu yasiyo jumuisha jamii yote, kwa ujumla….Sitaki kurefusha muda wenu, nadhani safari yenu ni kesho.

Ndio.

Nimekuja kuwaaga, na napenda mawasiliano yaendelee, na mimi nimefurahishwa kuonana na nyinyi.

Na sisi pia… nakushukuru.

Nina ombi, je unaweza kunipa kitabu?

Kwani nimemuomba rafiki yangu na kunieleza kuwa ni hii tu nakala moja alikuwa nayo.

Kwa kiasi hiki, kitabu ni muhimu sana kwako?

Kikao chetu cha siku ile kilinithibitishia kwamba mimi sijui Uislamu isipokuwa ni maneno ya juu juu tu, na ripoti za vyombo vya habari tu, na nimedhamiria kuijua dini hii, na jina la kitabu limenivutia sana.

Nitapanda chumbani na watoto na nitakuletea kitabu….Haya Maiko na Sali tuondoke.

Joji alitabasamu huku akicheka na kusema:

Haa haa, hivyo umekusudia kuusoma Uislamu?

Ndio.

Na je utakuwa Muislamu?

Je unategemea niwe kama Rais Gadhafi rais wa Libya aliyepita mimi nasoma kila fikra bila ubaguzi, na katika kikao kile nimegundua sijui chochote katika Uislamu pamoja na maarifa mengi niliyonayo kuhusu Uislamu lakini yote hayo hayana uhakika.

Mimi sijausoma Uislamu, nitausoma safari zijazo mbeleni, na kwa masikitiko sijakisoma kitabu na nilipenda kukisoma.

Samahani kitabu ni chenu na samahani kwa kukitaka kwa dharura.

Katarina alikuja na kitabu na kumpa John Luke ambaye alitoa karatasi na kalamu na kunukuu baadhi ya maneno ya kitabu kisha kurudisha kitabu kwa kuwashukuru….

Je hutaki kitabu?

Nimechukua tovuti ya kitabu katika mtandao wa kimataifa na hayo yanatosha, asanteni sana.

Joji na Katarina walienda chumbani… na Joji kufungua kompyuta, alikuwa akisubiri majibu ya marafiki zake kuhusiana na barua yake aliyouliza: Kama Paulo ndiye aliyepotosha torati au nani? Kwa mshangao majibu yao yote yalikubaliana kuwa ndie aliyepotosha, lakini njia za majibu yao zilitofautiana … aliandika majibu yote na kuwatumia tena wote…

Habib: Kihistoria… kwa masikitiko ndio. Tom: Ikiwa imepotoshwa sijali ni nani kaipotosha. Adam: Swali tata, sijui nani kapotosha. Levi: Na ni nani aliyeharibu Agano la Kale kama ni hivyo? Huenda ilikuwa ni tatizo katika uandishi na kuchelewa kwake kuandikwa, na sio kusudio ni kupotosha au kuharibu.

Kisha akawaandikia hao:

Sehemu ya nne: je wewe unahamu ya kuusoma Uislamu? Na kwa nini? Nasubiri jibu kwa ufupi samahani … kesho jioni nitakuwa London. Ni mimi Joji – Roma”

Aliwatumia rafiki zake wote, na akaongezea kwa mara nyingine Katarina na John Luke… na akaendelea kufungua email yake na kukuta ujumbe wa Tom:

“Kwa marafiki zangu wote, nahisi ukurasa wangu wa face book umeibiwa na nafanya mashauriano na mtandao kuurejesha tena, na mtanisamehe kwa kasoro yoyote mtakayoiona sio kutoka kwangu. Ni mimi Tom”

Alifungua ukurasa wa Tom na kukuta picha zake akiwa na wanawake wengi wasio jisitiri vizuri, akawa anajiuliza: Je Tom ameanza vita na Baraad? Kisha akakumbuka makala ya Adam kuhusu kubadilika fikra za daktari, na akasema: amesema kweli Adam, nadhani Tom alikuwa na bahati. Joji aliendelea kuangalia picha, na kugundua baada ya muda mfupi kuwa alikuwa akiangalia picha zile za wanawake huku akimtafuta Katarina humo, na akahisi kuwa hiyo ni shaka ambayo sio sehemu yake, wala haimfalii yeye Joji wala Katarina, alifunga Kompyuta nakuelekea kwa Katarina, na kumkuta amejilaza chali kitandani na kumbusu, Katarina alipata hisia za busu na yeye kumbusu Joji na kufungua macho yake na kutabasamu…

Nakupenda.

Na mimi pia nakupenda vile vile, nisogelee.

Siku iliyofuata ilipita kwa haraka sana, na hawakuwa na muda wa kutosha kabla ya muda wa kuelekea uwanja wa ndege, walikwenda sokoni na huko Katarina alimkumbusha Joji zawadi ya Adam. Ambae alitaka mkoba wa kifahari wa ngozi lakini wa bei rahisi sana, kiasi katika mzunguko wao walisimama katika duka la mikoba ya ngozi za asili na walikuwa wana seli ya baadhi ya mikoba, ikawa aina hizo za seli seli zinafikia discount ya asilimia 80 ya bei ya asili, na hivyo akamnunulia Adam mkoba mmoja wa kifahari kwa bei rahisi sana wakatoka hapo dukani wakishangazwa na maombi ya ajabu na bahati waliyopata
kununua.
Baada ya kula chakula cha mchana karibu na soko walilokwenda, walirejea hotelini na kufunga mizigo yao na wakaelekea uwanja wa ndege.