Njia ya furaha ni njia ambayo ndani yake inapelekea kwenye maadili hapana budi kwa mwenye kupita njia hiyo apate njiani mapenzi, usamehevu, ukarimu, haya, amani, kunyenyekea, kuwatanguliza wengine, uadilifu, ukweli na kushauriana; pamoja na yasiyokuwa hayo katika matukufu ya tabia.
Nayo pia ni njia ya kuiweka nafsi juu na matakwa yake kwenye tabia njema za juu na adabu kubwa, maadili mema sio mambo ya anasa ambayo mtu anaweza kuyaacha, bali nafasi yake huja mwanzo kabisa katika misingi ambayo yanasimamia juu yake muelekeo wa maisha, ikiwa maadili ya watu yatakuwa mazuri basi yatageuka kuwa mambo mazuri katika furaha ya maisha yao na maisha ya jamii zao, na ikiwa mbaya wataharibika na kudhalilika wote.
Kwa sababu hiyo Uislamu umefanya pupa kuotesha fadhila katika nafsi za wafuasi wake, na kuwahimiza kushikamana nayo, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ameainisha lengo la mwanzo la kutumwa kwake kwa kauli yake: “Hakika nimetumwa kukamilisha matukufu ya tabia.” (Imepokewa na Al-Baihaqi).
Ni kama kwamba ujumbe wa Uislamu ambao umepanuka na kuenea katika zama na maeneo mengi ili kujenga ustaarabu mkubwa kuliko ambao mwanadamu amewahi kuujua. Mwenye nao akatoa juhudi kubwa katika kufikisha nuru yake na kuwakusanya watu pembezoni mwake.
Haiiti zaidi ya kutengeneza maadili ya mwanadamu na kutakasa ubora wao na kuamsha ukamilifu wa upeo wa macho yao.
Hivyo basi kutumwa kwake (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ilikuwa ni kwa ajili ya maadili na kuyakuza, na kuzitakasa nafsi na kuzitoharisha, watu hapo kabla walikuwa katika upotofu mwingi zaidi ya maadili haya, hawayajui wala hawajali, Allah Aliyetukuka amesema: “Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.” (62:2)
Allah amesema vile vile; “Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu anaye tokana na nyinyi, anakusomeeni Aya zetu na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na hikima na kukufundisheni mliyo kuwa hamyajui.” (2:151).
UHUSIANO WA IMANI NA TABIA NJEMA:
Imani ni nguvu inayomsukuma muumini kwenye mambo mazuri na humzuia na mambo duni na makosa, hivyo udhaifu wa mwendo mwema kuhesabiwa kuwa ni dalili ya udhaifu wa imani, kama ambavyo tabia njema huhesabiwa kuwa ni dalili ya nguvu ya imani ya mtu, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amebainisha kuwa imani yenye nguvu mwishowe huzaa maadili mema ndani yake, na kuwa kuanguka kwa maadili hurejewa kutokana na udhaifu wa imani au kukosekana kwake.
Hivyo asiyekuwa na imani hufanya maovu, hajali chochote kile wala haogopi lawama, wala hadhani kuwa atalipwa kwa uovu wake, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Kwa hakika haya na imani vimeambatanishwa, kimoja iwapo kikiondolewa basi na kingine kitaondolewa hivyo hivyo.” (Al-Baihaqi).
Bali Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amefananisha tabia mbaya unayomfanyia jirani wako ni dalili ya kuzimika kwa imani (kupotea).
Anasema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam); “Wallahi! Haamini, Wallahi haamini, Wallahi Haamini, (Masahaba) wakauliza: Ni nani huyo Ewe Mtume wa Allah, (Mtume akasema:Jirani ambae jirani yake hatasalimika na Bawaiq yake, (Masahaba) wakauliza: Ewe Mtume wa Allah ni nini maana ya Bawaiq yake? (Mtume) akasema: Shari zake.” (Al-Bukhari).
Hivyo basi pindi Allah anapowalingania waja wake katika kheri au kuwakataza shari anafanya hayo katika muktadha wa imani iliyotulia katika mioyo yao na mara ngapi Allah Aliyetukuka amesema katika kitabu chake: “Enyi Mlioamini!”,
kisha baada ya hapo hutaja majukumu yao, mfano kauli yake: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.” (9:119).
Vivyo hivyo tunamuona Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) anapowafundisha sahaba zake maadili mema huunganisha hilo na imani vilevile, mfano wa kauli yake (Swala Llahu ‘alayhi wasallam):
“Atakayekuwa anamuamini Allah na Siku ya Mwisho basi na amkirimu mgeni wake, na mwenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho basi na amuhifadhi jirani yake, na atakaye kuwa anamuamini Allah na Siku ya Mwisho basi na aseme kheri au anyamaze.” (Ahmad).
Hivi ndivyo Uislamu unavyotegemea ukweli wa imani na ukamilifu wake katika kuotesha Fadhila katika nafsi.
Ibada katika Uislamu si kauli zilizofichika au harakati zisizo na maana, bali ni matendo na kauli ambazo zinatakasa nafsi na kufanya maisha yawe mazuri, faradhi katika Uislamu zina lenga katika kumhuisha Muislamu katika maadili mema, na aendelee kushikamana na maadili haya, vyovyote vile hali na mazingira yatakavyobadilika, Qur-aan Tukufu na Sunnah iliotoharika zimetubainisha hakika hizi; kwa mfano Swala ni wajibu ambao lengo lake ni kuondoa maadili mabaya, maovu na munkari, amesema: “SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda.” (29:45)
Zakkah katika Uislamu sio kodi inayochukuliwa kutoka kwa matajiri kwenda kwa masikini tu, bali ni mche unaopanda hisia za wema kwa mtu na upole, na kuimarisha uhusiano na kufahamiana baina ya watu wa tabaka tofauti, mbali na kutoharisha nafsi kutokana na uchafu na aibu, maovu, kujamiiana na kuelekea kwenye kiwango cha juu na heshima katika kuamiliana.
Hiyo ni hekima ya kwanza ya Zakkah, kama alivyosema Allah Aliyetukuka: “Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.”(9:103);
Na kwa ajili hiyo sadaka si kutoa mali, bali inakusanya idadi ya maadili ya juu ambayo yanachangia furaha ya jamii na watu wake, na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akapanua maana ya neno sadaka ambayo yampasa Muislamu afanye juhudi kutoa, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Kumimina kwako ndoo yako katika ndoo ya ndugu yako ni sadaka, na kuamrisha kwako mema na kukataza kwako maovu ni sadaka.” Katika riwaya nyingine: “Na kutabasamu kwako mbele ya uso wa ndugu yako ni sadaka, na kutoa mawe, mwiba na mfupa katika njia za watu ni sadaka, na kumuelekeza mtu aliyepotea njia ni sadaka.” (Al-Baihaqi).
Na funga hali kadhalika, Uislamu hauangalii kuwa ni kujinyima na kula na kunywa tu, bali umezingatia kuwa ni hatua ya kufikia hisia za ndani za mafukara na walionyimwa, na wakati huo huo huielekeza Nafsi na kumiliki matamanio yake, Allah Aliyetukuka amesema: “Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. ” (2:183).
Akasema Mtume: “Ambaye hatoacha maneno machafu na kuyafanyia kazi, basi Allah hana haja ya mtu Yule kuacha chakula chake na kinywaji chake.” (Ahmad)
Na akasema tena: “Funga si kuacha kula na kunywa tu, bali funga kuacha upuuzi na uchafu, ikiwa yoyote atakutukana au akakufanyia ujinga, basi na useme: Mimi nimefunga, mimi nimefunga.” (Ibn Khuzaima).
Ama Hijja, mtu anaweza kudhania kuwa safari tupu (rihla) kwa maana ya kimaumbile; kwa yaliyomo ndani yake katika ibada za ghaib, na hili ni kosa; ambapo Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) anazungumzia kuhusu ibada hii; “Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!” (2:197),
Na yote yaliyotangulia hubainisha umadhubuti wa uhusiano kati ya dini na tabia njema kwa hiyo, nguzo muhimu za Kiislamu kama vile Swala, Saumu, Zakah, Hijja, na utiifu mwingine katika Uislamu.
Zote hizo ni njia zenye kumfikisha mtu kwenye ukamilifu wa utu unaolengwa kumnyanyua mtu katika maisha mazuri ambapo ataneemeka kwa furaha na utulivu katika kivuli cha maadili mema na misingi mitukufu, kwa kuwa hizo ni ibada zenye kutofautiana katika matendo na mandhari yake. Lakini zote hizo zinakutana katika malengo aliyoyaweka Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) katika kauli yake: “Nimetumwa kukamilisha matukufu ya tabia.” (Baihaq); Hivyo basi njia ya furaha ni njia inayojikita kwenye maadili inazunguka kwenye sayari yake wala ndani yake maadili hayajitengi kabisa na ibada.
Njia ya furaha misingi yake ya kisheria, kimaadili na kiakida inasimama katika msingi wa maadili katika kila kitu, kuanzia kwenye kumfanyia adabu Allah Ta’ala, kupitia kwenye tabia na kuifanyia adabu nafsi, pamoja na marafiki, jamaa, ndugu na majirani, tabia njema pamoja na adui na hata kwenye vita, hadi (adabu) pamoja na wanyama na viumbe wengine, bali tabia njema pamoja na mazingira, miti na mimea, yote hayo yanakusanywa kwenye tabia njema katika mazungumzo, tabia njema katika matendo, tabia njema katika nyoyo na fahamu; Allah Aliyetukuka anasema akithibitisha misingi ya tabia njema katika mazungumzo: “…na semeni na watu kwa wema…” (2:83)
Na akizungumzia asili ya misingi katika maadili mema ya kimatendo Anasema: “Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo.” (23:96),
Na mwenye kuchunguza kitabu cha Allah atakuta kumejaa maamrisho ya tabia, zingatieni aya hizi zifuatazo, Allah Aliyetukuka amesema: “Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? ” (55:60),
Na akasema Aliyetukuka: “…Wala msisahau fadhila baina yenu…” (2:237),
Na akasema tena Aliyetukuka: “…Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza.” (12:18),
Na akasema tena Allah: “…Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri.” (15:85),
Na akasema tena Aliyetukuka: “Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili. ” (7:199),
Na tena: “Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga.” (28:55)
Na, “Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.” (41:34).
Tabia yake (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) ilikuwa ni Qur-aan, na vipi tabia yake isiwe hivyo wakati Allah Ta’ala akimsifu katika kauli yake: “Na hakika wewe una tabia tukufu. ”(68:4);
Kwa ajili hiyo ametumwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kwa ujumbe ambao umeweka maadili mema katika nafasi ya juu ambayo haijawekwa na wengine, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Ukamilifu wa waumini kwa imani ni ukamilifu wao wa tabia njema, na mbora wao ni mbora kwa wanawake wake.” (Baihaqi).
Na akasema tena (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) :
“Wema ni tabia njema, na dhambi ni kile chenye kuwasha kifuani mwako, na ukachukia watu kukiona.” (Muslim).
Kadhalika amesema:
“Kwa hakika uchafu na kujichafua havimo katika Uislamu kwa vyovyote vile, na mbora wa watu katika Uislamu ni mbora wao kwa tabia.” (Ahmad).
Katika hadithi nyingine amesema: “Hakuna kitu kizito katika mizani ya muumini Siku ya Kiama kuliko tabia njema, na ya kuwa Allah humchukia muovu mchafu.” (Baihaqi).
Na amesema tena:
“Hakika Mpendwa wenu zaidi kwangu ni wa karibu yenu zaidi kwangu ni mzuri wenu zaidi wa tabia, na ninayemchukia miongoni mwenu na aliye mbali nami zaidi miongoni mwenu akhera ni mbaya wenu na mwenye maneno mengi, wenye kujikalifisha katika mazungumzo, na wenye kujaza vinywa vyao maneno kwa kiburi.” (Ahmad)
KUMFANYIA ALLAH TABIA NJEMA:
Kumfanyia Allah tabia njema inakusanya mambo matatu:-
Kwanza: Kumuamini na kupokea habari zake kwa kuziamini; Allah Aliyetukuka amesema kuhusu nafsi yake: “Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Kwa yakini atakukusanyeni Siku ya Kiyama. Halina shaka hilo. Na ni nani msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu?” (4:87),
Kukubali maneno ya Allah kunampelekea mtu kumuamini Yeye, kumtetea, na kufanya jihadi katika njia yake, kiasi cha kutoingia shaka katika nafsi yake au utata katika habari zake Allah Aliyetukuka au habari za Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam).
Pili: Ni mtu kupokea hukumu za Allah kwa kuzikubali na kuzitekeleza, kwa hiyo hakatai chochote katika hukumu za Allah, na akikataa chochote katika hukumu za Allah basi huo ni ukosefu wa adabu kwa Allah Aliyetukuka; ndio maana Allah amekataza kutanguliza rai yetu au matamanio yetu juu ya maneno yake, Allah Aliyetukuka amesema: “Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (49:1).
Tatu: Kupokea Kudura za Allah kwa kuridhika na kusubiri, kwani tabia njema kwa Allah kwenye kudura zake ni mwanadamu kuridhia, kujisalimisha na kutulia kwa ajili ya kudura za Allah na hukumu zake; kwa ajili hii Allah amewasifu wenye kusubiri. Amesema: “Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” (2:156).
TABIA NJEMA PAMOJA NA WATU:
Allah ameamrisha kila mtu afanyiwe wema, na haswa wazazi wawili, na ndugu wa karibu, nao ni ndugu wa nasaba ambao inapasa kuwaunga, na majirani, Allah Aliyetukuka amesema: “Na tulipo funga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na semeni na watu kwa wema, na shikeni Sala, na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipo kuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza.” (2:83)
Na akasema tena, “Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao.” (2:177),
Na kadhalika katika aya zifuatazo: “Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.” (2:215),
Na, “Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema. Na watakao amini baadaye na wakahajiri, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni katika nyinyi. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.” (8:74-75),
Na, “Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri” (4:36)
Vile vile amesema Aliyetukuka: “Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.” (16:90),
Na, “Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni. Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanao tubia kwake. Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet’ani. Na Shet’ani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi. Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema nao maneno laini. ” (17:23-28),
Na akasema Aliyetukuka: “Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa.” (30:38),
Na, “Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.” (4:1)
Na akasema vile vile : “Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?” (47:22)
Na, “Je! Anaye jua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Wenye akili ndio wanao zingatia, Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji maagano. Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya. Na ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya Akhera. Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na walio wema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera. Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.” (13:19-25).
Maadili mema katika Uislamu hayahusiani na rafiki jamaa wa karibu na jirani tu, bali inawavuka hao hadi kufika kwenye tabia njema pamoja na adui, hata ikiwa adui huyo ni anaepigana vita nawe! Maadili haya humuenea kila mtu, Allah Aliyetukuka amesema: “Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.” (41:34),
Allah ameamrisha kuwafanyia uadui wale ambao wanatupiga vita nao, amesema Ta’ala: “Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.” (2:190),
Angalia maadili ya Kiislamu pamoja na adui anayepigana nasi, katika amri zake (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) pamoja na jeshi lake linalotoka kwa ajili ya kupigana jihadi katika njia ya Allah kupigana na adui; amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam):
“Msifanyiane hila, wala msipetuke mipaka, wala msiue kwa kutesa, wala msiuwe watoto wala watu wa mahekalu (wasiojishughulisha na vita).” (Ahmad).
Ajabu amri ya dini hii yenye kuamrisha maadili haya pamoja na maadui wanaotupiga vita, ama asiyekuwa mpiganaji (hata kama ni adui) Allah ameamrisha wafanyiwe wema na uadilifu, Allah Ta’ala amesema: “Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” (60:8)
TABIA NJEMA PAMOJA NA WANYAMA:
Uislamu umeleta tabia njema hadi kwa wanyama, kwa sababu Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Mwanamke aliadhibiwa juu ya paka, alimfunga hadi akafa, kwa sababu hiyo akaingia motoni, hakumlisha wala kumywesha alipomfunga, wala hakumuacha ale katika majani ya ardhi.” (Imepokewa na Al-Bukhari).
Bali Allah amewajibisha kufanyiwa wema hata katika kuchinjwa wanyama, amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Hakika Allah ameamrisha wema katika kila kitu, mkiua ueni vizuri na mkichinja chinjeni vizuri, na mmoja wenu anoe kisu chake, na akipe raha kichinjo chake.” (Imepokewa na Muslim).
TABIA NJEMA PAMOJA NA MAZINGIRA:
Pia Uislamu umeleta adabu hata pamoja na mazingira na mandhari yote; hivyo unalingania kutofanya ubadhirifu; na hivyo kutoharibu vyanzo vya asili, Allah Ta’ala amesema: “….Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.” (2:60)
Na akasema tena Aliyetukuka: “Wala msit’ii amri za walio pindukia mipaka, Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi.” (26:151-152),
Kadhalika vyanzo vingine vya asili kama vile maji na mfano wake ambao Uislamu umeupa nafasi kubwa, Allah Ta’laa amesema: “Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?” (21:30)
Na akasema vile vile: “Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika katika hayo imo Ishara kwa watu wanao sikia.” (16:65).
Mbali na Qur-aan Tukufu, Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amehimiza umuhimu wa kulinda mazingira na vilivyomo ambapo tunaona katika Sunnah yake lingano linalokaririwa mara kwa mara la kuhifadhi mazingira; hivyo basi kuweka mipaka katika kulinda mazingira mfano: mmomonyoko wa ardhi, ukame na kuzuia kupanuka kwa majangwa; na mfano wa hayo Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Epukeni vitatu vyenye kulaani: kujisaidia kwenye mapito ya maji na katikati ya njia, na kivuli.” (Imepokewa na Abu Dawuud).
Amesema tena Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam):
“Hakuna Muislamu yoyote anapanda mmea au anaotesha mche, akala kwenye huo ndege au mwanadamu au mnyama, ila hiyo itakuwa ni sadaka yake.” (Imepokewa Muslim).
Katika hadithi nyingine Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Kitakaposimama kiama na mmoja wenu akawa na mmea akiweza kabla ya kiama kusimama na kuupanda basi na afanye.” (Imepokewa na Ahmad).
Wakati mmoja Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alipita na Sa’ad alikuwa akitawadha; Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema:
“Ni Israfu gani hii? (Sa’ad) akasema: Je, katika udhu kuna Israfu?! (Mtume) akasema: Ndio na hata ingekuwa katika mto unaotembea.” (Imepokewa na Ibn Majah).
Na haya ndio waliyoyafanya wenyewe katika kutendea wema mazingira hata katikati ya vita dhidi ya adui yao, Abu Bakr (Radhiya Llahu ‘anhu) alimuusia jemedari wa vita kwa kumwambia: “Msiue watoto, wala mwanamke, wala mzee, wala msikate mti wenye matunda, wala msichinje mbuzi au ng’ombe ila kwa ajili ya kula wala msivunje jengo wala msikate mtende wala msichome moto.” (Imepokewa na Malik).
Tunapendelea hapa kuonesha idadi ya wasia wa kimaadili zilizokuja katika kitabu cha Allah na Sunnah ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) miongoni mwa hizo ni:
Kutoka katika Qur-aan Tukufu;
Allah amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (4:58)
Na akasema tena Aliyetukuka: “Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka. Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” (6:151-153)
Tena akasema: “Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wanao fanya mema.” (7:56),
Akasema Aliyetukuka: “Na subiri, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanao fanya wema.” (11:115),
Akasema Aliyetukuka: “Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi. Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona. Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa. Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa. Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa. Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na khatimaye ndio bora. Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa. Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima. Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi. Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa.” (17:29-39),
Na akasema Aliyetukuka: “Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu, Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema” (3:133-134)
Na kadhalika akasema Aliyetukuka: “Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu. Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” (49:11-13).
Na akasema Aliyetukuka: “Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna na kujifakhirisha. Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda.” (31:17-19).
Na akasema tena: “Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!” (25:63),
Na akasema tena Aliyetukuka: “Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri” (4:36)
Na, “Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.” (3:159).
KUTOKA KATIKA SUNNAH TUKUFU
Tukienda katika bustani ya hadithi tukufu za Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) tunapata kuwa ndani yake kuna miti mingi ya imani ambayo tunaweza kuchuma ndani yake kwenye matunda yaliyoiva ya maadili, mema na misingi bora, katika hiyo:
-Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Ameharamishwa motoni kila mnyonge, laini, mwepesi aliyekaribu na watu.” (Al-Tirmidhi).
-Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alimwambia mmoja wa maswahaba zake:
“Hakika ndani yako kuna tabia tukufu na upole na usubirifu.” (Ahmad).
Na akasema vile vile: “Kheri yoyote nilionayo sitoihifadhi dhidi yenu, (yaani kuwa nyinyi kwa nyinyi), na mwenye kujizuia (kuomba) Allah atamzuia, na mwenye kujihifadhi Allah atamtosheleza na mwenye kusubiri Allah atamsubirisha, na hakupewa yoyote kitu cha kheri na kikunjufu zaidi kuliko subira.” (Imepokewa na Muslim). Na akasema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Utajiri sio wingi wa mali, bali utajiri ni utajiri wa nafsi.” (Al-Bukhari).
Na akasema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Mkali sio kwa kukabana (na watu), lakini mkali ni ambaye anamiliki nafsi yake wakati wa ghadhabu.” (Al-Bukhari). Na akasema (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Hamshukuru Allah asiyewashukuru watu.” (Ahmad).
Katika hadithi zingine amesema: “Hakika Allah ameniteremshia wahyi kuwa muwe wapole, wala baadhi yenu wasiwadhulumu wengine.” (Imepokewa na Ibn Majah).
Akasema: “Kila jema ni sadaka, na miongoni mwa mema ni kukutana na nduguyo kwa uso mkunjufu, na kumimina kwenye ndoo yako katika ndoo ya nduguyo.” (Imepokewa na Al-Tirmidhi).
Mwishowe utaona kuwa uhusiano baina ya furaha ya kweli na tabia njema na uhusiano madhubuti ulioshikamana na kuambatana vizuri; hivyo basi tabia njema ni chanzo pekee cha furaha ya mwanadamu na bila hiyo hakuna furaha, na mwanadamu hatochuma katika maisha yake isipokuwa maovu na matarajio mabaya, hivyo basi furaha ni kichocheo muhimu kwa mwanadamu kuelekea kwenye tabia njema kwa sababu anajua kwa elimu ya yakini kuwa bila ya tabia njema hatofanikiwa furaha ya kweli na siku yenye furaha.