Akiwa katika hali ya uchangamfu Rashidi aliwakabili rafiki zake na kitabu huku akiwa amebeba laptop yake…. Alipowakaribia aliwasalimu haraka haraka wala hakusubiri majibu yao kisha akawaanza kwa kusema:
Leo hii nitaanza kwa kuitikia wito na hamu ya rafiki yangu Maiko…nipo tayari kuwaelezea misingi muhimu ya Uislamu, hawatofautiani wawili kwa misingi hii nayo ni: Imani kwa Mtume wa Uislamu….Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) nimewaletea kitabu cha mwana fikra wa Kimagharibi ambaye anamzungumzia Muhammad..sikilizeni anachosema …
Maiko: Pole pole rafiki yangu Rashidi…Nilikuwa nadhani kuwa kitu muhimu zaidi hususan katika Uislamu ni taswira yake kuhusu Mungu.
Rashidi: Hili ni kweli katika ujumla wake…hata hivyo umepetuka mpaka kwa sababu kadhaa, muhimu zaidi katika sababu hizo ni:
Uislamu kwa sifa yake ni Ujumbe wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) mtu asidai wala asidhanie kuwa taswira ya Uungu ni taswira iliyozuliwa na Mtume wa Uislamu, bali ni dini ya manabii na mitume tokea Adam hadi Masihi hadi kufika kwa Mtume Muhammad (amani kwao wote), bali ni asili ya dini ya wanadamu wote…na kilichotokea ni kuwa wanadamu walipotoka dhidi ya dini hii na wakapotosha taswira hii, ukaja Uislamu na kurejesha usahihi wa imani kwa Mwenyezi Mungu na kuwalingania watu wote kurejea katika upekee (tawhidi) wa Allah Mtukufu na kutomshirikisha kwenye ibada yake…Hivyo basi kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha katika Uislamu ni mfumo wa mnyororo uliyoendelea kupitia historia tokea alipoumbwa mwanadamu wala haiishii kwa kuondoka dunia…ni dini iliyopatikana kabla ya kuzaliwa kwa Mtume wa Uislamu.
Jambo la pili: Nilidhani kuwa tumeafikiana kwa hilo katika vikao vyetu vilivyopita, kwamba inatosheleza kuvuka nukta hii.
Rajev: Je unakusudia kuwa katika Uislamu sifa ya mungu wa kweli ipo?
Rashidi: Naam, hii ni sahihi kabisa!
Rajev: Hivyo basi, ni vizuri ututajie kwa ufupi taswira ya Uislamu kuhusu Uungu kabla ya kuhamia kwenye yale uliokuwa unataka kutuelezea.
Rashidi: Vizuri…katika Uislamu mungu ni mmoja aliyemuumba mwanadamu na aliyeumba ulimwengu, hafanani na chochote katika ulimwengu, yeye ndie aliyeweka kanuni za kimaumbile na akaweka kila kitu kwa kipimo chake na kanuni zake, yeye ni mtukufu wa kila kitu na mkubwa wa kila kitu, na yuko juu ya kila kitu.
Hafanani na yeyote katika dhati yake, sifa zake na matendo yake, ana ukamilifu wote wala hazukiwi na upungufu katika sura yeyote ile, yeye ni mtukufu hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hafanani na yeyote na hana mshirika na ni pekee ambaye anahuisha na anafisha.
Huyu ni Mola ni Mungu Peke Yake ambae hapaswi kuabudiwa asiyekuwa yeye, hana mshirika katika ufalme wake wala hana msaidizi, wala waziri, wala mshauri anayeabudiwa pamoja nae, wala hana wa kati aliye karibu nae zaidi, na anayeweza kufanya maombezi bila ya idhini yake, ibada ni halisi kwake peke yake tu kwa mambo yake yote.
Maiko: Kitabu ulichokuja nacho kinazungumzia nini?
Rashidi: Kinazungumzia Watukufu katika historia ya mwanadamu, cha mwandishi Dr. Michael Hart, nae ni mwanazuoni wa nyota, sayari na mahesabu ambaye anafanya kazi katika taasisi ya anga ya Marekani.
Maiko: Anahusika vipi katika masomo ya historia?!
Rashidi: Masomo na tafiti za historia huchukuliwa kuwa ni starehe na hamu za watu leo hii duniani, nae ameona kuwa miongoni mwa makumi ya maelfu ya mamilioni ya watu, vitabu vya historia havikumtaja isipokuwa watu ishirini elfu tu, hivyo akaweka vigezo na misingi kadhaa kwa kumchagua mbora wao zaidi katika watu wote hao, misingi hiyo muhimu ilikuwa:- Awe ni mtu wa kweli aliyeishi na isiwe ni ngano tu za kusimuliwa au mtu asiyefahamika, awe na athari kubwa, ni sawa sawa iwe athari hii ni nzuri au mbaya, na athari hii iwe ni ya kilimwengu na ienee katika historia ya wanadamu…nazo ni misingi mizuri kwa maudhui yetu.
Rajev: Ni mtu gani huyo mtukufu wa maoni ya mwandishi huyu?!
Rashidi: Mwandishi huyu amemchagua Muhammad, Mtume wa Waislamu kuwa juu kileleni kati ya watu mia moja aliowachagua, na uchaguzi wake huu sababu zake alizobainisha ni:-
Kisha Rashid akafungua kitabu na kuanza kusoma:-
“Nimemchagua Muhammad katika orodha hii na watu wengi watashangazwa na chaguo hili, na wana haki katika hilo, hata hivyo Muhammad ndie mwanadamu pekee katika historia aliyefanikiwa mafanikio makubwa zaidi kwa viwango vyote katika dini na katika dunia.
Yeye aliita watu katika Uislamu na akausambaza kama dini kubwa zaidi, na akawa ndio kiongozi wa kisiasa, kijeshi na kidini…na baada ya karne kumi na ya kifo chake, hiyo athari ya Muhammad ilibaki kuwa yenye nguvu mpya.”
“……na inaelekea ni kitu kigeni Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kuwa kileleni pamoja na kuwa katika orodha ile idadi ya Wakristo likuwa kubwa sana kulinganisha na idadi ya Waislamu na huenda ilionekana kuwa ni jambo geni kuwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kuwa namba moja katika orodha hii wakati ambapo Issa (‘Alayhi salaam) ni namba tatu na Musa ni wa kumi na sita.
Hata hivyo hilo lina sababu zake: Miongoni mwazo ni: Dini ya Muhammad ilikuwa ni kubwa na ya hatari zaidi katika kueneza Uislamu na kusimamisha misingi ya sheria yake kuliko ilivyo kwa Issa katika Ukristo. Pamoja na kuwa Issa ndie muhusika wa misingi ya maadili katika Ukristo, isipokuwa Paulo ndie ambae amesimamisha misingi ya sheria ya Ukristo, nae vile vile ndie muhusika wa maandishi mengi yaliyokuja katika Agano Jipya.
Ama Mtume Muhammad yeye ni muhusika namba moja na ni pekee aliyeweka misingi ya Uislamu, sheria na tabia za kijamii na kimaadili na misingi ya muamala kati ya watu katika maisha yao ya kidini na ya kidunia. Kama ambavyo Qur’an imeteremka kwake peke yake, na katika Qur’an Waislamu wanapata wanachohitaji katika dunia yao na akhera yao. Je, mnashangaa maneno haya?!
Rajev: Maneno yanayostahiki kutulia ndani yake, lakini niruhusu niseme: Mwandishi huyu hahusiki na tafiti za wanadamu.
Rashidi: Hata kama hahusiki katika tafiti za maisha ya watu lakini maneno yake yanakinaisha na yamejengwa katika misingi ya uwazi, wala hamna utata wowote katika kuegemea na kumpendelea Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam), Yeye ni Myahudi, na kama utahitaji ushahidi wa watu wengine niache nikuelezee baadhi yake…
Kisha Rashidi akatoa laptop yake akaanza kusoma baadhi ya faili alizo nazo na kusema:
Angalia bwana:
Anasema mshairi wa Kifaransa La Martine: “Ni mtu gani aliyediriki utukufu wa mwanadamu kama alivyodiriki Muhammad? ni mwanadamu yupi ambae amefikia ukamilifu kama alivyofikia Muhammad? Mtume Muhammad alivunja itikadi potofu ambazo zilifanywa watu kiunganishi baina ya Muumba na Muumbwa.”
Na mshairi wa Ujerumani wa kwanza, Goethe, anasema: “Nimechunguza katika historia kuhusu vigezo vya juu vya mwanadamu, nikavipata kwa Nabii Muarabu, Muhammad.
Mwanafasihi na mwanafalsa wa Kirusi na ulimwenguni, Testow: “Mimi ni mmoja katika waliofurahishwa na Muhammad aliyechaguliwa na Mungu mmoja ili awe mwisho wa ujumbe kutoka kwake, na yeye vile vile awe ni nabii wa mwisho.”
Ama mwandishi na mwanafikra wa Ki-Ireland, mashuhuri aliyekataa zawadi ya Nobel katika fasihi, George Bernard Shaw anasema: “Nimesoma maisha ya Mtume wa Uislamu vizuri mara nyingi, na sikupata ndani yake isipokuwa maadili kama yanavyofaa kuwa ni kwa kiasi gani nimetamani Uislamu kuwa ndio njia ya ulimwengu. Nimemsoma Muhammad nikamzingatia kuwa ni mtu wa ajabu, nikamuona kuwa, yuko mbali na ugomvi wa Masihi (‘Alayhi salaam), bali alipasa kuitwa muokozi wa wanadamu.
Maiko: Mazungumzo haya yanazunguka katika utukufu wa Muhammad, lakini kitu gani kinachothibitisha kuwa Muhammad ni Mtume wa Mungu?
Rashidi: Sikiliza ewe rafiki yangu anachosema mwanazuoni wa dini wa uswisi, Dr. Hanz Kin: “Muhammad ni nabii wa kweli kwa maana ya neno, wala hatuwezi kukanusha kuwa Muhammad ndie kiongozi na mshauri katika njia ya uokozi.”
Kuna dalili nyingi zenye kuthibitisha kuwa Muhammad ni Mtume wa kweli wa Allah.
Maiko: Ikiwa umeshatayarisha basi tuelezee, au kwa uchache wake.
Rashidi akiendelea kufungua baadhi ya mafaili kwenye kompyuta yake, kisha akasema:-
Katika uthibitisho wa ukweli wa Mtume: Ni vitabu vya mbinguni kunatabiri; katika kumbukumbu la Torati, Mungu anamwambia Musa: 18:15-30: “BWANA, Mungu wako, atakuondoshea nabii miongoni mwa ndugu zake kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Na kilicho maarufu ni kwamba ndugu wa Bani Israil ni Bani Ismail (yaani Waarabu), kama ambavyo mfanano kati ya Musa na Muhammad ni mwingi kuliko Mtume mwingine yeyote, na ibara “Nitamuwekea maneno yangu mdomoni mwake.” Ni ishara ya kutojua kusoma yaliyoandikwa kwa Mtume wa Uislamu.
Katika Injili ya Yohana Mtakatifu 14:15 “Masihi anawaambia wanafunzi wake: “Mimi naondoka, atakuja PERIQLYTOS, roho ya kweli; hazungumzi ya kwake mwenyewe, lakini yeye kama isemavyo, naye ananishuhudia mimi na nyie mnashuhudia; kwani mlikuwa nami.” asili ya neno PERIQLYTOS ni la kiyunani lenye maana himidi lenye maana la Ahmad au Al-Hamid au mwenye kushukuru sana nalo ni jina la kiarabu la Mtume Muhammad”
Katika dalili zingine vile vile: kumjulisha yasiyoonekana (Ghaibu), bali hata vipengele vyake vya ndani, na kumjulisha kuhusu mwisho katika mwanzo, na muujiza wa kisayansi wa ujumbe wake, na hukumu za kisheria.
Maiko: wapi? Yako wapi yote hayo?! Tupe mifano.
Rashidi: Yapo mengi kwenye Qur’an, kitabu alichoteremshiwa Muhammad, na ndio muujiza wake mkubwa.
Rajev: Kama ni hivyo, ni muhimu kuijua Qur’an hii kutokana nayo tutajua ukweli wa Mtume wenu, na tutaweza kujua misingi ya dini hii.
Rashidi: Ni kweli, na hili ndilo ambalo nataka kulipendekeza kwenu kuwa tuakhirishe hili hadi kikao kijacho.
Maiko: Kabla ya kuondoka nataka kujua: Kitabu hicho nitakipata wapi?
Rashidi: Kitabu ninacho kwa muda mrefu, lakini nimeona chapa mpya iliyotolewa hivi karibuni katika duka la vitabu karibu na tulipofikia, tunaweza kutembelea duka hilo kabla ya kikao chetu kijacho….