Rajev na Rashidi walimtangulia Maiko kungia katika chumba cha mjadala, mazungumzo kati yao yakaanza kwa Rajev kumwambia Rashidi,
Kuna jambo nataka kulizungumzia na ningependa kujua taswira ya Uislamu; kwa kuwepo uhusiano wa jambo hili na taswira hii.
Rashidi: Tafadhali, zungumza.
Rajev: Katika nchi yetu (India) kuna tabaka linaloitwa Untouchables
na leo hii wanaitwa Harijans au (watoto wa Mungu), na jina hili liliitwa na kiongozi mashuhuri wa India Mahatma Ghandi..pamoja na kuwa serikali ya India ilitoa tahadhari ya matumizi ya neno untouchables mwaka 1949 isipokuwa hilo liliendelea vijijini na miji midogo huko India.
Rashidi: Lakini nini tatizo la kutengwa huku?
Rajev: Sio tatizo, ni balaa kubwa…..balaa la wanadamu liko wazi katika kumwaga haki za binadamu katika sura mbaya za dhulma.
Maiko nae anaingia na kuwasalimia wenzake.
Rashidi: Karibu Maiko, Rajev ameanza mazungumzo muda si mrefu, utaweza kufahamu maudhui yenyewe pindi Rajev atakapokamilisha mazungumzo yake – Rajev karibu endelea.
Rajev: Hili linatokana na mgawanyo wa kitabaka kulingana na dini ya Uhindu, tabaka la juu zaidi ni: Brahmins, na kulingana na itikadi yao ni wale walioumbwa na mdomo wa Mungu: Katika tabaka hili kuna mwalimu, kuhani, kadhi/hakimu, kisha linafuatiwa na tabaka la Kshatriyas, hawa wameumbwa na mkono wa Mungu, wanasoma na hutoa dhabihu na hubeba silaha kujinda, na wakifuatiwa na tabaka la Vaishyas, hawa ni wale walioumbwa na Mungu kwa mapaja yake hawa ni wakulima, wafanya biashara na hukusanya mali na ndio wenye kutoa kwa kuendesha vyuo vya kidini, mwisho wa matabaka haya ni Shudras, nao ni wale walioumbwa na Mungu kwa miguu yake, nao ni wenye asili ya weusi, ambao ndio tabaka la waliotengwa (untouchables), na kazi zao zipo katika kuhudumia tabaka zingine tukufu, na kazi zao ni zile za kudharauliwa.
Rashidi: Nimekufahamu ulichokusudia.
Rajev: Samahani, bado hujafahamu.
Maiko: Je kuna yaliyo mabaya zaidi ya hayo? na je, mgawanyo huu bado upo?
Rajev: Ndio, nimemueleza Rashidi kuwa muamala wa waliotengwa kwa mgawanyo huu bado upo katika maeneo ya vijijini, na kuna matendo ambayo huwezi kudhania yanayofanywa dhidi ya tabaka hili; kanuni za Kihindu za Manu ambazo ziliwekwa katika karne ya tatu C.E. zimejengwa juu ya kudharau tabaka la Shudra na waliotengwa; miongoni mwao ni: Kuwa mtu ambae atamfundisha Shudra mambo ya dini basi mtu huyo ataingia Jahanamu pamoja na Shudra.
Na ya kuwa waliotengwa waishi mbali na vijiji, wala wasitumie vyombo visivyovunjika, wala hawana haki ya kumiliki chochote zaidi ya mbwa na punda, na asivae isipokuwa nguo za wafu, na watembee peku peku, mapambo ya wanawake wao yawe ya chuma, na mahusiano yao yote yawe kati yao tu, na waoane wao kwa wao, na kanuni ambazo bado zinatawala jamii ya Wahindu zinasema kuwa, Shudra yeyote anapozungumzia mambo ya dini basi na amwagiwe mafuta ya moto mdomoni mwake!! Bali zaidi ya hilo ni kuwa, huko vijijini bado walitengwa na wamekatazwa kutoka majumbani mwao kabla ya saa tatu asubuhi na baada ya tisa mchana; kwani kivuli chao kinakuwa kirefu muda huo, na Brahma wanaogopa kivuli cha waliotengwa kisije kuwa najisi na Brahma hawawezi kula chakula hadi wajisafishe na najisi ya waliotengwa!!
Maiko: Haiwezekani! Hili linatokea katika zama zetu?! Ni asilimia ngapi ya watu hawa katika jamii ya India?
Rajev: Waliotengwa ni asilimia 45 ya wakazi wa India, yaani asilimia 80 ya Wahindu, wakati ambapo matabaka mengine matatu yote ni asilimia 11 tu ya Wahindu.
Rashidi: Lakini umesema kuwa serikali ya India imepiga marufuku tokea mwishoni mwa miaka ya arobaini, karne iliyopita kutumia wasifu huu wa waliotengwa, hapana budi hilo kuwa la kisheria.
Rajev: Hili ni kweli, lakini tatizo linajificha katika fundo la nasaba safi na nasaba isiyokuwa safi, na tofauti ya watu ipo katika msingi huu, na huu ni msingi muhimu katika dini ya Uhindu; ambapo wanamuona asiyekuwa Mhindu na asiyekuwa katika tabaka tatu za juu kuwa ni mwanadamu mchafu.
Rashidi: Ni mfumo uliosimama juu ya dhuluma na kudhalilisha ubinadamu wa mtu, kubagua katika misingi ambayo mwanadamu mwenyewe hana mkono na mamlaka, hata hivyo ni uhusiano gani uliopo kwa uliyoyataja na taswira ya Uislamu?
Rajev: Uhusiano wake ni kuwa, wengi katika waliotengwa wanabadilika kuwa Waislamu na haswa kabla ya marufuku ile haijatolewa. Pamoja na kuwa waliishi wakati wa ukoloni wa Mwingereza ambapo jitihada za kuutangaza ukiristo kutoka kwao zilikuwa kubwa.
Rashidi: Huenda hilo linarejea kwa jinsi walivyouona Uislamu unavyoheshimu watu, kwani mwenye kuutambua ukweli wa Uislamu na haki za binadamu zilizo ndani yake, na usawa wake kati ya mkubwa na mdogo, na tajiri na masikini, na uhuru aliopewa mwanadamu, hapana budi aelekee kwenye dini hii na aingie…..nadhani waliliona hilo ndani ya kuishi kwao na Waislamu.
Maiko: Unataka kutuambia kuwa Uislamu unaheshimu uhuru wa watu na haki zao?....Uhuru na haki za binaadamu hazikufahamika kupitia dini bali zimewekwa na wanafalsafa na wanafikra wa Kimagharibi, wakapokwa na mataifa mengine katika mapigano mengi waliopigana dhidi ya dhuluma na kuvunjiwa haki zao na kupokwa uhuru wao…haki hizi hazipatikani kwenye Uislamu, uko wapi uhuru wa itikadi na haki ya kutoka katika dini ndani ya Uislamu? Uko wapi uhuru wa kujieleza na kusema? Wapi haki za wanawake?...isije ikawa imani yako kali kwa dini yako inakupelekea kuficha ukweli.
Rashidi: Umefungua mlango mpana katika masjala ya kifikra ewe rafiki yangu…nakuona unazungumza kwa lugha ya ushindi, kama kwamba Magharibi imekuwa ni kinara wa haki za binadamu… ikiwa Magharibi imefikia hali hii, unafasiri vipi hukumu nyingi zilizowaangukia wanafikra, waandishi na wanahistoria, kwa sababu tu walieleza rai zao.’ Kwa kutia shaka Holocust (Mayahudi kuunguzwa na manazi) wakikataa kutokea kwake au wakipunguza idadi ya wahanga wake. Je! huku hakukuwa kuvunja haki na kuwazuia watu kupata habari, matokeo ya utafiti, na uhuru wa fikra na kujieleza?! Je, kuna anayeweza kutekeleza haki yake katika kuasisi chama cha Republic katika Uingereza ya Malkia, au chama cha Nazi Ujerumani? .bali, je mtu kama mimi Muislamu ninaweza kuoa mke wa pili rasmi huku Uingereza? Pamoja na kuwa dini yangu inanipa haki hiyo, je, tawala hazitoingilia kuzuia haki hizi na kuninyima uhuru huu.
Maiko: Uhuru huu na haki hizi zinapingana kabisa na haki za wanadamu, haki hizi zimeshafinyangwa na kuwekwa katika sura za kanuni na sheria na hivi sasa yapasa watu wote kuziheshimu, shaka ya kuunguzwa (holocust) ni uadui dhidi ya Usemitiki nao ni ubaguzi kwa lengo la kueneza chuki, kama ni kinyume cha udugu na usawa nazo ni ‘tuli’ na ‘matukufu’ hatuwezi kwenda kinyume nayo hata kama uhuru mwingine wowote utazuiwa na kufungwa, na ndio hili hili la kukataza kuanzisha vyama ulivyotaja katika nchi hizo, kama ambavyo ndoa yako ya mwingine haingii chini ya haki katika (uhuru wa kuitakidi); kwa kuwa imetoka katika mipaka (mapenzi na dhamira ya mtu), na kwa sababu katika hilo ni kuvunja sheria na mkataba wa jamii wanayoishi, na ndani yake kuna uadui wa haki za wengine (mwanamke, hata kama atakuwa ameridhia), lakini wakati huo huo: imehalalishwa kwako kuishi na wanawake wengine nje ya mipaka ya kuwa ni mke, madamu hilo litakuwa ni kwa ridhaa yao.
Rashidi: Vizuri sana… Hivyo basi ninayoyaona mimi kuwa ni dhuluma na kunyimwa haki na uhuru wangu, wewe unaona kuwa ni udhibiti, na mfumo hakuna dhuluma ndani yake, na hilo ndilo haswa wafanyalo watu wa dini ya Uhindu ambao rafiki yetu Rajev ametuelezea, matendo ambayo yametuchafua sote, Je nao wanaona kuwa wanavunja haki za wengine? Bila shaka hulioni hilo.
Rajev: Ni Kana kwamba maneno yako yanaonyesha kuwa wao wana haki katika matendo yao na ubaguzi wao wa kitabaka unao chukiza.
Rashidi: Hapana kabisa… lakini kusudio langu ni kubainisha kuwa hatuwezi kutenga haki na uhuru kutoka katika mfumo uliotungwa wala katika mipaka ya kisheria ya jumla ambayo inaidhibiti na kuijenga, ikiwa kweli tutataka kurejea haki hizi na uhuru huu hebu na tuchunguze maadili na misingi iliyosimamishwa na sio utekelezaji tu wa wafuasi wake, ikiwa tutakubaliana katika hilo, tutaona tofauti ya msingi kati ya nadharia za Kiislamu na zile za Magharibi na hilo ni lazima liakisi katika nyanja za haki za binaadamu na uhuru wake….na tofauti hii kimsingi inarejea katika tofauti ya mtazamo wa undani wa (utu) na hakika ya (haki) na maana ya (uhuru), chini ya mtazamo wa ujumla wa mwanadamu na mwanadamu, na maisha, na hili ndilo lililotokea kwa rafiki yangu pindi alipotupa mtazamo wa (dini), na (udugu) na (usawa) kulingana na mfumo wa kifikra wa Magharibi kuhusu haki na uhuru, na kuufanya kuwa ni tuli usioweza kubadilika pamoja na matukufu, wakati ambapo ufahamu huu ni tofauti katika Uislamu.
Ama tukizungumzia msingi wa haki za binadamu katika Uislamu, tunaona kuwa imepanda hadi kuwa ni wajibu unaolazimishwa na jamii yote kwa mtazamo wa kidini, Uislamu umeweka wigo wa haki nyingi na taratibu za wote na huruma na maadili mema, ongezea mfumo wake wa kikanuni, bali ni kuwa haki katika Uislamu haishii kwa mwanadamu bali hata kwa mnyama.
Maiko: Sikudhania kuwa mnyama ana haki katika dini yenu.
Rashidi: Uislamu umekataza kuudhiwa kwa mnyama, na imekatazwa kuuwawa kwa ajili ya burudani kama inavyotokea katika kulenga shabaha au katika mieleka, na achinjwe kwa kuliwa tu, na pindi Muislamu anapofanya hivyo, basi anatakiwa afanye hivyo kwa ruhusa ya Muumba wake, kwa jina lake, na kwa sheria aliyo wawekea, kama ambavyo hilo lina adabu zinachungwa kwa ajili ya mnyama achinjwae, ambalo hatulioni wakati wa mtu kumchinja mtu mwenzake pindi wanapopetuka mfumo wa Mwenyezi Mungu, kisu hakinolewi mbele yake, wala mwingine hachinjwi mbele yake…Je unadhani dini yenye kumpa mnyama haki hiyo itamnyima mwanadamu?!
Rajev: Nadhani jambo hili linahitaji ufafanuzi zaidi kupitia vikao vingine.