Katika Alasiri ya siku ya jua safi, walikutana marafiki watatu kulingana na ahadi yao waliyowekeana pembeni ya Mto Seine, Rajev aliwaita rafiki zake wawili wachukue boti lililoonekana la kifahari…. Marafiki hao watatu walisimama wakifurahia mandhari nzuri ya mto na kijani chake kinachoizunguka pande zake….Rashidi aliangalia katika upeo wa macho yake na akawaambia rafiki zake:
Mito, bahari, mimea, wanyama, milima na wanadamu na kila tunachokishuhudia katika ulimwengu huu, bali hata ambayo hatuyashuhudii wala hatuyaoni…. Yote hayo ni dalili ya wazi juu ya hekima yenye miujiza ambayo imefanya vitu hivi viishi, na inaonyesha kuwa ulimwengu huu una Muumba na Mola, Je, hamuafikiani nami katika hilo?
Rajev: Tuliafikiana katika kikao chetu kilichopita kuwa katika umuhimu wa ulimwengu kuwa na Muumba, hata hivyo kuna baadhi ya kadhia zinazohusiana na ukinaishaji huku ambazo zinafaa kujadiliwa na kuzichunguza.
Maiko: Ninaona jambo la muhimu kuanza nalo ni yaliotangulia kutajwa na Mhandisi Rajev kuhusu sifa ambazo anasifika nazo Mungu wa kweli.
Rashidi: Hakika kile tunachokiishi na kukishuhudia katika uzuri wa umbile la ulimwengu kimeshikamana na unachokitafuta, kwani asili ya imani na yakini ni kuwa Allah ndie wa haki na wewe uwe na ‘mtazamo sahihi’ kwa ulimwengu huu, ikiwa pamoja na nafsi yako uliyonayo, na hilo ni kwa kujua vipengele vyake na mpangilio wake na malengo ya kuumbwa kwa kila kiumbe ndani yake.
Maiko: Tumekubaliana kuhusu uwepo wa Mola Muumba wa ulimwengu, lakini taswira hii ya Mungu inatofautiana kwa kila dini, lakini kati ya taswira hizi nyingi kuna tofauti kubwa, hali inayopelekea baadhi ya watu kutoroka utafiti katika maudhui haya na kuishi maisha yanayokaribiana na kukana uwepo wa Mungu, hata kama hawatokiri hilo waziwazi.
Rashidi: Mna haki enyi swahiba zangu, lakini na kuongezea kuwa kukimbia huko hakuwakatazi na hisia ya haja ya kuwa na Mungu, bali kwa hakika baadhi yao wanapokana uwepo wa Mungu wanajitengenezea Mungu wao wenyewe na kufanya matamanio ya nafsi zao kuwa ni Miungu yao, hivyo basi kiburi cha wenye kukana uwepo wa Mungu muumba kimewafanya wakimbie kukiri uwepo wa Mungu na kuamini mambo mengine, sifa na uwezo ule wa Mungu ambavyo haifai kuipa isipokuwa kwa Mungu wa kweli bila hata ya haki yoyote isipokuwa kutoroka katika taswira potofu ya Uungu waliyoushuhudia au kuuishi.
Rajev: Tukiingia katika maudhui yetu tunaweza kusema: Kwa hakika Mungu ni lazima awe ni mwenye kuogopewa na mwenye kupendwa kwa wakati huo huo, mwanadamu huhisi haja ya kumuelekea yeye, huu ni kwa upande wa mwanadamu, lakini sifa hizi katika hakika yake huwakilisha hali ya mwanadamu inavyokuwa kwa zaidi ya mtu mmoja kuelekea kwa zaidi ya Mungu, hivyo basi: tuoneshe sifa ya Mungu wa haki ambaye watu wanapaswa kuafikiana.
Rashidi: Maneno yako ni mazuri na sahihi…na jambo linalounganisha tulilpoanzia ndani ya kukiri kwetu ulazima wa uwepo wa Mungu, na kuafikiana kwetu kuwa ulimwengu huu mzuri ulioshikana vizuri una Muumba mkadiria ulimwengu huu na kuupata wakati haukuwepo, Muumba huyu ndie ambaye tunamsifu kuwa ndie Mola, na Mola huyu ambaye ndie Muumba wetu na Muumba wa kila kitu. Ukweli ni kuwa Muumba huyu anastahiki kufanywa Mungu na kuabudiwa na hapaswi kuabudiwa asiyekuwa yeye; yaani: Kama ulivyosema wewe yapasa asielekewe yeyote asiyekuwa yeye kwa kumuogopa kabisa, mapenzi, hofu, na kutarajia kabisa...na kuanzia hapa tunaweza kugusa sifa za Muumba huyu wa haki.
Rajev: Tukikubaliana na maneno yako, ninaweza kusema: Sifa za mwanzo ni kuwa Mungu huyu yupo na awe HAI, kama ambavyo Mungu huyu hana budi kuwa ndie Muumba.
Rashidi: Hili ni kweli kimsingi (linahitajia akili ya kuzaliwa) vile vile Mungu huyu asiwe kwa dhati yake na sifa zake ameumbwa; kwani Muumba hawezekani kuwa ameumbwa; kwani kama atakuwa ameumbwa basi atakuwa mfano wetu, atakuwa na Muumba, hivyo hawezi kuwa Mungu wala hapasi kuabudiwa,; na katika hilo vilevile viumbe vyote haviwezi kuwa Miungu.
Maiko: Kama ni hivyo, yatupasa tufahamu nini maana ya Muumba?
Rashidi: Kwa ufupi, naweza kusema: Kuwa hakika Muumba ni mwanzilishi wa vitu, bila mfano au mtindo kabla yake, yaani: aliyevipata vitu vyote baada ya kutokuwepo, nae pia ni muweza wa kuvipata kutoka kwenye kutokuwepo nae anakadiria vitu hivi na kuvijenga, katika makadirio yanayowajibishwa na hekima, yaani si mchezo wala kubahatisha.
Ama sifa za lazima kwa aliyeumbwa; Ni kutokuwepo kabla ya kuumbwa kwake; yaani mwenye kuzushwa, hapana budi wao kufa; yaani wawe na mwisho, vile vile wawe na uwezo wenye ukomo, na siku zote wanawahitajia wenzao.
Rajev: Ikiwa Mungu huyu ndie Mola Muumba, basi ni kawaida awe Mmiliki wa alichokiumba.
Na tunaposema vilivyomo mbinguni na ardhini ni vya Allah, vimeumbwa, ni lazima vyote vifahamike kwake; kwani kama vitajificha kwake basi mja huyo hatokuwa anafahamika na Mola wake, na atakuwa amejitenga na Muumba wake, kama ambavyo inathibitisha elimu yake; ustadi na umadhubuti ambao tunauona kwa viumbe, hili haliwi isipokuwa kwa ukamilifu wa elimu.
Rashidi:Yanayoambatana na umiliki; Kufanya atakayo katika Mbingu na Ardhi na vilivyomo baina yake, na juu ya elimu yake: Awe na haki katika kuyaendesha na kuweka miundo ya mambo, kanuni zake.
Maiko: Lakini na mimi vile vile nina miliki vitu, na mimi vile vile ninajua mambo mengi sana, Je, hayo yana maana na mimi ninazo sifa za Uungu? Hapana sidhani hilo kuwa ni sahihi!
Rashidi: Ugunduzi wako ni muhimu sana ewe rafiki yangu, nami naona kufafanua katika kutaja sifa hizi kwa njia hii kutarefusha pamoja na umuhimu wake, na tunaweza kufikia katika msingi wa jumla (kanuni kuu) ambayo tunaweza kuifanya kuwa ni kigezo cha sifa hizi, na tunaweza kwa kiasi kikubwa kutoa sifa kupitia kwayo; niruhusuni nioneshe sifa na alama za msingi huu; nayo kwa ukweli kulingana na taswira yangu iliyosimama juu ya utamaduni wangu wa Kiislamu.
Maiko na Rajev: Haya tafadhali tuelezee.
Rashidi: Tunaweza kufupisha msingi huu kwa yafuatayo:-
Kwanza: Tunaweza kugawa sifa katika makundi mawili:- Sifa pungufu na sifa kamilifu.
Ukamilifu ni: Kusifika na sifa nzuri pamoja na kuzuilika na kinyume chake cha sifa nzuri.
Na upungufu ni: Kusifika na sifa hasi pamoja na kuzuilika na kinyume cha sifa nzuri.
Hivyo basi: Ni juu yake kuzuia kusifika na sifa hii hasi yenye kuzuia kutakasika kwake, inatupasa kusifika na kinyume cha sifa hii, yaani; kusifika miongoni mwa sifa za ukamilifu; la sivyo kukana kutakuwa kukana upungufu; kwa sababu kutosifika kwenyewe ni upungufu na kushindwa.
Pili: Kitu ambacho kiumbe anajiona nacho, haiwezekani kukithibitisha kwa Muumba, kwa hiyo kila ambacho kiumbe anatakasika na anasifiwa nacho katika mambo yasiyopendeza ya aibu, hivyo Mungu Mtakasifu ndie mwenye haki zaidi ya kutakasika nayo na kutukuzwa wala haifai kuingia sifa mbaya na za aibu katika sifa zake kwa njia yoyote ile, kwani Mungu ni mkamilifu kwa njia zote.
Tatu: Kipambanuzi kilichokamilika kati ya Muumba na kiumbe, Muumba hana mfano wake na yoyote, ama yaliyokuja katika sifa ambazo anaweza kupewa Muumba na kiumbe; kama vile mfalme, elimu, huruma na mapenzi, hakuna mfanano wake katika maana ya kweli, kwa sababu sifa za Muumba aliyetakasika ni kinyume na sifa za kiumbe, kwani sifa za viumbe haziepukiki na upungufu.
Maiko: Laiti ungebainisha uyasemayo kwa mifano:
Rajev: Laiti ungelielezea nukta ambazo umezitaja na mifano halisi.
Rashidi: Vizuri, Nukta ya kwanza: Watu wote wenye akili wanakubaliana kuwa udhaifu ni sifa ya upungufu, vivyo hivyo kuhitaji wengine au vitu ni sifa ya upungufu, hivyo basi haifai kuwa Mungu wa kweli ni mwenye kusifika na moja ya sifa mbili hizi, bali hapana budi kuwa mwenye kutakaswa na sifa mbili hizi na (kuwa) mwenye kusifiwa kwa wakati huo huo na kinyume chake miongoni mwa sifa za ukamilifu ambazo ni: Nguvu, kutosheka, au kutowahitajia wengine, ndio maana Qur’an yetu imepinga Uungu wa masihi na mama yake (Juu yake amani ya Allah) kwa maneno matatu yaliogusa kiini cha maswala haya, nayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
“Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyo wabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa.” (5:75)
Ambaye atahitaji kula chakula kwa hakika anakula kwa sababu ya hisia yake ya njaa na yanayoambatana nayo kama vile udhaifu na unyonge, na mwenye kuhitajia chakula, na hivyo basi haifai wawe au mmoja wapo kuwa Mungu: kwani sifa za Mungu wa kweli hazithibitiki.
Vivyo hivyo: Kuwa na mtoto: Mungu wa kweli ametakasika na upungufu unaofanana na viumbe wenye kuhitajia, kwani mwenye kutaka mtoto anamtaka kwa kuendeleza utajo, msaada, urithi na mfano wake, nazo zote hizo ni sifa za upungufu, na uhitaji haumfai Mungu wa kweli.
Ama nukta ya pili: Watu wote wenye akili wanakataa kusifika na sifa ya kushindwa, kwa hiyo aula ni kutosifika mola wa haki na sifa hizi, bali hapana budi kusifika na sifa ya ukamilifu na sifa zinazokubaliana nae, ikiwemo sifa ya uwezo. Na hivyo basi ikiwa masihi hawezi kuzuilia nafsi yake na maudhi ya adui zake, au masanamu, wanyama wenye kuchukuliwa kuwa ni miungu kwa baadhi ya watu, hivyo hawezi kujilinda…basi hao watakuwa wanashindwa kuwalinda wenye kuwaabudu na wapenzi wao (hili ni suala la akili ya kuzaliwa) na hivyo basi ambae atashindwa hafai kuwa Mungu wa Haki Anayeabudiwa.
Wenye akili hawataki kusifika kwa sifa ya kudhulumu na hivyo basi: Mungu wa kweli hadhulumu, kwani yeye ni muadilifu….vivyo hivyo kila chenye kukana upungufu huwa na mkabala wa kuthibitisha kinyume chake.
Mwisho: Nukta ya tatu: Tuchukulie kwa mfano: Sifa ya elimu, nayo ni sifa nzuri na kinyume chake ni sifa hasi ya ujinga…ukamilifu ni kusifika na elimu na kuepushwa na ujinga, na upungufu ni kusifika na ujinga na kuepushwa na elimu. Mwenyezi Mungu Ndie Mwenye ukamilifu wote katika sifa ya elimu, kwani husifika kwa elimu timilifu na ujinga kwake unazuilika kabisa.
Ama mwanadamu ana ukamilifu wa kiwango fulani katika sifa ya elimu, kwani husifika na elimu katika baadhi ya mambo na husifika na ujinga kwa baadhi ya mambo mengine, hivyo basi ukamilifu wake ni mnasaba tu. Na mfano kama huo katika sifa nyinginezo.
Maiko: Nahisi baridi na haswa usiku unapoingia, nadhani haya yanatosha kwa usiku huu.