MIUJIZA KATIKA QUR-AAN NA SUNNAH

MIUJIZA KATIKA QUR-AAN NA SUNNAH

MIUJIZA KATIKA QUR-AAN NA SUNNAH

Miujiza katika Qur-aan

Kila Mtume ana miujiza inayothibitisha ukweli wa utume wake na ujumbe wake, kwa mfano miujiza ya Musa (‘Alayhi Salaam) ilikuwa ni ile fimbo yake, na miujiza ya Issa (‘Alayhi Salaam) ilikuwa ni kuponya mbalanga na ukoma na kuhuisha mauti kwa idhini ya Allah. Ama miujiza ya Mtume wa mwisho inawiana kwa kila zama na mahali muda wote mwanadamu akiwepo na ndio hii Qur-aan Tukufu, na ikiwa Qur-aan Tukufu ni kitabu cha mwongozo; basi kitabu hiki kitukufu ni miujiza wa kila kitu, na miujiza yake ni kusadikisha ukweli na utume wa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kuwa yeye ametumwa na Muumba, mwenye kutoa riziki Msimamia mambo yote milele, na kuwa ni kitabu alichotumwa nacho mwisho wa Mitume na Manabii, inayofaa kila zama na mahali na sehemu zake za miujiza yake ambazo tumezitaja huko nyuma; kwa hakika Qur-aan ni muujiza wa kisayansi na elimu mbali mbali kama ilivyokwisha oneshwa na watafiti wa kisasa katika kubainisha kuwa Qur-aan kugusa kwake mambo ya ndani ya kisayansi ambayo hayakuvumbuliwa isipokuwa katika karne hii, miongoni mwa hayo kwa mfano: awamu za kuumbwa mwanadamu na kitoto kilicho tumboni katika wasifu makini kabisa na wa ndani kabla watu hawajaweza kulijua hilo kwa mamia ya miaka, Allah Aliyetukuka amesema: “Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji. ” (23:12-14)

$Dr._YoshiodiKozan.jpg*

Profesa Yushudi Kusan

Mkuu wa Kituo cha Anga Tokyo.
Wasifu wa Kichanga
“Sipati tabu kukubali kuwa Qur-aan ni maneno ya Mwenyezi Mungu, kwani wasifu wa kichanga kilicho tumboni katika Qur-aan hauwezi kujengwa juu ya utaalamu wa kisayansi wa karne ya saba. Matokeo pekee yanayoweza kukubalika ni kuwa wasifu huu ni WAHYI (UFUNUO) alioupata Muhammad kutoka kwa Mungu.”

Na akasema Aliyetukuka: “Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?” (39:6)

Na pindi madaktari waliporejea katika rejea zao na katika ugunduzi wao walipata kama alivyosema Mjuzi wa yote.

Kwa kuongezea kubainisha sehemu ya hisia ndani ya mwili, Allah amesema: “Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” (4:56),

Na ubainifu wa upana wa anga, Allah Aliyetukuka amesema: “Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.” (51:47),

Na kubainisha mzunguko wa jua katika mzunguko wake, Allah Aliyetukuka amesema: “Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. ” (36:37-38).

Miujiza katika Sunna

Hali kadhalika Sunnah Tukufu ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) haikujitenga na miujiza hiyo; kutoka kwa Ummul Muuminina bibi Aisha (Radhiya Llahu ‘anha) amesema: amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam); “Hakika kila mwanadamu ameumbwa kutokana na mwanadamu kwa viungo mia tatu na sitini, yule atakayesema takbira, atakayemhimidi Allah, na akasema: ‘La illaha illa llah, akamsabihi Allah, akamuomba msamaha, na akaondoa jiwe kwenye njia za watu, au mwiba, au mfupa au kuamrisha mema au kukataza maovu akahesabu miaka ile miaka mia tatu na sitini mifupa na viungo vya mwili basi mtu huyo hufika jioni akiwa ameepushwa na moto.” (Muslim).

Kilichothibiti kisayansi leo hii ni kuwa bila ya viungo hivi katika mwili wa mwanadamu, asingeweza kuwepo katika maisha haya, wala kusimamia majukumu yake ya ukhalifa ardhini, na ndio maana inapasa mwanadamu kushukuru Allah Aliyetukuka kila siku kwa neema hii ambayo inathibitisha uwezo wa Muumba juu ya kila kitu.

Jambo la muujiza katika Hadithi hii ni kuainisha kuwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) idadi ya viungo vya kiwiliwili cha mwanadamu ni ainisho la kina kabisa katika zama ambazo hakukuwepo elimu hiyo kwa yeyote aliyeumbwa.

Watu wengi leo hii katika karne hii ya Ishirini na moja hawajui hilo, bali hata baadhi ya walimu wa tiba hawafahamu hilo!!! Hadi walipovumbua hivi karibuni kuwa idadi ya viungo vya mwanadamu ni mia tatu sitini kama ilivyoainishwa na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kabla ya karne kumi na nne zilizopita ambazo ndani ya viungo hivyo, viungo mia moja arubaini na saba (147) vya uti wa mgongo na Ishirini na nne (24) viungo vya kifuani na themanini na sita (86) ni viungo vya nusu ya juu ya kiwiliwili na themanini na nane (88) ni viungo vya nusu ya chini, na kumi na tano (15) na viungo vya Hodhi.

Ni nani aliyemfundisha haya Nabii asiyejua kusoma yaliyoandikwa?!

Swali linalojitokeza hapa: Kama sio Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Muumba Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) angewezaje kujua hakika hii ya kisayansi ya ndani zaidi, ambayo elimu ya mwanadamu haijaweza kuifikia ila mwishoni mwa karne ya Ishirini?!!

$Henri_de_Castries.jpg*

Henri de Castriesry

Luteni wa Jeshi la Ufaransa
Mtume Umiyi (Asiyesoma Yaliyoandikwa).
“Akili inashangaa! Iweje ayah zile zitoke kutoka kwa mtu asiyeweza kusoma yaliyoandikwa. Watu wote wa Mashariki wamekubali kuwa ni ayah ambazo fikra ya mwanadamu haiwezi kuleta mfano wake kwa lafudhi na maana.”

Nani ambaye anaweza kumlingania Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kuzamia mambo ya ghaib kama haya?! Kama sio Allah Aliyetukuka anayejua kwa elimu yake iliyozunguka kila kitu kuwa mwanadamu atafikia siku moja kufahamu hakika hii ya kielimu ya upasuaji kiwiliwili cha mwanadamu, na hivyo hili kuwa ni mng’ao wa nuru katika hadithi hii tukufu kuwa ni uthibitisho wa utume wa Mtume huyu wa mwisho kwa ukweli wa muungano wake na Wahyi wa mbinguni.

$Debora Botter.jpg*

Deborah Potter

Mwanahabari wa Kimarekani.
Miujiza ya Ulimwengu.
“Vipi aliweza Muhammad, mtu asiyesoma yaliyoandikwa, aliyeishi maisha zama za Ujinga aweze kujua miujiza ya Ulimwengu iliyoelezwa kwenye Qur-aan Tukufu, ambazo sayansi leo hii bado zinaendelea kushughulikia?! Bila shaka hapana budi basi maneno haya kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu.”

Hata hivyo njia ya elimu na ustaarabu madamu kama haitakuwa ni njia ya maadili basi ustaarabu huo utakuwa ni wenye kuangamiza na elimu yake itakuwa ya maangamizi na sio ya kuwafurahisha watu na kuwahudumia! Vivyo hivyo njia ya elimu na ustaarabu vile vile ni njia ya maadili, kama ambavyo njia ya furaha bila ya elimu na ustaarabu ni upotofu, na hali kadhalika njia ya elimu na ustaarabu bila ya maadili ni yenye kuangamiza watu, Umma na jamii za wanadamu.