Baada ya mapumziko ya usingizi mdogo wa mchana, marafiki wawili walibadilishana viti vyao ili kuimarisha nishati zao, kisha Maiko akaanza kuzungumza:
Kinachoonekana ni kuwa katika jamii nyingi za Waislamu talaka zimeenea, nami nadhani sababu yake ni Uislamu kuruhusu talaka.
Rashidi: Kwanza: Uislamu haukuwa wa kwanza kuleta sheria ya talaka, kabla ya Uislamu kulikuwepo na talaka takriban ulimwengu mzima, na wakati huo mwanamume akichukia tu humfukuza mwanamke awe na haki au makosa, bila hata mwanamke kuwa na haki au fidia kutoka kwa mwanamume, na pindi ustaarabu wa Kiyunani ulioposhamiri, talaka nayo ilishamiri bila kuwepo sharti au kifungo maalum, ama kwa Uyahudi ilikuwa ni dini inayoruhusu talaka na ilikuwa ni haki na matakwa pekee ya mwanamume, kama ambavyo alikuwa ana haki ya kumuacha mke wake bila hata ya udhuru, pamoja na kuwa waliona ni bora kuwepo na udhuru wa jambo hilo, na kilichoonekana katika talaka kwao ni kuwa: Mwanamke anapoolewa na mume mwingine hawezi tena kurudi kwa mume wake wa mwanzo.
Pili: Je, Talaka imeenea katika jamii ya Kiislamu hata tuseme kuwa Uislamu kuruhusu talaka ndio sababu ya hilo, hebu tuangalie takwimu mbali mbali ulimwenguni ili tulinganishe.
Huko Marekani wastani wa talaka kati ya mwaka 1992 hadi 1995 ilikuwa ni 502 (mia tano na mbili) Katika kila hali elfu za ndoa, na wastani huu unatarajiwa kuongezeka, na hii imepelekea serikali ya Marekani kuficha viwango hivi vya talaka pamoja na kuwa walikuwa wakitoa viwango hivyo hapo kabla, hivyo tokea mwaka 1999 hadi sasa imekuwa inafichwa. Huko Urusi wastani wa talaka kati ya mwaka 2001 hadi 2004 ilikuwa ni talaka 750 (mia saba na hamsini) kati ya ndoa elfu moja, huko Sweden katika miaka hiyo hiyo talaka 539 (mia tano thelathini na tisa) katika kila ndoa elfu moja. Uingereza kulikuwa na wastani wa talaka 538 (mia tano thelathini na nane) kati ya ndoa elfu moja baina ya mwaka 2000 hadi 2003.
Japan kulikuwa na wastani wa talaka 366 (mia tatu sitini na sita) kwa kila ndoa elfu moja kati ya mwaka 2000 – 2004.
Ama nchi zingine zilikuwa chini ya hapo, kwa mfano Jordan 184 katika ndoa elfu moja baina ya mwaka 2000 hadi 2004, ama Palestina ilifikia 142 katika mwaka huo huo katika ndoa elfu moja.
Huko Misri kati ya mwaka 2000-2003 kulikuwa na wastani wa talaka 134 (mia moja thelathini na nne) kati ya ndoa elfu moja, katika nchi ya Syria baina ya mwaka 2000 hadi 2002 kulikuwa na wastani wa talaka 84 (themanini na nne) katika ndoa elfu moja. Lybia ilifikia talaka 51 (Hamsini na moja) katika ndoa elfu moja kati ya mwaka 2000 hadi 2004, Iran ilifikia 97 (tisini na saba) katika ndoa elfu moja katika mwaka 2000 hadi 2003.
Je, baada ya hapo tutasema kuwa talaka imeenea katika jamii za Waislamu, na kuwa sababu yake ni Uislamu kuruhusu talaka?!
Maiko: Lakini inajulikana kuwa Uislamu ni maarufu kwa wepesi wa kutoa talaka ukilinganishwa na dini na mifumo mingine ya kijamii.
Rashidi: Wazo hili limebeba maudhui mengi, hebu niruhusu niyazungumzie kwa upana.
Maiko: Endelea.
Rashidi: Maudhui ya kwanza: Ni kuamini wepesi wa kutoka talaka moja kwa moja, bila ya shaka hakuna sharia au mfumo wowote wa kijamii ambao unahamasisha talaka…huenda nikakubaliana nawe kuwa huenda akapuuza jambo hili ambae hajilazimishi na mafundisho ya Kiislamu, na hutumia baadhi ya fursa vibaya, lakini wakati huo huo inabidi tujue kuwa mafundisho ya Uislamu yako mbali na tabia hizi, kwani ni mafundisho ambayo yapo wazi kiasi cha kuondoa athari mbaya, na kinachotokea katika baadhi ya jamii ni matokeo ya jamii hizi kuwa mbali na ukweli wa dini ya Kiislamu, sheria na mifumo yake.
Maiko: Je, unaweza kuifafanua nukta hiyo?
Rashidi: Asili ya ndoa katika Uislamu ni mkataba wa kudumu na ni haramu kuuwekea muda maalumu, kwa namna ambayo inawajibishwa maisha yao ya ndoa yaendelee na yadumu hadi mauti yatakapowatenganisha, mkataba huu wa ndoa umeitwa mkataba mzito, na hilo ni kwa vile inaelekeza kinacholingana kuuheshimu na kutofikiria kuuvunja, hata hivyo talaka ni jambo linalochukiwa katika Uislamu isipokuwa katika hali ya wakati wa dharura, wakati ambao Uislamu umeelekeza kufanyika jitihada za kusuluhisha na kuheshimu pande zote mbili na kuhifadhi mambo ya familia yaliyobaki.
Uislamu umelingania kwenye kukaa na mke bila kumpa talaka atakapochukizwa na sifa asiyoipenda, na ukamkumbusha kuangalia sifa zingine ambazo anaweza kupata na kumfanya akamatane na ndoa yake, na kulinda utukufu wa ndoa. Pia Uislamu ukahadharisha utani katika kutumia au kutoa neno la talaka, kama ambavyo imemuamrisha mume kudhibiti hisia zake na kufanya pole pole katika kumnyoosha mke, na Uislamu ukaweka taratibu kama wana ndoa hawawezi kutatua tatizo lao basi pande zingine ambazo maslahi ya wana ndoa zinawagusa ziingilie kati na kutatua tatizo lenyewe, kisha mwishowe ndipo linapokuja suala la talaka tena katika hatua tofauti kama jaribio la kutoa fursa ya kurudiana wanandoa, Uislamu haujahukumu kubomoa maisha ya wanandoa mwanzo wa ugomvi wao, bali umeweka mara tatu mume anaweza kumrudia mkewe baada ya talaka ya kwanza na ya pili, na hata katika talaka ya tatu Uislamu, umemruhusu mume kumrejea mkewe lakini hilo hutokea baada ya utaratibu ambao utawaumiza wote wawili, nao ni kuolewa kwa mke huyu aliyeachika na mwanamume mwingine.
Maiko: Haya ni maudhui ya kwanza, ni yapi mengine?
Rashidi: Nukta nyingine muhimu ni ule mtazamo mbaya katika kuangalia hali halisi ya jamii zingine zisizokuwa za Kiislamu, ukweli ni kuwa talaka inaweza kutokea kwa sababu ndogo, bila shaka unalijua hilo, kwa mfano Marekani inatajwa kuwa inawezekana kimahakama mmoja wa wanandoa akaachika kwa sababu ya uraibu wake mkubwa wa kompyuta au kufuatilia vipindi vya televisheni, huko Canada inatosha kuthibitisha kuwa mmoja wa wanandoa anakoroma anapolala ili wakati huo apate haki ya kumpa talaka, ama Italia talaka inaweza kutuka ikiwa mmoja wa wanandoa anamlazimisha mwenzake kazi za nyumbani, na Uingereza kuzembea jambo la mwanandoa mwenzake kunapelekea kwenye talaka.
Mahakama za Japan zimekubaliana kutoa hukumu ya talaka ikiwa mmoja wa wanandoa atalala kwa namna ambayo haitomfurahisha mwenzie mtaka talaka.
Maiko: Ulichokitaja bwana Rashidi ni sahihi, lakini huu ni uhalisia katika mahakama za kisekula zilizojitenga na dini. Ama Ukristo msimamo wake mkali kuhusu talaka unafahamika isipokuwa kwa sababu chache tu ambazo ni vigumu kuthibitisha.
Rashidi: Mimi ninadhani kuwa huku kushupalia talaka hakuendani na maisha ya mwanadamu, na hilo linafafanuliwa kuwa baadhi ya Wakristo waishio katika nchi za Waislamu wanaona tofauti kati ya dini hizi mbili, wanaweza kuacha dini zao kwa kukimbia taabu hii wanapofikia katika nukta ya kuyatenganisha maisha yao ya kijamii na wala wasipate majibu kutoka kwenye dini yao kwa mazingira ya maisha na ugumu wake.
Na hili ndilo lenye kuupambanua Uislamu, Uislamu unalazimisha maisha ya ndoa yawe ya milele, umewawekea sheria watu wanaoishi ardhini, wana mambo mahsusi na tabia zao za kibinadamu na mazingira yao ambayo yanaweza kubadilika, na huweka pembeni wakati huo huo makosa katika uchaguzi ambao hauwezi kuvumbuliwa isipokuwa ni kwa uzoefu tu, mabadiliko katika mazingira haya yanaweza kupelekea kuangukia katika kosa hili yanaweza kusababisha matatizo katika viwango tofauti, wakati mwingine yanaweza kutokea matatizo na yakawa makubwa yasiyoweza kuvumilika ila kwa hasara za kinafsi, kijamii na hata za kifedha au kiuchumi ikawa ni hasara kubwa, hivyo sharia ya Kiislamu imewawekea namna ya kushughulikia tatizo (matatizo haya) pindi maisha yanapokuwa magumu na njia zikawa za dhiki na njia za kusuluhisha kushindikana. Katika hili Uislamu ni dini inayokwenda na wakati, na ni dini yenye uadilifu kwa wote; mwanamume na mwanamke kwa pamoja na familia, hivyo kusahihisha muelekeo hadi kuachana na kuanza majaribio mapya ni bora kuliko kuungua kwa moto wa mifarakano na magomvi au kuendelea na hali hiyo pamoja na kukosekana kusudio la ndoa na lengo lake, ambapo malengo yake muhimu ni: Utulivu wa nafsi ndani ya mapenzi na huruma na kuasisi familia tulivu yenye mafanikio. “Talaka katika Uislamu ni suluhisho na kunyoosha njia, na fursa ya mabadiliko na kutoa nafasi ya maisha mapya yenye mafaniko zaidi.
Rashidi: Mimi naona sheria ya talaka iliyotajwa katika Uislamu ni katika ubora wa dini hii na kwenda pamoja na mazingira yake.
Maiko: Lakini kwa nini Uislamu umefanya haki hii ya kutoa talaka ni ya mwanamume peke yake, hivi hii sio dhuluma kwa mwanamke?.
Rashidi: Kwa mara nyingine, inapasa kuangalia mambo kwa upana wake na kuchunga maeneo yote, na ninakusudia kuangalia katika jambo hili kupitia mfumo kamili wa kijamii, kuanzia katika ndoa yenyewe na malengo yake na mtazamo wa familia na wadhifa wa kila pande na haki zake.
Hapa tutataja kuwa imethibitika kisayansi kwamba mwanamke kwa tabia yake ni mwenye hisia na kubadilika na mhemko kuliko mwanamume, kitu ambacho kinamfanya mwanamume kuwa na udiriki zaidi na kukadiria matokeo (mazuri) ya jambo hili, na hivyo kuweza kudhibiti hisia na hasira zake anapokuwa ameghadhibika.
Kama ambavyo hasara za utoaji wa talaka zinakuwa ni za mwanamume pekee, nae ndie atakayebeba hasara za mali, na inamlazimu mwanamume gharama za mali baada ya talaka wala hapana shaka yoyote kuwa gharama hizi za mali ambazo zimetokana na maamuzi hayo ya talaka itakuwa ni sababu za ziada ambazo zinafanya wanandoa kudhibiti nafsi zao.
Pamoja na hayo: Uislamu pamoja na kufanya talaka kuwa ni haki ya mwanamume peke yake, isipokuwa haukupuuza kumpa mwanamke njia ya kujitenga na mume atakapoona sababu za msingi za kufanya hivyo, na hili kisheria linafahamika kwa jina la Khulu’u yaani kuvua, kwa kutumia vidhibiti na sheria ambazo zitahifadhi haki za pande zote.
Rashidi: Je, rafiki yangu ungependa tuzungumzie hali ya mwanamke katika nchi zenu?!
Maiko: Naona tule chakula cha mchana.