Hoja za wujudi(kuwepo) na athari zake katika kuleta saada(furaha)

Hoja za wujudi(kuwepo) na athari zake katika kuleta saada(furaha)

Hoja za wujudi(kuwepo) na athari zake katika kuleta saada(furaha)

Watu wengi hudhania kuwa raha ndio furaha hivyo wakaanza kutafuta raha ambayo huenda ikawaletea kero nyingi na huzuni pamoja na upweke na tabu na hivyo husahau kuwa mara nyingi huhisi furaha wakati mwili wake ukitaabika, bali wakati mwingine tabu na mashaka ayapatayo mtu ndio furaha yenyewe.

Utakapoamua kujitupa ndani ya kisima ili kumuokoa mtoto aliyetumbukia utakuwa ni mwenye furaha pamoja na majeraha na maumivu utakayoyapata wakati ushukapo kwenye kisima.

Ama tabu na mashaka wayapatao wanazuoni na watafuta elimu wakati wa kutafuta kwao elimu huwapelekea katika furaha na huwanyanyua katika vyeo vya juu pamoja na maumivu wayapatao na mashaka makubwa!!

Vivyo hivyo mwanariadha hufurahi kwa michezo yake pamoja na jasho linalotiririka mwilini mwake, na yule mwenye kuhudumia wanyonge na wenye kuhitaji hufurahi katika kufanya kwake hivyo pamoja na kutoa kwake na kujituma na kutumia mali aipendayo kwa fukara na masikini, hivyo kutoa mtu ni sehemu ya raha yake na anachokipenda ili apate furaha ndani ya nafsi yake.

Dalida

Mwimbaji mashuhuri Ulimwenguni
Maisha Hayavumiliki!!
“Kabla ya kujiua aliandika barua yake ya mwisho. Alisema ndani yake:Maisha hayavumiliki!! Nisameheni.”

Hivyo matokeo ya maingiliano haya na mitazamo mbali mbali na taarifu za aina nyingi za furaha (bado) mwanadamu anabaki akiwa hajui katika kivuli cha utafiti wake wenye kuchosha maana na jinsi gani atakapopata furaha ya kweli.

FURAHA CHINI YA HAKIKA KUU ZA UWEPO

Hapana shaka ya kuwa mwenye akili yoyote au mwadilifu yeyote ana yakini kuwa ili mtu aweze kufikia njia ya furaha hapana budi afahamu hakika kuu za uwepo; baada ya hapo ni juu yake atarajie kupata furaha kupitia njia ya amani ya kuamiliana na misingi mikuu ya uwepo huu, nayo ni Mwanadamu, Maisha na Ulimwengu.

Mwanadamu

Ameumbwaje?!

Allah Aliyetukuka anasema: “Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanao kufa kabla, na ili mfikie muda ulio kwisha wekwa, na ili mpate kufahamu. (41:67),

Ndio …asili yake ni kutokana na udongo, maji dhalili na mwisho wake ni mzoga usio na roho na ndani yake anabeba najisi tumboni mwake na huhisi uchafu kila kinapotoka katika kiwiliwili chake, na baada ya yote haya huwa hasimu kwa Mola wake, ni kiasi gani ukanaji wake!! Allah Ta’ala anasema: “Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?Kwa kitu gani amemuumba? Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. Kisha akamsahilishia njia. Kisha akamfisha, akamtia kaburini. Kisha apendapo atamfufua. ” (80:17-22),

Pamoja na hayo bali amekirimiwa kuliko viumbe wengine, Allah ameamrisha Malaika kumsujudia babu yake Adam, na akamdhalilishia ardhi na wanyama, na kumkirimu kwa akili ambayo kwayo alimtengenezea miujiza mingi, Allah Mtukuka amesema: “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.” (17:70)

Hivyo kiini cha mwanadamu hakiwezi kufahamika isipokuwa kwa taswira ya hakika hizi mbili pamoja, na kwa taswira hii ulinganisho unasimama katika imani utanyooka na kuwa yote yatakayomfikisha mwanadamu katika utukufu, mali na elimu na yasiyokuwa hayo si chochote ila ni katika neema ya Allah Mtukuka juu yake, Allah Mtukuka amesema: “Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni madhara mnamyayatikia Yeye.” (16:53).

$Rosemary_Howe.jpg*

Rosemary Howe

Mwandishi wa habari wa Uingereza
Jibu Toshelevu
“Katika kutekeleza mafundisho ya dini ya Kiislamu mwanadamu anagundua tabia yake na haiba yake ya kweli ya kibinadamu na atajua dhati yake. Uislamu ni dini pekee iliyonipa majibu yenye kukinaisha kwa maswali yangu yenye kutatanisha.”

Ama mwanadamu mwenyewe hakuwa yeye isipokuwa ni mkusanyiko unaotokana na nyama na mifupa, nafsi yake inatukuka kwa (vitu) hivyo, ambayo anapenda kuinyoosha na kuilea kwa elimu yenye manufaa na matendo mema na ya kuwa pamoja na unyonge wake na udhaifu alionao ila ni kuwa Allah amemkirimu kwa sifa ambazo zitamuwezesha kubeba amana ambazo viumbe vingine vilivyo mzunguka haiviwezi, Allah Mtukuka amesema: “Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga.” (33:72)

Na atakapoharibu mwanadamu imani yake kwa sharti la lingano kati ya hakika mbili ima akili yake iondoke na kuelekea katika hakika ya mwanzo, na hivyo basi asiione nafsi yake isipokuwa ni kiwiliwili kichafu chenye matamanio kisichokuwa na malengo yoyote, hivyo kudhalilisha matamanio yake kama mnyama hadi imalize nafsi yake, Allah Mtukuka amesema: “…Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makaazi yao.” (47:12), Au avuke mpaka juu ya fikra ya hakika ya pili; ambayo humpelekea kuwa na kiburi na kufanya dhuluma akighafilika kuwa yeye atarejea kwa Mola wake, Allah Mtukuka amesema: “Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri Akijiona katajirika. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.” (96:6-8).

$11.jpg*

Thomas Edison

Fahamu uwezo wako.
“Hata kama hadhi yake ni ndogo na matendo yake ni machache kwa mtazamo wa watu, lakini (Edison ambaye alifukuzwa shuleni) aliipata Nafsi yake katika uvumbuzi: Fadhila zake kwa wanadamu zilikuwa ni kubwa sana, la msingi ni wewe kutengamana na Nafsi yako, ili uwe na furaha na kufahamu nafasi na uwezo wako.”

Ni juu ya mwanadamu kujua hadhi ya nafsi yake na kuitengeneza; kwani hiyo imekuwa ni sababu muhimu ya matatizo, kwani mwanadamu hajui sehemu yake katika jamii, wala hajui yeye ni nani na ni ipi nafasi yake na anaweza kufanya nini.

KWANINI AMEUMBWA?!

Allah Mtukuka ameumba yote yaliyomo, wala kuumba kwake hakukuwa kwa mchezo, upuuzi au bila ya maana. Allah Mtukuka amesema: “Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A’rshi Tukufu.” (23:115-116),

Bali ameumba viumbe ili vimuabudu kwa maana pana ya ibada ambayo inakusanya maisha yote ya mja hadi kazi zake michezo yake, na upuuzi wake na maisha yake yote, sio tu vile vipengele maalumu vya ibada pekee, amesema Mtukuka: “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” (51:56).

Ama asiyejua hayo mtu huyu ataendelea kuadhibika kwa ujinga huu, na ataendelea kuwa na shaka na babaiko ambalo atapata nalo shida katika maisha yake, na hivyo basi ibada yake itajitenga na furaha, ibada na maisha yake ya hapa duniani, na dunia itajitenga na akhera, Allah Mtukuka amemhalalishia mwanadamu yote yaliyomo mbinguni na ardhini, amesema Mtukuka; “Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.” (45:13),

Ni juu ya mwanadamu kujua kuwa yeye ni khalifa katika ardhi hii kutoka kwa mmiliki wake wa kweli na mmiliki wa mwanadamu ili kumpa mitihani, amesema Mtukuka: “Naye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa, ili akujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (6:165).

Maisha

Baada ya mwanadamu kujua ukweli wa kuwepo kwake nafsi yake inatarajia kuzingatia katika maisha yake ya ndani ambayo ameumbwa kwa ajili yake, huo ni msingi ambao unasimamia ladha zote na yenye kufurahisha hapa duniani, na juu yake husimama matarajio ya kupata nafsi ya mwanadamu kinachotamani na kuelekea kwake, Ni nini basi lengo la maisha haya?! Kwa hakika lengo la kuumba mauti na uhai ni kumpa mtihani mwanadamu ni yupi atatenda matendo mazuri, amesema Mtukuka: “Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.” (67:2).

Huo ndio ukweli, lakini watu wengi hawafahamu!! Naam hiyo ndio hekima ya hii dunia, amesema Aliyetukuka: “Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.” (10:24)

Akasema Ta’ala: “Na wapigie mfano wa maisha ya dunia. Hayo ni kama maji tunayo yateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha hiyo mimea ikawa vibuwa vinavyo peperushwa na upepo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.” (18:45).

Kwa hiyo maisha yetu ambayo tunaishi ni mapito na sio ya kudumu, na hilo ni daraja lenye kufikisha katika nyumba ya akhera, maisha hayaishi kwa kuisha dunia bali kuna maisha ya hakika yenye kubakia Akhera, hivyo basi maisha ya duniani ni mchezo na pambo na kujifakharisha kama alivyosema Allah Mtukuka: “Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.” (59:20);

Hivyo basi Aya hii inatoa taswira ya maisha haya ya dunia kwa sura ya udhalili inadunisha hadhi yake, na huzinyanyua nafsi na kuzitundika na akhera na kuzipa thamani.

Pindi maisha ya dunia yanapopimwa kwa vipimo vyake na kuangaliwa uzito wake katika macho na hisia za watu huonekana ni kitu kikubwa sana, lakini pindi inapopimwa na kuangaliwa uzito wake kwa vipimo vya akhera inaonekana kuwa ni kitu kidogo kisichokuwa na thamani; ni mchezo na upuuzi na pumbao na watu kujifakharisha na kutaka wingi (wa mali), huu ni ukweli ambao moyo unaujua pindi moyo huo unapotafuta ukweli, ukweli ambao Qur-aan hailengi kumtenga mwanadamu na maisha yake ya hapa duniani, wala kupuuza kuijenga kwake na kuiongoza, bali inalenga katika kusahihisha vipimo vya kihisia na kuinua thamani ya Nafsi kuliko kiburi au jeuri ya starehe fupi zenye kuondokana na mvuto wake na kuufunga na dunia.

Kwa hakika maisha ni daraja ambalo viumbe hupita njiani katika njia yao ya kuelekea akhera, na dunia hii ni ufupi wa maisha yake si kitu ambacho kinaweza kufananishwa na maisha ya milele yanayofuatia. Kadhalika akhera na upana usio na mwisho inategemea hali atakayokuwa nayo binadamu katika maisha haya ya mwanzo, yeye atakuwa katika awamu ya mitihani ya kudumu, na kila akionacho pembezoni mwake katika starehe mbali mbali au katika tabu na balaa na maumivu mengi yote haya muda wake ni mdogo sana wenye kupita haraka, yatawekwa katika mkono wa mizani ili kumweka mwanadamu huyo katika marejeo yake ya milele, Je, utachukua nini kwenda nacho kaburini? Mtukuka amesema: “Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai.” (6:94).

Watu wengi wameghafilika na ukweli huu na hili ndilo alilosema Allah: “Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.” (30:7)

Hali itakuwa vipi kwa aliyeridhia maisha haya duniani wala hataraji kukutana na Mola wake?! Mtukuka amesema: “Hakika wasio taraji kukutana nasi, na wakaridhia maisha ya dunia na wakatua nayo, na walio ghafilika na Ishara zetu, Hao, makaazi yao ni Motoni kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyachuma.” (10:7-8),

Ni ipi hali ya aliyeitanguliza dunia, Allah amesema: “Na akakhiari maisha ya dunia, Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! ” (79:37-41).

Ndio, kwa sababu wamechukua dini yao kuwa ni upuuzi na mchezo na maisha haya duniani yakawahadaa, Allah amesema: “Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo Sisi tunawasahau kama walivyo usahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu.” (7:51),

Ndio; kwa sababu wanataka kuipotosha, Allah amesema: “Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali.” (14:3).

Hii haina maana ya kudharau maisha ya dunia kwa mtazamo wa mwanadamu na aache kujenga ardhi na dunia kwa elimu na matendo na ajitenge na kuwa mbali kabisa na dunia na kusubiri mauti tu.

Hii haina maana ya kudharau maisha ya dunia kwa mtazamo wa mwanadamu na aache kujenga ardhi na dunia kwa elimu na matendo na ajitenge na kuwa mbali kabisa na dunia na kusubiri mauti tu.

Hasha …bali njia nzuri inayofaa ya kutangamana pamoja na dunia ni ile aliyoisema Allah Mtukuka: “Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.” (28:77)

Na amesema tena Allah: “Na chochote mlicho pewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayo baki zaidi. Basi je, hamfahamu?” (28:60).

Kwa mtazamo huu uliokamilika maisha kwa mtazamo wa mwanadamu yatakuwa ni Hazina yenye thamani ambayo inampasa mwanadamu kuwekeza; kama ilivyo yenyewe haimpasi mwanadamu kuipupia zaidi ya kuona kuwa ni daraja la kufikia furaha ya milele. Ama furaha, na aina ya mapambo na starehe ambayo mtu anakumbana nayo kwenye daraja hilo si chochote isipokuwa ni starehe za dunia na pambo lake kwani ni vizuri sana kuzitumia. Allah amesema: “Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema.” (3:14),

Na akasema Aliyetukuka: “Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.” (18:46)

Wala haichukizi vile vile kwa dhati yake ikiwa itatumiwa vizuri, Allah amesema: “Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.” (7:32),

$Mike_Tyson.jpg*

Mike Tyson.

Bondia Maarufu.
Uliza na Qur-aan itakujibu.
“Nimesoma Qur-aan nikakuta ndani yake kuna majibu ya kila swali kuhusu maisha.”

Na kwa ufahamu huu Muislamu anaingia katika msongamano wa maisha na utamu wake akiwa mwenye imani na hatua madhubuti baada ya kuyakinisha kuwa kila anachomiliki hakibakii, naye yupo daima katika kutafuta starehe bila ya kufanya israfu, pamoja na imani ya ndani kuwa alichokimiliki humo (duniani) katika miliki ya mkono wake na sio katika moyo wake. Aliyoyakosa humo hayamdhuru au aliyoyapata katika dunia yake, Allah Aliyetukuka amesema: “Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. Ili msihuzunike kwa kilicho kupoteeni, wala msijitape kwa alicho kupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna akajifakhirisha.” (57:22-23)

Na hivyo basi anastarehe kwa starehe na mapambo, naye ni mwenye kupata ujira na malipo kutoka kwa Allah, na kwake dunia inaungana na akhera na furaha za viwiliwili pamoja na furaha za kiroho, na furaha kwa mapambo ya dunia, na furaha kwa kuridhika na utulivu ndani yake.

Ulimwengu

Muislamu anahama katika kufikiria kwake katika kipengele cha tatu na cha mwisho katika kufahamu kwake uwepo; nao ni Ulimwengu ambao unakusanya viumbe vyote ulimwengu ambao unakusanya viumbe vyote vinavyomzunguka, fikra yake inaanzia katika kauli yake Allah Aliyetukuka:

“Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara Kisha anaendelea kusoma makumi ya aya ambazo zinamuita kwenye kufikiria kuumbwa kwake na uzuri wa sanaa yake ili atoke na matokeo yanayofanana na yale aliyoyapata mwanzoni kuhusu kufikiri kwake kulikotangulia kuhusu uhakika wa uwepo wake na maisha yake, na kugundua kuwa kufahamu kwake ulimwengu inapasa vile vile kuanzia pale alipofahamu ukweli ule uliokamilika ambao upo katika namna mbili:

Kwanza: Ukweli wa kuwa Allah Aliyetukuka amemdhalilishia vingi vinavyomzunguka katika viumbe; ya kuwa ubora na kutangulizwa kwake hakukuwa ni kwa sababu ya kuwa na sifa tu ya baadhi ya vipambanuzi, bali ni kule kumpelekea kudhalilishwa viumbe hivi kumhudumia ili lengo la maendeleo lifikiwe, Allah Aliyetukuka amesema: “Kwani hamwoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni viliomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za dhaahiri na za siri? Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu pasipo ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru.” (31:20),

Na akasema: “Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili.” (16:12),

Na akasema tena: “Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.” (67:15),

Muislamu atapata katika aya nyingi dalili kubwa ya kudhalilishwa ulimwengu huu na kumthibitisha yeye ndani yake, na katika hilo ni ishara nzuri ya umuhimu wa kujiliwaza na ulimwengu huu, na kujizuia kufadhaika pindi tatizo au balaa litakapompata, maumbile daima hayapo katika kupingana na mwanadamu dhaifu, na hivyo hivyo mwanadamu huyo hayupo katika kushindana na maumbile.

Pili: Ama ile hakika ya pili: ambayo ni kuwa ulimwengu haukumfichulia mwanadamu siri zote; pamoja na kumdhalilishia, na kumuwezesha (kumthibitisha) lakini kundi lingine katika ulimwengu huu bado ni siri iliyofichika kwa mwanadamu na zipo nje ya utawala wake.

Ulimwengu huu una Malaika, majini na huenda kuna viumbe vingine ambao bado hawajafahamika na mwanadamu au hata elimu ya kufahamu kuwepo kwao na uwepo wa mwanadamu katika ulimwengu huu ni sehemu ndogo tu ya atomi ambayo huwezi kuitaja mbele ya ukubwa na upana wa ulimwengu huu.

Kwa hakika hizi mbili ule mtazamo wa Muislamu unakamilika kwa ulimwengu unaomzunguka; yeye kujua kwa ukamilifu nafasi yake maalumu iliyopambanuliwa kati ya viumbe, kiasi cha Allah Aliyetukuka kumfanya kuwa yeye ni kilele cha uwepo ambao viumbe vingi vimedhalilishwa kwa ajili yake, na wakati huo huo akijua ukweli wa kuwa baadhi ya milango kufungwa kwake, na kuwa uwezo wake wa kustaajabisha vyovyote iwavyo hauwezi kugonga milango ile.

$Martin_Lings.jpg*

Martin Lings

Mwanafikra wa Kiingereza.
Dini ya Ubinadamu.
“Dhati yangu niliyoikosa kwa muda mrefu katika maisha yangu nimeipata ndani ya Uislamu na kwa mara ya kwanza, wakati huo nilihisi kuwa mimi ni binadamu. Uislamu ni dini inayomrejesha mtu katika tabia yake (asili yake) kwani inaafikiana na maumbile ya mwanadamu.”

Ama uhusiano wa mwanadamu na wanaomzunguka ni uhusiano unaodhibitiwa na hisia (heshima) ya hali ya juu na adabu kubwa, watu wenye kuishi katika hali ya fujo katika mahusiano yao huishi kwa shida na tabu nyingi kwa sababu mahusiano yao hayana uwiano na hayapo katika udhibiti mzuri hivyo basi mahusiano yao yanasimama katika ubinafsi, hasadi, dhana mbaya na kulipizana visasi na kuviziana.

Yote hayo yanamfanya mwanadamu kutokuwa na furaha na kutoridhika na kumfanya kuwa na wasiwasi mara kwa mara na kuwa katika hali ya dhiki muda wote, katika hali hiyo mtu huyu atapata wapi raha na furaha?! Allah Aliyetukuka amesema: “Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa. ” (41:34-35)

Ama mtu ambae amepangilia maisha yake katika misingi ya haki na majukumu mbali mbali mtu huyo hutekeleza wajibu wake na huwarahisishia wenye haki zake na husamehe mahasimu wake, mwisho wa yote hayo huwa ni mtu mwenye furaha bila ya shaka.

Mapenzi ni ngazi ya juu kabisa ya mtu kutangamana na nduguye mwanadamu, upole, urafiki una maana ya mapenzi kuzoeana nayo ni maumbile ya asili ya mwanadamu yalio sawa.

Mwanadamu kufanya suluhu pamoja na Nafsi na ulimwengu wake

$Fanaan moseh.jpg*

F. Mosey

Mwanafikra wa Kifaransa.
Dini ya Karama na Tabia Njema.
“Ni kwa sababu hii ndio nimechagua Uislamu ili ndani yake nipate raha. Na nimeukumbatia Uislamu ili nipate hisia na kufahamu kuwa nimechagua dini ambayo haitofautishi baina ya kiwiliwili, roho, na nafsi, inanitosha kuwa Uislamu ni dini nadhifu inasukuma kwenye tabia njema na kujipamba nayo na kwenye karama na kushikamana nayo. Kwa ajili hiyo nimeshuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wake na juu ya hilo nitakutana na Mola wangu.”

Kwa imani hii mwanadamu anafanya suluhu pamoja na Mola wake pamoja na Nafsi yake na ulimwengu unaomzunguka, yeye hufahamu kwanza kabisa ukweli wa uja wake kwa Mola wake Aliyetukuka, husimamia majukumu yake ipasavyo na kadhalika hujua thamani ya nafsi yake kama kiumbe ambae Allah amemkirimu kwa kumdhalilishia viumbe, na kuwa aliteremka ardhini ili apewe mtihani ndani yake kabla ya kurejea peponi, pepo ambayo imeumbwa kwa ajili yake, amekalifishwa kuijenga ardhi hii, Allah Aliyetukuka amesema: “…Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi.” (11:16),

Na amekalifishwa vile vile kuilea na kuizoesha nafsi yake katika kujizuia matamanio na kuwa chini ya mipaka ya kisheria kulingana na mahitaji yake.

Tukiwa na ufahamu huu kamili kuhusu Muumba Mtukuka, pamoja na nafsi na ulimwengu sasa ni haki kwetu kujiuliza kuhusu matokeo ya kimatendo baada ya kutekeleza ufahamu na mtazamo huu.

$Marshila_Michelangelo.jpg*

Marshila Michelangelo

Mwanadada wa Kitaliano aliyesilimu.
Neema ya Uislamu.
“Hakuna neema kubwa miongoni mwa neema za dunia ambavyo mwanadamu ananeemeka nayo mtu kuliko Allah kumfungulia mtu kifua chake kwa ajili ya Uislamu, na akaongoka kwa nuru yake hadi akaona hakika za duniani na akhera hivyo mtu akaweza kutofuatisha baina ya haki ya batili, na baina ya furaha na huzuni na mashaka. Nami namsujudia Allah na kushukuru neema hii tukufu aliyonipa, neema ambayo imejaza furaha ndani ya nafsi yangu na kunipa fursa kuwa chini ya kivuli cha mti huu mkubwa wenye matawi yenye vivuli na matunda (mengi), nayo ni mti wa familia ya Kiislamu na udugu katika Uislamu.”

Baada ya mwanadamu kujua ukweli ule atajua kuwa furaha ipo katika nyumba zote–Dunia na Akhera na zote hutegemea radhi za Allah kwa kutekeleza maamrisho yake na kusimama katika mipaka yake..yote haya huja katika kulinganisha baina ya matakwa ya kiwiliwili na kiroho; na baina ya matakwa ya mtu binafsi na matakwa ya kundi baina ya kujenga dunia na kujenga akhera na hivyo kubaki furaha duniani –vyovyote itakapokuwa ni furaha yenye upungufu, kwa sababu dunia ni nyumba ya kujitahidi na kufanya matendo na mitihani na akhera ni nyumba ya hesabu na atakayefuzu atapata furaha kamili ya milele, Allah Aliyetukuka amesema: “Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa.” (9:21-22)

Ili mwanadamu apate furaha na kuhisi utulivu na maisha mazuri yalio bora duniani na akhera hapana budi awe na imani na matendo mazuri, Allah amesema: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (16:97).