VYANZO VYA UISLAMU

VYANZO VYA UISLAMU

VYANZO VYA UISLAMU

Dini ya Kiislamu inapokea sheria yake, akida zake na hukumu katika ufunuo (Wahyi), kutoka kwa Mwenyezi Mungu (Qur-aan na Sunnah) hizo ndizo vyanzo vikuu viwili vya msingi vya Uislamu, na kutoka katika vyanzo hivyo ndio imepatikana sheria yake, itikadi zake na hukumu zake, ifuatayo ni taarifa zake kwa ufupi.

Qur-aan tukufu

$Bashir_Shaad.jpg*

Bashir Shaad

Muhubiri wa India.
Qur-aan ….Kitabu cha Mwisho cha Mbinguni.
“Nilipoamini tawhidi nikaanza kutafuta hoja na dalili mbali mbali ambazo zinathibitisha kuwa Qur-aan ni kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuwa Qur-aan ni kitabu cha Mwisho. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kutatua mas-ala haya: Qur-aan Tukufu ni kitabu pekee ambacho kinakubali na kutambua vitabu vyote kutoka mbinguni, wakati ambapo vitabu vyote vinapinga vitabu vingine. Kwa hakika hii ndio moja ya sifa kubwa inayopambanuka Qur-aan Tukufu.”

Allah ameteremsha Qur-aan kwa Mtume wake Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) kuwa muongozo kwa wamchao Mungu, desturi ya Waislamu, tiba ya nyoyo ambayo Allah ametaka kuwapa uongofu na taa kwa yule ambaye Allah amemtakia kufanikiwa na mwangaza.

Nayo inakusanya misingi ambayo kwa ajili yake Allah ametuma Mitume, na Qur-aan sio kitabu kilichozushwa miongoni mwa vitabu kama ambavyo hakuwa Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasalaam) Mtume miongoni mwa Mitume aliyezuka tu; Allah alishateremsha kwa Ibrahim Suhufi (maandiko), na akamkirimu Musa Taurati na Dawuud Zaburi na Issa akaja na Injili.

$Will_Durant.jpg*

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani
Nafasi ya Qur-aan na fadhila zake.
“Qur-aan imebakia karne kumi na nne imehifadhiwa katika kumbukumbu ya Waislamu ikihamasisha fikra zao, kutengeneza tabia zao, na kuchochea hamasa za mamia ya milioni ya watu, Qur-aan inaweka katika nafsi za watu imani nyepesi zaidi yenye utata mchache ambao ipo mbali na vifungo vya rasimu na mafundisho ya Kikristo. Qur-aan imekuwa bora katika kunyanyua viwango vya tabia za Waislamu na elimu. Na ndio iliyosimamisha ndani yao kanuni za mfumo wa kijamii na umoja wake, na kuwahimiza kufuata kanuni za afya na kufungua akili zao kutokana na dhana potofu na dhuluma na ususuavu (wa nyoyo) na kutengeneza vizuri hali za watumwa na kuingiza katika nafsi za wanyonge heshima na utukufu.”

Vitabu hivi ni Ufunuo (Wahyi) kutoka kwa Allah amewafunulia Mitume wake, na kinachothibitisha kuwa Qur-aan hii ni Wahyi kutoka kwa Allah, ni kuwa inathibitisha imani ya kila Mtume wa Allah wala haitofautishi kati yao, Allah amesema: “Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya, Hao ndio makafiri kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha. Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu. ” (4:150-152),

Isipokuwa vitabu hivi vilivyotangulia vingi vimepotea na kuharibika sehemu yake kubwa na vikaingiliwa na kubadilishwa na kugeuzwa.

Ama Qur-aan Tukufu Allah amedhamini hifadhi yake Allah Mtukufu amesema: “Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” (15:9),

Na akaifanya iwe ufunuo na kufuta vitabu vilivyotangulia katika vitabu, Allah amesema: “Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda…” (5:48),

Na yule aliyeiteremsha akaisifu kuwa ni ubainisho wa kila kitu; kwa hiyo Allah akasema: “…Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.” (16:89).

Ni muongozo na rehema; Amesema Allah: “…Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema….” (6:157)

$Sidney_Fischer.jpg*

Sydney Fisher

Profesa katika Chuo Kikuu cha Ohio-Marekani.
Kitabu Chenye Kukusanya
“Kwa hakika Qur-aan ni kitabu cha elimu, malezi na utamaduni, haina maana kwamba yote yaliyomo ndani yake ni maneno kuhusu faradhi za Swala na Ibada. Mambo mema ambayo Qur-aan inahamasisha Waislamu mambo mema kabisa katika mizani ya maadili mema. Muongozo wa kitabu hiki unaonekana zaidi katika makatazo yake, kama yalivyo wazi katika maamrisho yake pia.”

Na kuwa huongoza kwa yaliyonyooka (madhubuti), Allah amesema: “Hakika hii Qur’ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.” (17:9)

Humuongoza mwanadamu katika njia iliyonyooka katika kila jambo katika maisha yake,

Qur-aan imekusanya kila kitu anachokihitaji mwanadamu; kwani inakusanya misingi ya kanuni, itikadi, hukumu, miamala, maadili, adabu zake na mengineyo, Allah amesema: “…Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote….” (6:38).

Sunna za Mtume

Allah amemteremshia Mtume wake Qur-aan Tukufu na akampa Wahyi wa Sunnah ya Utume, Allah amesema: “Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa” (53:4)

$Etienne_Denier.jpg*

Etienne Denier

Mchoraji na Mwanafikra wa Kifaransa
Sunnah Tukufu
“Hakika Sunnah ing’aayo ya Muhammad imebakia hadi leo hii. Ikifunikwa na ikhlasi sahihi ya kidini, nafsi za mamilioni ya wafuasi wa Sunnah yake wametapakaa kwenye mgongo wa dunia.”

Nayo ni kama Qur-aan Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Jueni mimi nimepewa Kitabu (Qur-aan) na mfano wake pamoja nao, jueni, mimi nimepewa Kitabu (Qur-aan) na mfano wake pamoja nao” (Ahmad). Ni Wahyi kutoka kwa Allah kwa Mtume wake Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kwa sababu Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) hazungumzi kwa matamanio, Yeye hufikisha kwa watu aliyoamrishwa, Allah amesema: “…Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.” (46:9).

Kwa hiyo Sunnah ni chanzo cha pili katika vyanzo vya Uislamu, nayo ni yote yaliyopokewa kutoka kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) kwa sanadi sahihi inayoungana hadi kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) nayo ni maneno yake, kauli, kukiri au wasifu, nayo ni yenye kusherehesha na kubainisha kwa ajili ya Qur-aan Tukufu; Allah amemuidhinisha yeye abainishe yaliyo ndani ya Qur-aan katika mambo ya jumla, au mahususi, Allah amesema: “…Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.” (16:44);

$Jack_Ressler.jpg*

Jack Rislow

Mustashrik wa Kifaransa.
Qur-aan na Hadithi bega kwa bega.
“Qur-aan ina kamilishwa na hadithi ambazo ni mtiririko wa maneno yanayofungamana matendo ya Mtume Muhammad (Swala Llahu ‘Alayhi Wasallam) na maelekezo yake. Katika hadithi mtu anapata yale yote yaliyokuwa yakitokea kwa Mtume (Swala Llahu ‘Alayhi Wasallam). Ni kipengele cha msingi katika tabia zake mbele ya hakika zenye kubadilika katika maisha. Hivyo basi Sunnah ndio yenye kubainisha Qur-aan wala haijitoshi peke yake.”

Kwa hiyo Sunnah inabainisha Qur-aan na kufafanua ayah zake, na hupambanua hukumu zake za jumla, kama vile Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alivyokuwa akipambanua yaliyokuwa yakiteremka mara nyingine kwa maneno, wakati mwingine kwa vitendo, na wakati mwingine kwa njia zote pamoja.

Huenda Sunnah ikajitegemea bila Qur-aan Tukufu kwa kubainisha baadhi ya hukumu na sheria zake.

Sunnah iliotoharika ndiyo utekelezaji wa vitendo vya Uislamu kwa hukumu, itikadi, ibada, miamala na taratibu zake.

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alikuwa anatekeleza aliyoamrishwa, na kuyabainisha kwa watu na anawaamrisha kufanya mfano wa matendo yake, Allah amewaamrisha waumini kumfuata yeye (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) katika matendo yake na katika maneno yake ili imani yao ikamilike, Allah amesema: “Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” (33:21).

$Leopold_Weiss.jpg*

Leopold Weiss

Mwanafikra wa Austria.
Muongozo wa Sunnah
“Kuitekeleza Sunnah ya Muhammad ni kuhifadhi kiini cha Uislamu na kuuendeleza, na kuacha Sunnah ni kuangusha Uislamu. Sunnah ndio msingi wa chuma ambalo juu yake Uislamu umesimama na ukiondoa muundo wake usishangae kuona jengo lile likianguka kama vile nyumba ya vikaragosi.”

Masahaba wamenakili na kupokea kutoka kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) matendo ya Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) hadi wale waliokuja baada yao, nao wamepokea hadi kwa waliokuja baada yao kisha wakasajili katika Rejesta (diwani) za Sunnah.

Wapokezi wa Sunnah walikuwa wakishadidia (wakiweka mkazo na msisitizo mkubwa) katika yale waliyokuwa wakipokea kutoka kwao, na wakitaka wale wanaopokea kwao wawe watu walioishi zama moja na wale wanaopokea kutoka kwao, ili isnadi iungane kutoka kwa Rawiy (Mpokezi) wa Hadithi hadi kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kuwa wapokezi wote (walio katika mtiririko wa ile sanadi) ni watu madhubuti (wenye kuaminiwa) na waadilifu, wakweli na waaminifu.

$Jack_Ressler.jpg*

Jack Rislow

Mustashrik wa Kifaransa.
Kukusanywa kwa Sunnah za Mtume.
“Hadithi hizi ambazo mkusanyiko wake unatengeneza Sunnah zimeandikwa kutokana na yaliopokewa kutoka kwa Masahaba au kunakiliwa kutoka kwao kwa umakini mkubwa katika kuzichagua kwake; na kwa namna hii kiasi kikubwa cha Hadithi kilikusanywa.”

Inapasa kuamini Qur-aan na Sunnah kuwa ndio vyanzo vikuu vya dini ya Uislamu ambavyo yapasa kuvifuata na kuvirejea na kufuata maamrisho yake, kuacha makatazo yake, kuamini habari zake na majina matukufu ya Allah yaliyo ndani yake, sifa zake na matendo yake, na yote aliyoandaa Allah kwa ajili ya mawalii wake waumini, na aliyokamia nayo adui zake makafiri, Allah amesema: “La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.” (4:65)

Na akasema vile vile Allah: “…Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho….” (39:7)

Ni furaha iliyoje kwa atakayefuata njia hii nayo ni njia ya Furaha!!!