Amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) “Ikisimama kiama na katika mkono wa mmoja wenu kuna mche basi na aoteshe.” (Ahmad). Wakauliza: Ewe Mtume wa Allah Je, mmoja wetu atayaendea matamanio yake kisha atakuwa na ujira? Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: “Je unaonaje kama angeyaweka katika haramu, Je atapata madhambi? Vivyo hivyo akiweka katika halali atapata nayo ujira.” (Muslim).