SIRI YAFICHUKA

SIRI YAFICHUKA

013-SIRI YAFICHUKA

(1)

Joji alijisikia ni mwenye nguvu na furaha zaidi baada ya kurejea kutoka Roma, na kujikuta amekuwa mwepesi baada ya kuwa na msongo wa mawazo, hali iliyomfanya kukesha na kujiulizia maswali haya: Je alivyo kuwa akihisi ni kwa sababu ya kazi na kusoma sana, hali ambayo imemchukua muda mwingi? Au ni kwa sababu ya kuchanganyikiwa na mawazo yasiyokuwa na majibu kuhusiana na Biblia na Mungu, bali na kwa Yesu na kila migawanyiko yake? Au haya anayojisikia sasa hivi isijekuwa ni furaha ya mchezo wa mtoto mdogo kwa kuvunja au kumharibia mchezo wake. Na je hali itakuwaje baada ya kanisa, au mapapa, au wa Biblia litakapovunyika katika nafsi yake, wapi atapata pakwenda? Au atakaa bila dini (kafiri)? Mwenye kukosa upando wa kiroho wa furaha? Kisha alitoa sauti ya kusema, ‘Ewe Mungu, Ewe Mungu’.
Katarina alifurahia safari hii, na kurejea na furaha kubwa sana…..hivi ni kwa ajili ya mume na watoto wake?! Au ni furaha iliyofunua pazia ya yale aliyokuwa akiyashangaa na kufurahishwa nayo, kwani alikuwa akiyatafakari maisha kwa mtazamo tofauti? Kwani alikumbuka mgongano wake na kasisi pamoja na udhaifu wake, na kukumbuka udhaifu wake mbele ya Mmisri na Kitabu chake, na kimya chake mbele ya John Luke na hoja zake na akawa anajiuliza mwenyewe: Mimi nina yakini bora zaidi kushinda shaka, kisha akajiuliza: Kwa nini nina furaha kwa sasa hivi?!
Walipofika nyumbani, na nyoyo zao kutulia. Joji alifungua barua pepe yake kuangalia je amejibiwa na rafiki zake au bado? Na kwa bahati alikuta tayari amejibiwa na wote. Alifuta na kuanza kuwatumia wote kama alivyofanya kwa mara ya mwisho kwa hawa wafuatao:

Levi: Ndio, ijapokuwa ninawachukia Waislamu waliomuua baba yangu lakini hilo ni kwa ajili ya kujua shari ambayo itawafanya kuishi kwa salama. Habib: Ndio, hiyo ni dini ya mbinguni, pamoja na kuwa ujuzi wetu kuijua ni mdogo. Tom: Ndio, huenda nakutana na vitu ambavyo sijaviona kwingineko. Adam: Ndio hasa, maudhui yanahitaji utafiti ili kujua kila dini za mbinguni. John Luke: Ndio, mimi napenda kusoma na kujua kila kitu.

Joji hajapata jibu lolote kutoka kwa Katarina kwa sababu hajafungua barua pepe yake tangu waliposafiri kwenda Roma…..Joji aliandika sehemu ya tano na kuwatumia hao wote…

“Sehemu ya tano: kwa: Hakika nimeshtushwa na majibu yenu wote, Jibu la ndio, na hata kama sababu zinatofautiana. Sasa swali langu la leo ni: Naomba kila mtu aowanishe kwa kifupi kati ya vitabu vya dini tatu za mbinguni: Agano la Kale, Agano jipya na Qur’ani. Joji (London)”.

Zilipita dakika chache baada ya kutuma ujumbe wake, mara simu yake inaita kutoka kwa Tom na Sauti yake ilikuwa inajulisha wasiwasi na huzuni….

Kuna nini?

Hakuna kitu, nilitaka kujiridhisha tu mmefika? Na napenda kukutana nawe, je lini tunaweza kuonana?

Tumefika kabla ya dakika 45, na muda umepita, je tunaweza kuonana kesho? Au kama vipi njoo sasa hivi?

Oh, samahani sikujua muda, nisamehe kwa hilo, basi nitakuja kesho saa nne asubuhi nyumbani kwako.

Nitakusubiri, Mungu akipenda ni kheri tu kwa mapenzi ya Mungu.

Nakushukuru Joji, pia narudia kusema nisamehe.

Simu ya Tom ilimtia wasiwasi Joji kisha haraka alikumbuka ujumbe wa Tom uliosema kuwa kuna mtu amepenya katika kompyuta yake kuingia katika face book yake, na ugomvi wake pamoja na Baraad, kisha alifungua tena kompyuta yake na kufungua ukurasa wa Tom wa face book. Ghafla aliona picha ya Katarina akiwa amevaa vibaya akiwa pamoja na Tom! Alijaribu kuchunguza kwa wawili hao nakukuta ishara ya uso wa Katarina ukiwa dhahiri kutohusika na jambo hilo, picha hizo zilikuwa ni pigo kubwa kwake zilizomsahaulisha furaha yake ya Roma pamoja na starehe zake. Na alijiuliza kwa kusema:

Inavyoonekana kila kitu ni uzushi na kuongopeana mpaka kujua ukweli wake!

Alijaribu kutaka kuwasiliana na Tom lakini aliamua kusubiri mpaka kesho saa nne ili kujua nini kitatokea. Alijaribu kulala ila hakupata usingizi na muda wote fikra za Katarina na Tom hakuziacha kuzifikiria, na hajui nini kilichomfanya kuamini uongo wa Katarina na Tom? Maisha gani haya? Na tabia gani nzuri watu wanajisifia huku wakiongopa? Urefu ulioje wa muda kuondoka! Na hata muda naona unachelewa mara mrefu na mara mfupi ijapokuwa hali hiyo ni moja tu.
Katarina aliamka saa tatu asubuhi, hali ya kuwa Joji bado alilala….alijaribu kumsogelea na kumbusu na kumnong’oneza kwa kusema:

Mpenzi wangu, naomba ruhusa naenda kununua mahitaji ya nyumbani.

Kwa haraka baada ya Katarina kutoka, Joji aliamka akimsubiri Tom aliemuahidi kufika saa nne kamili asubuhi, na mara alimpokea kwa uso wa hasira usio na furaha.

Nasikitika kwa usumbufu masuala ni mepesi ila yenye kusikitisha.

Sema ulichotaka kusema.

Hakika nimeanza vita vikali na Baraad.

Je hukuwa unategemea hilo?

Naam kwa maana (ndio) lakini ni vita vibaya na vichafu.

Je unategemea kutoka kwa Baraad lisilokuwa hilo?

Hapana niache nikamilishe samahani, kwa hakika alinitaka nishirikiane nao katika genge la kuuza madawa ya kulevya au kufanya machafu, nikamkatalia, akanitisha na kurudia kunitisha nikamkatalia, na nimeshtushwa ghafla kabla ya siku chache nikagundua kompyuta yangu sehemu ya face book haifungui, nikajua huenda kuna tatizo katika mtandao, mara tu nikashitukizwa kuona picha zangu za zamani ambazo sio nzuri zinatokea katika akaunti yangu.

Na hili limetokea kwa asilimia100% sio hivyo?

Niache nikamilishe samahani, baada ya kudhihiri picha hizo aliendelea kuniomba nishirikiane nae nikakataa na hapa ikaanza kazi chafu kama mwanzo yakuweka picha za kuzusha ambazo sio za kweli juu yangu. Kwa kuzishusha kwenye mtandao.

Kisha nini unataka kutoka kwangu?

Sijui nikuambie nini, kwani ameunganisha picha ya Katarina na mimi tukiwa kanisani na kuniunganisha na picha yangu akiwa uchi.

Unataka kusema picha hiyo ni uongo na sio kweli katika face book yako?

Ndio sio yenyewe kwa kweli.

Najua unayemzungumzia hapa ni mke wangu na mimi nina hakika kuwa ni picha yake.

Ndio ni picha yake, ila ni picha iliyopandikizwa na sio kweli.

Inatosha Tom…yatosha kunichezea!

Ichunguze picha kwa undani, utajua ni ya kupandikiza.

Toka! toka nyumbani kwangu.

Usinidhulumu na ukamdhulumu Katarina, ewe Joji.

Toka, toka.

Joji alijilaza katika ukumbi hajui cha kufanya, alikuwa katika hali ngumu sana. Simu yake ilianza kuita na kukuta ni namba ya Adam, alisita sita kwa kudhani anamcheza shere na mimi ndio wapekee mjinga wa kuchezewa…nini anataka huyu sasa?!

Hallo, ndio Adam!

Karibu, tumekukumbuka.

Unataka nini?

Hamna kitu, nilitaka kukusalimia tu!

Nashukuru, asante sana, kwa heri.

Joji aliweka simu yake huku akifikiri nini cha kumwambia Katarina atakae fika muda sio mrefu, baada ya kuhisi kudhalilishwa na udhalili wa hiyana na wa kukusudia…alijizuia kidogo kusema baada ya kumuona Katarina anaingia akiwa na tabasamu.

Bado chai haijawa tayari hotelini kama Roma, je umepata kifungua kinywa au unapenda nikuandalie chochote?

Sitaki chochote.

Kama ni hivyo kunywa kikombe cha maziwa au chai?

Ahsante.

Nisaidie tule pamoja japo kidogo.

Nimekuambia sitaki kula chochote hunielewi?

Joji una nini?

Siri imefichuka ewe Katarina.

Siri gani?

Alifungua ukurasa wa Tom mbele yake….na kuondoka kwa hasira chumbani huku akifoka kwa maneno.

Tazama, ewe mfanya ibada na mchamungu, wewe ni mnyama mdogo na ukiingia katika utawa utakuwa mnyama mkubwa kwa matendo machafu kama makasisi, na watawa makanisa –angalia.

Katarina aliangalia zile picha na kumrudia Joji huku akilia…..

Tom ni muongo sana, hizi sizo picha zangu.

Je unataka kuwa msanii uliobobea kwa kuendeleza maigizo? Ili kesho mlale pamoja…..

Niamini, mimi sio mwenye kufanya haya, huu ni uongo wa wazi wa Tom. Je hukuniambia mara kwa mara kwamba yeye sio mtu mwenye tabia nzuri tena asie na dini?.

Sio wewe ulie nisisitiza niende kwake? Sio wewe uliomfundishia dini? Sio wewe uliyesema amebadilika!

Sikutegemea unishuku tena…

Katarina aliishiwa na nguvu huku akilia kwa uchungu kisha akajikaza na kwenda katika kompyuta kwa mara nyingine akawa anaangalia zile picha huku akitukana na kumlaani Tom wakati akiwa anazichambua, mara jicho lake likaona picha ya kupandikiza na kuipeleka kwa Joji haraka.

Angalia picha iliyotengenezwa, je kifua hiki ni sawa na kichwa hiki?!

Maneno kama ya Tom, ya kusema picha ya kupandikiza, je huu ni mlango wa pili wa maigizo?

Angalia vizuri.

Huenda ikawa hivyo, lakini sitaki kuwa mjinga kwa mara nyingine wa kuamini maigizo yenu kwangu!

Vipi Tom anasema ni ya kupandikiza wakati yeye ndio aliyoiweka?

Tom amekuja na kudai Baraad ameiba kompyuta yake na yeye ndie aliyetengeneza na kuweka picha hii kwa kumkomoa.

Baraad! Kwa nini anafanya hivyo kwa kumkomoa?

Hili ni hitimisho la maigizo katika tamthilia, eti kwa kuwa amekataa kushirikiana nao katika kuuza madawa ya kulevya.

Mimi sijamuelewa anachodai, ila naamini picha hizi ni za kupandikiza bila shaka.

Inawezekana ni za kubuni au ni za kweli, je hajakutumia ujumbe ya kuwa akaunti yake ya face book imeibiwa? Au tumefungua ukurasa mpya wa maigizo?

Sijamuona Baraad tangu tusafiri kwenda Roma, hebu nipe kompyuta niangalie huenda nikakuelewa.

Katarina alifungua akaunti yake katika face book na kukuta barua mbili….barua ya kwanza inayompa taarifa kuwa Tom ameibiwa akaunti yake na barua ya pili inaonyesha picha mbaya za kufedhehesha, kama picha ile ya Tom iliyopo katika face book yenye ujumbe usemao: (Huu ndio ushahidi wa kweli wa kujivua) aliziangalia kwa umakini na pembeni ya Tom alikuwa ni Joji na sio yeye!

Bali wewe ndio ulionifanyia hiyana, angalia picha hizi.

Nikufanyie hiyana na nani sasa?!

Na Tom, je huoni ni kinyume na tabia za watu ewe Mprotestanti?

Joji alizichunguza picha na kujua ndio zenyewe na kwamba ni za kupandikizwa…Joji aliinama chini kidogo kisha kuinua kichwa chake kwa sauti kali yenye kutisha….

Unajua nimemfukuza Tom hapa nyumbani.

Joji unanishuku mimi?

Na nimekata simu ya Adam nikidhania kuwa anataka kuendelea na kutaka kukamilisha igizo kwa makubaliano na Tom!

Yote haya ya nini Joji?!

Adam amenisihi sana kutokuchukua maamuzi wakati wa hasira au unyonge, sijui nifanye nini sasa?! Samahani Katarina, nimekuvunjia haki yako.

Yatosha msamaha tu baada ya yote haya?!

Unataka nini nikufanyie?

Sijui ila msamaha unatokea baada ya ukubwa wa makosa?

Nakuomba nisamehe, nitaangalia nini naweza kufanya kuhusu Tom na Adam.

Ijapokuwa umenijeruhi kiasi kikubwa ila sikutegemea kama unaweza kunifanyia hivi, pamoja na hilo nakusamehe kwa sharti la kufuata nasaha za Adam ulizonitajia.

Asante Katarina, wewe ni mtu mwenye moyo mzuri sana, sijui nikushukuru vipi na kukusahaulisha makosa yangu kwako, kisha alisimama na kumkumbatia na kusema, nitazingatia suala langu hili na Tom na Adam, je unaniruhusu nipumzike kidogo peke yangu?

Sawa karibu, japo umenijeruhi ila nitamuomba Mungu akusaidie kwa msaada wake.

Joji alikaa mbele ya kompyuta yake na kufungua barua pepe yake kwa kumuandikia ujumbe Tom unaosema hivi:

“Rafiki yangu Tom. Baada ya kutokea yaliyotokea kati yangu na wewe, naomba nisamehe kwa kukuvunjia heshima yako, umekuja nyumbani kwangu kuomba msamaha na nilitarajia kukusamehe, nirudishie kama nilivyokufanyia, na ukitaka nije kwako na unifukuze kama nilivyokufanyia mimi nipo tayari kuja, narudia kusema nisamehe sana Mimi Joji.”

Baada ya hapo alimpigia Adam pale pale na kumuomba msamaha….

Adam, hakika nimekuletea mkoba mkubwa na kwa bei nafuu sana.

Je umepata? Na kwa sifa hizi?

Ndio, na lini utakuja kunitembelea ili unichukue?

Haa haa…angalia muda wako unaofaa mpaka usije kuniambia maneno kama ulivyoniambia leo.

Ni muda gani unaokufaa, nisamehe kwani nilikuwa katikati ya udhaifu na wasiwasi, huenda tukikutana nitakueleza.

Njoo kwenye mgahawa, kwani muda mrefu hujanitembelea hapo.

Vizuri… nitakutembelea leo au kesho.

Alimaliza maongezi, na akawa anatafuta barua pepe huku akisubiri ujumbe kutoka kwa Tom…akakuta ujumbe ambao Tom aliutuma kwa Katarina alimtumia naye vile vile wakati akiendelea kutafuta, alipokea ujumbe wa jibu la barua yake.

“Sikia na utekeleze yale ninayokuambia, huenda nikakusamehe: Utakuja kesho katika zahanati saa moja jioni, na mimi nitaamua kukufukuza au hapana. Usirudie muamala huu mbaya wa kuhamaki. Tekeleza yale ninayokueleza haraka iwezekanavyo baada tu ya kuusoma. Ni mimi Dr, Tom”.

Joji alimjibu:

“Rafiki yangu Tom mimi nakubaliana na wewe na hata ukinifukuza mimi bado nimekosea. (Joji).”

Baada ya kumjibu Tom aliwasiliana nae kwa kumkaribisha…

Karibu

Asante, naomba tena nisamehe kwani nilikuwa nina hasira.

Usijali, lakini mimi nimesahau kutaja sharti lingine, na ni lazima ukubaliane nalo…

Lipi hilo?

Ha ha ha… Joji kila kitu kimeisha, nilikuwa najoki tu na wewe, kesho tuonane katika mkutano wetu muhimu sana.

Nakushukuru Tom.

Ikiwa utachelewa katika… ha ha ha, mimi nakusubiri.

Nitakuja katika wakati huo ili unifukuze…narudia kusema nisamehe.

(2)

Mwishoni mwa mazungumzo ya Joji na Tom alikumbuka ahadi yake ya kukutana na Adam.

Nitakwenda sasa hivi kumtembelea Adam pale mgahawani.

Adam ni mtu wa hekima na mwenye akili, na nisingekuwa na kazi ningeenda na wewe.

Kweli, lakini sijui yeye anafaidika nini na usuhuba wangu?!

Urafiki sio mpaka tubadilishane na vitu kama pesa.

Huenda ni kupata chakula cha mchana pamoja na hii ndio faida pekee anayoipata kutoka kwangu kwani yeye anaishi peke yake.

Joji aliwasili mgahawani na kupokewa na Adam, na kumwambia muda wao hapo mgahawani ni nusu saa tu na akamshauri anywe kahawa ndani ya muda huo. Baada ya hapo Adam alimaliza muda wake na kuelekea kwa Joji na kuamua kwenda kupata chakula cha mchana katika mgahawa wa furaha.

Mbele yetu tuna muda wa saa moja kwenda na kurudi pamoja na kula chakula sawa… Sasa niambie vipi ngome ya kanisa Katoliki na kituo chake kikuu?

Je hutakasirika nikikueleza?

Inavyo onekana unaguswa sana na mambo, nini cha kunikasirisha ewe Joji?!

Haiwezekani kusadikisha Agano la Kale wala kuiamini, kwani halinifai, sio Uyahudi, Ukatoliki, Uprotestant wala Uislamu.

Kwanza, kwa nini juhudi zote hizi dhidi ya torati? Je hiyo ni kwa sababu ya kipande cha maneno ulichotutumia?

Hili ni moja, lakini nina sababu zingine mia moja mfano wake kwamba imepotoshwa.

Na Agano Jipya?!

Nalo ni hivyo hivyo, japo hilo lina afadhali.

Na Qur’an?!

Kwa sababu inaamini agano la kale na linalopita na kama hizo vile vile

Nakuomba usiwe na haraka kutoa hukumu.

Pamoja na yote hayo, kuna masalia ya hisia zangu kuwa nitapata majibu ya maswali yangu.

Kwa dhati kabisa utapata majibu.

Tatizo ni kuwa hakuna dini yoyote iliyokuwa sahihi; kwa maana hiyo suluhisho ni kukana Mungu!

Haiwezekani hata siku moja ukanaji Mungu ukawa ndio njia ya furaha.

Kwa hiyo njia ni ipi?

Endelea kutafiti na utapata jibu.

Haa haa, huenda ni Uislamu au dini ya ugaidi!

Pindi ulipotuuliza ni nani ambaye anataka kuujua Uislamu majibu yalikuwa ni ndio pamoja na kuwa na dini zetu tofauti, kwa nini sasa wewe hutaki kuusoma Uislamu na kuujua?!

Mimi nakuzidini sana katika kutaka kuujua Uislamu, kwa sababu nyingi tu zaidi ya hizo mlizozitaja, zatosha kama hazifai hazitafaa dini nyinginezo.

Sijui kama utasoma dini kwa njia hii!

Tumeshafika hoteli ya furaha laiti tungeifikia njia ya furaha, tumalizie mazungumzo yetu ndani.

Walichagua meza yenye kuwafaa na mhudumu hakuchelewa kuchukua oda yao ya chakula nakuondoka, na wakati huo Adam alimuangalia Joji kwa umakini.

Nitakamilisha niliyotaka kukueleza, ulipokuwa unajiandaa kwa safari ya Roma, na kusoma kuhusu Ukristo nilikueleza nini?

Nilikueleza: Tengemana nayo kwa uhuru zaidi, yaani usome kwa kujua kabla ya kulihukumu jambo kwanza.

Na mimi nakueleza hilo tena sasa, na wala usipende kusoma Uislamu bila kutumia njia hiyo.

Na nimeanza kufikiri jambo hilo nikiwa kwenye ndege ni vitabu vipi nitavisoma kuhusiana na Uislamu.

Je unataka nikushauri?! Anza kuisoma Qur’an kabla ya kitabu chochote kile.

Kwa nini nisingeanza na Uyahudi na Ukristo kwa kusoma vitabu vyao mwanzo?

Kwa sababu Uyahudi haukusukumi kusoma Agano la Kale bali wanaficha baadhi ya aya kwa malengo yao, na Ukristo haukuvutii kusoma Agano Jipya moja kwa moja, bali inapasa uelewe kama waelewavyo wanazuoni wa kiyahudi na makasisi.

Na Qur’an je?

Sijakueleza wewe kwamba hutaujua Uislamu, kwani Uislamu umeifanya Qur’an ndio chimbuko la elimu, na kutoa habari njema, maonyo, ujumbe kwa Waislamu na wasio Waislamu.

Adam inaonekana umeusoma sana Uislamu, je umeusoma kupitia masomo yako ya dini mbali mbali?

Ndio.

Kwa kweli ni ipi rai yako kuhusu Uislamu?

Mfano wako, si wa kupewa rai, soma Qur’an na uchukue ushauri na uamuzi mwenyewe.

Kwa dhati ni ipi dini yako? Nilidhani tangu mwanzo wewe ni Myahudi au Mkristo ila kwa sasa unaonyesha wewe ni Muislamu.

Je haiwezekani pia nikawa Mbudha au Mhindu, unakumbuka nilipokuambia kuwa ni vizuri kuujua Ubudha au Uhindu, napenda kukuhakikishia kama mtu hatakuwa na akili yenye kufikiri mbali zaidi na kuondokokana na akili finyu, hatopata maendeleo kamwe, kama ambavyo nataka kukueleza dini na dhehebu langu baada ya kutaka kujua kila unachotaka kujua kunako njia ya furaha, na huenda ikawa njia hii ndio mbadala wa dini zote.

Sijapata mbadala wa dini zote katika akili yangu katu.

Isome Qur’an, halafu yaliyo andikwa na Qur’an juu ya Uislamu na Mtume wake, kisha linganisha na dini zote, uwezo wa kufungamanisha kati ya maudhui na maarifa uliyonayo ni jambo muhimu sana kufaulu.

Vipi nitafungamanisha kati ya maudhui haya?

Ili usipoteze dira ambayo unakwenda nayo, kumbuka kile usicho kitaka katika Ubudha au Uhindu na uhakikishe hakipo katika Uyahudi, kisha katika Ukristo na sasa hakipo katika Uislamu, na kile unachokiendea katika Ubudha kwa mfano uthibitishe kuwepo katika Uyahudi au Ukristo na Uislamu na kwa hivyo utaoanisha kati ya maudhui.

Mtazamo huo wa mambo kwa ujumla wote unanipendeza kati ya ninachotaka na nisicho kitaka.

Na uchunguze mfanano kati ya dini mbali mbali na tofauti zilizopo pia.

Kwa masikitiko naona mfanano wa dini ni mkubwa kuliko tofauti iliyopo.

Ukifungamanisha itakuzidishia akili na kufikiri zaidi, na hakikisha kuwa unafungamanisha kadhia za jumla na sio katika vipande vipande tu.

Kwa kuwa mimi naona kuna kufanana kwani wote wanaamini Agano la Kale, na naamini kwamba mwenye kuamini hivyo ni mwenda wazimu.

Lakini Wakristo wanaamini kwamba Agano Jipya limekuja kukamilisha Agano la Kale kwa Imani yao hiyo. Wakati ambapo Wayahudi na Waislamu hawaamini kama wanavyoziamini, kadhalika wanaamini kuwa imepotoshwa, na ya kuwa hii iliyopo sasa sio maneno kutoka kwa Mungu, na wanaiamini Qur’an, na ndio imekuja kufuta yaliyotangulia, je mpaka hapo huoni kuwa kuna tofauti kubwa?

Ndio…tofauti kubwa sana, kwa tabia yangu mimi naangalia katika kufanana zaidi kuliko tofauti, na wala silinganishi baina ya maudhui sana.

Vizuri, kujua tatizo ndio suluhisho, hivyo utakuwa umefikia kwenye suluhu ya maudhui, na utakuwa na uwezo wa kuangalia kwa ukamilifu wake, ikiwa umemaliza kula ni vizuri tuanze kuondoka ili nisichelewe kazini.

Ndio nimemaliza, haya twende, nisije kusahau, mkoba wako mkubwa sana wa bei rahisi ninao kwenye gari.

Japo umenicheka ila umeniletea kwa sifa nilizozitaka.

Ghafla kulikuwa na duka moja linafanya seli ya baadhi ya mikoba, na huu ndio ulikuwa mkoba wa mwisho kwa ukubwa huu.

Jambo lolote la ghafla na lisilotarajiwa linabainisha ni kiasi gani watu wasivyojua kile alichowakadiria Mungu, kwa masikitiko wengi wetu hatujui kulitumia neno ‘bahati’ wakati hatujui limetokeaje jambo, na kwa hili, tunajiona tunajua kila kilichopo ulimwenguni ikiwa kitatokea kitu hatukijui tunalitumia neno ‘bahati’ kama kwamba kutokujua ni kutokuwa na elimu na bila shaka ni katika aina ya mshangao, kujidanganya, ghururi isiyotakiwa…au ni aina ya kuathirika na ukafiri pasina kujua hilo.

Umenichosha na falsafa yako na istilahi zako ngumu, haahaa. Mungu ameniwezesha kufika na ikawa mkoba mmoja umebakia, je nimefaulu mtihani wangu?

Haa haa, kwa sharti begi hilo liwe kubwa sana na rahisi pia.

Ikiwa ni hivyo nimefaulu na hili hapa begi, chukua.

Vizuri, kwa hakika umepita mtihani, na hii ina maanisha kuwa wakati mwingine hatuwezi kufahamu uhakika wa jambo kwa akili zetu tu.

Lakini haiwezekani uhakika ukatofautiana na akili, kwani haiwezekani ukweli halisi uwe kinyume na ufahamu wa akili yenyewe, vinginevyo moja wapo sio kweli.

Swadakta, umetofautisha ilivyo, kwa idhini ya mwana falsafa?!

Leo nimemkosea Tom kwa kumfukuza nyumbani, na nimemuomba msamaha na amenisamehe, na kwa mnasaba kesho nina kikao nae.

Umemfukuza nyumbani na umemuomba msamaha akakusamehe! Kweli ni mtu mzuri, sikutegemea Tom anaweza kubadilika haraka kiasi hivi!

Unakusudia nini?

Tom kama ulivyonitajia amekuwa anabadilika kuwa mwema, kwa kawaida mtu hahami kutoka katika tabia mbaya kwenda katika maadili mema kwa haraka.

Je hukukutana na Tom tena baada ya kufahamiana nae hospitalini?

Ndio, mara nyingi tu tunakutana.

Mara kwa mara?!

Ndio, kwa hakika nimefurahishwa nae, na yeye pia inaelekea amenifurahia pia?

Ni ipi tathmini yako kwake?

Ni mtu mwenye akili, mwerevu na yupo katika kipindi cha mabadiliko makubwa.

Anabadilika kutoka hali gani kwenda ipi?

Mabadiliko kutoka hali aliyokuwa nayo na kwenda kuzuri zaidi.

Ni ipi hiyo hali nzuri zaidi?

Inawezekana ni njia ya furaha ambayo nawe unaitafuta.

Aipate yeye… nisiipate mimi?

Je nawe hauko katika mabadiliko hayo vile vile kama yeye? Kama kwamba una muonea wivu hutaki aipate hali hiyo!

Sawa, la muhimu zaidi, itakuwaje utakapo kutana nae kikaoni?

Kama kawaida

Kama kawaida?

Wewe unajua zaidi kuliko mimi.

Kawaida huwa ananiuliza niliyoyasoma kwanza na mijadala niliyofanya, kisha tunaanza hatua nyingine mpya.

Hili ndio lenye kutarajiwa.

Je unategemea nijadiliane nae juu ya Ukristo ulio haribiwa? Au niusome Uislamu usio na maendeleo?

Naam, ndio, nategemea yote hayo.

Na ili nikamilishe yote hayo kwa uadilifu kama nilivyo fanya katika dini zilizopo duniani pamoja na Uyahudi na Ukristo lazima nisafiri katika milima ya Tora bora, je bado lipo hilo kwenye akili yako ewe Adam?

Haa haa, ndio… nadhani bado ninafikra hiyo, kama unafikra hiyo kama ulivyosema ni kuwa muktadha wa uadilifu ni usafiri huko kama ulivyosafiri kutafuta dini nyinginezo….haahaa ha, lakini sio lazima kwenda Tora bora!

Mimi sio Muislamu ili niweze kusafiri kwenda Makkah, labda nijifanye Muislamu, ndio niende huko.

Je unafikiri utafikia njia ya furaha kwa uongo?!.

Nini nitafanya ikiwa Uislamu ni mgumu? Nimesafiri mpaka Roma ijapokuwa mimi sio Mkatoliki, bali unaweza kuingia hata Vatican hata kama wewe sio mwanadini (kafiri).

Najua unachokusudia, je inawezekana kwa mtu kutoka Makah na kuingia Uingereza bila kukamilisha masharti ya kuingia?

Nimefahamu unacho kusudia lakini masuala hapa ni tofauti.

Hakuna tofauti hapo, kama hujakamilisha sharti huruhusiwi kusafiri popote duniani, na je inawezekanaje kwa fukara kuingia na kula katika mgahawa wa kifahari kama tulivyokula sisi na huku hana hela?

Sahihi…ila huenda nikawa sina masharti ya kuwa Muislamu.

Huenda lakini nani anajua.

Wewe leo hii umekuwa mtu wa ajabu kabisa, tumekaribia mgahawani, lakini tuna ahadi ya kukutana hivi karibuni.

Haa haa, kwa furaha tele nasubiri simu yako…au tutaonana huko Tora bora.

(3)

Joji alifika kwa Tom katika muda uliopangwa na kukuta mlango wa kliniki ukiwa umefungwa aligonga na Tom alimfungulia kwa kumkaribisha.

Karibu…samahani kliniki imefungwa mpaka zogo la Baraad litakapotulia, kwani bado ana waathiri watu wote kazini na utaratibu mzima wa kazi.

Sasa utafanya nini?

Sijajua ila litaisha kwa hali yoyote.

Kwa nini hufanyi mazungumzo ya kupatana nae?

Nipatane nae! Juu ya nini?

Sijui, muhimu ni kujikinga na shari na maudhi yake.

Shari na maudhi yake ni bora kuliko yale anayonitaka, japokuwa maudhi yake yamezidi, lakini ni mwenye furaha kuliko hapo nilipokuwa pamoja na huduma zake nyingi!

Maisha yamejaa mifarakano mingi na mambo ya ajabu. Mtawa anafanya machafu, na Mtume anavua nguo, na Mungu anaua, pamoja na hivyo hatupaswi kupinga au kukosoa.

Acha tuingie katika maudhui yetu, vipi umelionaje kanisa Katoliki kwa ukweli wake?

Kwa kweli nimeliona katika hali ambayo akili haisadikishi.

Huenda ikawa hivi kwa vile wewe ni Mprotestanti ndio maana!

Kanisa la Kiprotestanti lina fanana sana na Katoliki! Naamini tatizo sio hili na lile….

Tatizo lipo wapi?

Kwa kweli tatizo lipo katika upagani.

Upagani?!

Nimechoshwa sana katika kulifikiria hili, lakini huu ndio ukweli, upagani wa kipapa, upagani wa utatu, upagani wa masanamu, upagani…

Huenda ikawa tatizo lipo kwenye kanisa?!

Hapana, kiini cha tatizo lipo kwenye kitabu kitakatifu chenyewe, sawa katika Agano la Kale au Jipya (torati na biblia). Nakuondoa utata huu, Kanisa Katoliki limeona kuwa kitabu kitakatifu kisisomwe ila na makasisi tu. Na wao ndio watawawekea wazi watu, ama kanisa la Kiprotestant linawahimiza wafuasi wake kusoma na kufasiri kama watakavyo.

Uchambuzi wa kina kabisa, lakini nini kimesababisha hayo yote kwa mtazamo wako?

Sababu ni kwamba mwandishi wa kitabu kitukufu amekibadilisha yaliyomo ndani, kisha makasisi wakakifanyia mageuzi, kisha kikabadilishwa na kubadilishwa, na hakihesabiwi kitabu hiki chenye migongano ambacho kiko kinyume na uhalisia wenyewe wa kiakili ulivyo kuwa kimetoka kwa Mungu.

Na kwa nini hakikuandikwa kipindi cha Masiya?

Kwa sababu wakristo walikuwa wanateswa sana! Na kuandamwa kila sehemu; na kwa hiyo hakikuandikwa ila baada ya kufa kwake kwa muda mrefu, na tena walioandika ni watu wasiojulikana kihistoria tena kuna tofauti ndani yake, na kwa lugha nyingine ambayo sio lugha ya Yesu, kwa kifupi ni mtego, haiwezekani kutoka katu, na ndio maana kukaonekana kupingana kwake na nakala mbali mbali, bali hata katika nakala moja pia kuna mgongano wa akili, mantiki pamoja na uhalisia na elimu.

Inatosha haya, inavyoelekea wewe unachuki na kitabu kitakatifu!

Sina chuki nacho kamwe, ila niamini kuwa nimejaribu kukiheshimu na kukitii kwa kadri ya uwezo wangu!

Hebu niweke wazi vipi umekiheshimu na kukitii?

Nitakupa mifano miwili, kwanza: Hakika naamini kilichopo kwenye kitabu kitakatifu, kwani natezwa nguvu mpaka nisitumie akili yangu, na ikiwa nitaitupa akili yangu basi sitaelewa maana yake kwa asili yake.

Ni falsafa nzuri ya vitendo…kwa akili nzuri.

Mfano wa pili ni: laiti nikiamua kukielewa na kuheshimu na kuweka akili yangu kando, basi kitabu chenyewe kinaniambia: “sio chako”!

Vipi sio chako?! Weka wazi.

Je katika kitabu kitakatifu hakuna kauli ya Yesu isemayo: “Sikupelekwa ila kwa kizazi cha wana wa Israel waliopotea.” Na mimi sio katika wao, kwa hivyo hakutumwa kwangu kabisa.

Kwa hivyo wewe sio mkristo?!

Huenda, niamini, sijui …naogopa nisije kuwa mpingaji Mungu kwa sababu yako!

Hii ilikuwa ni mbinu yangu ili ukufuru, na nachelea kusema kuwa umefanikiwa, lakini nimebadilika kwa jinsi nilivyokuwa, na narudia kukuambia mimi kwa uchache naujua ukafiri kuliko wewe, hakuna ukafiri wa kweli; isipokuwa ni madai ya kutaka kukimbia mambo haya, unaweza kukimbia ukafiri, au pombe, au kuzini au kitu kingine chochote, ili uishi maisha ya shida na mabaya, huku ni kukimbia ukweli wa mambo kuliko uhalisia wa ndani.

Ndio, inaelekea mbinu yako imefaulu, naogopa kukosa matarajio ya kufikia katika njia ya furaha.

Huenda ni kwa ajili ya kutojua kwetu tumepetuka mpaka na kuacha kuchunguza na kujua mambo vizuri, kwa vyovyote vile tusichukue maamuzi kabla ya kufikia mwisho.

Una maana gani kwa kauli yako: Kwa ujinga wetu tunaacha kitu tusichojua?! Msemo huu ni kama msemo wa Kikatoliki.

Kuna ukweli kiasi fulani, lakini haiwezekani akili na mantiki kukubali fikra kuwa tumekosea, au tunaelekea kukosea?

Ndio, akili inakubaliana na hilo, lakini kinyume chake hakikubaliwi, na kujiona siku zote kuwa upo sahihi huko ni kwenda kinyume na akili.

Haa, haa, vizuri. Kwa hiyo Ukatoliki una nasibiana na akili…cha muhimu tumekubaliana tusichukue maamuzi mpaka mwisho.

Naomba isijekuwa huu ni utangulizi kama ilivyokuwa ni ada; ili uniambie tusome Uislamu kwanza.

Kamwe nitakuambia hilo, bali mimi kwa hakika nimeanza kuusoma Uislamu, na najipinda kuusoma kwa dhati, je sijakueleza kwamba nimeanza kutafiti njia ya furaha pamoja na wewe?

Joji aliupiga mkono wake kwa mkono mwingine:

Inavyoonekana tumeanzia na njia isiyokuwa na mwisho wake.

Nimeanza jana kuisoma Qur’ani, kitabu kitakatifu cha Waislamu.

Haa haa, hata mimi amenihimiza Adam kuisoma, ila sijamjibu, lakini nahisi nitapoteza muda wangu tu.

Adam ndio alionipa nakala zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza kwa matarajio ya kwamba huenda baada ya kusoma nitaingia katika Uislamu.

Anakutaka uingie katika Uislamu! Nini faida yake kwa hilo?

Kila watu wanawalingania watu kuingia katika dini zao na kufuata fikra zao.

Sijakuelewa! Unakusudia nini?

Kitu gani hujakielewa, Adam anataka niingie katika dini yake, sasa kitu gani hapa hakipo wazi?

Adam ni Muislamu?

Ndio, bila shaka anaonekana wazi katika sura yake yeye ni Mwarabu, hukuwa unalijua hilo?

Ndio, sikuwa najua, na jina lake sio la Kiarabu, fikra yangu ilikuwa kwamba yeye ni Mkatoliki mwenye asili ya India, nina shaka asije kuwa Adam ananichezea.

Ama kwa upande wa jina lake ni jina la baba wa watu wote, lipo kwetu sisi na kwa Waarabu, ama kuhusu kukutania nadhani sidhani kama ni kweli, ila kama atakuwa amekuongopea, je umejaribu kumuuliza?

Nimemuuliza zaidi ya mara moja lakini hakunijibu, la msingi je alikuwa akinielekeza ili nifike katika Uislamu? Sipendi kufanywa mpumbavu?

Je mtu akiwa anakuita kwenye dini yake ndiko kuwa mpumbavu?!

Hapana, lakini naogopa tu.

Hakuna kitu cha sisi kuhofia, ila kama unaogopa kuingia katika Uislamu!

Ndio naogopa kuingizwa katika kitu nisichokuwa na elimu nacho au kutumia akili.

Je wewe ni dhaifu kiasi cha Adam kukukokota, wakati makasisi na wengineo hawakuweza kukukokota na kukukinaisha?! Au ya kuwa Adam ana nguvu kiasi kikubwa akakufanya wewe kumuogopa?

Joji aliashiria kwa mkono wake:

Sio hili wala lile, kwanini unaniambia hivyo?!

Kwa sababu wewe ulikuwa ni simba kwa kila dini na sasa umegeuka na kuwa sungura kwa kuuhofia Uislamu.

Sio kama naogopa, nitausoma Uislamu…na kwa mnasaba wa maongezi yako kuwa nimebadilika, Adam ameanza kuandika kuhusiana na mabadiliko yako.

Mabadiliko yangu?! Mimi bado sijamalizana na Baraad, anaripoti nini tena huyu?

Ameingiza ukurasa wake katika facebook, na soma yale yaliyoandikwa.

Nitarejea kwake, lakini tuachane na hili, la muhimu utasoma Uislamu kwa akili huru iliyotulia kama ulivyo soma dini nyingine kabla yako?

Sawa, tumekubaliana.

Na utakosoa kama ulivyofanya kwa dini zingine kabla yake?

Ndio, tena zaidi ya hapo.

Hapana, huku sio kuwa huru ambapo tunakuzungumzia, kauli yako ina ukosoaji mkubwa, kujifunga na kukosoa kupita mpaka, usome bila upendeleo kama ulivyosoma dini za duniani au kama Uyahudi na Ukristo.

Haa haa je unanitaka nisilimu wala nisiukosoe?!

Bali nataka uusome kwa kufunguka, kwa kuchunga elimu, kisha baada ya hapo uukosoe kama ulivyoukosoa Uyahudi, Ukristo na Ubudha.

Lakini hata hizo nilisoma na kuzikosoa kwa kadri nilivyoelewa kwa akili yangu na kubaini upotoshaji wake kwa uchache.

Kama ni hivyo tafuta upotofu wa Uislamu vile vile, lakini nitapendelea tusome zaidi, na baada ya hapo tuchukue maamuzi, kwani tutagundua ambayo yalikuwa hayapo katika ufahamu wetu.

Na baada ya kugundua yasiyofaa na tofauti zake tutakuwaje? Je tutarudi katika ukafiri?

Sijui?! Ila ninachokijua huenda kikatokea kitu ambacho hatukitarajii kama nilivyokuambia hapo kabla.

Kwa kuwa umeshaanza kuisoma Qur’an, vipi umeionaje?

Nilianza jana na sijasoma sana ila kidogo tu, lakini ni nzuri.

Haahaa, inaelekea nimeanza kuwa na wasiwasi ninahofu huenda na wewe ukawa ni Muislamu pia.

Hapana…kuwa na tumaini, mimi sio Muislamu.

Kwa hiyo wewe ni nani?

Mimi ni kama wewe tu, sijui, nahisi nimebadilika haraka.

Maneno yako ni kama ya Adam juu yako, kwamba unabadilika.

Huenda maneno yake ni kweli, nitasoma alichoandika kuhusu mimi leo, lakini jina lake kwa ukamilifu ni lipi ili nilione kwenye facebook?

Kuna barua pepe yake utaiona katika ujumbe wangu, utaweza kuupata ukurasa wake.

Vizuri, la muhimu tuusome Uislamu kwa moyo safi ulio huru.

Haahaa, tutasafiri kwenda Afghanistan au Tora bora ili tupanue mawazo vizuri.

Sijajua kwa nini unasema hivyo kama kwamba kwa hakika utakuwa Muislamu?

Hiyo ni dharau tu.

Kwa mnasaba je, hujazozana na Katarina kwa sababu ya fikra yako juu ya Ukatoliki?

Ndio, inaelekea amejisalimisha nami kabisa.

Kwa nini ameenda kanisani? Nilikuwa nahisi ukweli wa imani yake na mapenzi yake kwa Yesu.

Ndio, ni kama hisia zangu, lakini cha mshtuko uliomtokea katika Ukatoliki na itikadi zake ni mkubwa, fikiria alibabaika sana tulipokutana na Muislamu Roma!! Na alichanganyikiwa alipojua kuwa yule kasisi aliyemfundisha imani na yakini hakuweza kunikinaisha juu ya shaka nilizonazo!

Nimefurahishwa sana na dini na imani yake!

Kama ni hivyo na wewe elekea kwenye Ukatoliki.

Pia ni kiasi gani nakerwa na mgongano na kuwa kinyume na elimu!

Haa haa, kama ni hivyo, kuwa Muislamu basi? Na uende katika milima ya Tora bora.

Ninaamini ikiwa nitaridhishwa na Uislamu, na ikawa ni budi kwenda kusafiri Tora bora nitaenda.

Napenda hamasa na kuazimia huku, ila nasikitika sioni pa kutokea mwisho wa safari.

Na hata mimi, ila nina uhakika itadhihirika hata kama ni ghafla tu, ila usiniulize vipi, lakini mwenye imani sana na hilo.

Nami nina imani na hisia kama zako.

Hukututumia japo kwa ufupi majibu yetu juu ya ujumbe wako kama unavyofanya siku zote!

Umesema kweli, jana sijaona ujumbe kwa sababu ya picha zako, nitatuma leo, na leo nitakuwa makini na majibu ya Adam kwani ni majibu ya Muislamu.

Alikuwa wazi sana katika majibu yake yaliyotangulia.

Huenda, mimi sijachunguza, na kiujumla ameandika hivyo kuhusu mimi kwa sababu sifungamani na maudhui, matukio, mijadala pamoja na mafunzo.

Mafungamano ni muhimu sana.

Ni kama maneno ya Adam, inaelekea unapendezwa sana na yeye.

Sikujua kama hii ni rai yake, kwa kweli sikuvutiwa na raia yake zaidi kuliko kuvutiwa zaidi na mlingano wake wa ndani.

Naungana na wewe kwa huo mlingano wa ndani, na mimi nimevutiwa na fikra zake pia, kwa mnasaba je umeshaondoa kifaa cha kunasa sauti alichokiweka Baraad?

Ndio, mara ngapi natamani kuachana na Baraad na maudhui yake, ana niunganisha na ulimwengu wa zamani wenye huzuni!

Utaachana nae karibuni tu, je utaniruhusu niondoke?

Ndio, naona tumeshamaliza kikao cha leo, kwa mtazamo wangu naona kilikuwa ni kikao muhimu sana.

Kwa hivyo basi tutaanza na Uislamu, nitarejea kazini na kumkabili Kakhi, ni kiasi gani nawachukia!

Akina nani unawachukia?

Uislamu pamoja na Kakhi.

Umerudi tena kuukosoa kwa mara nyingine.

Oh, nimesahau, sikutanabahi, haa haa, ukweli ni kuwa Kakhi na Uislam ni kitu gani kinachotusubiri unavyoona!

(4)

Joji alifungua barua pepe yake jioni alipowasili nyumbani… na kukuta marafiki zake wakiwa wamemjibu swali alilowauliza kuhusiana na ulinganifu kati ya dini tatu:

Levi: Sijaisoma Qur’an lakini nadhani dini zote tatu zina fanana sana. Habib: Zinafanana kwa sababu zote zinatoka kwa Mungu, ila Qur’an ni tofauti katika uthabiti wa kuandikwa kutoka kizazi kwenda kingine, ila sijaisoma kwa umakini na mazingatio yake. Adam: Zote zinatoka kwa Mungu, kwa masikitiko torati na biblia zimebadilishwa. Tom: Sijaisoma Qur’an ili niilinganishe na torati na injili. Katarina: Agano la Kale na Jipya zote ni kutoka kwa Mungu, sidhani Qur’an kama inatoka huko, ijapokuwa sijaisoma huenda nitafanya hivyo. John Luke: Jana nimeanza kuisoma Qur’an kwa mara ya kwanza, na naona inatofautiana na torati na Biblia, ijapokuwa sijui utofauti huo!

Joji alikuwa makini na jibu la Adam, na kuangalia njia ambayo anaitumia pamoja nae… kwani marafiki zake wote walisema wazi kwamba wao hawakuisoma Qur’an, au wamesoma juu juu bila mazingatio, Adam peke yake ndio hajaashiria katika hilo. Joji alirudia tena kuwatumia marafiki wake wote na kuwaandikia sehemu ya sita:

“Sehemu ya sita: Nani miongoni mwenu anaweza kuisoma Qur’an, na achunguze katika kadhia hizi nazo ni: Kuthibiti kwake au kutothibiti kubadilishwa au kutobadilishwa, nasubiri ukosowaji wenu kwa muda wa wiki kuanzia leo. Joji.”

Baada tu ya kutuma barua pepe, aliwasiliana na Adam.

Ijapokuwa tulikutana ila nimepatwa na hamu na kupenda tuonane kwa mara nyingine tena, je kwa kesho inafaa?

Hapana shaka, labda tufanye baada ya saa mbili, kwa muda wangu wa kazi kesho unaishia saa mbili, haa haa, na tutakula chakula cha usiku pamoja.

Muda muwafaka, kwani mimi nitarudi kesho kazini, karibu wiki tatu hivi sijauona uso wa Kakhi.

Kwa hivyo nitakusubiri, kwa heri.

Katarina alirejea nyumbani na kumkuta Joji akiwa mbali kwenye skirini ya kompyuta, alimbusu na kumuegemea mabegani….

Mpenzi samahani kwa kuchelewa, kwani nilipitia super market; kuchukua baadhi ya mahitaji muhimu, nyumba ilikuwa tupu tangu turejee kutoka safari…uzuri ulioje wa safari.

Ndio, ni nzuri sana, na kilichopendezesha zaidi ni kuwepo kwako wewe Katarina.

Asante sana kwa maneno yako haya murua, safari iliisha haraka sana.

Vitu vizuri vinaisha haraka zaidi, na kubakiwa na mawazo yenye huzuni kwa muda mrefu, na hata kitabu kizuri kinasomeka kwa mara moja tu, mara nyingi, na kile chenye kuchosha utakaa nacho siku nyingi bali wiki kadhaa…na ndio maana nimekimaliza haraka mara moja tu kile kitabu ulichopewa na Khalid.

Unakusudia kitabu cha “Mapenzi makubwa kwa Yesu yamenifanya kuingia katika Uislamu?!” Je hakikuwa ni kizuri sana chenye kusisimua.

Kwa hiyo unafikiri kuisoma Qur’an, kama ulivyosema katika barua pepe yako uliotuma?

Kwa hakika, nimenunua nakala ya Qur’ani jana, kwa ajili ya kuisoma.

Haa haa, oh –oh, hayo ni mabadiliko hatari sana ewe Katarina, Katarina anasoma Qur’an? Je utakuwa Muislamu?

Nitaisoma; ili nipate kuikosoa na kubainisha kasoro zake na migongano iliyopo ndani yake.

Nilikutumieni barua pepe muda si mrefu kuwaomba sote tuisome Qur’an, makubaliano yaliyoje haya, ama kwa upande wangu nitachukua nakala kwa Adam kesho.

Kwa nini iwe kwa Adam pekee?

Kwa sababu ndicho kitabu chao kitukufu.

Kwani Adam ni Muislamu? Je hukuniambia kuwa yeye ni Mkatoliki?

Kwa hakika lilikuwa ni jambo la mshtuko kwangu nilipojua kuwa yeye ni Muislamu, na nitakutana nae kesho kwa kadhia hii hasa.

Japokuwa ninafurahishwa na Adam ila sifurahishwi na Waislamu, huenda nilimpenda kwa kuwa nilifikiri ni Mkatoliki.

Hayo uyasemayo hayana uadilifu wala mantiki, je haitoshi kumuangalia bila kujali imani yake?

Hapana, kipimo muhimu cha kumuangalia mtu ni dini, je, unataka nimfananishe muamini wa Kikatoliki awe sawa na Muislamu gaidi?! Je, kuwa mara nyingi tunampa thamani msomi kuliko mwingine, na mwenye tabia nzuri kuliko mwenye tabia mbaya? Tabia nzuri, usomi wa mtu na dini ndio njia ya kutathmini bila ya shaka.

Inawezekana, lakini inafaa hilo lau kama unaitakidi kuwa dini yako haina shaka katika usahihi wake, kama ilivyokuwa hakuna shaka katika tabia njema, usomi, je unaamini hivyo?

Kwa kiasi fulani, lakini je kwa upande wako dini daraja lake ni la chini zaidi kuliko tabia njema na usomi?! Haa haa inavyoonekana una chembe chembe za ukanaji dini ewe Joji.

Huenda ikawa ni hivyo, lakini ni kwa nini ulikuwa unaogopea Sali na Maiko pale kanisani? Je ulikuwa na chembe ya ukanaji dini pia?

Sikuwa naogopa chochote, wewe unadhania na kuisadiki nafsi yako, kisha kwanini niogope?

Nilikuwa nakutania tu, basi wewe hukuwaogopea kanisani, na hukuwa na hofu yoyote na kitabu ulichopewa na Muislamu, cha msingi kitabu kiko wapi kwani sijakisoma.

Nafahamu sana unachoashiria, watu wote huwa wanaathirika kwa wanachosikia na kusoma na kufikiria.

Nitakuuliza swali halafu nataka unijibu wazi wazi bila kuficha.

Karibu, uliza swali lako.

Je unaweza kuuacha Ukatoliki?

Niache Ukatoliki? Kwa kitu gani?

Halafu uwe Prostestanti au Myahudi au Muislamu au uchague dini yoyote?

Laiti ungeniuliza swali hilo kabla ya mwezi hivi, basi ningekujibu bila kificho kuwa hapana. Ama kwa sasa hivi utanisamehe; ila nitakujibu pia hapana, lakini sijui kwa nini imani yangu imeshuka kuliko mwanzo, japokuwa unajaribu kunitikisa na maswali yako ila unanifanya niwe imara zaidi na nafsi yangu.

Wewe Katarina ni mfano mzuri wa imani kwangu, na kile unacho nikumbusha kuhusu kubadilika huenda ni dalili tosha ya kuongezeka kwa imani yako, japokuwa mimi ni Mprotestanti na sio Mkatoliki ila nasadiki imani yako, na wewe ndio taa inayoniongozea njia.

Bali wewe ni mtafiti mzuri wa kutaka kujua ukweli na utafanikiwa, na kupenda Joji.

(5)

Asubuhi ilipofika Joji alienda kazini na kuelekea ofisini kwake moja kwa moja hakutaka kukutana na Kakhi, alikuwa anahisi kumchukia kwa upande wake. Je hilo linarejea kwa sababu yeye ni Myahudi, au kwa sababu ni mtu mwenye tamaa, au kwa sababu ya tabia yake mbaya au kwa sababu tabia zote hizo anazo? Hiyo sio sababu kwa kuwa amefurahishwa sana na Levi japo yeye ni Myahudi, na ni mtu aliyeshikamana na dini yake…hakuwa akimchukia mtu kwa dini yake bali alikuwa anachukizwa na migongano iliyopo kwenye dini na ushirikina na upotofu wake.
Pamoja na hivyo ni lazima kukutana na Kakhi kwa hali yoyote ile, na kwa hivyo lazima awasiliane nae kabla Kakhi hajajua kuja kwake na kuwasiliana nae….wakati akiwa katika hali hiyo mara akaona karatasi iliyokuwa na bonasi nyingi kwa juhudi kubwa aliyofanya kwa ajili ya shirika lake. Hiyo inatokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika kuingia mikataba huko India na Tel Aviv ikiwa imetiwa sahihi na Kakhi. Joji alijiuliza: Je alimchukia Kakhi kiasi hiki, au ajirudi kwa hisia mbaya alizokuwa nazo pindi alipofahamu kuwepo kwa bonasi kubwa kiasi hiki? Je posho ile inathibitisha wema aliokuwa nao, au ni rushwa kama rushwa aliyompa Benjamin huko Yerusalem?!
Simu iliita, Joji alipokea simu, ghafla Kakhi alikuwa upande wa pili.

Karibu Joji, nilipojua kuwa unakuja nilikusubiri ofisini kwangu lakini hukuja, je utakuja au mimi nije ofisini kwako?

Nitakuja baada ya dakika hivi, nilikuwa napanga karatasi tu.

Kama ni hivyo nitakusubiri.

Joji alikusanya baadhi ya makaratasi na kuyapanga, lakini hakuweza kupangilia mawazo yake na akili yake vizuri kutokana na ushawishi na bashasha ya Kakhi kwake, alielekea ofisini kwake, na alipoingia tu alimkaribisha kwa furaha….

Karibu, kwa hakika nilikuwa na hamu sana na wewe Joji, vipi afya yako? Habari za Roma pamoja na TelAviv?

Mimi ni mzima, kwa hakika nimepona maradhi yaliyonipata, ama kuhusiana na TelAviv nimewekeana mikataba kwa ukamilifu na nimeshaituma kwenu, ama kuhusu Roma safari ilikuwa ni nzuri, vipi hali zenu? Na vipi habari za shirika?

Mikataba ya TelAviv italisukuma sana shirika letu kwa sababu makundi shawishi ya Kiyahudi yapo katika nchi nyingi, na kwa sababu sisi tumetiliana saini na TelAviv hii itasaidia kupanua wigo zaidi Ulaya yote na hata Amerika, na idara kuu imekuzawadia bonasi nzuri, je umeiona?

Asante sana Kakhi kwa hisia hizi, nilichokifanya ni wajibu wangu wa kikazi.

Sijui vipi uliweza kuvuka vigingi, wewe ni dereva mgunduzi!

Hakukuwa na vikwazo vyovyote, ametia saini mara moja.

Je hakutaka fedha zingine kwa ajili yake mwenyewe?

Unakusudia rushwa, hilo alichukua.

Je hajataka kitu kingine?

Kama kitu gani?

Achana na hilo, ni mara ngapi umelala na Levi? Najua yeye anapenda starehe wakati mwingine, hali yakuwa ni mwenye dini.

Sijalala nae katu, na siwezi kufanya hivyo.

Benjamin ni mchafu, je hajakutongozea.

Kweli ni mchafu, kwani amechukua rushwa, na mimi sikumuomba aongee na Levi, sasa vipi unanitaka mimi kukubali amchukie Benjamin kwa mambo hayo ya ngono?

Haa haa, cha muhimu ni kuwa ametia saini mkataba, kiasi gani nikitaka ustarehe, lakini wewe ndie hutaki, ningekuwa sehemu yako muda wote ningelala nae, kwani hajakupendeza?

Mimi nimeoa ewe Kakhi, je unataka nimfanyie hiyana mke wangu? Siwezi kujivua na misimamo yangu.

Achana na misimamo kwanza, sisi tunalitumia tu neno hilo hasa tunapotaka kufanikisha malengo yetu.

Labda unaongelea kitu kingine kisichokuwa msimamo. Ama misimamo haiwezekani kuivuka.

Je wajua kama Levi analala na mimi kila siku ninaposafiri kwenda TelAviv? Na yeye ndio mzungumzaji mkubwa wa misimamo.

Huo ni udhaifu wa kibinadamu tu.

Na hii ndio falsafa ya misimamo, tukitaka kufanikisha mambo yetu tunasingizia misingi hii ya misimamo na tukitaka mambo mengine tunasema ni udhaifu wa kibinadamu.

Maneno ya Kakhi yalimuathiri kiasi fulani katika moyo wa Joji, kweli na yeye pia alitoa rushwa kwa Benjamini na kusingizia udhaifu. Je na yeye anafuata nadharia ya Kakhi juu ya misimamo na misingi bora?

Huenda, lakini katika mambo mabaya kabisa ni kuishi bila kuwa na maadili, na hivyo ni kwa mujibu wa maslahi yako, kinyume chake hatakuwa tofauti na wanyama.

Ha haa, udhuru wa wanyama ni bora kuliko wa binadamu, kwa sababu ameumbwa hivyo na habadiliki na ukitaka yaite hayo kuwa ndio maadili yao.

Umesema kweli, watu kama hawana maadili ni waovu kuliko wanyama, na wanageuka kuwa wabaya zaidi, hawaoni la muhimu zaidi ya mali, ngono na utawala.

Ni mhadhara mzuri ewe mwenye maadili, achana na hayo kwa sasa, rudi katika kazi, je upo tayari kwa safari mpya ya kuweka mikataba huko Sweden?

Safari mpya kwenda Sweden?

Ndio …baada ya wiki hivi, na Idara imekubaliana wewe uende, na waliakhirisha safari hiyo zaidi ya mara moja hadi utakaporejea.

Mkataba wa nini?

Ni kama mkataba wa TelAviv, bali unashabihiana sana na huo.

Vipi? sijaelewa!

Kuna fedha kwa ajili ya mkurugenzi wa Idara ya utaalamu, pamoja na ushirikiano wa kidiplomasia kutoka kwako na baada ya hapo kutia saini mkataba.

Nimekufahamu unachokusudia, mkurugenzi wa utaalamu hapa ndio Benjamin wa huko. Je kuna Levi mwingine huko Sweden?

Ha ha ha, si umeniambia kuwa hujastarehe na Levi, sasa kwa nini tena unamuulizia Levi Sweden? Yako wapi maadili.

Sijakusudia hivyo, bali nilikuwa natafuta vipengele vyenye kufanana.

Ndio, yupo mfano wa Levi huko Sweden na jina lake ni Ingrid, ni sawa na uzuri wa Levi, kuwa na amani tu.

Vizuri, ili usifikirie kuwa nakataa kwa ajili ya uzuri wake.

Sifahamu?

Sitokwenda, ili usifahamu kuwa tatizo lipo kwa sababu hakuna masiku mekundu.

Na kwa nini huendi?

Je hukuniambia kuwa mimi ni mwenye maadili? Rushwa inapingana na maadili yangu.

Kwani hukumpa pesa Benjamin ili atie saini mkataba ewe mwenye misimamo na maadili?

Ni kweli nimekosea, na ukitaka unaweza kuuita ni udhaifu wa Kibinadamu!

Je sijakwambia kwamba tunatumia maadili ili kufanikisha malengo na maslahi yetu, unataka nini?

Sitaki chochote, sitaki tu kwenda.

Unaonaje nikikwambia kuwa bonasi yako ijayo ni mara mbili zaidi ya iliyopita, kwa maana ni sawa karibu ya mishahara yako ya miezi mitatu.

Sio hoja..

Sitaki unijibu sasa hivi, una siku mbili za kufikiri, naamini hutaiachia fursa hii.

Ni fursa gani hiyo?

Fursa ya safari, bonasi na kupanda cheo?!

Kupanda cheo?!

Ndio, katika muundo mpya wa shirika. Ikiwa utawezesha mkataba na Sweden utakuwa mkurugenzi mkuu wa shirika, utashika nafasi yangu na idara imependezwa na mafanikio yako.

Na wewe?

Huenda nikawa mkurugenzi mkuu wa shirika la makabidhiano wa shirika letu, fikiria vizuri, ila naamini hutaipoteza fursa hiyo, na unaweza kupanga muda wako muwafaka, haa haa na wakati huo utaamua kutumia maadili yako vizuri, unaweza kutoa au kutotoa rushwa tena.

Na kama sijasafiri?

Utakuwa umejihukumu mwenyewe kwenye shirika, na sidhani mwenye akili mfano wako anaweza kufanya hivyo, niamini nilitaka kwenda mimi mwenyewe ila idara imesisitiza uende wewe kwa ajili ya kusaini mikataba mikubwa, wao wamefurahishwa sana nawe.

Nitakujibu baada ya masiku kadha.

Mimi ni mwenye imani na akili yako na busara zako, kwa hivyo nitawajulisha watu wa mahusiano wakuandalie safari yako kuanzia sasa hivi. Utaletewa makaratasi na mikataba, na maelezo kamili ya makubaliano.

Naomba ruhusa, nataka kumalizia baadhi ya kazi.

Joji alikwenda ofisini kwake, huku akijiuliza..Je maadili kama alivyosema Kakhi ni suala la maslahi tu? Ambayo yanabadilika kwa mujibu wa malengo yetu? Au ni taa tosha za kutuangazia njia tuiiendayo, na inatupasa kufuata muongozo wake? Na kama ni hivyo, ni kwa nini alimpa rushwa Benjamin huko Tel Aviv? Je afanye nini? Inaelekea maudhui ya safari ndio muhimu sana kwa Kakhi, bali ni la kuamua kama ataendelea na kazi au kufukuzwa..ikiwa maadili ni kweli hayana thamani yoyote; hiyo ina maana kuwa sisi tutabadilika kuwa ni wanyama tunakulana wenyewe kwa wenyewe, Aakh, Aakh…kwanini Mungu hakupanga mambo haya? Au Mungu amewaacha watu wajipangie mambo yao bila kuingilia?!
Pindi alipokuwa amezama kwenye mawazo hayo, aliletewa makaratasi na fomu za safari, alianza kuziangalia bila kujali, ikiwa maamuzi yake ni: Je atasafiri au hapana na hilo ndio muhimu kwake, na kama hataki kusafiri kwa nini anajihangaisha kuyasoma makaratasi hayo?
Joji alisubiria mpaka mwisho wa siku ya kazi iliyoonekana kuwa ni ndefu sana kwake; ili aende nyumbani na amshauri Katarina katika uamuzi wa safari yake, alipofika nyumbani alimkuta Katarina anasoma kwa umakini na utulivu wa hali ya juu….

Yaelekea kitabu unachosoma ni kizuri sana?

Kiasi fulani, nasoma kitabu kitakatifu cha Waislamu ambacho ni Qur’an.

Kwa maana hiyo umeanza kukisoma?

Ndio, lakini pamoja na pupa na ufahamu wangu bado najikuta kukirudia kusoma tafsiri za sura zaidi ya mara moja.

Kwa nini?

Sijui, huenda kwa sababu ni tofauti na vile nilivyovizoea…!

Vizuri, lakini je inawezekana kuacha maudhui haya na kitabu, nina jambo nataka ushauri wako.

Haya tafadhali sema.

Kakhi ameniomba nisafiri kwenda safari nyingine mpya.

Hii ni mara yako ya kwanza tokea uanze kazi na shirika hili umefululiza kusafiri kiasi hiki, safari hii ya kwenda wapi?

Kwenda Sweden.

Sweden ni nchi yenye hadaa.

Hili silo tatizo.

Kwa hivyo kadhia ni ipi?!

Kipindi nimesafiri Israel kuweka saini ya mkataba na maafikiano, nilipewa rushwa kubwa nimpe mkuu wa shirika lingine ili kuweka saini, na wananitaka tena kufanya hivyo huko Sweden.

Japokuwa nachukia rushwa na siipendi, lakini kuna kipya gani kwako? Wakati ulikwishawahi kutoa mara ya kwanza.

Maneno kama ya Kakhi.

Namchukia mkurugenzi wako huyu, lakini…..

Chukulia nimekosea mara ya mwanzo, je nirudie tena kosa hilo mara nyingine? Kwani hakuna njia ya watu kujitakasa kwa makosa yao?

Katika Ukristo tumemtoa Kristo kwa kujitoa kwake mhanga kwa ajili ya watu.

Na hili sio mahususi kwa mtu bali kwa mkosaji na mwingine.

Bado sijakuelewa?!

Kwamba sote sisi hatuna dhambi na tumetakaswa, na kwa nini tuiache wakati tunajitakasa kwayo?! Nafikiri huu ni mwanzo mzuri wa biashara ya kuuza cheki ya kusamehewa madhambi.

Nimekuelewa unachokusudia, haya ni katika Ukristo, ama katika Uislamu mwenye kutubu na kuomba msamaha Mungu atamsamehe.

Maendeleo yalioje haya, umekuwa unauongelea Uislamu, yote haya ni baada ya kusoma kitabu kimoja tu?! Hivi Waislamu hawaendi kwa makasisi na watawa kutubia? Vipi kuhusu misa ya kufuta makosa?

Hakuna misa yeyote, kutubu ni kumuelekea Mungu pekee, tunatakiwa tumuombe msamaha kwa makosa yetu, na kuazimia kwa dhati kutorudia kufanya dhambi.

Kwa wepesi tu hivi!

Ndio.

Yote haya ni mafunzo yanatokana na kitabu ulichopewa na Muislamu huko Roma!

Bali ni kutoka katika kitabu kitakatifu cha Waislamu kinachoitwa Qur’an.

Turudi katika maudhui ya Kakhi.

Sijui, vigumu kuwa na uchaguzi, ima ufungamane nao katika yale yanayokwenda kinyume na maadili yako na kupoteza thamani yako mbele ya nafsi yako, au kukataa; na hivyo basi kupoteza kazi yako.

Ndio, uchaguzi ni mgumu, na nina fursa ya kumjibu kwa muda wa siku mbili, lakini lau ungekuwa wewe katika hali yangu ungefanya nini?

Mimi ningekuwa katika mtanziko kama wewe, na ningekuomba ushauri wako hasa kwangu mimi, lakini umenitangulia na sipendi kukuongezea uliyonayo.

Vipi?

Sikuridhika na kile ninachokifundisha shuleni, nafikiri kuacha kazi yangu.

Unaacha kazi yako?

Kama ulivyo wewe hupendi kwenda kinyume na maadili yako, na mimi pia sipendi kwenda kinyume na maadili yangu, mengi ninayosema katika darasa bado sijaridhishwa nayo, ima niyaseme na hapo tena nienda kinyume na maadili yangu ya kutosema isipokuwa yale ninayoyaamini, vinginevyo naacha kazi, na hapo utakatika mshahara ninaopokea kutoka kwao.

Ni badiliko la hatari, je hukufikisha miaka kumi unafundisha hili tu? Ni kipi kipya basi? Ikiwa sote tutaacha kazi zetu tutaishi vipi katika kivuli cha ukosefu wa kazi unaozidi hapa Uingereza na hata ulimwengu mzima?

Jipya ni kwamba ridhaa yangu ya Ukatoliki imetikisika, je hukuwa unataka hivi?! Kwa ujumla mimi sijachukua maamuzi mpaka muda huu.

Samahani kama nimekukera bali nilikuwa nafanya mzaha tu na wewe.

Kinyume chake, kwa hakika umeondosha matongotongo yaliyokuwa machoni mwangu, lakini sijakueleza kwamba sitaki kukujuliisha isije ikakuzidishia mawazo?

Kweli, umeniongezea mawazo juu ya niliyokuwa nayo, nitafikiri zaidi na kuchukua maamuzi kwa muda wa siku mbili hizi zijazo, na wewe chukua maamuzi yako, ama kweli maisha ni maamuzi.

Ni wajibu kuomba ushauri ewe Joji.

Lakini nani anafahamu matatizo ya kazini?

Mtu yeyote miongoni mwa marafiki zako, kwa nini hutumi barua pepe kama unavyotutumia ukitaka ushauri huo?

Ni fikra nzuri, nitatuma sasa hivi.

Joji alipanda kwenda katika chumba cha ofisi yake, na kufungua kompyuta yake, na kuwaandikia marafiki zake akiwataka ushauri.

“Sehemu ya saba: Nimekabiliwa na tatizo naomba mnipe ushauri wenu kabla ya kujibu swali langu la sehemu ya sita. Kwa kifupi swali ni hili! “Je niungane na maadili yangu japokuwa yanaharibu maisha yangu? Au nifuate maslahi ijapo kuwa yanaharibu maisha yangu? nategemea jibu la kweli na uwazi, jiweke wewe katika nafasi yangu, je maadili na maslahi yanaweza kuwa pamoja bila kugongana? Joji”.

Baada ya kuituma, alifungua ukurasa wa Tom katika face book na kukuta majibu yale yale kama yaliyopita, na kuandika kutaka msamaha kwa picha za uongo na kupandikizwa zilizo sambazwa katika ukurasa… alijihisi vizuri kidogo; Inavyoelekea Tom ameweza kurejesha face book yake na kumaliza tatizo la Baraad. Halafu alifungua face book ya Adam na kukuta ameandika makala mpya yenye anuani, “Mafunzo kutoka kwa rafiki yangu anayetafuta furaha4”

“Rafiki yangu anapambana na kipindi kigumu zaidi, na unaweza kuangalia nukta hizi zifuatazo katika utafiti wake: 1-Mwanaadamu kujua yale asiyo yataka ni rahisi kuliko kujua yale anayo yataka, na kujua njia hii sio ya furaha pia ni rahisi kuliko kujua kuwa njia hii ni ya furaha, mabadiliko na kuhama kutoka hali fulani kwenda nyingine ni kugumu kwa mtu. 2-Maamuzi yoyote yanahitaji ujasiri mkubwa kutoka katika nafsi ya mtu, na ushupavu ndio anuani ya mafanikio ya kifikra, au kijeshi au maadili, na rafiki yangu ni shujaa bila shaka, lakini hitajio lake la ushupavu kwa sasa ni zaidi kuliko zamani, je ataweza kuwa hivyo? 3-Rafiki yangu anaishi katika wakati ambao ni wa mabadiliko ambao hauoni sana, wala hayuko makini kwa hilo, yeyena hili ni jambo la ajabu kabisahadi sasa hajui kama mimi ni Muislamu, na atashitukizwa kuona kuwa watu wanaomzunguka waliokuwa karibu yake wanaishi katika kipindi cha mabadiliko makubwa mfano wake. 4-Japokuwa rafiki yangu yupo katika kutaka kujifunza kwa pupa ila hajachukua maamuzi ya kujifunza Uislamu kwa njia nyepesi, na hilo huenda limesababishwa na vyombo vya habari! Vilivyoathiri sana mtazamo juu ya Uislamu, na huenda sehemu nyingine inatokana na upungufu na makosa ya Waislamu wenyewe. Ila bado nina imani kuwa rafiki yangu yupo katika hatua za mwisho za kutafuta na kufuata njia ya furaha na katika kutafuta majibu ya maswali makubwa ya maisha, nitawajulisha hayo katika darasa zijazo.” Adam.”

Joji alirudia kusoma tena kwa mara ya pili kile kilichoandikwa na Adam kwa umuhimu mkubwa, na kujiuliza mwenyewe nafsi yake: Hivi Adam anaamini kwamba Uislamu ndio njia pekee ya kufikia maisha bora ya furaha?! Kwa nini hajaniambia hivyo tangu mwanzo? Je ananitania mimi? Au Uislamu unaruhusu udanganyifu? Na kama anaamini Uislamu ndio njia bora ya maisha na ya furaha kwanini anajificha na kutokuwa muwazi? Je Uislamu una kasoro mpaka auepuke? Au ndio siri miongoni mwa siri za dini kama siri za kanisa? Pindi alipokuwa katika tafakuri hiyo mara aliingia Katarina.

Njoo usome aliyoandika Adam juu yangu? Nimeanza kumtilia shaka mtu huyu.

Ameandika nini?

Karibu usome.

Katarina alisoma makala kwa umakini akisha akamgeukia Joji.

Sijakuelewa sehemu gani una shaka nayo!

Yeye ni Muislamu mwenye kuamini kwamba Uislamu ndio njia bora ya furaha ambayo itatatua matatizo ya maisha yangu!

Ndio, na hili ni jambo la kawaida, ni desturi mtu kuamini kile alicho nacho kuwa ndio njia ya furaha maishani.

Lakini ni kwa nini hakunijulisha tokea mwanzo, na kwa nini ananidanganya?

Je kakudanganya na kukwambia kitu ambacho si cha kweli?

Hapana, lakini amenificha Imani yake na dini yake.

Nahisi yeye amekueleza kweli tu hilo, ila wewe hukugundua.

Ki vipi?

Kwa hakika ameandika dini yake katika face book, na yeye hajifichi katu bali anajifaharisha kwayo, kwani ameandika mimi ni (Muislamu na najifaharisha).

Fikiria yote haya sijayaona pamoja na kuwa nafungua sana face book yake, amesema kweli Adam ila mimi sifungamani vya kutosha.

Je, hujatuambia sisi katika barua pepe kwamba sote tuisome Qur’an na tukupe jibu? Je wewe umeanza kuisoma?!

Hapana, kwani Kakhi amenishughulisha sana na matatizo yake, nitaonana na Adam leo, na leo hii hii nitaanza kuisoma Qur’an, na nitajaribu kuwa na maamuzi leo ya shirika au kesho.

Adam asiwe ndio mwamuzi wetu, msikilize kwa utulivu au tuache tujifunze zaidi mpaka tuweze kumjibu kwa hoja zenye nguvu….huenda yeye anatutaka tuingie katika Uislamu pamoja nae, sasa sisi tumfanye awe mkristo pamoja nasi.

Nitajaribu kwenda kwake sasa hivi, na nitajaribu kumsikiliza kwa makini na kujifunza mpaka nimjibu vizuri kwa elimu, na ninadhani nitakula chakula cha usiku pamoja nae.