Nilikwenda kwa mhudumu ambaye nilikuelezea habari zake jana na tukapata chakula cha jioni pamoja.
Kikao kilikuwaje? Je rai yako kwake iko vile vile?
Mkutano ulikuwa mzuri; yule bwana ni mwanafunzi wa mambo ya dini, lakini anazungumza kwa lugha nyepesi na ya kukinaisha kabisa, na..
Inatosha..inatosha, basi, sifa hizo zinatosha jamani. Inaonekana kakukosho roho sana. Hahaha hiyo ni hali ya kawaida kwa mwanafunzi wa mambo ya dini ni lazima awe hivyo. Je kakuambia nini huyo bwana?
Maneno yake yanafanana na yale ya mzee kikongwe yule niliye kutana naye hapo nilipokuwa nimekusudia kujinyonga. Je wamkumbuka?
Ndiyo!
Na maneno hayo yatafanana na yale ya yule mpagani. Dokta Tom. Hili ni jambo la ajabu, maneno ya mtu wa dini kufanana na maneno ya mpagani!?
Naona unamwita daktari kuwa ni mpagani. Mimi sikudhania kuwa yuko hivyo licha yakuwa nilikaa naye.
Unakusudia pale tulipokwenda mimi na wewe? Au kuna kikao kingine?
Joji! ndiyo kikao pale tulipokwenda mimi na wewe. Nilimweleza kuwa shughuli zangu ni kufundisha dini Kanisani lakini hakuniletea maneno ya upinzani wala ubishi. Bali alivutiwa nayo.
Yule anajisifu kuwa ni mpagani, na hayo waweza kuyaona ndani ya face book yake Joji akamkazia macho mkewe (kisha akasema): Nadhani ana jambo kuhusu maudhui yako ya dini.
Una maana gani?!!
Wala! wala hamna kitu, bali ni fikra tu imeibuka kichwani mwangu. La muhimu hapa ni kuwa nitakuwa na safari ya India; Unasemaje?
Nzuri sana, safari hiyo iko lini?
Baada ya siku kumi hivi.
Wewe unajua kuwa mimi nina asili ya India na hasa huko Delhi.. India ni nchi yenye maajabu mengi, Joji, utasahau matatizo yako mengi, na mwishowe utahisi utulivu. Sasa unafanya nini kuhusu miadi yako na daktari?
Tuna miadi Jumatatu, nitamwomba miadi mingine ipelekwe mbele zaidi mpaka nikirudi.
Vizuri.
Leo haiwezekani.
Kwanini?
Hahaha, kwa kuwa daktari ana ahadi muhimu sana leo saa mbili usiku.
Ni muhimu kiasi hiki?
Huenda ikawa ni hivyo, kilichokuwa muhimu ni kuwa huwezi kutanguliza ahadi uliyokwishaweka kabla, kisha baada ya hapo akacheka kicheko kikubwa.
Nitakuja saa moja unusu, na akichelewe mgonjwa katika ahadi ya saa mbili basi mimi nitaingia badili yake.
Hahaha, nimekuambia haiwezekani, na ahadi hiyo aliyokuwa nayo Dokta sio hapa kwenye kliniki…na kwa istihzai akasema: unaonekana una hamu sana ya kuja muda huu, najua unalotaka!! Njoo nitakujulisha yote uyatakayo, na kukutatulia matatizo yako, kisha akacheka kicheko kikubwa kama cha mwanzo, kisha akaendelea kusema: nitakusubiri na usichelewe.
Adam..ulishawahi kumshuku mtu uliokuwa naye karibu? Aliuliza Joji.
Hapana, sijawahi lakini ni jambo gumu!
Je umeoa?
Hapana.
Vipi uhusiano wako na wanawake?
Sina uhusiano wowote na wanawake! Unataka nini na kukusudia Joji?
Je si nilishakwambia kuwa daktari wangu si mwenye tabia njema?
Ndiyo.
Na je sijawahi kukuambia kuwa mke wangu anakunywa sana pombe na kukesha katika mikesha yenye shaka hali ya kuwa ni mwanamke mwenye dini?
Ndiyo!
Aah, nimeanza kushuku uhusiano usiokuwa mzuri baina yake na mke wangu, je kwa hilo ni kwa sababu ya kuwa mimi ni mwenye wasiwasi?
Sijui niseme nini, najua huzuni na hisia ulizonazo..lakini asili ya mambo ni kuwa na muamala mzuri na watu na kuwadhania vizuri, na kwa sababu bado hujawa na hakika usifanye haraka kuwatuhumu watu.
Ana ahadi nae leo ya mkesha!
Je una hakika na hilo? Kisha ulishawahi kunieleza kuwa anakunywa sana pombe na kukesha, kuna tofauti gani ya kuwa katika mkesha akiwa na Tom au mwengineo?
Uhusiano wa Tom na wagonjwa wake siku zote ni wa mashaka mashaka, naye si mtu mwenye tabia nzuri, na Katarina hali kadhalika mikesha yake ni ya mashaka mashaka vile vile, kisha mke wangu aliamua kunificha kuhusu uhusiano huu na …maneno ya Baraad yalikuwa ya kushangaza sana!
Baraad huyu ni nani?
Huyu ni sekretari wa Tom, ni mtu asiyependeza kwa tabia vile vile, na huwa anagundua vitu vya ajabu kabisa na vyenye kuchukiza.
Sasa hivi ni saa moja usiku, kwa nini usimpigie simu Katarina na kumualika chakula cha usiku katika hoteli ya kifahari.
Nitajaribu hilo!
Unaona, amekataa kwa kisingizio cha hafla kanisani!
Kumbe ni hafla kanisani, kwanini sasa unamtuhumu?
Cha kusikitisha ni kuwa fedheha za hafla za kanisa ni nyingi. Hutoa harufu yake.
Huenda ikawa ni hivyo lakini sijui!
Sijui ni kwa nini ninakukera kwa mambo binafsi! Naomba upokee samahani yangu.
Usiombe msamaha, natamani kama naweza kukusaidia lolote, tutaonana wakati mwingine…hata hivyo ninapenda kukuambia kitu: tahadhari na Baraad uliyenihadithia mambo yake, usimuache akuchezee, mara nyingi tunakuwa katika hali ya udhaifu pindi shaka inapotutamalaki.
Kwa kweli nimechoka na ni bora nikapata ufumbuzi kabla ya saa mbili kufika! haya tutaonana.
Hallo..uko wapi? nakusubiri, Tom ameshakwenda katika ahadi yake muhimu!
Kaenda wapi?
Katika ahadi yake, unataka kujua nini?
Nimechoka!
Hahaha, njoo, nina utatuzi wa matatizo yako.
Una utatuzi? vizuri nitafika mara moja.
Yuko wapi Tom?
Ametoka muda si mrefu.
Pamoja na nani?
Wewe unajua, karibu tukae katika ofisi ya Tom!
Mimi sijui lolote, unataka nini kwangu?
Tom ametoka na Katarina.
Nini kinanipa dhamana kwamba hudanganyi!
Mimi sidanganyi!
Ni nini hiki?
Hahaha, je inawezekana Katarina kasahau mkoba wake?! Hii ni dalili ya ukweli niliousema kwako.
Wamekwenda wapi?
Wana mkesha…nadhani kanisani.
Lakini Tom hana dini..
Kwa nini usiende pamoja nao? Kwa kuwa wana jambo lao haliwezi kufanyika kwa kuwepo kwako? Akacheka kwa sauti kubwa…kisha akaendelea: ewe rafiki yangu najua hisia uliyonayo, nina kitu kitakachokusaidia katika msongo wako huu wa nafsi.
Ni nini hicho?
Kidonge kimoja cha furaha, nadhani ulishasikia kuhusu heroin, hata hivyo naamini kuwa hujui kiwango cha furaha anachohisi mtumiaji wake, kidonge kimoja tu kitakupa furaha unayoitafuta, je utahitaji?
Kidonge kimoja tu!
Ndio Joji.
Nimethibitisha lile nililokuambia.
Chukulia mambo kwa wepesi wake, hata ukithibitisha kutoka kwao pamoja, je hilo lina maana anakusaliti?
Adam, kwa hakika nimechoka, Baraad ameniacha kwa muda kidogo huenda baada ya muda akaniletea kitakachonituliza kichwa changu.
Ni kipi hicho kitakachokutuliza?
Ameniambia ni kidonge cha furaha, kidonge kimoja tu!
Mihadarati! mwendawazimu nini? Je sikukwambia kuwa watu wanaweza kutuchezea tunapokuwa na shaka na wasiwasi…Joji una nini? huku ni kukimbia matatizo, je unadhani utapata furaha kwa kukimbia matatizo? nakuomba njoo huku mara moja.
Ole wangu, na huyu bado hajarudi, vizuri, vizuri.
Unajisikiaje sasa? unaonaje tufanye mazoezi pamoja?
Mazoezi! huu si wakati wake.
Mara nyingi natembea au ninakimbia kila siku kiasi cha kilomita tatu hadi tano, na katika siku ambayo sikufanya mazoezi ni leo, njoo Joji jirani na nyumba yangu pana sehemu nzuri ya kutembea.
Vizuri.. hamna neno!
Unadhani mazoezi yanaweza kumpa mtu furaha kwa mtu aliyeharibikiwa na kuvunjika moyo kama mimi, nifanye mazoezi huku mke wangu akiwa amekumbatiwa na mtu mwingine?
Mazoezi humfanya mtu awe na ari, hata hivyo ikiwa peke yake haitoshelezi na haimfurahishi mtu, furaha inatokea ndani mwetu, si sehemu nyingine bali ndani ya mioyo yetu, hailetwi na mazoezi wala mihadarati na vilewesho vingine!
Kwa hakika nilikuwa katika hali ya udhaifu mno na Baraad akawa ananichezea.
Tusiwape fursa watu wabaya kutuchezea wakati wa udhaifu wetu!
Kwa hakika ninahisi kuvunjikwa kwa moyo kwa ndani nami nikiwa natembea nawe nahisi mauti ya roho yangu mara kwa mara.
Ulikuwa ukifanya nini siku za nyuma inapokujia hali hii ya huzuni kama hii?
Nimekumbuka, nilikuwa nakunywa kidonge cha kutuliza hali hii nilichopewa na daktari wangu zamani, ingawaje kidonge hicho kinanifanya nihisi usingizi.
Kidonge kinachotuliza kutoka kwa daktari mtaalamu na sio kutoka kwa jambazi, je vidonge hivi unavyo sasa hivi?
Ndio, vipo kwenye gari.
Turudi nyumbani ili uchukue kimoja.
Nitarudi nyumbani nichukue.
Kichukue, na leo ulale kwangu.
Nilale kwako na sijui Katarina yupo wapi?
Usifanye shaka yako ndio dalili ya kumhukumu, huenda alikuwa na Tom kwa kumshawishi Ukristo!.
Huenda, lau ningehakikisha hilo, hilo ni jepesi kuliko shaka niliyokuwa nayo.
Habari za asubuhi, chai tayari.
Hivi ni saa ngapi?
Ni saa nne.
Samahani, nimekuchelewesha kazini, nami nimechelewa kazini kwangu.
Usijali, nimeshaomba ruhusa kazini, nawe ni msaidizi wa mkuu halitokudhuru hilo.
Vizuri, inabidi upate utulivu zaidi, mabadiliko yasiyotarajiwa ni moja katika mambo yanayoondosha furaha ndani ya moyo wa mtu.
Una maana gani?
Kwa mfano kama utaweza kujibu maswali ya msingi utaweza kushughulika na matatizo yako katika hali iliyokuwa bora zaidi, hali yako ya ndani itakuwa nzuri katika kushughulika na msongo wa nafsi.
Una maana kuwa maudhui ya Katarina ni ndogo?
Hapana, sina maana hiyo, ninachomaanisha ni kuwa furaha iliyo ndani ya nafsi zetu zinaondosha shaka zetu na hutatuwa matatizo madogo madogo tuliyonayo, na hivyo unajimakinisha katika kufikia kwenye furaha na kufikia njia itakayokuwezesha kujibu maswali yako, na wakati huo utaona jinsi gani unavyoweza kuyafasiri maisha zaidi na muono wako kwa ujumla.
Nakuahidi katika hilo pamoja na kuwa sikufahamu baadhi ya mambo katika mazungumzo yako.
Maelezo yangu yako wazi, tilia maanani kadhia kubwa zaidi katika maisha yako kwa njia nyepesi na kwa undani zaidi, wakati huo utaona furaha ikitoka katika roho yako na utatatua matatizo yako.
Huenda ikawa hivyo, asante sana, nimekutaabisha …nitakwenda kazini sasa, na leo nina ahadi na daktari.
Jitahidi kukaa na Katarina na Tom katika hali ya kawaida, kwani si muda mrefu utasafiri kwenda India, na utakaporudi katika kila mazungumzo kuna tukio lake, na hakikisha kufanya mambo yako kwa wepesi na katika hali ya kawaida na bila kuyakuza, katika hali ya furaha bila ya kuwepo kwa huzuni.
Nitajaribu.
Umetorokea wapi jana?
Sikutoroka, nilikuwa nina kazi.
Kwanini hukunisubiri?
Mimi nachukia mihadarati, na nachukia kuyakimbia matatizo yangu.
Mhmh, vizuri. Je umepambana na matatizo yako?
Nina miadi na Tom, je yupo au niondoke?
Hahaha..yupo, mimi nina hakika kuwa utahitaji kidonge cha furaha, na utakirudia siku nyingine, karibu daktari anakusubiri, ana hamu ya kukutana na mume wa Katarina!
Je umepata majibu ya maswali yangu ya msingi?
Ndio na hapana.
Vipi, hebu nibainishie.
Nina majibu niliyokinaika nayo, lakini si majibu kamili.
Haya nieleze, majibu tunayapata wapi?
Jibu: kwanza tuamini maswali mepesi na si mazito yake, na wakati huo tutayapata majibu moja kwa moja na kwa wepesi.
Njia ya falsafa inajengwa siku zote katika kuyafanya mambo kuwa magumu ili tu kuonesha kuwa tuna akili na tunajua mengi lakini sio kuyafanya kuwa mepesi.
Lakini wepesi una kina, na kuweza kujibu maswali kwa undani kabisa, nadhani ni hivyo?!
Nadhani umeanza kuyafanyia maudhui yetu falsafa…kisha akasema kwa sauti ya kuonesha changamoto: wepesisha swali kama utakavyo, wapi tunaweza kuyapata majibu ya maswali yetu haya?
Nimechunguza yaliyomo na viumbe, nikaona ya kuwa hatuwezi kuyapata kwa vitu visivyo na uhai wala wanyama..kumebakia nini?
Hahaha, watu!
Umesema kweli, kwa watu au kwa Mola wao aliyewaumba.
Siamini kuwepo kwa muumba wa watu!
Hawa viumbe wametokea wapi kama hawakuumbwa?!
Sipendi kuikera nafsi yangu kwa maswali haya, tusema kwa bahati, au kimejiumba chenyewe, tuseme jambo lingine lolote!
Huku ndiko kukimbia maswali, na huu sio mfumo wa falsafa ewe mwanafalsafa! Mambo yote uliyoyataja hayawezekani na si mantiki; kitu hakiwezi kujiumba na kuiumba akili yake mwenyewe, na haiwezekani kuwa mambo haya yamejitokezea hivi hivi tu kwa umakini huu tunaouona. Sina zaidi ya hapo, kisha Joji akaamka kwenye kiti alichokalia, na akaendelea kusema: Nitafuata njia yako, na tutaona tutafika wapi, tuyaweke maswali yetu hadi yatufikishe katika ukweli hata ikiwa hatukinaishwi nayo hapo mwanzoni.
Hukujibu maswali yangu..majibu ya maswali yetu tutayapata wapi?
Ni nani aliyeumba watu; kwa sababu yeye ndiye anayewajua kuliko wanavyojijua.
Maneno yako yananifurahisha pamoja na kutofautiana nawe, sitojadiliana nawe kwa uliyosema, lakini nitaendelea kukuuliza maswali ambayo yatabainisha makosa yako, tujaalie kuwa uliyoyasema ni sahihi..Je huyo Mola wa watu ambaye atatujibu ni Mola wa Budha au Jua, au Masiya au roho mtakatifu au…? miungu ya watu ni mingi na hubadilika mara kwa mara; tutawezaje kujua mungu wa haki kutokana na miungu yote hiyo? Je hujui kuwa dini ni nyingi mno?!
Najua, zipo zaidi ya dini kumi elfu (10,000), Ukristo ni dini na ni dini moja yenye zaidi ya makundi 33,830.
Mimi nipo mbele ya mtu mwenye kufanya mjadala, mwenye maarifa mengi na mtu msomi, nitazingatia kuwa jibu lako ni sahihi, hebu tukamilishe: ni nini dhamana ya kuwa jibu hilo ni sahihi?
Uwepesi wake: Iwe ni nyepesi au rahisi na isiwe ngumu, ituletee furaha, isigongane na akili na mantiki au elimu au kugongana na nafsi zetu kwa ndani, na kuenea katika maeneo yote ya maisha yetu.
Jibu sahihi, jepesi na makini..ina maana jibu lolote linaloelekea kuwa kweli, lakini halituletei furaha au kwenda kinyume na akili au mantiki, au kuwa gumu, au halienei katika maisha yote ya mwanadamu hatulikubali!
Naam..bila shaka!
Vizuri, ukipata jibu hili mimi nipo pamoja nawe, kisha alitabasamu na akasema: nitakupa maswali mapya, na utabaini ukweli wa majibu yetu na usahihi wa njia yetu na makosa yake …kisha akatabasamu na kusema: pamoja na kuafikiana nawe kuhusu dalili potofu wanazoamini wakana dini na kumkana Mwenyezi Mungu, ila naendelea kuamini kuwa hakuna Mungu..kwa jumla tutapita katika njia hatuijui itatufikisha wapi, swali langu kwako: ni Mungu gani huyo tutakayechukua majibu kutoka kwake? na katika njia ya dini gani?
Turahisishe maudhui yetu: kuna makundi mawili ya dini na fikra za watu zinapotoka, dini za mbinguni na dini za ardhini, je wewe unauliza kuhusu lipi katika hayo?
Umesema kweli..dini ni nyingi, ni vizuri kurahisisha mambo kwa kugawa katika makundi makubwa, kwa hakika sikufikiria hilo, wewe utasafiri kuelekea India hebu tubadilishe swali kwa: Ni dini ipi iliyo bora: dini za ardhini za watu au za mbinguni? Na baada ya kila jibu tutaingia katika vipengele vyake kulingana na majibu yako katika ahadi yetu baada ya wiki mbili, nadhani utaona dini zilivyo huko India na kitakupelekea pale nilipo kwenye ukanaji na kujitenga na dini zote.
Nitasafiri kwenda India! umejuaje?
Nimejua kutoka kwa…nimejua kutoka kwa Katarina..nilimuona kwa bahati kanisani.
Vizuri kwa mkanaji dini anayepinga Mungu kwenda kanisani!
Nimekwenda kanisani kusoma tabia za watu wenye kuabudu, na sio kufanya ibada.
Mhmh, umemuonaje Katarina.
Mwanamke mwenye akili, mfanya ibada. Bado fikra za mashariki zikiwa zimemtawala kwa roho yake na umbile lake.
Inaonesha umevutiwa nae.
Kwa kweli nimevutiwa na kuabudu kwake na yakini aliyokuwa nayo, nakupongeza, anakupenda sana.
Mkanaji dini anapenda waamini? jambo la ajabu kabisa!
Huenda ikawa hivyo, kisha akajaribu kubadilisha maudhui: hushibishwi na uzuri wa Wahindi na sasa unataka kusafiri kwenda India?
Sifahamu unalosema?
Haikutoshi uzuri wa Katarina, unakwenda sasa kutafuta starehe na wahindi wengine wazuri! na kucheza nao?!
Achana na hili..mimi nitasafiri kujua hizo dini na mifumo ya maisha, kadhalika kuingia katika mikataba ya kazi, kwa heri, ahadi yetu ni baada ya wiki mbili.
Tumeafikiana, nina hakika utaachana na kila dini utakayojaribu kuwa nayo karibu, nakutakia kila la kheri na faida na starehe za huko India.
Umenipa wasiwasi, ulikuwa wapi jana, hukulala nyumbani?!
Wewe hukurudi jana isipokuwa usiku sana, inakuhusu nini mimi kulala nyumbani au nje.
Ndio, jana tulichelewa kanisani, hafla ilikuwa ni muhimu na nzuri kabisa.
Bila shaka ilikuwa nzuri kwa kuwepo kwake.
Unamkusudia nani?
Ulikuwa na nani katika hafla?
Wengi, wengi tu.
Ni nani katika waliohudhuria ninaowafahamu?
Joji, haya ni maswali ya uchunguzi? hata hivyo nitakujibu: Padri Morris, Sali, Peter, Hillary, Simpson na…
Tom mtanashati!
Naam…! na daktari Tom alikuwepo, alikuja kuzidisha imani na yakini kwa Bwana wake na alihudhuria misa yote pamoja nasi!.
Vizuri sana..mkanaji Mungu anahudhuria misa, au anafurahia kunywa, kucheza na mkesha?
Wewe unanidharau na kulidharau kanisa, una maana gani? na ni nani aliyekuambia amehudhuria mkesha? nakusudia?
Hapana, sikudharau wala kulidharau kanisa, yeye ndiye aliyeniambia kuwa alifurahia mkesha pamoja na Katarina mzuri anayepagawisha watu, na Tom ambaye anataka kuzidisha imani yake ndiye aliyenihamasisha kwenda India nikastarehe na uzuri wa wanawake wa Kihindi na kucheza nao!
Yeye ndiye aliyesema hivyo!
Ndio, nini kigeni kuhusu hilo?
Hakuna! lakini…
Mimi nimechoka na nataka kulala, samahani nakwenda kulala chumbani.
Nipe habari nzuri, umeamua nini Joji?
Nitakwenda India mwisho wa wiki tukimaliza mapatano ya kazi baina yetu, nimeshapanga mambo yangu.
Vizuri sana, tutahitaji vikao virefu vya mara kwa mara; ili kuweza kujua vipengele vya mkataba inayotakiwa, kadhalika kujua hali za watu kule.
Baada ya saa nitakuwa kwako tuanze vikao vyetu leo kwa muda wa saa tatu na kesho kwa muda huo huo.
Je una maelezo mengine yoyote unataka kujua?
Hapana, sina, mambo yamenifungukia zaidi, pamoja na kuwa mshikamano ambao msingi wa faida unasimamia hautoshi bali ule uliosimama katika maslahi ya pande mbili zaidi ndio utakaodumu zaidi na wenye nguvu zaidi.
Kuhusu faida ni kupata zaidi na kwa matumizi madogo…kisha akatabasamu, mimi nahitaji faida ya mali zaidi na wewe utapata faida zingine zinazotokana na misingi imara ya kihisia.
Tumeafikiana!!
Nimesahau kukujulisha ule mshangao wangu niliokusudia.
Mshangazo gani?
Je unakumbuka kuwa nilikwambia kuwa nitakushtukiza na jambo ambalo litakusahaulisha maswali yako, na yatakusahaulisha daktari wako pia.
Ni lipi hilo?
Jaribu starehe za India.
Unakusudia starehe gani?
Mbona wewe mpumbavu wakati mwingine, jaribu wanawake wa India, na watakujibia kila swali utakalouliza…Maiko atakutayarishia kila kitu. Maiko ni Mkuu wa Shirika la Ajira nililokuelezea..kisha akacheka kicheko chenye kuonesha dharau ndani yake, na akasema: Je sijakwambia kuwa yeye ni Mkristo mwenye dini tena sana.
Jumatano asubuhi ndio safari yangu, je unataka chochote kwangu?
Safari njema, na nakutakia ufanikiwe uingie katika mikataba yenye faida ya kimali na maslahi zaidi na sio misingi ya kimaadili, na nakutakia starehe na wanawake wazuri.
Haituhusu anakuwa nani, madamu anatupa fursa ya kuingia katika mikataba na kubadilika…na kwa kicheko cha kubeua aliendelea kusema: huku ndiko kuamini kwa kutumia akili, atakayenifurahisha zaidi basi nipo tayari kumtumikia na kumuabudu.
Unakusudia uzuri gani?
Uzuri wa wanawake wa Kihindi na michezo yao ya kimashariki.
Mpenzi wangu umechelewa, nimekusubiri masaa mawili?!
Nilikuwa na vikao virefu pamoja na Kakhi kuhusu safari yangu.
Kweli! nimesahau, hukuniambia kikao chako jana na daktari Tom kilikuaje?
Nilimjibu kwa yale majibu ya yule mhudumu! nilikinaishwa nayo na kadhalika naye alikinai na majibu yale.
Vizuri sana..la muhimu ni kuwa mnakwenda sawa.
Amenipa pia maswali mapya!
Maswali gani hayo mapya?
Nimwambie ni dini gani iliyo bora zaidi ambayo tutaweza kuchukua ndani yake, na Mungu yupi ambaye atatupa majibu yetu.
Majibu yako wazi. Mungu, na masiya na roho mtakatifu, hawa watatu ni mmoja wao ndie aliyemuumba mwanadamu, na anayesema kinyume na hivyo basi amekana..kisha akaanza kucheka.
Ameninasihi kuangalia dini wakati nikiwa India. Kisha baada ya hapo nimwambie ni dini gani sahihi za mbinguni au ardhini (za wanadamu)?
Safiri na utaona India maajabu yake usiyoweza kutarajia; ni nchi ya maajabu, na utarejea ukikiri maneno yangu.
Na vipi kuhusu usia wa Tom wa kustarehe na wanawake wa India?!
Usimtii katika hilo, mpenzi wangu.
Je unanishuku?
Asili yangu ni India na pamoja na hayo sikuiona India kwa zaidi ya miaka ishirini, je unaweza kuniletea zawadi kutoka India?
Kwa furaha kabisa…unataka nini?
Nataka msalaba uliotengenezwa kwa mkono.
Nitakuletea msalaba uliokuwa bora kutoka India, lakini nina sharti dogo.
Karibu, sema.
Nataka usiku huu wa leo uwe usiku bora zaidi kwetu..haya twende tukalale.