BAINA YA UHAI NA KIFO

BAINA YA UHAI NA KIFO

BAINA YA UHAI NA KIFO

(1)

Joji alipanda ndege na moyo wake ukiwa umeshughulishiwa na Levi, aliuteka moyo wake pamoja na kuwa muda wa kukaa kwake ilikuwa siku nne tu.. Ni nini siri yake?! Alionekana kama Malaika tohara katika jamii dhalimu na ngumu, alikumbuka mijadala ya Levi kuhusu mwanamke na haki zake zilizosulubiwa katika Uyahudi, dini gani hii ambayo imemrithisha mwanamke kama vile chombo cha matamanio na wanamzingatia kama vile uchafu na mbwa harithi, na ya kuwa hana haki zozote? Na akakumbuka mjadala wa kupotoshwa kwa torati na chuki yao kwa Waislamu wauaji wa baba yao na kwa kizazi kilichochaguliwa ambacho kinaua na kuiba na kupoka watoto wa Shilo, alikumbuka hadithi kuhusu athari zisizokuwepo ambazo ndizo dalili ya kweli ya kuwepo kwa Uyahudi katika eneo hili…alitabasamu akiwa anakumbuka maneno ya Levi kuwa hatohama kutoka kwenye mazonge ya Uyahudi na kuelekea kwenye mazonge ya Ukatoliki wakati akiwa katika kumbukumbu hiyo alikatishwa na abiria aliyekuwa pembeni yao:

Hii ni sindano ya nini mkononi mwako ewe Bwana?

Nimepewa na daktari, na akanitaka nipande nayo kwenye ndege; kwani huenda joto langu likapanda ghafla.

Je naweza kuiona?

Chukua, je wewe ni daktari?

Aliiangalia ile sindano, na akasoma maelekezo yaliyopo kwenye karatasi iliyokuja na sindano.

Mimi ni mfamasia, inaelekea kuwa sindano hii ni muhimu sana, kwa ujumla ni dawa iliyokuwa nadra kutumika.

Kwa nini unatumia? Sijui, daktari hakunijulisha.

Sijui, lakini sindano hii hutumika kwa ajili ya hali za dharura sana; kwa lengo la kupunguza aina ya virusi ambao ni vigumu kuwamaliza.

Nadhani hii inatokana na marafiki zangu kunijali mimi, hata hivyo afya yangu ni njema.

Huenda ikawa ni hivyo, hata hivyo sidhani kama ni sahihi, sindano hii haiuzwi ila kwa maelekezo maalumu ya daktari na katika hali za dharura mno.

Labda, sijui, hata hivyo siha yangu ni nzuri.

Siha ya mtu na afya yake ni taji juu ya vichwa vya watu wenye afya nzuri, haioni isipokuwa mgonjwa tu, samahani kwa kukusumbua.

Si hivyo. Nakushukuru.

Joji alijisalimisha na kumbukumbu zake kwa mara nyingine… moyo wake ulikuwa kwa Levi, alihisi kuwa anahitaji kumshukuru kwa yote aliyomfanyia, pia alimkumbuka Habib ambaye usuhuba nae ulikuwa mzuri pamoja na kuwa alikuwa ni mwarabu, alikuwa na mijadala nae kuhusu Waislamu, na alipomwambia: Wewe ni Muislamu uliyejificha nyuma ya Ukatoliki… Ama kwa hakika safari hii ilikuwa imejaa mambo mengi na yenye kufurahisha sana… mara mhudumu wa ndege akamkatiza.

Samahani, unapenda chakula gani zaidi? kuku au nyama?

Nyama

Msafiri mwengine aliyekuwa jirani yake aligeuka na kumwambia:

Inaelekea uko mbali sana!

Ooh… ndio, safari yangu hii ilikuwa nzuri na nimejifunza mambo mengi.

Umekaa Yerusalem muda gani?

Siku nne

Siku nne tu!

Ndio, lakini kama kwamba nimekaa miezi, siwezi kamwe kuwasahau watu wazuri niliokutana nao, nimejifunza kutoka kwao mengi katika ardhi hii tukufu.

Je wewe ni Myahudi?

Hapana ….kwa nini?

Mimi ni Myahudi….Samahani, lakini hakuna mwenye kuhisi hali ya raha hapa Yerusalem asiyekuwa Myahudi, kwani nchi imetayarishwa kwa ajili yao. Ama Wakristo na Waislamu hali zao si nzuri, hivyo uliponiambia kuwa umefurahishwa na uliokutana nao nikafikiri ni Myahudi?!

Nimekutana na Myahudi na Mkristo Yerusalem, wote hawa walikuwa ni watu wazuri sana.

Maneno haya yanafaa kusemwa Uingereza, Ama TelAviv dini ndio inayowaendesha watu na mataifa.

Wewe ni Myahudi, je ninaweza kukuuliza?

Uliza, usijali

Je wewe umekinaishwa na mafundisho ya torati?

Hapana, huwezi kuifahamu vizuri ila baada ya kufahamu mafundisho ya Talmuud.

Vizuri, je nakuhusu mafundisho ya talmuud? Je umekinaishwa nayo?

Ha ha ha, hapana vile vile, lakini hili ndilo mbeleko letu.

Samahani, mgongano huu haukukeri ndani ya nafsi yako?

Hakuna asiyesumbuliwa na hilo, hata hivyo watu wanatofautiana katika kuyachukulia mambo yanayowakera.

Kwa vipi?

Mimi naukimbia mgongano huu kwa kujishughulisha sana na kazi zangu na kuna watu wengine wanaukimbia kwa kunywa pombe au kwa kujishughulisha na wanawake mbali mbali, na wengine wanaukimbia kwa kufanya utafiti wa kielimu katika kadhia hii na wengine kwa kuzidisha sana kuabudu.

Vizuri, umekuwa mkweli sana wa nafsi yako.

Asante sana.

Lakini linabaki swali; je huku kukimbia kunapelekea raha na utulivu au hapana?

Nadhani kwa maafikiano ya watu wenye kutumia akili zao vizuri na kuwa ambae ataishi bila ya dini atakuwa mgonjwa; na hivyo basi kukimbia ni njia ya jitahada za kukimbia maradhi ya wakanao dini na dhulma yake na kuwa mbali na mgongano wa dini.

Ila yule ambaye kimbilio lake ni la utafiti wa kielimu wa kadhia hii, au sivyo?

Ndio, ila mimi sipendelee hilo, kwani linakufanya uwe na huzuni na ghamu na mgongano katika kufikiri.

Kama kwamba unaniambia hakuna suluhisho ila kukimbia tu?

Ndio na hapana.

Ha ha ha, kwa vipi?

Naam; Mimi sijui suluhisho lingine ila kwa kukimbia tu, na ni hapana; kwa sababu haiwezekani Mwenyezi Mungu akatuwacha hivi hivi tu tukapotea na huu mgongano na kukimbia.

Unaelekea zaidi kuwa ni mwanafalsafa na sio mfamasia.

Kitakachonichosha ni kutafuta kwangu ukweli, njia za kisomi na kielimu zinagongana na ninachokisema, na nimejifunza katika ufamasia nisizungumze kitu ila kwa njia ya kisomi.

Kutafuta ukweli au kama ninavyopenda kuuita njia ya furaha ni yenye kufurahisha wala haihuzunishi.

Njia ya furaha! Maelezo mazuri.

Samahani kama nitakukata, je huoni kama ndani ya ndege kuna baridi? Najihisi baridi sana.

Mfamasia aliweka mkono wake juu ya kipaji cha uso cha Joji kuhisi joto lake, kiwango chake cha joto kilikuwa kikubwa.

Huenda kwa ajili hii ukawa umepewa sindano hii uliyokuwa nayo, unajihisi vipi sasa?

Baridi imezidi, nahisi uchovu sana, usijali baada ya muda hali itakuwa nzuri, je umependezwa na njia ya furaha?

Achana na njia ya furaha kwanza, je unaweza kunipa hiyo sindano na katarasi ya maelezo ya daktari?

Hii, chukua tafadhali.

Mfamasia alimuulizia mhudumu kwenye ndege kama kuna daktari, akamjibu hapana, alitarajiwa kuwepo lakini amechelewa.

Hamna neno, nitampiga sindano mwenyewe; kwani nimepata mafunzo ya kutosha kuhusu huduma ya kwanza, nyongeza ya kuwa mimi ni mfamasia vile vile, hata hivyo atapoteza fahamu kidogo na naamini hatoamka ila baada ya kufika kwetu, je unaweza kumuagizia gari la wagonjwa itusubirie uwanja wa ndege wa London.

Inaelekea hali ya hatari, hakuna haja ya hilo, mke wangu ananisubiri na gari la wagonjwa, nadhani umezidisha zaidi.

Sijazidisha, hata hivyo sipendi kuvuka mipaka ya njia za kielimu katika kushughulikia mambo mbali mbali.

(2)

Joji aliamka kutoka kwenye usingizi mzito na kujikuta yupo hospitalini London, pembeni yake akiwemo Katarina huku akitabasamu.

Namshukuru Bwana kwa usalama wako mpenzi.

Nipo wapi? yuko wapi yule mfamasia?

Wewe upo hospitalini London, lakini ni nani huyu mfamasia?

Hospitalini? yuko wapi yule abiria niliyekaa nae pamoja kwenye ndege?

Ooh, nimefahamu, hakuondoka hadi alipokufikisha kwenye gari la wagonjwa, na akahahikikisha afya yako, alichukua anuani yako na kuondoka, namshukuru Bwana Mungu.

Unaendeleaje mpenzi wangu, nimekutamani sana, samahani kukutaabisha na kukusumbua, sikujua kuwa itafikia kiwango hiki.

Daktari amesoma ripoti yako na akachukua sampuli ya damu yako na wakaangalia hapo hospitalini kwa eksirei na wakasema kuwa watahakikisha vipimo hapo kesho.

Tutakwenda wakati gani nyumbani?

Sijui, baada ya kutoka matokeo ya vipimo. Amesema watatujulisha lakini kwa uchache ukae hospitalini kwa muda wa wiki nzima kama walivyosema.

Wiki nzima?!

Cha msingi sio wiki, bali ni kutumaini afya yako, na wanashangaa ni kwa nini hukubaki hospitalini huko?

Walitaka sana hilo na wakajaribu, lakini niliwakatalia….kwani kuna nini huko?

Nitachukuwa likizo na kukaa pamoja nawe, huenda huu ni munasaba wa kukaa pamoja; nina hamu sana ya kukaa nawe.

Nami hali kadhalika nahitaji hilo sana, natamani turudi pamoja nyumbani.

Tutatoka karibuni, usihofu mpenzi… je umetembelea Kanisa la Kiama?

Ndio…na nilikuahidi kulitembelea, kadhalika nimetembelea Kanisa la Bikira Maria.

Furaha iliyoje kwa kila anayesali katika Kanisa hili lililobarikiwa kiasi gani natamani kulitembelea.

Nimeswali kwa ajili yako kama nilivyokuahidi, lakini kuna furaha gani katika hili?

Sijui furaha nyingine zaidi kuzama katika kumuabudu Mungu.

Vivyo hivyo ndilo wanalosema Mayahudi wa siasa kali hata ikiwa sikukuu zao na ibada zao ni za huzuni na kilio!

Kweli kabisa, lakini wao wanamuabudu Mungu kwa dini iliyokwisha futwa na kuisha baada ya kudhihiri Masihi Kristo amani iwe juu yake, bali walimpiga vita na kumuuwa Masihi Kristo na kuwaadhibu wafuasi wake.

Je kwani Wakristo hawaiamini torati kwani ndilo Agano la Kale?

Ndio, wanaiamini.

Sasa kwanini uniambie kuwa ni dini iliyokwisha kwa kudhihiri Kristo?

Unaelekea kuhamasika sana na Uyahudi, kama dini imekwisha, yamebaki mafundisho tu ya torati.

Iwaje uamini na upate mwongozo wa mafundisho yaliyokwisha potea?

Yaliyokwishabadilishwa nani aliyekuambia hivyo?

Maelezo yamekuja katika torati kuhusu watoto wa kike wa Shilo:

Akawausia watoto wa Benjamin kwa kusema: “Nendeni Kromu na jificheni humo na subirini hadi watakapotoka wasichana wa Shilo ili kucheza nendeni kwa haraka kwao, na kila mmoja wenu amteke mmoja kisha torokeni nao hata kwenye ardhi ya Benjamin”, je unawajuwa hawa wasichana wa Shilo? Je unaamini kuwa maandiko haya ni ya Mungu?

Nawajua vizuri watoto wa Shilo, sipendi kuzungumzia hilo, ni maelezo ambayo tunaweza kuyapata kwa maelezo ya Maaskofu na Mapapa.

Imekuja katika torati vile vile: “Alisema Bwana Mungu wa Israil: Kila mmoja wenu abebe panga lake na azungukie sehemu mlango hadi mlango na amuuwe ndugu yake, rafiki yake na jirani yake” Je, maneno haya ya kikatili yanaweza kuwa ni ya Mungu?

Samahani napenda ubadilishe maudhui, nayajua vizuri maandiko haya na mengine mfano wake, na sipendi kuyajadili, kadhalika wewe unatakiwa upumzike.

Kwa nini?

Nimekuambia sipendi kuzungumzia maudhui haya…Nadhani unao muda wa kutosha hapa hospitalini wa kutafiti na kusoma.

Umesema kweli la muhimu niwe na kompyuta, kadhalika napenda kununua baadhi ya vitabu, nataka kusoma kuhusu Ukristo na madhehebu yake mbali mbali.

Vizuri sana, huenda ukawa Mkatoliki.

Huenda ikawa hivyo!

Kusoma kwako huku kutakuwa kitangulizi kizuri cha safari yetu, umeshasahau mpenzi wangu?.

Sijasahau, nitajaribu kesho pamoja na daktari ili iwe karibu iwezekanavyo, hata hivyo inabidi muda wangu huu wa kuwepo hospitalini niutumie vizuri kwa kusoma.

Usijali sana kukaa kwako, nitakuwa pamoja nawe na kuzungumza pamoja.

Kiasi gani nakupenda mpenzi wangu Katarina.

Nami hali kadhalika, Je, utaniruhusu niondoke sasa hivi nije kesho? Usiku unaingia, na mimi tokea jana nipo hapa.

Samahani, nimekuchosha, nitakusubiri kesho mpenzi wangu, lililo muhimu ni kuwa nileteeni kompyuta yangu na simu yangu iwe jirani nami, nataka kumalizia baadhi ya kazi zangu.

Nitaweka kompyuta yako na simu yako mezani hapo karibu yako, lakini kwa sharti usijichoshe, nataka upumzike mpenzi wangu, tutaonana kesho.

Joji hakutaka kulala, bado ilikuwa ni mapema mno, aliamua kusoma kidogo, na kuanza kusoma barua pepe zake na kukutana na barua ya Levi ikimtaka kumuelezea kuhusu afya yake, akamjibu na kumuelezea kilichotokea, na akamshukuru mno kuhusu sindano aliyompa, na mapokezi yake, na kila alichompa. Na akamkumbusha kuwa hakusahau ahadi yake, lakini hata hivyo alikuwa bado hajawasha kompyuta na simu yake ila muda mfupi tu uliopita. Kadhalika alimuhakikishia kuwa yupo katika ahadi yake aliyompa kuwa ataendelea kumpa habari za njia ya furaha, na akamtaka amtolee shukurani nyingi Habib vile vile.
Alikutana na barua nyingine kutoka kwa Adam inayoelezea kuhusu starehe ya kiwiliwili kwa mateso ya roho ikisema:

“…ikiwa roho haitopata furaha pamoja na kiwiliwili, basi nilichokiita furaha ya kiwiliwili ndio huzuni ya kiwiliwili na ya kiroho, na falsafa hii itaendelea kubakia kuwa ni falsafa nyeusi, falsafa ambayo inazingatia kuwa maisha ni huzuni na hakuna furaha ndani yake. Swali linalojitokeza hapa je tumeumbwa ili tupate tabu na kuhuzunika au tumeumbwa ili tuwe na furaha? Ule muono wa kuwa sisi tumeumbwa ili tupate tabu ni muono uliokuwa wa karibu sana na muelekeo wa wakanao kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ambao unamtuhumu Mola kwa kila upungufu au dini za wanadamu za kipagani zilizo mbali kabisa na ufahamu wa tabia ya Mwenyezi Mungu na tabia ya mwanadamu na tabia ya dini, au kwa dini ambazo zimeathirika na upagani kwa sababu ya kubadilishwa kwake na kuchafuliwa mafundisho yake. Kwa ujumla muono huu unakupa sura ya mtu mwenyewe asiye na furaha na migongano ya ndani aliyokuwa nayo kuliko hata ilivyo rai ya kisomi au ya kifalsafa au hata ya kidini….nataraji utakuwa umeshawasili kutoka safari yako, baada ya mapumziko ya safari yako tutaonana ili tuendelee kujadiliana katika hilo.”

Joji alimaliza kusoma barua na akairejea mara ya pili, kisha akajisemeza: Adam kama ilivyo ada yake, sijui ni kwa sababu yeye ni mwanafalsafa mkubwa au ni kwa sababu yeye ni Mprotestanti au ni Myahudi? Na sijui ndani ya maneno yake –pamoja na udogo wa umri wake na ukawaida wa kazi aliyokuwa nayo nayaona kuwa ni maneno ya kawaida lakini ya kina katika wakati huo huo? Amesema kweli Adam: Roho haiwezi kuwa na furaha peke yake kadhalika kiwiliwili hakiwezi kupata furaha peke yake: Mwanadamu ni kitu kimoja kilichokamilika na kumgawa ni aina ya ujuu juu wa kadhia za kina kabisa, yaani ni starehe gani ya kiwiliwili ya kupita ambayo itafuatiwa na maradhi ya kiroho na ya kiwiliwili, na starehe gani ya roho katika utawa na kuyaacha hata ikiitwa kuwa ni ya kimaadili au ya kiroho kama ilivyo utawa wa KiBudha. Ama kwa hakika njia ya kuelekea furahani ni lazima roho iungane na akili pamoja na kiwiliwili, muungano ambao utaufanya ufurahi na sio kuuadhibu, ili baada ya hapo kiwiliwili kwe furahani na kustarehe kwa akili iliyo nyoofu iliyozungukwa na furaha ya kiroho itakayofanya kuwa juu! Baadhi za dini zimeikimbia hali hii, hali ya starehe ya kiwiliwili ili ufurahishe roho, na dini zingine vile vile zimekimbia starehe za roho ili zishughulike na kiwiliwili tu. Na zote hizo hazikuweza kuzifurahisha sio kiwiliwili wala roho hali kadhalika.
Joji aliangalia saa yake, ilikuwa inaashiria saa mbili, hivyo akampigia Adam.

Ndio Adam, nimeshafika London lakini nipo hospitalini, na ndio maana siwezi kuonana nawe, Je, unaweza kuja kunitembelea ili tumalizie falsafa yako na mjadala wetu?

Pole sana… Nitakutembelea, na sito kukera na mjadala wangu au falsafa yangu kama unavyoiita, nataraji nisikuchoshe.

Sijakusudia hivyo, kwa hakika ninafurahishwa na mjadala wa pamoja nawe na falsafa yako, hivyo usinielewe vibaya.

Nami sijakusudia kuwa nimeghadhibika kwa maneno yako, hili jambo ni la kawaida na dogo na mimi ninapenda mambo madogo ya kawaida, nitajaribu kukutembelea kesho jioni.

Nitakusubiri Adam, natamani mazungumzo nawe

Ha ha ha, tutaonana kesho, inaelekea unachanganya baina ya hamu ya mazungumzo na hamu ya kunywa kahawa, kwa heri.

Joji alizima simu akawa anafikiria…Ni siri gani inayomfanya avutike na Adam? Yeye sio Mwingereza anaweza kuwa ni Myunani au Mtaliano au ni mtu kutoka Latini; ila napata tatizo kutoka kwake; Itakuwaje kama Levi atanikuta na Adam?. Atamuonaje? Ha ha ha, je Adam ataweza kuwa na subira akimwona na yale macho yake ya kibluu na nywele zake nyekundu? Au atakuwa kama vile (Kakhi) mwingine, nasaha zake ni nadharia tu kama walivyo watu wengi? Ha ha ha bali kama ndio nilivyo mimi?! Kwa ujumla kesho itafika, na nitamueleza kila nililo kutana nalo…

(3)

Nesi alimwamsha Joji mapema, na wakati huo huo akimuwekea kifungua kinywa mezani mwake.

Muda gani atafika daktari?

Saa tatu asubuhi daktari atawazungukia wagonjwa, la msingi ni kuwa ukihisi kupanda kwa joto niambie upesi, sisi tutapima joto kila baada ya saa moja kuanzia saa mbili ambapo nguvu ya ile sindano uliyopewa inapokuwa imekwisha.

Asante, inaelekea kuwa swala la joto ni la hatari na linaangaliwa mara kwa mara.

La msingi ni kuwa ukihisi kupanda kwa joto mwilini mwako au ukihisi baridi tujulishe upesi.

Vizuri, vizuri.

Joji alimaliza staftahi yake, alikaa akifikiria maneno ya nesi, na akakumbuka jinsi Levi alivyomtahadharisha kuhusu sindano alipokuwa akimpa… alihisi hali ya hofu na – akisubiria kuja kwa daktari ambaye alifika chumbani saa tatu na nusu.

Je unaweza kunijulisha hali yangu?

Uchunguzi wetu hadi sasa hivi ni sawa na matokeo ya uchunguzi uliopita uliofanyiwa Yerusalem.

Samahani, sijui matokeo ya uchunguzi wa vipimo vya Yerusalem ni yepi hayo?

Kuna virusi vimeingia katika mishipa ya akili, na ghafla bila ya onyo lolote lina sababisha kupandisha joto, hivyo basi tunalazimika kukubakisha hospitalini pamoja na kuwa upo katika hali ya kawaida kabisa na husumbuliwi na tatizo lolote, hivyo basi joto la kiwiliwili chako likipanda tunalazimika kukupa sindano yenye kutuliza na kushusha joto, ambayo nguvu yake inadumu kwa muda wa siku moja hadi mbili.

Hadi lini nitakuwepo hospitali?

Kwa sasa hivi siwezi kujua, kwa ujumla ni kuwa kuna vipimo vingine ambazo tunasubiria matokeo yake, ambayo yatakuwa tayari baada ya siku mbili zijazo, katika hali yoyote ni kuwa haitozidi zaidi ya wiki mbili, kama jambo lingine halitojitokeza.

Ni nini sababu ya virusi hivi?

Hadi sasa haijulikani, hata hivyo usijali, tutajaribu kukupa utulivu kadri iwezekanavyo, kadhalika tutakujulisha maendeleo mara kwa mara, hayo ndio ninayofahamu hadi sasa kuhusu maradhi yako.

Nakushukuru kwa muamala wako mzuri.

Daktari aliomba ruhusa na kuondoka…Joji alichukua Kompyuta yake, ili apange muda wote atakapokuwa hapo hospitalini autumie vipi. Joji aliamua kuwa muda atakaokuwa hapo hospitalini autumie kwa ajili ya kujisomea, haswa kwa sababu yupo katika njia ya furaha, ambapo anahitaji kufahamu kuhusu dini muhimu zaidi ambayo ndio dini yake, akaanza kujiuliza huku akiitilia shaka nafasi yake akiwa katika hali ya kukariri maneno. “Kuijua dini yangu! Kuujua Ukristo na madhehebu yake, kama alivyokwisha toa maamuzi autumie muda wake mwingi –kujadiliana na Katarina; ambaye ni mwanazuoni wa Kikristo. Kadhalika pamoja na Tom na Adam, vile vile na katika mijadala mbali mbali kwa njia ya barua pepe na Levi na Habib ikiwezekana. Kisha baada ya hapo akachukua muda kusoma na kila kundi asingeweza kumaliza.
Ilipopindukia usiku wa manane Katarina alifika hospitalini akiwa na Maiko pamoja na Sali, Joji alifurahi sana kuwaona, alikuwa na hamu nao, aliwakalisha pembeni yake ili aweze kuwatania na kuwachezea. Joji alikuwa katika hali ya furaha pindi alipokuwa akicheka nao, na hapo hapo akakumbuka furaha yenye kufurahisha roho na kiwiliwili kwa pamoja na akajua ya kwamba hali hii ya starehe hupata kwa kukaa pamoja na wanawe. Akajizungumzisha lau kama watu wote watafahamu kitakachowaletea furaha ambacho kitafurahisha roho na kiwiliwili na hapa ndipo hatima ya furaha itakapofikiwa…..
Aliwaangalia watoto wake wawili… kisha ikamjia fikra akilini….

Nini kinachokufurahisha zaidi ewe Maiko katika maisha?

Kucheza na wewe baba, na ninapenda mpira wa miguu.

Na wewe Sali?

Nami napenda kucheza nawe baba, na vile vile napenda kuchezea midoli.

Na mimi napenda kucheza nanyi, je kuna chenye kuwafurahisha kingine zaidi ya michezo?

Maiko kwa mshangao:

Wakati mwingine napenda kufurahi lakini sijui kwa nini? Na wakati mwingine nahisi tabu na sijui kwa nini? Ni kwa nini baba?

Wewe unadhani kwa nini Maiko?

Huenda ikawa furaha kwa sababu nimemsaidia mwenzangu shuleni au rafiki yangu, na tabu na huzuni kwa sababu ya jambo nililofanya.

Tabasamu kubwa lilijitokeza kwa Katarina kwa mjadala huu mzuri wa kifamilia. Kisha Katarina akasema: Mpenzi wangu huenda furaha inakuwa kwenye moyo tunapowapenda watu na kuwatakia kheri.

Una maana kuwapendea watu kheri, hata kama hatujafanya jambo lolote mama.

Ndio, na mfano wake kuwachukia watu na kuwataka shari, hata kama hatujawafanyia lolote.

Joji alipendelea mjadala ule uendelee zaidi kisha akasema: Maiko na Sali kama ni hivyo kwa nini watu wasijifurahishe wenyewe na wachague wenyewe huzuni na tabu?

Maiko: Kwa sababu wao ni wapumbavu.

Sali: Au ni kwa sababu hawajui.

Katarina: Au yanaweza kuwa yote mawili, na nyongeza ni kuwa uongofu na kufanikiwa katika kufanya ya kheri na furaha zote ni neema kutoka kwa Mungu.

Joji: Kama ni hivyo, basi ni bora tukatafuta njia ya kuelekea kwenye furaha.

Maiko: Nimekusikia ukimwambia mama kuwa utasafiri kwenda Yerusalem; ili kutafuta na kufanya utafiti ilipo njia ya furaha, je njia hiyo ya furaha ipo Yerusalem tu?

Ha ha ha, sivyo mwanangu, ninachokitafuta ni haki, na safari yangu kikazi inanipeleka Yerusalem kwenda kuingia mikataba ya kazi huko, na ni fursa kwangu kutumia fursa hiyo kujifunza, na kufahamiana na watu.

Sali alisema bila kujitambua:

Siwapendi wakazi wa Yerusalem.

Joji katika hali ya mshangao:

Kwa nini?

Kuna msichana ninasoma nae shule anasema, jamaa zake mara kwa mara wanakwenda Israel na haswa katika mji wa Yerusalem, na anasema kuwa Israel yote ni mauaji na magereza na adhabu na milipuko, na kwa sababu hiyo siipendi wala sipendi watu wake.

Katarina alishangazwa na maneno ya binti yake, kisha akasema: hakuna mwenye akili anayependa ugaidi na mauaji. Sheria zote za ardhini (za wanadamu) na za mbinguni (kutoka kwa Mungu) huamrisha uadilifu na wema.
Alipokuwa akizungumza Katarina Joji alikumbuka ubudha, na sheria mbali mbali za Agano la Kale kuhusu mauaji ya wanawake na watoto wa Shilo, kisha akatabasamu na kusema:

Yerusalem kuna watu wazuri wa kila dini katika wayahudi, wakristo na waislamu

Sali: Kwa hivyo basi simpendi Levi binti wa Kiyahudi, yeye anapenda mauaji haya na magereza.

Joji: Ni nani huyu Levi?

Mwenzangu ninasoma nae shule, binti wa Kiyahudi.

Joji: Vizuri ni vizuri enyi wanangu kupenda na kuwachukia watu kwa misimamo yao au tabia zao, na sio kwa sababu ya maumbo yao wala nchi zao.

Maiko: Nami simpendi mwenzangu David, yeye hazungumzi chochote isipokuwa Pombe.

Joji alimuangalia Katarina kwa muono wa kumuibia…kisha akatabasamu….

Ehe katika pombe kuna nini Maiko?

Sijui, ninachokijua nikuwa inapoteza akili ya mtu.

Uso wa Katarina ulionesha kubabaika, akafanya haraka kumjibu mwanae…

Umefanya vizuri Maiko, ni kweli, vile vile ni haramu katika dini yetu kama ilivyokuja katika Agano Jipya, “Pombe na kilevi usinywe.”

Katarina aliona jicho la mshangao kwa Joji, hivyo akabadilisha maudhui.

Ulikutana na daktari ewe Joji?

Ndio.

Kuna mpya?

Hakuna mpya, inaelekea ni vipimo vile vile na matokeo ya hospitali ya TelAviv, nami sikujua matokeo ya vipimo vile vya TelAviv.

Ajabu, je daktari kule hawakukujulisha matokeo ya vipimo?

Kwa huduma nilizokwenda kutoa huko, kuna mmoja wa wafanyakazi wake aliyefuatilia vipimo hospitali, na hivyo basi Levi ndie aliyekuwa akijua majibu ya vipimo vile, nilijaribu kutaka kujua ukweli akakataa na hakunijulisha ili nisije kupata mshtuko.

Wivu ulijitokeza usoni mwa Katarina, na akasema; inaelekea Levi ni mzuri na mwenye kukujali sana!!

Sali: Baba ikiwa Levi huyo kama yule mwenzangu shuleni basi sio mzuri wala si mwema.

Joji: Levi alikuwa mwema sana kwangu.

Katarina: Mayahudi wanawake ni wepesi sana kijinsia (kama ilivyo katika Agano la Kale.

Maiko: Je katika Agano la Kale inahimiza matendo ya kijinsia ewe mama.

Katarina: Nilikuwa nakutania Maiko, kisha akamgeukia Joji na kusema: Au sivyo Joji?!

Ndio….mama yako anapenda sana utani….hakuna dini ya haki inayohimiza kuuwa watu au kunywa pombe au ngono zembe wala hatuamini kwa hili juu ya dini ya haki.

Katarina alifahamu ujumbe wa Joji pindi alipokuwa anaongea na Maiko, akajaribu kubadilisha maudhui kwa mara nyingine na kusema:

Nitaondoka sasa hivi Joji; niwapeleke watoto nyumbani kwani tumechelewa, kisha nitarudi upesi kwako.

Nitakusubiri mpenzi wangu…..kisha akawageukia wanawe na kusema: mnitembelee kila baada ya siku mbili kwa uchache enyi mashujaa, ninawapenda.

(4)

Joji alisalimu amri na fikra alizonazo, baada ya kuondoka kwa Katarina na watoto wake na kubakia peke yake. Alianza kujiuliza: Je nitaendelea katika maisha yangu yote kuwa katika migongano ya kifikra na falsafa na dini mbali mbali?! Kwa nini dini hizi zisikubaliane katika furaha kwa kila mwanadamu?! Kwa nini watu wasifuate dini ya hakika ambayo itawafurahisha watu wote?! Kwa nini wanadamu wote wasiishi katika amani ndani ya nafsi zao?! Na amani wao kwa wao?! Kisha akatabasamu huku akijisemesha: Huenda nimebadilika na ghafla nimekuwa Plato mwanafalsafa mkubwa. Ajabu maisha haya wakati mwingine yanatubadilisha kuwa ‘kufikirika’ ambayo haipo ila katika akili za watu! Nafikiria kama watu wote wataweza kumfikia Mungu wao bila ya tabu yoyote, huenda maisha yakawa ya uchovu, au huenda tulikuwa ni viumbe vingine na sio wanadamu kwa udhaifu wao. Tukifikia wakati huo shari haitokuwepo, bali hata kheri haitokuwepo vile vile, kwani kheri haitofahamika ila kwa kuwepo shari, bali kuwepo vyote ni dalili kuwa sisi tupo katika maisha haya. Aakh…..ni kiasi gani mwanadamu anapotea katika falsafa yake na fikra zake kama hatokuwa amefahamu maana ya maisha yake na maana ya mauti yake na wapi atakwenda?
Joji alikuwa akisubiri kurejea kwa Katarina pamoja na kuwa si muda mrefu tokea aondoke, hali kadhalika alikuwa akisubiria ziara ya rafiki yake Adam….alifungua kompyuta yake, kisha akaangalia barua pepe, akakuta barua kutoka kwa Kakhi akimshukuru kufani –kisha kazi zake na akamwambia kuwa alijua maradhi yake kutoka kwa mke wake, na kuwa leo au kesho atakuja kumtembelea, kisha baada ya hapo akaingia katika facebook ya Adam, na hakuomba urafiki ili Adam asije kutanabahi kuwa Joji anasoma kila analoandika. Ndani ya face book ya Adam alipambana na makala yake ya pili yenye anuani “masomo kutoka kwa rafiki yangu mtafuta furaha2….” Ambapo ndani yake aliandika yafuatayo:

“Rafiki yangu mtafutaji anashikilia kuijua njia ya furaha, na nimejifunza kutoka kwake yafuatayo: Mambo makubwa; kama vile kutafuta furaha, inahitaji juhudi kubwa na mitihani mingi. Kushikilia jambo kunatengeneza fursa mbali mbali, kila anapozidi rafiki yangu kushikilia huzalika mbele yake fursa ya kusoma na kujifunza mambo mapya. Ushindi mkubwa na mafanikio ayapatayo mtafutaji kuhusu furaha ni kuishinda nafsi yake, na sio kuyashinda matukio ya maisha yake. Pamoja na nguvu na kushikilia kwake rafiki yangu na azima aliyokuwa nayo, lakini ninachokihofia anachokitaka kiasi cha kutosha. Subirini mafunzo yafuatayo hivi karibuni….salamu zangu kwenu nyote Adam.”

Joji alirejea kusoma yaliyoandikwa kwa mara nyingine tena kwa utulivu na umakini zaidi, alikuwa akihisi kuwa Adam anajua yanayopita kwenye fikra zake, na akawa anajisemesha anakusudia nini aliposema mtihani mkubwa? Na pale, alikuwa na maana gani aliposema: Mwanadamu aishinde nafsi yake? Je Adam anajua kuwa rafiki yake amefeli mtihani wake na akauza misimamo yake na kutoa rushwa? Je anajua kuwa alimbusu na kumkumbatia mwanamke mzuri? Na alikuwa anataka kumfanyia hiana mke wake? Je anajua kuwa hadi sasa hajachukuwa maamuzi ya kuondoka katika shirika linaloongozwa na mtu asiyekuwa na maadili kama Kakhi, bali humsaidia wakati mwingine kutoa rushwa? Kisha nini maana ya nukta ya mwisho? Kwa nini aniogopee mimi kujua kila ninachokitaka na sijui ninachokitaka? Je haikuwa sawa kujua kila anachokitaka, ina maana bila shaka ni kujua anachokitaka? Ni kweli anataka kuwa kafiri mpinga Mungu aliyepotea, wala sio ubudha au Uhindu uliopotea akiabudu ng’ombe au maelfu ya miungu. Wala hataki awe Myahudi mgumu hivyo ni nini anataka? Inaelekea kuwa hofu ya Adam ipo sehemu yake, atajaribu kujadiliana nae leo kuhusu hilo bila ya kumjulisha kuwa amesoma kutoka kwenye web site yake chochote kile; ili aendelee kuandika kwa uhuru zaidi.
Joji alihisi kuwa chumba kinazidi kuwa baridi, alisimama apunguze, na hapo hapo akahisi uchovu, na nesi alimwona katika hali hiyo na akamjia upesi upesi.

Je unahisi baridi?

Kidogo, huenda joto limepungua.

Hali ya hewa ipo sawa haijabadilika, jinyooshe kitandani, nitawasiliana na daktari na kukuletea sindano upesi, dakika moja tu.

Nesi aliondoka upesi na akarejea akiwa na sindano ya Joji…

Hii ni sindano mpya uliyoandikiwa na daktari.

Mpya?!

Ndio, hii inachukua muda mrefu kuliko ile ya mwanzo, lakini utapoteza kumbukumbu kabisa, samahani kwa hilo, inatakiwa nikupige upesi, je unaweza kunyoosha mkono?

Nesi alimpiga Joji sindano dakika chache zilizofuata alipoteza fahamu akawa hahisi chochote.
Katarina aliporudi alimkuta Joji katika hali hii. Alikaa pembeni yake akisubiri azinduke, alikuwa akimuangalia alivyojilaza kitandani, alihisi mapenzi yake kwake Joji. Katarina anafahamu wema kwa Joji na mapenzi ya Joji kwake. Hata hivyo haachi kujadiliana nae, wala hataki kujisalimisha kwa Mungu kama wasemavyo Wakatoliki…..Alikaa akifikiri, hata hivyo yeye Katarina anapenda kufanya nae mijadala, pamoja na kuwa mwenyewe Katarina anababaika sana na kujihisi vibaya. Maswali mengi ya Joji kwake hayana majibu yaliyokuwa wazi, ni bora angejisalimisha kwa Bwana ili apumzike na maswali yote haya na mijadala hii, au huenda ikawa kujisalimisha ni aina ya kukimbia na kutoroka majibu kwa njia isiyokuwa ya Kimantiki. Ni ukweli usiopingika kuwa migongano iliyopo kwenye Ukatoliki inamsumbua wakati mwingine, lakini hata Uyahudi au Uprotestanti ni hivyo hivyo kuna migongano kama hiyo, na huenda ikawa ni mingi kuliko ya Ukatoliki! Si bora basi kujisalimisha bila ya mjadala ni raha zaidi kwake yeye kuliko aina hii ya ukimbizi? Wakati mwingine kukimbia ni bora kuliko mapambano ambayo mwisho wake ni hasara, hata hivyo kwa nini mapambano yasipelekee ushindi na kupata faida? Ooh…Nisamehe ewe masihi, sijakusudia kuwa hujatukomboa lakini… hapo
alimkumbuka Levi binti mzuri wa Kiyahudi ambae alimzungumzia…ana muamini sana Joji na anajua misimamo yake na uaminifu wake kwake. Hata hivyo kwa nini amerejea kutoka Yerusalem na mazungumzo ya jinsia na wanawake kisha akatabasamu huku akifikiri wivu wake kwake, na wivu huu uko wapi pindi alipokubali Tom ambusu, je Joji sio ndie mwenye haki zaidi katika hilo? Kwa nini ninywe pombe na mimi ninajua kuwa Agano Jipya linakataza, bali ndivyo ninavyowafundisha wanangu! Ole wangu kwa nini nimemwambia hayo alipokuwa anajadiliana nami…
Wakati Katarina anaendelea kuzama katika kufikiri, alisikia sauti ya mtu akimwambia nesi: Yuko wapi, Joji ewe binti mzuri? Muangalio wake kwa yule nesi ulikuwa ni mbaya zaidi kuliko hata maneno yake….Yule nesi alimuashiria yule mtu chumba cha Joji na alipoingia tu alikwenda kumpa mkono Katarina.

Hallo, je wewe ni mke wa Joji?

Ndio, mimi ni Katarina, karibu, wewe ni nani?

Mimi ni Kakhi, mwenzake Joji kazini, nilimpigia simu jana na kuniambia yupo hospitali, vipi hali yake?

Nzuri… inaelekea ana homa, joto lake limepanda na hivyo wamempa sindano yenye kutuliza na kushusha joto lake; amelala na kupoteza hisia ya waliomzunguka.

Huelekei kuwa ni Mwingereza!

Mimi ni Mwingereza lakini mwenye asili ya Kihindi.

Ha ha ha, uzuri wa Mashariki uko wazi, ndio maana Joji akatosheka na hili pindi alipokwenda India….

Ametosheka na nini?

Ametosheka na wanawake wazuri wa Kihindi, ha ha, ha kwa ujumla nakupongeza, inaelekea Joji anakupenda sana.

Hasira ya dhahiri ilikuwa katika uso wa Katarina

Hii ndio mara ya kwanza nakuona, huenda Joji alikuwa anaficha uzuri wako kwangu, hata hivyo nina bahati ya kufahamiana nawe, nipo tayari kukuhudumia kwa lolote na hata kama utataka kufanya kazi katika shirika letu tupo tayari.

Asante sana, mimi ni mwalimu wa dini, na nimejitoa kwa ajili ya Kanisa.

Kwetu sisi malipo ni zaidi na huenda ni bora zaidi na kuna raha zaidi.

Mimi nimejitolea kwa Kanisa nasitaki kuacha kazi yangu.

Ni juu yako kufikiri, Joji amelihudumia shirika sana na bodi ya menejimenti imefurahishwa nae na uzuri wa kazi yake, haswa baada ya hii safari yake ya mwisho TelAviv. Hebu fikiri, safari zote mbili zilizofuatana ameweza kusaini mikataba inayotakikana, na kwa uhodari wa hali ya juu na kwa maridhiano na wakala wetu.

Huenda hili limetokana na maelekezo yako; kwani wewe ndie mkuu wake wa kazi.

Huenda, sidhani hivyo, na haswa katika maudhui ya wanawake.

Katika hali hii mara mtu akagonga mlango chumbani na kuuliza:

Samahani ….je hiki ni chumba cha Joji?

Ndio, na huyu hapa mwenyewe, hanafahamu, mimi ni mke wake, karibu, nani wewe?

Mimi ni Adam rafiki yake, alizungumza na mimi leo akiwa katika afya njema. Amepatwa na nini?

Maradhi yake yanaibuka ghafla na joto lake limepanda; kinachofanya apewe sindano ya kutuliza na kuunguza joto lake, na ndio inayomfanya muda mrefu kuwa katika hali hii ya kupotewa na fahamu….

Nasikitishwa na hali yake, je kuna lolote ninaloweza kulifanya kumsaidia rafiki yangu?

Asante kwa hisia zako njema, tafadhali karibu uketi

Asante!

Adam alielekea kwa Kakhi amsalimu, Kakhi akampa mkono wa dharau Adam akamwambia kwa haya:

Samahani…sijafahamiana nawe?

Mimi ni Kakhi, mkuu wake Joji katika shirika, na wewe ipi kazi yako?

Mimi ni Adam mhudumu katika Mgahawa, na rafiki yake Joji.

Mhudumu?!

Uso wa Adam ukabadilika na kuwa mwekundu, na akaficha hasira zake, kisha akazungumza kwa upole wa mwenye hasira:

Unaweza kumuuliza atakapozindukana! Pamoja na kuamini kuwa urafiki unajengwa juu ya ukumbi wa nafsi na roho na fikra na sio ukuruba wa mali!

Katarina aliingilia mazungumzo yale upesi, na alikerwa sana na maneno ya Kakhi:

Si neno Adam, Joji alinizungumzia sana kuhusiana nawe! Kwa hakika anafurahia urafiki wenu, rai yako na hekima zako.

Huu ni katika wema wake na tabia zake nzuri, kisha akamwangalia Kakhi na akaendelea kuzungumza: Vinginevyo yeye ni mhandisi na mtaalamu mkubwa, na mimi ni mhudumu tu!!

Kakhi kwa jeuri na dharau

Kweli kabisa

Kakhi tafadhali mheshimu rafiki yake Joji.

Ha ha ha, unaniambia mimi hivyo kwa ajili ya mtu ambae kipato chake hakizidi mfagizi wangu.

Yeye ni rafiki wa Joji, kisha mali sio kila kitu, unadhani kuwa thamani ya mtu inalinganishwa na mali?

Unafanana na Joji….ama mimi hainipendezi kukaa na muhudumu, cha msingi Katarina ofa yangu ipo pale pale uje ufanye kazi pamoja nasi…hii ni kadi yangu na kuna namba yangu, na ukitaka chochote wasiliana nami, kwa heri na ugueni pole.

Nakuomba samahani Adam kwa kila kilichosemwa.

Hakuna haja ya kuomba samahani, thamani yangu ipo ndani yangu, na sio kama anavyosema yeyote kuhusiana nami, kisha wewe hukusema chochote ili uombe msamaha.

Inaelekea Joji ana haki kwa mengi aliyosema kuhusu wewe.

Asante sana, huu ni wema wako na wake.

Amenieleza sana kuhusu kushikamana kwako na dini na hekima yako na nasaha zako.

Joji ni mtafuta ukweli kabisa, na atafikia lengo lake; Mungu ni mkarimu hamuangushi mtu anayetaka kumfikia.

Maneno ya kina kuhusu imani ya Mungu, lakini usihofie akiacha dini zote kwa jinsi anavyoona migongano iliyopo!

Sidhani hivyo.

Kwa nini unajiamini hivyo?

Hakuna mgongano katika dini ya kweli na atafikia huko.

Je wewe ni Mkatoliki au Mprotestanti?

Samahani, sitojibu swali lako.

Ni swali tu.

Nitakuja kumtembelea Joji wakati mwingine, kwa sasa nitaomba ruhusa.

Atafurahi sana Joji kwa ziara yako kesho, hivyo usichelewe.

Nitajaribu kesho au kesho kutwa, nitawasiliana nae kesho ili nijue hali yake, kwa heri

Athari ya sindano iliyomlaza ilianza kupungua kidogo kidogo….Joji akaanza kuwahisi waliomzunguka, ila alikuwa anahisi mzito sana, na alikuwa anaanza kufungua macho yake. Alipokuwa katika hali hiyo alikuwa amekwisha sikia yaliyokuwa yakipita baina ya Katarina na Kakhi na Adam, baadhi ya mazungumzo yalikuwa wazi kwake na mengine yalikuwa yamechanganyika hakuyafahamu vizuri. Baada ya kuondoka Adam alijihimu kufungua macho yake na alikuwa ameanza kujisikia vizuri, hata hivyo aliamua kuyafunga macho tena baada ya kusikia sauti ya mtu aliyekuwa akija chumbani. Alipotoa salamu Joji alimfahamu kutokana na sauti yake, alikuwa ni daktari Tom.

Vipi hali ya mwanafalsafa wetu?

Hallo Tom, Kwa bahati mbaya amejiwa na homa ya ghafla; wamempa sindano ya kutuliza, hajazindukana bado.

Namtakia siha njema, Joji ni mfano wa nadra, pamoja na kuwa nagombana nae sana, ila ni kuwa mimi nafaidika nae sana kuliko anavyofaidika nami.

Wewe ni mwema, amepata nafuu sana tokea alipoanza kuja kwako.

Bali mimi ndie ambae nimekuwa mzuri sasa, huenda wewe na Joji hamnifahamu vizuri, mimi nilikutwa ni daktari mchezaji, hamu yangu kubwa ni wanawake na starehe. Na wala sijui kwa nini falsafa za Joji na kusoma kwangu kuhusu dini mbali mbali kwa muda huu, kadhalika ziara yangu kanisani pamoja nawe imebadilisha sana maisha yangu? Naomba sana samahani kwa busu nililokupiga, niamini sikuwa na kusudia wala sikuwa najua ninalofanya?

Maudhui yenyewe yamekwisha kabisa, huenda kosa kubwa likawa kwangu; nilikuwa nimekunywa sana siku ile.

Kwa hali yoyote ile sisi tunapenda tufanyie falsafa maneno yetu, makosa yetu yakuwa sio hatujui au ya kuwa sisi tumelazimishwa au sio hiyari yetu, achana na hayo, hebu niambie, daktari anasemaje kuhusu hali ya Joji?

Mambo hayako wazi kabisa, lakini natamani yawe wazi kwa timu ya madaktari baada ya siku mbili zijazo.

Atakuwa katika hali nzuri, na Mungu atamlinda.

Joji alijifanya kama ni mzito wa kufungua macho yake, kana kwamba ndio kwanza anaamka….akiwa anauliza kinachoendelea….

Joji mpenzi wangu umeamka.

Tokea muda gani niko hivi?

Tokea muda wa masaa matatu, na nesi ameniambia kuwa umepiga sindano kabla ya kuja kwangu kwa muda mfupi, tunamshukuru Mungu kwa hali yako..kisha akamgeukia Tom na kusema: daktari wako amekuja kukujulia hali.

Hali yako Joji?

Nzuri, vipi hali daktari wangu?

Hali nzuri nilimuuliza Katarina kuhusu siha yako, na akanipa tumaini, sitaki kukuchosha, nitakuja wakati mwingine kukutembelea.

Nipo hospitalini, lini kikao chetu kijacho?

Muda utakaotaka, na itakuwa hapa chumbani.

Vizuri, hivyo itakuwa hivi karibuni.

Kama utakuwa na muda hospitalini basi tumia muda huo kujisomea kuhusiana na dini mbali mbali za mbinguni, ili kikao chetu kiwe na manufaa zaidi.

Vizuri, tumekubaliana.

Katarina alitabasamu akiwa ameshika moja ya vitabu vilivyokuwepo pembeni ya Joji, kisha akasema:

Alishaanza hilo tokea jana.

Vizuri sana Joji.

Nitajaribu muda mrefu niwe hapa kwenye mjadala –kisha alimgeukia Katarina na kutabasamu na kusema: Katarina hapendi mjadala na anakasirika upesi.

Katarina alibadilika na kuwa mwekundu.

Ninawaahidi ya kuwa sitofunga mjadala huu.

Ha ha ha, vizuri, nitakuja kukutembelea zaidi ya mara moja, nikipata wasaa; ili nijadiliane nawe, nakutakia ponyo la haraka, na mimi naomba ruhusa.

Alipoondoka Tom, Katarina alimgeukia Tom huku akitabasamu.

Samahani mpenzi kukata mjadala wenu, lakini nisaidie nisifanye hivyo.

Nilikuwa natania.

Hata hivyo unayo haki katika hilo… nilitaka kukuuliza; huyu mwendawazimu anayejiita Kakhi, mkuu wako wa kazi ni nani?

Kafanya nini Kakhi?

Alifika hapa leo, alifanya mambo ya kipumbavu na ukosefu wa adabu, na kama sio kujizuia kwa ajili yako ningemfukuza.

Kunijali! ungemfukuza tu hata hivyo kafanya nini?

Macho yake, jinsi anavyoangalia watu ni upumbavu mtupu, muamala wake na watu ni wa hovyo, fikiria alikuwa anamdharau Adam, eti kwa sababu ni mhudumu tu, na yeye Kakhi ni mkuu wa shirika! Na anazungumza na nasi vibaya!

Je Adam alifika?

Ndio, lakini Kakhi hakumtendea vizuri hata kidogo, hata hivyo Adam alikuwa ni mwenye adabu.

Adam ni mtu tofauti kabisa na alivyo Kakhi.

Pamoja na kuwa umri wake sio mkubwa na kazi anayofanya ni ya kawaida tu, huzungumza kwa hekima ya watu wazima na wanafalsafa.

Kama ni hivyo nilisema kweli nilipokuambia kuhusu Adam?

Umesema kweli katika kila ulichoniambia na hata kile ambacho hukuniambia, mimi nakupenda Joji, Kakhi ameniambia kuwa wewe upo kinyume nae kabisa kuhusu wanawake, nami najua ujinga wake na heshima yako.

Na Omela mwenye kufitini wanaume na Levi mzuri?

Mimi nakuamini sana mpenzi wangu, niamini mimi ni mwenye imani na tabia zako, je wewe unaniamini?

Ndio.

Pamoja na mkesha wangu na Tom?

Tom alinijulisha kilichotokea baina yenu katika mkesha wa mwisho.

Niamini sikujua ilitokea vipi?

Aah, makosa yetu mengi hutokea na hatujui yametokea vipi? Mimi nakuamini kwa dini yako na tabia yako mpenzi wangu.

Mimi nakupenda Joji.

Katarina aliangalia saa yake na kusema:

Inapasa niondoke sasa hivi, nitakuja kesho.

Nitakusubiri kesho, umeniahidi mjadala, na itakuwa nitakachojadiliana nawe ni yale yaliyokuja kwenye Injili: “Pombe na kilevi usinywe.”

Tumekubaliana mpenzi nitakuwa muwazi kwako kuhusu hilo.

Tumekubaliana.

(5)

Katarina aliondokaJoji alifumba macho yake; akijaribu kukumbuka alichokisikia mwanzoni pindi alipotaka kuamka, maneno ya Tom yalikuwa wazi zaidi kuliko ya mwingine yeyote yule, na alichokisema kuhusu kubadilika kwake na kufaidika na Joji. Habari hizi zilimstua, na akahisi ukweli wake.
Kadhalika alikumbuka kidogo katika maneno ya Kakhi na dharau yake kwa Adam, na akakumbuka utulivu wa Adam na muamala wake. Kisha akatabasamu kwa ndani aliposikia Kakhi na bodi ya shirika likimsifu kwa kufanikisha mikataba kisha akajiuliza: Je anao ujasiri wa kutosha ili ajiuzulu kazi yake baada ya kutoka hospitalini, ili aachane na kuwa chombo kisichokuwa na maadili kinachotumiwa na Kakh, au mapenzi ya mali kwake na cheo kitaghilibu misimamo yake?
Katika hali hiyo ya kuogelea kwenye fikra, alisikia sauti ya nesi akizungumza nae:

Hallo, vipi homa yako ikoje sasa?

Hali yangu kwa sasa ni njema.

Tulitaraji utazindukana kabla ya muda wako.

Kweli … nimezinduka muda kidogo uliopita, hata hivyo nilijihisi kuchoka; nikaendelea kufumba macho.

Hamna neno, joto lako kwa sasa ni zuri, haya naomba ruhusa kutoka.

Asante, na nakuomba samahani kwa mgeni wangu kukukosea adabu, mke wangu ameniambia kilichotokea.

Sikuwa mimi, ni mwenzangu, hata hivyo tumezoea hali hii na kuwepo na watu mfano wake, usijali hilo, na kushukuru kwa muamala wako mzuri….Jina langu ni Zinta, kama utanihitajia unaweza kuniita muda wowote nikuhudumie.

Zinta jina lako ni geni kidogo!

Asili yetu Austria na sio Uingereza.

Namjua Mwaustria mwema kama wewe.

Inashangaza, Waustria ni wachache Uingereza.

Levi sio wa Uingereza, bali nimejuana nae Tel Aviv.

Yahudi! Mayahudi wameharibu Ulaya, tumewatoa na kuwakabidhi Palestina na Yerusalem.

Inaelekea una kasumba dhidi ya Mayahudi!

Huenda ikawa hivyo, lakini wewe hukuishi sana na Mayahudi. Kwa ujumla ukinihitaji niite wakati wowote, chakula chako cha jioni kitaletwa sasa hivi; hukula chakula cha mchana na inabidi upumzike.

Asante kwa wema wako.

Asante bwana Joji.

Asubuhi ya siku iliyofuata Joji aliamka mapema akiwa mchangamfu jambo alilokuwa akilikosa siku za hivi karibuni, kiasi cha kutamani ikiwezekana aondoke hospitalini, kwani alikwisha choshwa na kukaa pale. staftahi yake ilikuja mapema, alikula kisha akaamua kujishughulisha na kusoma kwa bidii akitaraji kuja kwa daktari, ambapo atalinganisha baina ya Uyahudi na Ukristo na atasoma hali ya mwanamke katika Ukristo huku akilinganisha hilo katika Uyahudi. Yote haya anaweza kujadiliana na Katarina na kuandikiana kuhusu maudhui haya na Habib pamoja na Levi.
Daktari aliingia na kutoa salamu, kisha Joji akaanza kumuuliza:

Je kuna mpya kuhusu vipimo?

Hapana, baadhi yametoka na mengine tunasubiria, hata hivyo usijali na kuhofia.

Sihofii kamwe, ni swali tu nauliza, na vipi hivyo vilivyotoka?

Tunasubiria hivyo vingine kabla hatujahukumu, sitaki kukusumbua, lakini huenda ukahitajia operesheni.

Operesheni?.

Nimekuambia usihofie, ponyo itabakia katika mikono ya Mungu na sio mikononi mwetu bali sisi ni sababu tu.

Niamini sihofu kabisa, lakini nashangazwa na hali yangu kufikia kiwango hiki!

Najua hilo, nesi ameniambia kuwa muda wote unashughulika na kusoma na kufanya mjadala, na hakuwahi kukuona ukiwa na huzuni, hili ni zuri sana… sisi tunasubiria matokeo kesho au kesho kutwa.

Tusubiri matokeo, na mimi ninaamini yatakuwa ni ya kheri tu.

Vizuri, je unaweza kunielezea kwanini una imani kubwa sana hivyo?

Bila ya shaka Mungu anatuhurumia zaidi kuliko tunavyojihurumia.

Kama ni hivyo, basi wewe ni mtu wa dini, watu wenye dini kwa ujumla ni wenye uwezo wa kupata raha zaidi na furaha; na wenye kututaabisha ni wenye maradhi ya kukana Mungu ambao wanadhani kuwa dunia ndio kila kitu kwenye maisha yao.

Samahani, sikukusudia ninachokisema, nilichokusudia ni kuwa Mungu anatuhurumia sana duniani, pamoja ya kuwa nilichokisema kina maana ya kina zaidi, nayo ni kwamba waamini wana maisha mengine akhera, lakini hili ni maalumu kwa wafuasi wa dini za mbinguni tu.

Inaelekea wewe ni mwanafalsafa, nami nina kazi…lakini niambiwe kwa ufupi: Kwa nini hilo haliwezi mwenye kufuata dini ya Ubudha au Uhindu?

Kwa sababu hawaamini kama kuna maisha yajayo bali wanaamini kuwa roho zao zinahamia kwa wengine.

Ha haha hizi ni itikadi za watu wa kale, pamoja na utamu wa mazungumzo lakini nalazimika kuondoka, kila la kheri.

Joji alizama kusoma na kufanya uchambuzi, hakukatishwa na chochote isipokuwa simu kutoka kwa Adam akitaka kujua hali yake.

Hallo vipi Adam, Katarina alinijulisha kuhusu ziara yako, asante sana.

Je kuna chochote naweza kukusaidia ewe rafiki yangu?

Neno zuri ‘rafiki yangu’, nimefurahishwa sana nawe ningekuwa nahitaji kitu ningekwambia …. Samahani nimekumbuka kitu nakitaka kutoka kwako.

Karibu, kwani wewe unanifurahisha na kunihisi kuwa sisi ni marafiki.

Ombi langu ni kuwa tuonane, nina mijadala mingi nataka kutoa kwako.

Nitakuja kesho, sio leo, samahani kwa hilo, leo tuna kazi kubwa mgahawani; kuna mfanyakazi mmoja hayupo.

Vizuri…hamna neno, tutaonana kesho.

Katarina alifika pindi Joji alipomaliza mazungumzo, aliingia chumbani akiwa na tabasamu kubwa.

Mpenzi wangu ameamkaje leo?

Nzuri, katika hali njema, vipi hali yako?

Namshukuru Bwana Mungu kwa neema zake.

Ni neema gani ya Bwana uliyopata?

Neema ya kuwa muamini mwenye dini na nikishughulishwa Kanisani… na …. na neema ya kuwa wewe ni mume wangu.

Hivyo basi kuwa na dini kwa muono wako ni neema?!

Je kuna shaka kuhusu hilo? sio mbaya kuliko mtu kutokuwa na bwana ambaye utatulizana kwake.

Vipi kuhusu mkanaji Mungu kwa muono wako?

Ukweli na bila kuficha…rai yangu ni kuwa ukanaji Mungu ni maradhi kabla ya kuwa ni dini ya mtu. Ni maradhi ya nafsi na roho, ni maradhi ya akili na mantiki, na ni maradhi ya ulimwengu na viumbe vyake.

Nakubaliana nawe kabisa, lakini kuna neema gani kama mumeo ni mgonjwa?

Nakusudia wewe mume wangu, na sikusema neema ya kuwa wewe ni mgonjwa.

Kuna neema gani katika hilo?

Kuna wanaume ambao hawawathamini wanawake wala kuwapa hadhi zao bali wanawadharau, sio wanaume waaminifu kama ulivyo mume wangu.

Je haikuwa kumdharau mwanamke inakwenda sambamba na dini ya mtu?!

Kwa vipi?

Kila muda ambao dini inaongezeka ndipo dharau kwa mwanamke inapoongezeka.

Kwa mara nyingine, ni nani aliyekuambia hivyo?

Ni mafundisho ya Kiyahudi yanamuelezea mwanamke kwa sifa chafu mbali mbali.

Wewe unasema kuhusu Uyahudi; kwa nini basi unaeneza maneno hayo kwa Ukristo pia?

Je si kwamba Paulo amesema katika waraka wake wa kwanza kwenda kwa Wakorintho: “Na wanawake wanyamaze katika makanisa, hawaruhusiwi kuzungumza, bali wawe wanyenyekevu.”

Leo unaelekea kuwa ni mwanazuoni mkubwa wa itikadi za dini na mambo ya kimungu.

Kwani sijakwambia kuwa nitatumia muda huu kusoma tu kuhusu Ukristo muda wote nilipo hapa hospitalini, hata Tom alilisema hili nawe ukiwepo.

Vizuri… hili litakuzidishia uamini wako….na linaweza likakubadilisha kutoka Uprotestanti kwenda Ukatoliki…

Huenda ikawa hivyo, hata hivyo turejee kwenye maudhui yetu, je si ukweli kuwa hali ya mwanamke kwenye Ukristo ni mbaya kama ilivyo kwenye Uyahudi?

Nimekuahidi kuwa mkweli, na nitaendelea kwenye mijadala, nitaendelea pamoja na kuchukizwa nayo.

Sipendi uendelee kwa unachokichukia, naamini kwamba mimi nitakusamehe na mjadala.

Hapana, nitaendelea, na mimi naona kuwa kama unavyohitajia kujisalimisha kwa bwana, na mimi nahitaji kutumia akili na kufikiri.

Nakubaliana nawe, hakuna imani bila kujisalimisha kwa bwana, lakini bwana muadilifu hawezi kutukalifisha kwa mambo yenye kugongana au kwa yale ambayo hayaingii kwenye akili zetu.

Vipi?

Je dini inaweza kuja na kitu ambacho hakiingii akilini?

Mfano wa nini?

Mfano wa kuwa bwana ni dhaifu, au yakuwa anawahitajia waja wake, au huuliwa na waja wake, atakuaje huyu Mungu?!,

Pamoja na hatari ya maelezo yako lakini ni hoja tulivu.

Unakusudia nini?

Hii sio maudhui yetu, maudhui yetu ni mwanamke katika Ukristo au sivyo?

Haswa….ndio.

Ukweli ni kiasi gani nimetamani kama ningekuwa mwanamume, mwanamke katika Ukristo nafasi yake ni duni kuliko mwanamme.

Ooh, mfano wa Uyahudi?

Huenda ikawa hivyo, kwa uchache. Torati na Talmudi zimeharibiwa kuna mafundisho yenye upogo ndani yake na yamejaa mawazo ya kijinsia yasiyovumilika…. Ama Injili mwanamke ni duni kuliko mwanamme, na kuna mambo mabaya kuhusu mwanamke lakini hayafikii yale yaliyopo kwenye Uyahudi.

Nimeona ombwe katika maandiko hayo katika Agano la Kale.

Mfano wa nini?

Mwanamke anarithiwa kama kilivyo chombo.

“Watakapokaa ndugu pamoja na mmoja wao akafa, na hakuwa na mtoto, mke wa aliyekufa hafai kwa mtu wa nje, bali ni kwa ndugu wa mumewe na ana haki ya kumuingilia, na kumfanya mke wake. Atafanya yote yanayomwajibikia ndugu wa mume.” Na mwanamke harithi “Wamezungumza (wana wa Israel) wakisema: Mtu atakayekufa akiwa hana mtoto wa kiume basi miliki yake ihamishiwe kwa binti yake.” Na kuhusu mwanamke mwenye hedhi: “Kila mmoja wao ni najisi, afue nguo zake na akoge maji, na ataendelea kuwa najisi hadi jioni.” Inatosha au niendelee?

Tosha tosha… ukweli ni kuwa Ukristu umemkomboa mwanamke katika mengi ambayo yalikuwa katika Uyahudi pamoja na kuwa hedhi yake kwetu ni mbaya vile vile, lakini sisi ni bora kuliko kwenye Uyahudi.

Kwa vipi?

Imempa mwanamke haki zake; kwa mfano Uyahudi, katika zama za Masihi walikuwa wakitoa talaka kwa sababu za kipuuzi, hata kama mwanamke ataharibu chakula. Masiya alipokuja akanadi kuwa talaka haitolewi ila kwa tatizo la zinaa, na hivyo kumkomboa na utawala wa mwanamme ambae atamtaliki kwa sababu yoyote ile na wakati wowote ule, na hivyo kumsalimisha na kuchezewa.

Vizuri… Je unaweza kukamilisha kwa mfano mwingine.

Kwa hakika kitabu kitukufu kimejaa maandiko kama niliyotaja; ila vile vile kimejaa maandiko mengine yanayotoa dalili ya kumtukuza mwanamke.

Ni maandiko gani hayo yaliyokuja kutoka kwa Mungu? Kwani haiwezekani maandiko yakapingana na hapo hapo yakawa ni sahihi?

Umeyaingilia maudhui makubwa, nami nimechoshwa na mjadala mrefu, niamini sikimbii mjadala.

Ni maudhui gani hayo magumu tuyazungumze wakati mwingine?

Ni maandiko gani ni ya Mungu na yapi ya watu?

Tufunge mjadala kwa sasa, tutajadiliana wakati mwingine.

Je utanielezea kuhusu kanisa la Kiyama sasa?

Kama utakavyo, nimekwenda kanisani kama nilivyokuahidi, nilikwenda siku ya Ijumaa, na kulikuwa na msongamano mkubwa njiani.

Alikatishwa na Baraad aliyekuja kumtembelea Joji.

Hallo Joji … hallo Katarina.

Karibu!

Nimejua kuhusu ugonjwa wako, na nimekuja kukutembelea, huenda ukanihitajia:

Asante.

Baraad alimgeukia Katarina akiwa na tabasamu bandia na kusema:

Ooh Katarina yupo hapa, nilidhani upo na Tom.

Unakusudia nini?

Hamna kitu, usikasirike bibie.

Joji alikaa vizuri, na kusema:

Sidhani kama hii ni kazi yako.

Huenda ikawa, lakini mara nyingi Tom ana mzungumzia Katarina na uzuri wake, na hivyo nilitarajia atakuwa nae.

Joji katika hali ya ghadhabu.

Wewe ni muongo, na huna adabu.

Tom aliniambia vile vile kuwa wewe unataka kwenda Tora bora, je ananiongopea na hili vile vile?

Macho yalimtoka Katarina kwa mshangao: Tora bora!?!

Usinifanye nikatoka kwenye tabia yangu ya kawaida, asante kwa ziara yako Baraad, naomba uondoke upesi, nataka kupumzika.

Nitaondoka lakini ole wenu Tom asiwachezee kwa maneno yake matamu, yeye ni mtaalamu wa kuwachezea watu kwa maneno yake. Mnaweza kuwauliza wanawake aliokwisha wachezea. Ama wewe Joji kama nilivyokujulisha nina dawa ya matatizo yako, nasubiri simu yako, kwa heri.

Alipoondoka tu Baraad… Katarina alijiangusha kwenye kiti, huku akiwa amevimba kwa hasira.

Nimemchukia sana mtu huyu.

Nami namchukia vile vile, asie na maadili wala utu.

Lakini alikuwa anakusudia nini?

Katika jambo gani?

Je ni kweli unataka kwenda Tora bora?

Ha ha ha, je unajua Tora bora?

Ndio, milima ya magaidi huko Pakistan na Afghanistan, cha msingi kuna nini?

Kuna jambo si la kawaida limetokea, Tom alikuwa akinijulisha kuhusu dini mbali mbali na kuhusu Uislamu, kisha akaniambia huku akinitania: Ukisilimu utakwenda Tora bora, na cha kushtusha pindi tu nilipotoka ofisini kwake nilikutana na Baraad naye akaniambia: Je utakwenda Tora bora!?

Yeye na Tom ni waongo wanayoyasema kuhusu mimi usiwaamini.

Najua uongo wa Baraad, ama Tom amenijulisha kuhusu busu, na kuniambia kuwa hajakusudia lolote, na sijui kwa nini nimemuamini?

Kwa bahati mbaya maneno ya Tom ni sahihi, hili limetokea na wa kulaumiwa ni mimi, kama nisingekuwa nimelewa asingethubutu kufanya alichofanya.

Huenda sikufahamu alichofanya Tom, kwani jambo lilitokea bila utambuzi wake, lakini nashangazwa na kudumu kwako kunywa pombe!

Ukweli: ni…….

Kisha nashangazwa na maneno uliyomwambia mtoto wetu Maiko kuhusu pombe: “Pombe na kilevi usinywe.”

Mtu anaweza kucheza na mantiki ya makosa yake anayoyafanya, lakini nitakuwa mkweli nawe na nafasi yangu.

Samahani kukukatisha, unakusudia nini kucheza na falsafa ya mantiki ya makosa:

Mafundisho mengi ya dini tusiyoyafahamu, na mengi katika mafundisho hayo ambayo tunayafahamu, tunakwenda kinyume nayo. Tatizo ni kuwa sisi hatukubali makosa yetu, na hivyo basi kuibua tafsiri ya kimantiki au ya kifalsafa au hata ya kidini ili tusionekane kama tunakosea. Mfano mzuri wa hilo ni Pombe katika Ukristo.

Je unaweza kunibainishia vizuri?

Kimsingi pombe imeharamishwa katika Agano la Kale na Agano Jipya. Katika Agano la Kale: “Hafai kwa mamluki kunywa pombe wala wakubwa kulewa; wasije wakanywa na kusahau majukumu yao na kubadilisha hoja ya kila mwana madhila.” Katika Agano Jipya: “Msinywe pombe ambayo, ni kivutio cha uovu bali jazeni kwa roho.”

Vizuri, hiyo basi ni haramu, kwa msingi huu uharamu wenyewe wa wote au vipi?

Usinikebehi, nitakuwa mkweli kwako, maandiko yamekuja kuwa manabii wamekunywa vile vile pombe, sisi kanisani tunakunywa na tunaifanyia falsafa ya kuwa masiya Yesu alisema kuhusu nafsi yake katika Injili akimfundisha Yohana: “Mimi ni mzabibu wa kweli.” Na akasema kuhusu wafuasi wake: “Nyinyi ni matawi.” Kama ilivyo juisi ya mzabibu kwenda kwenye matawi yake ili kuzilisha. Hivi ndivyo Bwana wetu Masiya alivyochukulia juisi ya mzabibu akaashiria damu yake tukufu ambayo tunainywa, na hivyo basi ikaingia kwenye mishipa yetu ili kuitukuza damu yetu na kiini cha miili yetu kwa ndani. Bwana Masiya hakutupa juisi ya mazabibu tupate utamu wake tu na kulewa; bali ametupatia kwa lengo tukufu lenye kutoharisha, haijui isipokuwa waamini tu.

Ooh, falsafa iliyobuniwa.

Usinikebehi, vinginevyo sitokamilisha.

Ha ha ha, vizuri vizuri, kwa hivyo basi unywaji pombe umetukuzwa!

Unaona jinsi tunavyotumia falsafa na mantiki na hatutaki iwe ni dini kwetu?

Hili linakubalika katika dini zilizotungwa na wanadamu, wanaandika wanavyotaka, lakini halikubaliki kwa dini kutoka mbinguni, dini kutoka kwa Bwana Mungu.

Aah, usipate shida na mjadala, mimi nalazimika kwenda nyumbani ili kuwapokea Maiko na Sali, na nitajaribu kurudi baadae…wakati huo tutamalizia mjadala wetu, lakini nihurumie kidogo kwenye mjadala, kwani ndani ya nafsi yangu naungulika na hivyo kunichosha, haswa zaidi kama kuna migongano ya ndani ya nafsi zetu kabla ya kuwa kwenye dini zetu.

Nitakusubiri mpenzi wangu, na nakuomba msamaha kama nimekukera, hata hivyo sipendi ujikalifishe, na kama hutoweza kuja leo hamna neno….

Katarina alimbusu Joji kwenye paji lake la uso na kwenye mashavu yake, kisha akaondoka… alikuwa mwenye furaha sana na mazungumzo yaliyokwisha fanyika. Kwa mara ya kwanza aliamini kuwa ameweza kujieleza na hivyo basi akili yake kuishinda nafsi yake. Kadhalika Joji alikuwa katika furaha kuu, kwani aliweza kugundua uwezo wa juu usio wa kawaida wa Katarina wa kifalsafa na kimantiki na wa kielimu, uwezo ambao umejificha katika kujisalimisha tu kwa imani yake Joji alijilaza akirejea mjadala ule kwenye nafsi yake. Ulikuwa mjadala wa kina, kisha akatabasamu alipokumbuka pindi pale Katarina alipoweza kumalizana na lile swali: Kwa nini tunakunywa pombe kwa njia ya ubunifu kabisa, na hakufedheheka kwa tendo lake.