Profesa Haroon Mustapha Lion

quotes:
  • Akili na Mantiki
  • “Katika vivutio vya Uislamu ni kuwa kwake dini inayosimama kwa kutumia akili. Haumtaki kamwe mfuasi wake kufuta kipaji hiki alichopewa na Mungu. Kama ambavyo Uislamu unapenda utafiti na kuulizia mambo. Kadhalika inalingania wafuasi wake katika kusoma na kufanya utafiti, uchunguzi na kuangalia kabla ya imani. Uislamu unaunga mkono hekima isemayo: Thibitisha ukweli wa kila jambo kisha shikamana na kheri. Hili si jambo geni: Kwani hekima ni jambo lililompotea muumini popote alipatapo basi ni mwenye haki nayo zaidi. Uislamu ni dini ya matumizi ya akili na mantiki: Hivyo basi tunakuta kuwa neno la kwanza lililoshuka kwa Nabii Muhammad ni: “Soma”, kama ambavyo tunaiona kauli mbiu ya Uislamu ni kulingania katika kuangalia na kutafakari kabla ya kuamini: Kwani Uislamu ni haki na silaha yake ni elimu, na adui yake mkubwa ni ujinga.”