- Sheria ya kweli
“Sheria ya Kiislamu haitofautishi baina ya dini na baina ya ambacho ni dunia. Sheria hiyo inaonesha mahusiano ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu na wajibu wake kwa Mungu na kuyapanga kama inavyofanya kwa hali ya mahusiano ya mtu kwa ndugu yake mwanadamu. Na amri zote za Allah na makatazo yake –katika yanayofungamana na mambo ya dini na dunia na mengine kwenye Qur-aan na ndani yake pana ayah elfu sita au ziada ya hapo, miongoni mwa hizo ayah elfu ni kuhusu sheria.”