Maumbile sahihi na akili zilizotua zinakiri kuwa Ulimwengu huu una Mola, na Viumbe hivi vina Muumba; na vimethibitisha kuwepo kwa Uungu wake na ya kuwa Yeye ni Mmoja katika Uungu na Uola wake, hana mshirika katika Uungu wake, na dalili zake ni nyingi na zipo wazi, miongoni mwazo ni:
haiwezekani kuwepo na Miungu wawili katika Ulimwengu huu?!!
Lau kwamba kungekuwepo na miungu wawili (kwa ajili ya mjadala tu) swali litabakia: Vipi kama watapingana na kila mmoja kuekeleza matakwa yake?!! Mmoja akataka jambo na mwingine atake kinyume chake?!
haiwezekani ila mmoja kuwa juu ya mwingine, na hahesabiwi mwingine kuwa ni mnyonge au dhaifu, Je, mnyonge anaweza kuwa ni Mungu?!! Na kubakia Mungu kuwa ni mmoja tu, Allah Mtukuka amesema: “Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo.”(23:91-92).
Cha kushangaza ni mtu kumuabudu asiye na uwezo wala nguvu, hana umiliki wa mbingu na ardhi, hawezi kuumba chochote, hamiliki chochote katika nafasi yake mbali ya kuwamilikisha wengine –madhara au manufaa, mauti wala uhai wala ufufuo Allah Ta’ala amesema: “Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote. Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo. Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka.” (25:1-3).
Vinginevyo kama jambo ndilo kama wasemavyo washirikiana kuwa pamoja na Allah kuna miungu ambao huabudiwa ili kumkurubisha kwake aombewe basi hao waabudiwa wanamuabudu na wanajikurubisha kwake na kutafuta kwao wasila na ukuruba, Allah Ta’ala amesema: “Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi. Subhanahu Wa Taa’la, Ametakasika na Ametukuka juu kabisa na hayo wanayo yasema. ” (17:42-43),
Bali Yeye ni Allah mmoja Mkusudiwa, ambaye hakuzaa wala kuzaliwa wala hafanani na chochote.
Hawa wenye kuabudiwa hawamiliki chochote wala hawawezi; Allah amesema: “Sema: Waite mnao wadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata uzito wa chembe hichi katika mbingu wala ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao. Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipo kuwa kwa aliye mpa idhini.” (34:22-23)
Yaani, Waambie washirikina wanaomshirikisha Allah na viumbe vingine ambao hawanufaishi wala hawadhuru, ambao hawana uwezo na, pamoja na udhaifu uliopo lakini bado wanashikamana nao, wabainishie ubatili wa ibada zao; Waombeni hao wanaodai kumshirikisha Allah, kama kweli maombi yenu yanawafaeni, kwani hakika kuna sababu za udhaifu na kushikamana kwao, na kutoweza kujibu dua kutoka popote, kama ni hivyo hawamiliki chochote; hawamiliki hata udogo wa mdudu chungu mbinguni wala ardhini kwa kujitenga au kwa kushirikiana katika hilo. Na Miungu ile ambao mnadai wapo mbinguni na ardhini ambayo mnamshirikisha kwayo Allah haina uwezo wa kumiliki chochote kile, si kidogo wala kingi. Miungu ile ya kishirikina haina ufalme wala ushiriki, labda isemwe: Huenda wakawa ni wasaidizi wa mfalme, na mawaziri wake, hivyo basi maombi yao huenda yakawa na manufaa; (kwa sababu Mfalme ana haja nao) basi atawatekelezea haja zao kwa wale waliokuwa nao karibu; na hilo Allah Ta’ala amelikana daraja hili kwa kusema: “ana nini”; yaani Allah ni mmoja Mtenza nguvu “miongoni mwao.” Yaani: kwa waabudiwa “msaidizi” yaani msaada na waziri ambao humsaidia katika ufalme wake na mipango yake.
Mwenye kuuangalia Ulimwengu huu na mwenendo wake ataona mpango uliopangika kwa utaratibu wa hali ya juu; na hii ni dalili ya kuwa kuna mwenye kuiendesha naye ni Mungu mmoja Mzuri Mwenye uwezo, amesema Ta’ala: “Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia. ” (2:163-164).
Je, utaratibu huu haukuwa ukienda mwaka mzima wala haiharibiki wala kusimama sekunde moja jambo ambalo lingeharibu ulimwengu huu tulionao, yote hayo makadirio yake yako kwa Allah, Je, utaratibu haukuwa kutoka kwa Muumba mpangaji wa mambo mmoja, asiye na mshirika?! Je, hii si dalili ya wazi ya kutowezekana uwepo Uungu zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye akili?! Allah Ta’ala amesema: “Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana ‘Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A’rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.” (21:22).
Yaani lau katika mbingu na ardhi kungekuwa na miungu wawili basi yangeharibika na kuharibika yaliyomo kwa viumbe, kwa hakika ulimwengu huu (kama inavyoonekana) katika ukamilifu utakavyokuwa katika islahi na kufuata utaratibu ambao hauna kasoro wala aibu yoyote, wala katazo, wala upinzani na hii inathibitisha kuwa mpangaji wake ni mmoja, na Mola ni mmoja na Mungu ni mmoja lau kama kungekuwa na wapangaji wawili na Mola wawili au zaidi ya hao; basi utaratibu wake ungeharibika, na nguzo zake zingebomoka basi bila ya shaka zingezuiana na kupingana, na kama mmoja wao angetaka kupanga kitu na mwingine hataki hilo, basi ingeshindikana wote kufanikiwa katika matakwa yao, na kufanikiwa kwa matakwa ya mmoja bila ya mwingine ni uthibitisho wa udhaifu wa mwingine, na kutokuwa na uwezo, na kukubaliana kwao na kuafikiana kwao katika jambo moja katika mambo yote ni jambo lisilowezekana; hivyo basi yapasa kwa mmoja mwenye nguvu na uwezo apate muradi wake peke yake bila ya kuzuiwa wala kupingwa na huyu ndie Allah Mmoja Pekee Mwenye nguvu na uwezo.
Manabii wa wateule wote tokea zama za Adam (‘Alayhi Salaam), hadi Nuuh, Ibrahim, Musa, Issa na Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) nao ni watu walioepushwa na madhambi ya nafsi zao na wenye akili angavu na kauli ya ukweli na amana ya kufikishana uongofu juu ya kumpwekesha Allah Ta’ala na kuwa Yeye ndiye Hapana Mungu ila Allah, Allah amesema: “Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu. ” (21:25)
Na akasema vile vile kumsifu Nuhu (‘Alayhi Salaam) “Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu.” (7:59)
Na akasema kuhusu Issa (‘Alayhi Salaam) “Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.” (5:72)
Na akamuamrisha Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) awaambie watu wake: “Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu? ” (21:108)
Hivyo basi ni jambo la msingi kwa wenye akili nzuri kufuata Mtume wao, na kumpwekesha Allah Ta’ala na kumuamini Yeye Mola wao mlezi na Mungu wao, ili wapate furaha ya duniani na ya Akhera, Allah Ta’ala amesema: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (16:97).
Kwa hakika matendo mema pamoja na imani malipo yake ni maisha mazuri katika ardhi hii, sio lazima yawe ni yenye neema sana au utajiri wa mali, bali inaweza kuwa hivyo au isiwe hivyo, na maisha yanaweza kuwa mazuri lakini mtu bila ya kuwa na mali au utajiri; Katika maisha kuna mambo mengi ambayo sio mali wala utajiri, bali baadhi ya mambo ambayo mtu katika maisha yake anayafurahia, ni kama:-
i-Mawasiliano ya mtu na Mola wake, kumuamini na kuwa na utulivu na ulezi wake na stara yake, na kuridhiwa naye.
ii-Kuna suala la afya ya mtu na utulivu wake, kuridhika na kupata baraka, kuishi katika nyumba na mapenzi katika mioyo.
iii-Kuna suala la mtu kufurahi kwa kufanya kwake matendo mema na athari yake katika dhamira yake, na katika maisha yake, Na hayakuwa mali katika maisha ya mwanadamu isipokuwa ni kipengele kimoja tu katika pambo katika maisha yake: “Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini. ” (18:46).
Itakapokuwa moyo wa mwanadamu unaungana na kitu kilichokuwa kitukufu zaidi na chenye kubaki zaidi kwa Allah Ta’ala basi wakati huo maisha ya mtu huyo yanakuwa na maana nyingine, na furaha hali kadhalika inakuwa na maana nyingine katika maisha.
Mwanadamu huyo akikataa ila kuipa mgongo, basi atakuwa ameiridhia nafsi yake njia nyingi za tabu na balaa ambazo kupata mara kwa mara bila kukatika, na huenda mtu huyo akawa ameridhia nafsi yake njia nyingi za tabu na shida na mashaka anaelea hapo bila kuacha, Allah Ta’ala amesema: “Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini.” (6:125),
Atakaye mpwekesha Mwenyezi Mungu mmoja bila ya kumshirikisha basi mtu huyo atakuwa na moyo uliofunguka na raha na utulivu.
Ama yule aliyempoteza anaufanya moyo wake una dhiki, tabu na kero, Allah atulinde, naye ni mfano wa aliyeamini na kumpwekesha Allah pekee, na yule ambae amemshirikisha Mwenyezi Mungu na kupotea, Mwenyezi Mungu ametoa mfano mwingine; aliposema: “Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na bwana mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao? Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui.” (39:29).
Mtu mshirikina ni kama vile mtu anamilikiwa na idadi ya watu wenye tabia mbaya nao wanashindana, mmoja anamwambia njoo, na mwingine anamwambia kaa, na mtu wa tatu anamwambia simama; mtu huyu anababaika katika jambo lake hana raha ya kiwiliwili wala hana raha ya dhamira yake au nafsi yake, na mwenye kumpwekesha Allah ni kama vile mtu aliyehusika na bwana mmoja tu, angemwamrisha na kumkataza ni mtu mmoja tu, Je, watu hawa wawili wanalingana?! Alhamdulillah, shukran na himidi ni zake Allah pekee, na kusifiwa kuzuri ni kwake, na kuwa Yeye hapana Mola isipokuwa Yeye tu, ama wale ambao hawafahamu wanaishi maisha ya taabu na migongano ya ndani na yanayosuhubiana nayo miongoni mwa tabu na kero na sononeko na babaiko, mgongano na kujiuwa.