Dalili za Rububiya(kuwepo MwenyeEzzi Mungu)

Dalili za Rububiya(kuwepo MwenyeEzzi Mungu)

Dalili za Rububiya(kuwepo MwenyeEzzi Mungu)

Mzuri wa Kuumba

-Je, huoni Ulimwengu huu Mkubwa na yaliyomo katika mbingu na ardhi?!

-Je, umefikiria hata siku moja kuhusu Uumbaji wa mbingu na yaliyomo katika sayari?!

-Je, hukuwahi kuwa na mazingatio katika ardhi ile na vilivyomo ndani yake katika mito, bahari, mabonde na milima?!

-Je, uratibu huu uliopangwa vizuri kwa ubunifu na ufanisi wa hali ya juu haujakufurahisha?.

-Je, ni nani aliyeumba Ulimwengu huu na ukawa katika hali hii ya ubunifu wa hali ya juu iliyopangiliwa kwa mpangilio wa juu kabisa na kupambwa katika umbile hili lenye muujiza kiasi cha kuwa ni alama na ishara ya ukamilifu, na katika isiyokuwa na mfano uliotangulia?!

-Je, ameiumba nafsi yake?! Au katika Ulimwengu huu kuna Muumba mwenye uwezo? Allah amesema: “Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili, Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.” (3:190-191).

$Lord_Kelvin.jpg*

Lord Kelvin

Mwanafizikia wa Scotland
Mungu ni Kweli
“Utakapofikiri kwa kina; Sayansi itakulazimisha kuamini kuwepo kwa Mungu.”

Je, haijawahi kukupitia akilini mwako siku moja kuhusu kuumbwa kwako? Allah amesema: “Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?” (51:21)

Sasa ni vipi alivyoumbwa mwanadamu? Allah amesema: “Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. ” (52:35-36)

Na kama hakuumbwa hapo kabla alipokuwa si kitu, (achilia mbali kwamba wao hawakujiumba na kuumba nafsi zao, bali hawakuumba mbingu na ardhi), hakuna shaka yoyote kuwepo kwa Muumba wa Ulimwengu huu na vyote vilivyomo, nae si mwigine bali ni Allah Mtukuka, cha kushangaza mno ni ile hali wanaopinga kuwepo kwa Allah muumba, mwenye kusawiri kila kitu baada ya ishara zote na dalili mbali mbali!!

Mwitikio wa kimaumbile

$Robert_Morris_Page.jpg*

Robert Morris Page

Mwanasayansi
Hisia za Kimaumbile
“Mungu ambae tunajisalimisha kwa uwepo wake, haishii kwenye Ulimwengu wa Mada, wala hisia zetu dhaifu haziwezi kumdiriki (kumpata), na katika hilo ni mchezo kujaribu kuthibitisha uwepo wake kwa kutumia sayansi: kwa sababu Mungu mwenyewe huchukua duara lisilokuwa duara lake finyu lenye ukomo. Kwa hakika imani ya kuwepo Mwenyezi Mungu ni katika mambo mahususi ambayo yanaota katika hisia ya mwanadamu na dhamira yake na kukua katika mzunguko (duara) wa uzoefu wake binafsi.”

Kwa hakika viumbe wako katika fitra ya kukiri uwepo wa Allah Ta’ala bila ya shaka yoyote ile, kama vile ambavyo anavutika katika kupenda kheri na kuchukia mambo mabaya, bali bila ya shaka kukiri kwao uwepo wa muumba ni katika mambo makubwa yaliyomo na kudumu kwenye fitra kiasi cha kutohitaji dalili yoyote au uthibitisho wowote ule, Allah amesema: “Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui. ” (30:30)

Na Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) naye akasema: “Hakuna mtoto anayezaliwa ila huzaliwa katika fitra” (Bukhari na Muslim).”

Umma zimekubaliana

$Justin_Barrett.jpg*

Justin Barret

Mtafiti katika chuo kikuu cha Oxford
Imani ya Mungu ni maumbile (Fitra)
“Akili zinazokuwa katika hali ya kawaida kwa watoto zinawafanya kuelekea katika kumuamini Mungu Muumba, badala ya makuzi ambayo sio ya kawaida ya akili za binadamu na ugumu wa kukubali na kudhibiti.”

Ummah mbali mbali zimeshakubaliana tokea zamani kunasibisha maumbile na uumbaji wa Ulimwengu huu kwa Allah Ta’ala hivyo kukawepo makubaliano–yaliyodumu ya kuwa Allah Ta’ala ndie muumba wa Ulimwengu huu bila ya mshirika, hivyo Ummah wote hauwezi kuacha kuzingatia kuwepo Muumba wa Mbingu na Ardhi, au Mruzuku asiyekuwa Allah Mtukuka, bali pindi wanapoulizwa kuhusu hayo hukiri (pamoja na ushirikina wao) ule Uungu wa Allah Ta’ala. Amesema Yeye mwenye shani; “Na ukiwauliza; Nani aliye umba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kuti’ii amri yake? Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanako geuzwa? Mwenyezi Mungu humkunjulia, na humdhikishia, riziki amtakaye katika waja wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.” (29: 61-63)

Na akasema vile vile: “Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi” (43:9)

Ama hali ya watu kumkana Mwenyezi Mungu na kukufuru kwao Allah Ta’ala (kama ilivyotangulia kuelezea) ni hali ya kujitenga, yaani ni hali ya kujitenga wafuasi wake wa fikra hii ya kumkana Allah na kundi la watu wenye akili, na kukadhihirika kufeli kwa fikra hiyo katika uhalisia wake.

Ni dharura ya kiakili

$John_Cleveland_Cothran.jpg*

John Cleveland Cothran

Profesa wa Sayansi katika Chuo Kikuu cha Dolth
Kuwa Mwenye Akili
“Je, inawezekana mwenye akili kupima au kuamini kuwa mada tupu ya akili na hekima imejitengeneza yenyewe kwa kubahatisha tu” ?!

Kwa nyongeza ya yaliyotangulia katika dalili na ushahidi mbali mbali yakuwepo kwa Allah na Uungu wake; basi akili ya mtu ni miongoni mwa dalili kuwa ya kuwa Uumbaji huu wa Ulimwengu katika hali hii haiwezekani kabisa kuwa imejiumba yenyewe; yaani kiumbe kilichotokea tu na kuzuka na bila ya shaka yoyote kuwa kila chenye kuzuka hakikosi mzushaji.

Swali lenye kujitokeza hapa; ni mara ngapi umepata dhiki au msiba au lawama, umeelekea kwa nani? Umenyenyekea kwa nani? Nani umemuomba akuondoshee dhara yako na kufariji humumi na huzuni zako?! Allah Ta’ala amesema: “Na taabu inapo mfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyo kuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu njia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni.” (39:8)

$Francis_Bacon.jpg*

Francis Becon

Mwanafalsafa wa Uingereza
Falsafa na Dini
Falsafa kidogo inamsogeza mtu kwenye kumpinga Mungu. Ama kubobea katika Falsafa humrudisha mtu kwenye dini.”

Katika aya nyinginezo Allah amesema, “Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wamesha zongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru. Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. ” (10:22-23)

Na amesema vile vile, “Na wimbi linapo wafunika kama wingu, wao humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapo waokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa sawa. Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliye khaini kafiri mkubwa. ” (31:32).