Rashidi na Maiko walimaliza kula chakula cha mchana. Rashidi aliangaza macho yake juu, kisha akamuwahi rafiki yake:
Rafiki yangu mpenzi Maiko, umeninyeshea kwa mishale ya kunikosoa na umeuweka ustaarabu wangu kizimbani.
Maiko: Sio mishale wala sio tuhuma ewe sahiba yangu, ni mjadala na ukosoaji wenye lengo la kufikia kwenye ukweli, na nadhani sisi tumepiga hatua kubwa katika mijadala hii na yote yenye kuhusiana nayo, kadhalika nashukuru uungwana wako na mtazamo mpana, lakini je, mazungumzo yangu yoyote yaliyotangulia yamekutia dhiki?!
Rashidi: Hapana, hapana, hukuniudhi, lakini nimekusudia ili picha yetu ikamilike hapana budi kuangalia maeneo yake yote, na pia tulinganishe hali ya mwanamke kwenu na kwetu vile vile, yaani ustaarabu wenu na wetu, na nadhani mazungumzo yetu yaliyopita kuhusu mwanamke yameweka wazi kiasi fulani cha taswira ya kadhia ya mwanamke katika ustaarabu wa Kiislamu, kilichobaki ni kuangalia katika kadhia hii kwa miwani ya ustaarabu wenu.
Maiko (Huku akicheka): Sawa nafungua kichwa changu kwa mishale na nafungua mlango wa kizimba.
Rashidi (Akitabasamu): Kwa nini tunajiweka katika eneo la kupigana? Mahusiano yetu haya yanaweza kuwa ni mahusiano ya mjadala na ushirikiano ili kufikia kwenye ukweli kama ulivyotaja.
Maiko: Nakubaliana nawe kabisa, ungependa tuanzie wapi?!
Rashidi: La kwanza ambalo linafaa kuliangalia ni nafasi ya mwanamke katika rejea mbali mbali za ustaarabu.
Maiko: Mtazamo kwa mwanamke na njia ya kuishi nae inatofautiana na mtazamo wa mtu binafsi na kumtathmini kulingana na makuzi yake, malezi na elimu yake, kadhia hapa sio kuangalia nafasi na hadhi ya mwanamke huyu katika kitabu hiki au rejea ile.
Rashidi: Hili ni sahihi, hata hivyo wakati huo huo hatuwezi kuacha rejea ambazo zinatengeneza utamaduni wa mtu yule na kutengeneza maadili ambayo yanaathiri mtazamo wake wa mambo, na ninaposema ‘rejea’ sikusudii vitabu au kutengeneza mwamko wa mtu na utamaduni wake, inaweza kuwa katika rejea hizi huenda kukawa na rejea za kielimu lakini vile vile kila chenye kuathiri katika kutengeneza mazingatio ya mtu na utamaduni wake, baadhi ya visa vya watu na makabila mbali mbali na visa vya kale vyenye kuchukua sura ya sanaa za jadi, hali kadhalika semi, methali na hekima ambazo huvutwa kutoka katika fikra za ndani za watu kwenda kwenye mtazamo wa mtu binafsi, kwa hiyo rejea kwa mtazamo huu kwa nafasi yake huathiri katika malezi na makuzi ya mtu.
Maiko: Mimi naamini kuwa hadhi ya mwanamke na mtazamo kuhusu mwanamke hautofautiani baina ya vitabu vitakatifu vya mbinguni; katika kitabu chetu kitakatifu kuna kufanana mno na Qur’an yenu, muhtasari wa mtazamo huu ni kuwa: Namna alivyoumbwa mwanamke ameumbwa kutokana na mwanamume, na mwanamke ndiye sababu ya dhambi ya kwanza na sababu ya kutolewa peponi, na nafasi yake kijamii na majukumu yake.
Rashidi: Maneno haya kuna pande ambazo nitatofautiana nawe; suala la dhambi ya kwanza na kutolewa kwa Adam na Hawa peponi katika Qur’an inatofautiana na kitabu chenu kitakatifu. Hawa sio sababu ya shetani kumshawishi na kumpoteza Adam, hivyo basi suala la kutolewa peponi sio la mwanamke.
Ukweli ni kuwa mtazamo kuhusu mwanamke na nafasi yake imekuja katika kitabu kitakatifu kuwa: Uzawa wa mwanamke unaongeza unajisi wa kina mama! Injili inasema: “…Mwanamke akipata mimba na kuzaa mtoto wa kiume, unajisi wake utakuwa siku saba kama kwenye hedhi, kisha baada ya hapo hukaa siku thelathini na tatu kutoharisha damu yake…., lakini akizaa mtoto wa kike najisi yake itakuwa kwa muda wa wiki mbili kama kwenye hedhi yake, kisha hukaa siku sitini na sita katika kutoharisha damu yake.”
Rashidi: Ama matendo ya mwanamke katika jamii kwa mtazamo wa Ukristo ni kuwa wanawake wanakatazwa kufungua midomo yao kanisani, katika kitabu kitakatifu cha Wakhorinto ya kwanza 14:34-35 katika kitabu cha Agano Jipya imeandikwa: “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii kama vile inenavyo torati. Nao wakitaka kujifunza neno lolote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.” Haya yote hayana mfano wake kwenye Qur’an.
Maiko: Kwa ujumla ni kuwa yale maendeleo yaliyotokea katika jamii yetu hayawezi kufahamika bila kuunganisha na mizizi ya utamaduni wa Kigiriki na Kiroma ambayo yamechanganyika nayo, na kama hayatachukuliwa mazingatio taathira ya harakati za kidini na islahi za Protestanti ndani yake, pamoja na athari ya fikra za mwamko wa Ulaya na mapinduzi ya Ufaransa na mabadiliko ya jamii wakati wa mapinduzi ya viwanda katika jamii hii.
Rashidi: Ama kwa kuwa umetaja utamaduni wa Kigiriki na Kiroma, kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu mtazamo wa mwanamke kulingana na wakati tunaouzungumzia au hata maendeleo na ustaarabu ambao tunaushuhudia hivi sasa, na tunapofungua ukurasa wa historia ya mwanamke wa Kigiriki tunaona jinsi alivyonyang’anywa uhuru wake na matakwa yake binafsi na nafasi yake katika jamii, walikuwa wanadharau nafasi yake na kumuona ni mnyama wa kuuzwa na kununuliwa, na kumnyang’anya uhuru wake wa matumizi, na kumuharamishia urithi kisheria, hivyo pindi ustaarabu wa Kigiriki ulipopata maendeleo hali ya mwanamke ilibadilika haraka sana, ikawa mwanamke anachanganyika na wanaume na kuingia katika vilabu, kilichopelekea kwenye uchafu na uzinifu, na malaya wakaonekana ni viburudisho vya watalii na wanayo nafasi katika ustaarabu wao na jamii yao, hivyo sanamu za wanawake walio uchi zikatengenezwa kwa jina la sanaa na fani.
Pamoja na tofauti zilizopo, msimamo wa ustaarabu wa Kiroma haujabadiliki sana, nao ni kumdharau, na kumchukulia kuwa yupo chini ya mwanamume ambae ana haki ya kumfanya anavyotaka, sheria ya Kirumi imemvua mwanamke na haki zote za kijamii katika hatua zote za maisha yake, kisha baada ya hapo sheria kuhusu mwanamke ikaanza kubadilika, mabadiliko haya yanatokea katika mfumo na sheria zao zinazohusu familia na ufungaji ndoa na utoaji talaka; mambo yakabadilika kichwa chini miguu juu, na hivyo ufungaji ndoa kwao ukawa hauna maana na mwanamke kupewa haki zote za kurithi na kumiliki, kisha mtazamo wao kuhusu mahusiano ya mwanamume na mwanamke yakabadilika kwa kutokuwepo mkataba wa kisheria kati yao.
Maiko: Na kuongezea: Kwa ujumla kumetokea maingiliano na kupelekea kuathiriana kati ya ustaarabu wa Kigiriki na Kiroma na ule wa Kanisa kuhusu mwanamke pindi Ulaya ilipoingia katika Ukristo, mtazamo na rai za watu wa dini kuhusu mwanamke zikaathirika na kubadilika kwa hali halisi waliyokuwa wakiishi nayo.
Rashidi: Naam, pindi viongozi wa Kanisa walipoona muelekeo wa hali hiyo katika jamii za Kiroma katika kuenea kwa uchafu na maovu na kilichopelekea katika tabia chafu katika jamii, walimchukulia mwanamke kuwa ndie aliyesababisha yote haya; na wakatangaza kuwa mwanamke ni mlango wa shetani na inampasa kuonea haya uzuri wake; kwani ni silaha ya ibilisi kwa fitna na ushawishi….Watu wa Magharibi wakaendelea kumdharau mwanamke na kuzuia haki zake zote katika karne za kati, hata katika zama ambazo ilidhaniwa kuwa mwanamke ameshapata nafasi yake katika jamii, bado haki za matumizi ya mali yake hakuwa nayo ila kwa idhini ya mume wake.
Maiko: Lakini, huoni rafiki yangu kuwa mjadala wetu umegeuka somo la historia?! Tunaweza kuruka kutoka katika hatua hii ili kufikia pale mabadiliko yalipoanza ambayo ndiyo yaliyotufikisha hapa, ninakusudia zama zile za mwamko, kisha mapinduzi ya Ufaransa na yaliyofuatia baada ya hapo.
Rashidi: Sio historia, lakini ni utafiti wa chanzo chenyewe, kwani mimi ninaona kuwepo kwa mahusiano kati ya hali hizi na rai ambazo zinaonwa kuwa ni historia na baina ya hali halisi ya mwanamke katika nchi za Magharibi leo hii pamoja na tofauti ya muonekano wake.
Je, huoni kufanana baina ya hakika hizi za kihistoria na haki za mwanamke katika nchi za Magharibi?!
Maiko: Unakusudia nini kwa mfano?
Rashidi: Mfano: Mwanamke kutumika kama chombo cha kustarehesha wanaume, ilipodhaniwa kuwa mwanamke wa Magharibi amepata haki zake kwa kuwekewa sheria za usawa kati yake na mwanamume katika sehemu zote, mara ikaonekana kuwa amegeuka kuwa ni chombo cha kuchezea katika mikono ya mwanamume, mfano jina la mwanamke kuwa chini ya kivuli cha mumewe na katika himaya mali yake vile vile; ambapo haiba ya mwanamke ilikuwa imefichwa na mumewe na hili halikuondoka ila ilipoanza karne ya ishirini.
Maiko: Lakini mwishowe, mwanamke alipata haki zake, na kwa hiyo akawa sawa na mwanamume katika nyanja zote, hata katika kupata kazi katika vitengo mbali mbali.
Rashidi: Lakini ukandamizaji wa mwanamke Magharibi na kunyimwa haki zake, pamoja na kuwa zingine zimenyanyuliwa kwa kuwekewa kanuni, mikataba na sheria mbali mbali, ila hali ipo kwa kiwango kile kile, hata kama jina la ukandamizaji wenyewe litabadilika na malengo yake kwa jina la harakati hizi, ambazo mwanamume alimtumia mwanamke kama mtego wa kukusanya mali na starehe kadhalika, na mwanamke akabadilika na kuwa bidhaa ya kiwiliwili kuwaridhisha wateja katika sehemu za starehe na michezo na njia ya kupata mali kwa watangazaji biashara, na hii ni kilele cha udhalilishaji wa utukufu wa mwanamke; kiasi cha kumfanya mwanamke aje juu katika baadhi ya nchi na kutaka kutotumika katika matangazo ya kibiashara.
Kadhi wa Sweden, Briggette Hoff Haher akizungumzia uhuru, usawa na ukombozi wa mwanamke anasema: Kwa hakika mwanamke wa Sweden ghafla amegundua kuwa amenunua hali ya kufikirika (anakusudia uhuru aliopewa) kwa thamani inayotisha nayo ni furaha yake ya kweli.”
Ripoti ya Msemaji wa nchi za Ulaya akizungumzia hali ya mwanamke katika nchi za Ulaya na vipi yale madai ya uhuru na ukombozi wa mwanamke kupata haki zake zilikuwa ni kauli mbiu kavu zisizo na maana wala hazina ukweli wowote ule, imekuja ripoti kuwa mashirika ya Ulaya hayafanyi juhudi za kutosha ili kuvunja (kizuizi hiki) ambacho kinawafanya wanawake wasipate nafasi za juu za utawala.
Ane Demanto Pole, msemaji wa nchi za Ulaya katika mambo ya kijamii: “Ulimwengu wa kazi na biashara unaonesha tofauti kati ya jinsia mbili kwa sura iliyo wazi, wakati ambapo-mwanamke anatamaliki kati ya asilimia 20% -30% ya wadhifa wa juu ulio rasmi na utawala wa sekta za umma huko Ulaya, ama nafasi zake katika mashirika binafsi haizidi asilimia 25 huko Ufaransa, 6.3% Uingereza, na nafasi yake ya juu katika benki haizidi asilimia 5% tu.
Kadhalika msemaji huyo wa Ulaya alionesha tofauti nyingine ya mishahara iliyopo kati ya mshahara wa mwanamke na ule wa mwanamume, haswa katika nyadhifa za utawala; ambapo mwanamke anapata mshahara chini ya asilimia 16% ya mshahara wa mwanamume.
Maiko (Akimkatiza): Naona treni imefika kituo chake cha mwisho…tutayarishe mizigo na tukusanye.