HEKIMA YA KUUMBWA KWA ULIMWENGU

HEKIMA YA KUUMBWA KWA ULIMWENGU

HEKIMA YA KUUMBWA KWA ULIMWENGU

Tafakuri katika maumbile ya ulimwengu

Je, umewahi kufikiria Umbile la Ulimwengu?!

$Dr._Paul_Murdin.jpg*

Dr. Paul Murdin

Professor wa Mambo ya Unajimu Chuo Kikuu cha Cambridge
Ewe Mola Wangu!
“Nilipoona baadhi ya picha za anga za hivi karibuni jibu langu la kwanza lilikuwa ni kupiga mayowe nikisema Ewe Mola wangu! Kazi imezaa matunda. Kwa ujumla wake katika umri wangu hicho ni kitu cha kuvutia!!!”

Kwa hakika tafakuri ya Viumbe vya Allah ni moja ya njia nyingi ambazo zinampelekea mtu katika imani, huzidisha yakini kwa mwanadamu, na kumtambulisha kwa ukubwa wa Muumba na upeo wa elimu na hekima yake, Allah Ta’ala Ndie aliyeumba mbingu na ardhi kwa haki, hakuziumba kwa batili wala kwa mchezo wala hakuumba hivi hivi bila ya lengo. Allah Ta’ala amesema: “Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini.” (29:44).

Katika ulimwengu huu kuna viumbe kiasi gani ambao hawahesabiki! Unadhani wameumbwa kwa hekima ipi?!

Katika Ulimwengu huu kuna alama na dalili mbali mbali ambazo zinaonyesha kwa uwazi uwezo wa Allah Ta’ala na elimu mambo leo inaendelea kuvumbua na kutafiti dalili na alama mbali mbali ambazo zina mfanya mwanadamu ahisi utukufu wa Muumba huyu.

Lau mtu akifikiri kwa undani zaidi kwa Ulimwengu huu na yaliyomo katika Viumbe vya Allah atayakinisha ukamilifu wa yakini kuwa Ulimwengu huu umeumbwa kwa uwezo usio na ukomo kwa ufanisi wa hali ya juu kabisa, na aliyeumba ni Mungu Mwenye hekima, mwenye uwezo, Mjuzi amepima na akaufanyia uzuri kipimo chake.

$Edgar_Mitchell.jpg*

Edgar Mitchell

Wa sita katika wanaanga waliokwenda mwezini
Miongoni mwa dalili za Uungu
“Kuona kwangu sayari yetu ilikuwa ni ishara (maono) ya kiungu.”

Inatosha kufahamu kwa kuzingatia ya kuwa ndani ya Ulimwengu huu na mbingu zake na sayari na nyota zake na yaliyomo kama vile ardhi yetu, bahari, mito, ardhi, milima, wanyama, na miti ambao imeumbwa na Allah na ambayo haikuwepo hapo kabla ili pate hisia ni kiasi gani uwezo wa Allah, elimu yake na hekima yake, Allah Ta’ala amesema: “Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini? Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka. Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake. Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea. ” (21:30-33).

$James_Irwin.jpg*

James Irwin

Mwanaanga
Huu ni Uumbaji wa Mungu!!
“Kuona jambo hili kutambadilisha mwanadamu, na kumfanya mtu kuthamini viumbe vya Mungu na kumpenda Mungu.” Akizungumzia kuhusu Ulimwengu.

Na pindi mwenye akili anapofikiria katika viumbe wa Allah, mtu anakuwa anafahamu kwa elimu ya yakini kuwa yaliyo katika Ulimwengu huu yanamuabudu Mola wake; kila kiumbe chake kinamsabihi kwa himidi zake Allah, Allah Ta’ala amesema: “Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima. ”(62:1)

Na kusujudu kwa utukufu wake, Amesema Allah Ta’ala “Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda apendayo.” (22:18).

$Deborah_Potter.jpg*

Deborah Potter

Mwanahabari wa Kimarekani
Mungu Kumkirimu Mwanadamu.
Uislamu ambao ni kanuni ya Mwenyezi Mungu tunauona ukiwa ni wazi katika mazingira yanayotuzunguka; Kwa maamrisho pekee ya Mwenyezi Mungu, milima, bahari, sayari, nyota zinakwenda na kuongoka katika mapito yake (mzunguko wake). Vivyo hivyo kila atom katika ulimwengu huu (hata viumbe visivyokuwa hai) ila mwanadamu amevuliwa (anaondolewa) katika kanuni hii; kwani Mwenyezi Mungu amempa uhuru wa kuchagua; kwa hiyo anaweza kujisalimisha kwa amri ya Allah au akaweka kanuni zake mwenyewe na kwenda katika dini yake ambayo anairidhia, kwa masikitiko njia ya pili ina vizuizi vikubwa.”

Vivyo hivyo, viumbe hivi vinamsabihi Allah Ta’ala na kumswalia, Allah amesema: “Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa vilivyomo katika mbingu na ardhi, na ndege wakikunjua mbawa zao? Kila mmoja amekwisha jua Sala yake na namna ya kumtakasa kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua wayatendayo.”(24:41),

Hivyo basi muumini ataona kuwa Ulimwengu wote huenda na kutembea kama vile ni msafara mmoja katika muelekeo mmoja kwa Allah, hivyo basi pia atakwenda kwa furaha kwa muelekeo huu mzuri uliobarikiwa na maisha yake na utulivu wa roho yake.

Dalili ya kuumbwa ulimwengu kwa kumpwekesha Allah

Kwa hakika Ulimwengu huu mpana na yaliyomo ndani yake katika viumbe na miujiza ni ushahidi mkubwa wa utukufu wa uwezo wa Allah Ta’ala na ukamilifu wa maumbile yake na hii ni dalili ya kumpwekesha Allah Ta’ala, na kuwa hana Mola asiyekuwa yeye wala Mungu asiyekuwa Yeye, Allah Ta’ala amesema: “Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote. Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao sikia. Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na tamaa. Na hukuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao zingatia. Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapo kuiteni mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi. Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamt’ii Yeye. ” (30:20-26)

Katika aya nyingine amesema: “Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha naye? AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka. Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui. Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia. Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye. Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.” (27:59-64).

Kumkirimu na kumdhalilishia mwanadamu

$Deborah_Potter.jpg*

Deborah Potter

Mwanahabari wa Kimarekani
Miongoni mwa dalili za Utume.
“Vipi Muhammad (mtu asiyesoma yaliyoandikwa) ambaye amekulia katika jamii ya Jaahiliya amejua miujiza ya Ulimwengu ambayo imeelezwa na Qur-aan Tukufu. Ambayo hadi hivi sasa sayansi inaendelea kuyatafiti?! Hapana shaka basi maneno haya kuwa ni maneno Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

Mwenyezi Mungu amemuacha huru mwanadamu na kuabudu vitu; na hivyo kujaalia vyote vilivyomo katika ardhi hii vikiwa vimedhalilishwa kwa ajili ya mwanadamu kama ni fadhila na takrima kwake kutoka kwa Allah peke yake; kwa lengo la kufanikisha uimarishaji wa ardhi, ukhalifa, na zaidi ni kukamilisha utekelezaji wa ibada ndani yake, na kudhalilishwa hapa ina maana mbili: kudhalilishwa kwa ajili ya kumfahamu Allah, fadhila zake, ukarimu na utukufu wake. Na kudhalilishwa kwa maana ya kumkirimu mwanadamu na kunyanyua hadhi yake ukilinganisha na vile vilivyodhalilishwa kwake; Allah Ta’ala amesema: “Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake….” (45:13)

Na amesema vile vile Allah mtukufu: “Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni. Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu. Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.” (14:32-34)

Hadi tutakapokuwa na yakini ya kukutana na Allah

Hakika katika umbile la mbingu na ardhi (tuache suala la kuumbwa kwa mwanadamu) ni uthibitisho ulio wazi kuhusu ufufuo baada ya kifo, je, haikuwa suala la kurejesha maumbile ni rahisi na mepesi zaidi kuliko kuumba mara ya kwanza?! Allah Ta’ala amesema: “Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake….” (30:27)

$John_Glenn.jpg*

John Glenn

Mwanaanga wa kwanza wa Kimarekani
Haki ni Moja
“Kuangalia aina hii ya kiumbe wala usimuamini Mwenyezi Mungu hilo kwangu mimi ni jambo lisilowezekana ….Hili limezidisha imani yangu. Natamani pawepo na maneno yenye kuelezea tukio hili.

Bali kwa hakika kuumbwa mbingu na ardhi ni kukubwa kuliko maumbile ya mwanadamu, Allah Ta’ala amesema: “Bila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu. Lakini watu wengi hawajui.” (39:57)

$027_7.jpg*

%%

Uko wapi ndani ya Ulimwengu huu.
“Picha hii ni ya mkusanyiko mkubwa wa sayari (galaxies) Sehemu yake ndogo huwakilisha sayari na njia zake ni zaidi ya 1,000,000,000,000 ya jua. Na jua ni kubwa kuliko ardhi kwa mara 1,300,000, na ardhi ni kubwa kuliko nyumba yako (kwa mfano ukubwa wa nyumba yako ni mita 500)kwa mara 1,020,144,000,000 na nyumba yako ni kubwa kuliko wewe mwenyewe kwa mara ngapi.”?!’

Na Allah Mtukufu akasema: “Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona, ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt’ii, kila kimoja kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na Mola wenu Mlezi.” (13:2).