- Mtake Msaada Mwenyezi Mungu.
“Pengine ingewezekana kuokoa maelfu ya wanaoadhibika kwa kupiga makelele katika hospitali za wendawazimu, lau wao wangeomba msaada kwa ulinzi Mwenyezi Mungu badala ya wao wenyewe kuingia kwenye mapigano na Nafsi zao bila ya msaada wala muokozi.”
- Mtu wa Dini na Mgonjwa
“Nakumbuka yale masiku ambayo hakukuwepo na mazungumzo ya watu isipokuwa kuhusu ugomvi baina ya elimu na dini. Mgogoro huu uliisha bila kurejewa, kwani elimu ya sasa ya tiba ya nafsi inatoa habari nzuri kuhusu misingi ya dini. Kwanini?!! Kwa sababu matabibu wa nafsi wamegundua kuwa kuwa imani yenye nguvu na kushikamana na dini na swala hutosheleza kushinda wasiwasi, khofu na msongo wa mawazo na kutibu nusu ya maradhi ambayo tunayoyalalamikia. Hadi Dr. A. A. Bell akasema: ”Kuwa mtu mwenye kushikamana na dini hasumbuliwi na maradhi ya nafsi.”
- Kuwa Mbobezi
“Mwanafalsafa Francis Becon alisema kweli aliposema, “Falsafa ndogo humpelekea mtu kwenye kumkana Mungu. Ama kubobea katika falsafa humrejesha mtu kwenye dini.”
- Kushika Dini ni tiba ya Maradhi
“Matabibu wa nafsi wamegundua kuwa imani madhubuti na kushikamana na dini inamtosha kushinda khofu, wasiwasi na msongo wa nafsi na kuponya maradhi haya.”
- Starehe ya Kiroho.
“Kinachonishughulisha mimi sasa hivi ni ninachokipata katika neema za dini. Kama vile ambavyo ninajali neema tunayopata kutokana na umeme, chakula bora na maji safi. Haya yote hutusaidia kuishi maisha mazuri yenye neema. Ama dini hunipa mengi zaidi ya haya. Hunipa raha starehe ya kiroho, au hunipa (kama aliyozungumza William James) msukumo wa nguvu wenye kuunganisha maisha. Maisha yenye nafasi, yenye furaha maridhawa, kwa hakika inanipa imani, matarajio na ujasiri na huniondolea khofu, sononeko na wasiwasi. Vile vile hunielekeza kwenye malengo katika maisha na hukunjua mbele yangu upeo wa furaha na kunisaidia katika kujenga chemchem ya maji na rutuba katikati ya jangwa la maisha yetu.”